Na Mwandishi Wetu.Mwanza
Bingwa wa fainali za mashindano ya mbio za makasia
Wanaume, chini ya udhamini wa Bia ya Balimi Extra Lager yajulikanayo kama
“Balimi Boat Race 2014” anatarajia kujinyakulia kitita cha pesa taslimu
Shilingi Milioni 2,700,000/=,Kikombe pamoja na medali za dhahabu kwa
wanakikundi hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya
Balimi Exra Lager, Edith Bebwa alisema fainali hizo zitaanza majira ya saa tatu
na asubuhi na kuendelea katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo jumla ya
vikundi 15 vya Wanaume kutoka katika mikoa mitano ya Kanda ya ziwa vitachuana
kumtafuta bingwa wa Kanda kwa mwaka 2014 na vikundi 11 upande wa Wanawake.
Edith alisema mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoshiriki ni
Kigoma,Kagera,Mwanza,Musoma na Kisiwa cha Ukerewe ambacho kinabeba hadhi ya
Mkoa.
Mshindi wa pili Wanaume atazawadiwa pesa taslimu Shilingi
2,300,000/=,mshindi wa tatu Shilingi 1,700,000/= na wa nne 900,000/=.Wakati
mshindi wa tano hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 400,000/=
kila kikundi alisema Edihi.
Upande wa wanawake bingwa wa mwaka 2014 ataibuka na
kitita cha pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,kikombe na medali za dhahabu kwa
wanakikundi wote.Mshindi wa tatu atazawadiwa Shilingi 1,700,000/=,wa tatu
Shilingi 900,000/= na wa nne 700,000/= wakati mshindi wa 5 hadi wa 10
watazawadiwa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi.
Nae Meneja wa Kampuni ya Bia nchini Kanda ya Ziwa, Malaki
Sitaki aliwaomba wakazi wa jiji la Mwanza na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi
katika ufukwa wa Mwaloni kushuhudia fainali hizo zenye mvuto wa pekee na mwisho
wafahamu nani atachukua ubingwa wa mbio hizo kwa mwaka 2014.
Meneja matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela
alisema vikundi vyote vimeshawasili jijini Mwanza tayari kwa mpambano wa
kumpata bingwa wa mwaka huu na maandalizi kwa ujumla yamesha kamilika hivyo nae
aliwaomba watu wajitokeze kushuhudia mbio hizo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.