ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 6, 2014

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU KUANZA DISEMBA 17-21, 2014 JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi  21 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link Education, Abdulmalik Mollel, alisema lengo la maonyesho hayo ni kutambulisha wadau wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.

Alisema ushiriki wa asasi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi utakuwa na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney, alisema wakati umefika kwa Watanzania kujua umuhimu wa maonyesho ya Elimu maana yamekuja kutatua matatizo mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wazazi pindi wanapokuwa wanawatafutia shule na vyuo watoto wao.

Aidha alisema maonyesho hayo yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa.
Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’

Friday, December 5, 2014

KAMATI YA BLOGGERS TANZANIA YAANZA KUJADILI RASIMU.

Mwenyekiti wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers).  Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, Othman Maulid.
Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha (kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati,  Henry Mdimu.
Wajumbe wa kamati wakipitia rasimu hiyo. Kulia ni William Malecela na Mariam Ndabaganga.
Mwenyekiti wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha,  Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Longue, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.


Na Dotto Mwaibale,

WAJUMBE wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers) wameanza vikao vyao kujadili rasimu ya katiba ya umoja huo kabla ya kufanya usajili wa chama chao kitakacho waunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao hiyo Tanzania.

Akizungumza leo katika vikao hivyo vinavyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania, Joachim Mushi amesema wajumbe waliokutana ni wawakilishi wa wamiliki wa mitandao hiyo kutoka makundi mbalimbali ya waendeshaji hao wa mitandao ya jamii nchini.

Alisema pamoja na mambo mengine wajumbe hao wanatarajia kufanya majadiliano baada ya kuipitia rasimu ya Katiba ikiwa ni kuelekea mchakato wa kupata Katiba ya Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania. Alisema masuala mengine ambayo yataongoza mjadala huo ni pamoja na kuangalia muundo wa chama, uendeshaji wake, maadili ya chama kwa wanachama katika utekelezaji kazi zao.

"Kikao hiki kinashirikisha wajumbe wa kamati ambao ni wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya jamii Tanzania na kazi kubwa ambayo wataifanya leo kwa pamoja ni kupitia rasimu ya uumoja wetu. Wajumbe wote walikabidhiwa rasimu hii wiki mbili zilizopita kuipitia wenyewe kabla ya kukutaka katika majadiliano ya leo," alisema Mwenyekiti wa Muda, Mushi.

Aidha aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mchango wake wa dhati wa kuwaunga mkono Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania hasa katika kipindi hiki cha mchakato kuelekea uundwaji wa chama chao. 

Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo ya muda waliokutana ni pamoja Shamim Mwasha (Katibu Msaidizi) Khadija Kalili (Katibu), Joachim Mushi (Mwenyekiti), Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe), William Malecela (Mjumbe), Othman Maulid (Mjumbe-Zanzibar) na Francis Godwin (Makamu Mwenyekiti - Iringa).

Mkutano wa mafunzo wa idadi kubwa ya wawakilishi wa wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini (Bloggers) uliofanyika Novemba 11, 2014 jijini Dar es Salaam ulioitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania uliibua uundwaji wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania chini, ambapo kamati hiyo ilipewa jukumu la kupitia rasimu kabla ya kushughulikia usajili wa chama cha jumuia hiyo.
(Imeanadaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

BINGWA MBIO ZA MITUMBWI KANDA YA ZIWA KUONDOKA NA 2,700,000/=

Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za fainali za Kanda za mashindano ya bio za makasia zijulikanazo kama “Balimi Boat Race” zinazo dhaminiwa na bia ya Balimi Extara Lager zinazo tarajiwa kufanyika katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza leo.
Na Mwandishi Wetu.Mwanza
Bingwa wa fainali za mashindano ya mbio za makasia Wanaume, chini ya udhamini wa Bia ya Balimi Extra Lager yajulikanayo kama “Balimi Boat Race 2014” anatarajia kujinyakulia kitita cha pesa taslimu Shilingi Milioni 2,700,000/=,Kikombe pamoja na medali za dhahabu kwa wanakikundi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya Balimi Exra Lager, Edith Bebwa alisema fainali hizo zitaanza majira ya saa tatu na asubuhi na kuendelea katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo jumla ya vikundi 15 vya Wanaume kutoka katika mikoa mitano ya Kanda ya ziwa vitachuana kumtafuta bingwa wa Kanda kwa mwaka 2014 na vikundi 11 upande wa Wanawake.
Edith alisema mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoshiriki ni Kigoma,Kagera,Mwanza,Musoma na Kisiwa cha Ukerewe ambacho kinabeba hadhi ya Mkoa.

