ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 11, 2024

KIJANA MOLINGO AFARIKI DUNIA;HIKI NDICHO CHANZO CHA KIFO CHAKE

 Kijana Frank Patrick (Mchekeshaji wa Mtandaoni ) Maarufu Kama Molingo (17) Mkazi wa wilaya ya Chato , Mkoani Geita amefariki Dunia usiku wa Disemba 10 2024 akiwa nyumbani kwao Chato ambako alikuwa akiuuguzwa na Mama yake Mzazi.

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka kwa Rafiki ake ambaye alikuwa akiishi naye Mudi Msomali alisema Molingo alikuwa anaugua mara kwa mara na nyakati kadhaa alikuwa anavimba mwili na kuishiwa Damu. Lakini zaidi hii hapa simulizi kamili kupitia kipindi cha Mchakamchaka na Jembe FM.........

'RAIS SAMIA AZIOKOA NDOA ZETU' BAADHI YA WANAUME ARUSHA WAKIRI

📌Majiko ya Gesi ya Ruzuku yawafikia 

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya 50% katika halmashauri hiyo.

Wametoa pongezi hizo Desemba 10, 2024 wakati wa utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo.

Walisema mradi umefika wakati mzuri kwani kwa sasa upatikanaji wa mkaa ni mgumu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kwamba inasababisha kupanda kwa gharama za maisha.

"Tumefurahi kufikiwa na mradi, suala la kuni na mkaa hapa kwa sasa ni shida; tunatumia muda mrefu kuwasha moto maana kuni ni mbichi," alisema Neema Rumas mkazi wa kijiji cha Siwandeti.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Siwandeti, Daniel Mitiweki amesema ujio wa mradi huo ni mkombozi wa mazingira kwani suala la ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa lilikithiri katika kijiji hicho lakini kufuatia mradi huo miti inakwenda kusalimika.

Akizungumza wakati wa zoezi la usambazaji na uuzwaji wa majiko hayo ya ruzuku wilayani humo, Msimamizi wa Mradi wa REA Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro na Arusha), Mhandisi Gift Kombe aliwasisitiza wananchi kuzingatia elimu inayotolewa ya matumizi sahihi ya majiko hayo ili yaweze kuleta tija inayokusudiwa ikiwa na kuendelea kujaza mitungi hiyo pindi inapoisha.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.

"MSIJIKITE KWENYE TAARIFA ZA MATUKIO TU BALI PIA MJIKITE KWENYE HABARI NA MAKALA MBALIMBALI ZA KIMKAKATI" TCRA

Meneja wa Kanda ya Ziwa TCRA Mhandisi Imelda Salum akitoa Semina kwa wandishi wa habari wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) juu ya Mchango wa vyombo vya Habari katika kuzichangamkia fursa zilizopo kwenye uchumi wa kidigitali, semina hiyo ilifanyika saa chache kabla ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Jumatatu ya tarehe 10 Disemba 2024 katika ukumbi wa TMDA Buzuruga jijini Mwanza.
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza Ndg, Edwin Soko akitoa neno la shukurani baada ya Semina toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyotolewa na Meneja wa Kanda ya Ziwa TCRA Mhandisi Imelda Salum kwa wandishi wa habari ikihusu Mchango wa vyombo vya Habari katika kuzichangamkia fursa zilizopo kwenye uchumi wa kidigitali, semina ilifanyika saa chache kabla ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Jumatatu ya tarehe 10 Disemba 2024 katika ukumbi wa TMDA Buzuruga jijini Mwanza.
Sehemu ya wadau wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC)
Sehemu ya wadau wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC)
"Msijikite tu kwenye taarifa za matukio bali pia wekezeni kwenye habari na makala mbalimbali za mipango na miradi ya kimkakati" Ni kauli ya Meneja wa Kanda ya Ziwa TCRA Mhandisi Imelda Salum akitoa Semina kwa wandishi wa habari wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) juu ya Mchango wa vyombo vya habari katika kuzichangamkia fursa zilizopo kwenye uchumi wa kidigitali.