Mshindi wa pili Wanaume atazawadiwa pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,mshindi wa tatu Shilingi 1,700,000/= na wa nne 900,000/=.Wakati mshindi wa tano hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila kikundi alisema Edihi.

Upande wa wanawake bingwa wa mwaka 2014 ataibuka na kitita cha pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,kikombe na medali za dhahabu kwa wanakikundi wote.Mshindi wa tatu atazawadiwa Shilingi 1,700,000/=,wa tatu Shilingi 900,000/= na wa nne 700,000/= wakati mshindi wa 5 hadi wa 10 watazawadiwa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi.

Nae Meneja wa Kampuni ya Bia nchini Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki aliwaomba wakazi wa jiji la Mwanza na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi katika ufukwa wa Mwaloni kushuhudia fainali hizo zenye mvuto wa pekee na mwisho wafahamu nani atachukua ubingwa wa mbio hizo kwa mwaka 2014.


Meneja matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema vikundi vyote vimeshawasili jijini Mwanza tayari kwa mpambano wa kumpata bingwa wa mwaka huu na maandalizi kwa ujumla yamesha kamilika hivyo nae aliwaomba watu wajitokeze kushuhudia mbio hizo.

MANJU MSITA KUPEPERUSHA BENDERA MOZAMBIQUE FASHION WEEK 'MFW-2014'

Mbunifu wa Mavazi nchini Manju Msita kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wake katika Mozambique Fashion Week yatakayoanza desemba 10 mpaka 14 ambapo atakuwa akipeperusha bendera ya taifa
Mwanamitindo Matukio Chuma kulia akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa kutangaza  upeperushwaji wa bendera ya tanzania katika nchi ya mozambique fashion week ambayo mbunifu wa mavazi Manju Msita atashiriki na kupeperurusha bendera ya Tanzania kushoto ni mwanamitindo Vivian Williams ambaye anafanya shughuli zake za uwanamitindo nchini Barcelona .Spain
Mwanamitindo anaefanya shughuli zake nchini Barcelona Spein Vivian Williams kushoto akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wake nchini kwa ajili ya kushiriki maonesho ya SwaHILI fASHION WEEK yatakayoanza ijumaa ya Desemba 5 mpaka 7 kulia ni Mwanamitindo Matukio Chuma
Mbunifu wa Mavazi nchini Manju Msita katikati akiwa na wanamitindo anaefanya shughuli zake nchini Barcelona Spein Vivian Williams na Ieva Stropule anaeishi ujerumani
Mbunifu wa Mavazi nchini Manju Msita katikati akiwa na wanamitindo anaefanya shughuli zake nchini Barcelona Spein Vivian Williams na Ieva Stropule anaeishi ujerumani.
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila kushoto  akiangalia zawadi  aliyopewa na mwanamitindo Matukio Chuma iliyotoka kwa Manju Msita.
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila kushoto  akipokea zawadi kutoka kwa mwanamitindo Matukio Chuma iliyotoka kwa Manju Msita. 
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila kushoto  akipokea zawadi kutoka kwa mwanamitindo Matukio Chuma iliyotoka kwa Manju Msita.

AIRTEL YATOA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 15 KWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (kushoto) akikabidhi jezi kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akikabidhi jezi kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya kifurahia jezi baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akikabidhi kikombe kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akimkabidhi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akimkabidhi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.

Airtel yatoa vifaa vya michezo kwa chuo kikuu cha Dar es saalam
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vifaa vya michezo kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali yanayotegemea kuanza jumatatu ijayo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mchango huu ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuendeleza michezo nchini inayodhirishwa kupitia mpango wake wa kuinua soka la vijana chini ya miaka 17 wa Airtel Rising Stars mpango ambao umewawezesha vijana wakitanzani na Afrika kwa ujumla kuonyesha uwezo wao wa kisoka na kuweza kufikia malengo yao.
Akiongoe wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Leo tunatoa vifaa vya michezo ikiwemo seti 12 za jezi, shinguard, soksi, glovu za goalikipa pamoja na makombe yatakayowezesha kuendesha mashindano haya yanayoshirikisha wanafunzi kutoka vituvo mbalimbali chuoni hapa. Niwazi kwamba michezo ni burdani na ni sehemu ya kujenga mwili na afya hivyo ni muhimu pia kwa wanafunzi kutenga muda wao wa masomo na kushirikia katika michezo mbalimbali.  Natoa wito kwa wanafunzi wengi kujitokeza na kushiriki mashindano haya.”.
“Udhamini wetu leo ni mwanzo wa mkakati wa kutoa ofa kabambe itakayowapatia wanavyuo uhuru wa kuongea na kupata dhamani yamatumizi ya pesa zao
Ofa hii ya huduma maalumu ijulikanayo kama UN255 Itazinduliwa rasmi wakati wa kilele cha michuano hiii mwishoni mwa wiki ambapo wanafunzi watafurahi huduma zetu nyingi ikiwa ni pamoja na internet, ujumbe mfupi , kupiga simu kwa gharama nafuu. Aliongeza Mmbando
Kwa upande wake Naibu Makamu mkuu wa chuo Profesa Yunus Mgaya alisema” nawashukuru sana Airtel kwa mchango wa mkubwa na kwa kutuwezesha kupata vifaa vya michezo zitavyotuwezesha kuvitumia muda wote wa mashindano. Sisi kama chuo hatukuwa na bajeti ya kununua vifaa hivi hivyo msaada huu umekuja kwa wakati muafaka hivyo nawapongeza sana Airtel kwa mchango wao.”
“Vifaa hivi vitaleta tija kwa wanafunzi na kuinuua michezo chuoni hapa na ofa hii  UN255 itawawezesha wanafunzi na pamoja na  familia yetu yote ya chuo kikuu cha Dar es saalam kufurahia huduma za mawasiliano bora na kwa bei nafuu” aliongeza Mgaya

TAHADHARI KUTOKA MICHUZI MEDIA GROUP


MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA MICHUZI MEDIA GROUP (MMG) ANAPENDA KUTAHADHARISHA WADAU POPOTE WALIPO KUHUSIANA NA UJUMBE (PICHANI) AMBAO UPO KWENYE FACE BOOK NA HATA KWENYE TWITTER) KWAMBA UJUMBE HUO  HAUHUSIANI KWA LOLOTE NA ANKAL MUHIDIN ISSA MICHUZI,  WALA MMG AMA WAKALA WAKE. 
HIVYO TUNAWASIHI TUSIHUSISHWE NAYO NA PIA TUNAWAOMBA KUWA MACHO NA MAMBO KAMA HAYA,MAANA ULAGHAI NA UTAPELI MITANDAONI NI MWINGI MNO.

AHSANTENI SANA
ANKAL

Thursday, December 4, 2014

HILI NDILO PICHA KAMILI NA TAARIFA YA MAFURIKO YALIYOTOKEA MWANZA.

MVUA kubwa iliyonyeesha juzi (jumanne) asubuhi imeleta mafuriko katika maeneo mbalimbali Jijini Mwanza  huku eneo la mabatini likiathirika zaidi na mafuriko hayo yaliyoambatana na mvua kubwa iliyonyeesha takribani  kwa muda usipoungua  masaa mawili.

Mafuriko hayo yalisababisha maji kujaa katika nyumba za wakazi wa maeneo ya mabatini,pia mafuriko hayo yalisababisha magari kutopita eneo la daraja la mabatini linalotumiwa na waenda kwa miguu baada ya maji hayo ya mafuriko kuigawa barabara ya mabatini hali iliyosababisha kukatika kwa mawasiliano.

Juhudi za jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao walifika mapema eneo la tukio zilisaidia kuokoa baadhi ya wakazi wa nyumba zilizokumbwa na mafuriko yaliyosababisha nyumba hizo kujaa maji ndani.
Katika zoezi hilo la uokoaji watu mbalimbali waliokolewa wakiwepo watoto wadogo na akina mama huku mali mbalimbali zikiwemo runinga,vitanda,magari yakisombwa na mafuriko hayo.
Akizungumzia tathimini ya zoezi nzima la uokoaji Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Jijini Mwanza,Andrew James Mbate amesema zoezi la uokoaji lilienda vizuri na walifanikiwa kuokoa maisha ya watu waliokowepo ndani ya nyumba huku akitanabaisha changamoto mbalimbali walizokutana nazo katika zoezi zima. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Wanajeshi wa Kikosi cha zimamoto Mwanza wakimvusha mama huyu kutoka juu ya paa la nyumba moja hadi upande wa pili penye usalama kupisha maji yaliyokuwa yamefurika hata kuzifunika nyumba za wananchi eneo la Mabatini jijini Mwanza. 
“Zoezi la uokoaji lilienda limeenda salama na linaendelea vizuri tunashukuru wenzetu wa shirika la umeme waliwahi kukata umeme mapema hali iliyopelekea sisi kama Jeshi kuanza kazi mara moja tulivyofika eneo la tukio”. Aliongeza Gadafi ambaye ni msemaji wa jeshi la Zimamoto

Akizungumza juu ya mafuriko hayo mkazi wa mabatini,Charles Samson alisema wamepoteza vitu vyao vya thamani huku wakioomba serikali iwasaidie kuhama mabondeni kwani madhara yaliyowakuta ni makubwa.

Tanesco walizima umeme kwaajili ya tahadhali.




Kivuko asilia ni ajira kwa wengine.
Gari hili nyang'anyang'a mara baada ya kusombwa na mafuriko na kubinuliwa kisha kutoswa mtaroni. 
Msaada tutani.
Eneo la mabatini ni eneo ambalo mto mirongo unapita hali iliyosababisha mafuriko hayo kuwa makubwa kwa kuwa maji yam to huo yanatoka sehemu mbalimbali za wilaya zilizopo Mkoani Mwanza ikiwemo wilaya ya magu.

MAMA ALIYETELEKEZWA NA MUMEWE AOMBA MSAADA KWA WASAMALIA WEMA

WANAWAKE wengi duniani bado wananyanyaswa kijinsia kwa sababu za kijamii, kiuchumi na kipato licha ya kuwepo kwa elimu kuhusu haki zao.

Mwanamama Ester Charles ambaye ni mkazi wa Mwambani wilayani Ilemela ametelekezwa na mumewe aliyetajwa kwa jina la Albinus na kubakizwa na watoto wawili wadogo wanaohitaji uangalizi na usimamizi. Pichani mwanamama Ester akiwa na mtoto wake mdogo anayetaabika na ugonjwa wa kupooza. 

KWA UFUPI
Mumewake alipopata mwanamke mwingine alihama nyumba aliyokuwa akiishi na mama huyu na kupanga eneo jingine kabisa bila kuikumbuka familia yake katika matumizi na mahitaji muhimu.

Alipomfikisha mumewe huyo mbele ya mikono ya Sheria alikubali kutoa huduma lakini ndani ya kipindi kifupi alitorokea kusikojulikana.

Amefika mbele ya GSengo Blog kuomba msaada toka kwa wasamalia wema watakaoguswa na simulizi yake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Hali ya afya ya kwa mtoto Jr. Albinus si ya kuridhisha na haijafahamika nini kinachomsibu kwani bado hajafika hospitali kupata matibabu ya kina. Mtoto huyu pichani hawezi kutembea, hawezi kuzungumza kwa ufasaha wala kukaa, zaidi ya kulala tu muda wote.

CHANGAMOTO ALIZONAZO MAMA ESTER.
Hana pesa kwaajili ya chakula cha watoto.
Hana nguo kwaajili ya kuwavisha watoto na yeye binafsi.
Anadaiwa pesa ya kulipia nyumba anayoishi kiasi kwamba mwenye nyumba anataka kumfukuza.

Amejaribu kuomba kazi kwenye kaya mbalimbali na kukosa, akipewa majibu kuwa hawezi kuajiriwa akiwa na watoto (atashindwa kufanya majukumu ya mwajiri) naye hana sehemu ya kuwahifadhi iwe ndugu au majirani.

Jeh! Umeguswa tafadhali wasiliananaye kupitia namba 0753804881.


MUNGU AWABARIKI.

Wednesday, December 3, 2014

PICHA TANO ADIMU NDANI YA BIHARAMULO MKOANI KAGERA.

Mwanafunzi wa shule ya msingi Msalabani iliyoko Wilayani Biharamulo akiwa katikati ya ramani ya Afrika Mashariki iliyochorwa kwa sanaa kupitia nyumba za konokono.
Taswira.
Ngoma hizi nilizozifuma kwenye moja ya shule za msingi wilayani Biharamulo zilinikumbusha ladha ya moja ya shule za msingi nilizopita enzi naskuli primary. Hinduki Primary School Malampaka wilayani Maswa mkoani Shinyanga.
Pikipiki ya Mwalimu mkuu chini ya mti wa kengele ya shule ya Msingi Mkunkwa iliyoko wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Kilimo kwa vitendo mashuleni.
Msalaba huu umedumu mpaka leo bila kuoza (najiuliza ni mbao gani hii) umekuwepo mahali hapa tangu mwaka 1932, enzi za ukoloni ukiwa kama kielelezo kilichowekwa na wamisionari cha barabara kuelekea Kanisa kuu la Jimbo  kijijini hapa. Kijiji kinaitwa Msalabani kipo wilayani Biharamulo mkoani Kagera nchini Tanzania.
Huu ni kama utalii vile...!!

KAMPUNI YA BRITAM YAONGEZA UWEPO WAKE KATIKA SOKO LA AFRIKA MASHARIKI.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Insurence Business ya Britam, Stephen Wandera akizungumza muda mfupi baada ya kampuni hiyo kuungana na kampuni ya 
Real Insurence Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya bima ya Real na Britam wakigongesha grasi baada ya kampuni mbili hizo kuunga pamaja katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Picha na Jumanne Juma

PRESS RELEASE

KAMPUNI YA BRITAM YAONGEZA UWEPO WAKE KATIKA SOKO LA AFRIKA MASHARIKI.

Dar es Salaam…Kampuni ya Bima ya REAL Tanzania sasaimekuwa ni mojakatiya makampunimakubwarasmichini ya Kampuni ya Britamambayoinatoahudumambalimbali za kifedha. Hiiinafuatiakununuliwawa Kampuni hiyo ya Bima na Kampuni ya Britamkutoka Kenya.

Kufutiahatuahiyo Kampuni ya REAL itakuwa na wigompana wa kutoahudumaza bimazikiwemobima za Afya na Bima za maishaambazotayarikampuni ya Britamimekuwaikitoa kwa mudamrefukatikaukandahuu wa AfrikaMashariki. Muunganohuuutaboreshahuduma za bimanchini Tanzania naAfrikaMasharikiambayo kwa sasaBritaminanguvu ya kifedha, kiteknolojia na rasilimaliwatu.

Kufutiahatuahii, Britamsasainaongozakwaukubwa wa kijografiakuliko Kampuni zoter za BimaAfrikaMashariki, pia Kampuni hiyoinashikilianafasi ya pilikulingana na pato la ziada.

Mchakato wa ushirikiano na muungano wa Kampuni hizombiliumekuwaukiendelea kwa miezi kadhaasasana kufuatiwa na kupatakibalikutoka kwa mdhibiti wa Mamlaka ya Masoko na  Mitaji ya nchiniKenyana kutekelezwa na washirikikutokaBritam na REAL kwa kusaidiwa na Kampuni ya Usimamizi wa Kimataifa ya Mckinsey na washauriwengine.

“Kutokananamuunganowa Kampuni hizi mbili, uwepowetuumekuwa kwasehemukubwasana,” alisemaBwana Peter Munga, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REAL na Britam Tanzania.

Bwana Mungaaliendeleakusemakwambamuunganohuonimojakati ya makampuni ya kutoahuduma za BimakatikaAfrikaMashariki, kwanisasa Kampuni hizozinatoahudumakatikanchi 7 tofautiambazo ni; Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini, Malawi na Msumbiji.



Piaaliwahakikishiawamilikiwahisa, wauzaji, watoahuduma za bima na wadauwenginekwambawotewenyemikataba na Kampuni hizombilibadozitaendelakudumuhadimwishonimwamwaka na kila Kampuni itawajibika kwa madeniyeyotewanaodaiwa kwa kipindikilichobaki.
Kuunganakwa Kampuni hizombili ni fursa kwa Britamkuongezauwepo wake katikasoko la kitaifa na AfrikaMashariki na piakuongozasokokatikabiasharazoteambazoinazifanya.
Muunganowa Kampuni hizombilipiaunaonekanakamahatua ya kwanza ya kuimarishasekta ya Bima Tanzaniaambayoinaushindanimkubwa. Soko la Bima Tanzania lina zaidi ya makampuni 29 yanayofanya kazi katikasokohilo.
MuunganohuuinaiwezeshaBritamkutekelezamkakati wake we kupanuabiasharayake ya Bimanapiakutoahudumazinginembalimbalikatikamaeneomuhimu ya kijografiakama Tanzania ambayoyameonyeshauwezomkubwawa kukuwakiuchumibaraniAfrika.


Maelezo mafupikuhusu British-American Investments Company (Kenya) Limited
Britamnikampunitanzuinayoongozakatikahudumatofauti za kifedha na iliyokatikasoko la hisa la Nairobi Securities Exchange. Makampuniyaliyochini ya Britamyanamaslahi na vitegauchumikatikamakampunimbalimbalindani ya AfrikaMashariki.

Britaminatoahudumambalimbali za kifedha, za Bima,Bishara za Vitegauchumi,Ununuaji na uuzaji wa Nyumba, Utunzaji wa vitegauchumivyaBiashara na huduma za Benki.

Britaminazohudumatofautikama vile Bima za maisha,Bima za Afya na huduma za bima za mudamrefu na mfupi, huduma za pensheni, Uwekeji wa Hisa, Mifuko ya Hisa,Mipango na Uwekezaji, Uwekezji wa nje na Ndani na huduma za Pensheni ya uzeeni.

Kwa maelezo Zaidi tafadhalitembeleatovutihiihttp://www.britam.co.ke/

CHEREKO LA USIKU WA SUMAI, BONGE LA PARTY LA SEND OFF LAFANYIKA JEMBE BEACH MWANZA

Sumai Kazi (with white dress) akiwa na dada ake wakiingia eneo la ukumbi kwa kutumia boat maalum ili kujumuika na ndugu jamaa na marafiki waliofika Jembe Beach kushuhudia Send Of Party yake.
Wakishuka kwa kutumia ghati tayari kuingia ukumbini.
Sumai (L) akiwa na dadayake (R) sanjari body guard wake. 
Sumai's Night.
Body guard namba moja.
Mazingira ya juu ukumbi wa bustani tulivu ya Jembe Beach Mwanza mahali ambako kulifanyika Usiku wa Sumai.
Sumai akiwakabidhi keki wazazi wake Mr& Mrs Kazi.
Sumai akikabidhi keki familia ya upande wa Bwana Harusi mtarajiwa.
Kitu cha udrinki wa milipuko....kilihusishwa kama sehemu ya ufunguzi wa sherehe na kusherehekea usiku wa Sumai.
Sumai akitosti na familia ya wakwe zake.
Sumai akimkumbatia shangazi yake.
Sumai akimvisha zawadi mumewe mtarajiwa Jully Ilunga Mbwebwe mara baada ya kumtambulisha kwenye hafla maalum iliyofanyika katika bustani yenye maadhari ya mvuto wa kipekee ya Jembe Beach aka Jembe ni Jembe jijini Mwanza.
Sumai Kazi akiwa na mumewe mtarajiwa Jully Ilunga Mbwebwe ambaye wapambe wake wanamuita Weston Grand Packeboo.
Familia ya ndugu na jamaa wa Jully Iluga Mbwebwe walikuwa na zawadi maalum kwa Sumai, na hapa walimkabidhi vito vya thamani na kumvisha.
Misosi tyme.
Apple thing.
Pacho Mwamba ni msemaji wa Familia na hapa akiungana na wageni kupata chakula.
Wakijinafasi.
Hapo vipi....!!?
Sister Sisters kutoka kushoto ni Sis-Kanengo, Sis-Matata na Kebby. 
Utamaduni wa Mwafrika kanga muhimu kuhusika.
Mambo ya vidole juu kwa akinamama na akinadada.
Sumai hapa alioga fedha mpaka baaasi.
Mama ni Mama.
Mr & Mrs Kazi wakizawadiwa kwa kuzaa chema.
Mizawadi mpwachaa!!
Kapu la mama.....hilooooo!!!
Mijihela....!!
Shavu....!!
Mkono wa kheri.
Hapa zilimwagika dorali kama gunia saba hivi....
Zawadi za Sumai kwa Baba na Mama.
Kamati ikiwasilisha mchango wake kama sehemu ya zawadi.
Kisha ikajitambulisha.
Bye Bye...!!
Dance la Bwana harusi mtarajiwa na nduguze lilikuwa nowmer siunajua tena wakongomani na masebene walisebenuka ile kisawasawa....!!
Mc G.Sengo (L) na mwanamuziki wa Fm Academia Patchou Mwamba (R) ambaye ndiye aliyefanya utambulisho  wa familia ya Jully ambaye ndiye bwana harusi mtarajiwa.
Kisha ngoma juu ya ngoma.
PICHA NA GSENGO