"Kila mtu anatamani kuwepo mtandaoni lakini Jeh! huko mtandaoni anapeleka nini?" amehoji Mhandisi Imelda na kuongeza "Fursa ni nyingi ila zisipodhibitiwa au kuwekewa mipaka na wataalamu kama ninyi zitatuliza au kugeuka sumu kwa kizazi kijacho kwakuwa hakuna tafiti zitakazo kuwa zimeiainisha kweli iliyo kweli" 

"Nataka m-move from UDAKU and UMBEA to FIKRA chanya za Maendeleo"

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza Ndg, Edwin Soko akitoa neno la shukurani baada ya Semina toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyotolewa na Meneja wa Kanda ya Ziwa TCRA Mhandisi Imelda Salum kwa wandishi wa habari ikihusu Mchango wa vyombo vya Habari katika kuzichangamkia fursa zilizopo kwenye uchumi wa kidigitali, semina ilifanyika saa chache kabla ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Jumatatu ya tarehe 10 Disemba 2024 katika ukumbi wa TMDA Buzuruga jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.

TRA TANGA YASHIRIKIANA NA UMIVITA KUTOA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WATU WENYE ULEMAVU

Na Oscar Assenga,TANGA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na (UMIVITA) wametoa elimu ya kodi kwa watu wenye ulemavu ili kuwaongezea uelewa.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya elimu ya mlipa kodi kwa watu wenye ulemavu yaliyotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Tanga,Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi Kitengo cha Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano Tanga,Flavian Byabato alisema wameona watoe elimu hiyo ili kuweza kuwapa uelewa jamii hiyo.

Alisema kwamba wanatoa elimu hiyo ikiwa ni muendelezo wa mamlaka hiyo kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari na kutoa elimu ya kodi kwa wadau ili waweze kupata uelewa wa mambo yanayohusiana na kodi katika kuendeleza nchi .

Aidha alisema kwamba maendeleo yanafika kutokana na kulipa kodi hivyo wakaona ni muhimu washirikiane na chama hicho katika kutoa elimu ya kodi kwa manufaa yao na Serikali kwa ujumla.

Hata hivyo alisema kwamba elimu waliyoitoa ni pamoja na usajili wa biashara, kulipa kodi stahiki sambamba na hayo wamewajulisha haki ambazo wanazo katika masuala mbalimbali ya kodi ikiwemo kupewa taarifa na elimu ya kodi.

"Tunashukuru kwamba wameitikia vema na tunategemea kuwa huu ni mwanzo wa hatua ya kukamilisha wajibu wao, tunategemea watakuwa walipaji waziri wa kodi na kuweza kueneza hii elimu ambayo wameipata" amesema.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Umoja wa Miradi kwa Viziwi Tanzania (UMIVITA) alishukuru kwa mafunzo hayo huku akieleza baadhi ya watu wenye ulemavu mkoani humo wameshindwa kurejesha mikopo ya asilimia mbili inayotolewa na Serikali kutokana na kukosa elimu juu ya ufanyaji wa biashara

Alisema hivyo mafunzo hayo wameyapata wakati muafaka na yatawaongezea maarifa ya kuwa na kuona umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari ili kuchochea ukuaji wa maendeleo nchini.

Amesema mikopo hiyo ni mzuri na inawasaidia sana katika kuendesha biashara zao na kujikwamua na umasikini, ambapo wengine wanafanikiwa kurejesha na baadhi kushinda huku wakiishia hata kuhama makazi yao.

Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba elimu waliyopata itawanufaisha kutokana na awali hawakuwa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayotokana na ulipaji wa kodi hivyo wamepata mwanga mpya.

Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la watu wenye ulemavu Mkoa wa Tanga (SHIVIAWATA) Subira Hoza amesema kabla ya kupata elimu hiyo watu wenye ualbino Mkoa walikuwa wanafahamu kuhusu elimu ya mlipa kodi kwa asilimia 30.

Monday, December 9, 2024

MAKONDA AFANYA KUSANYIKO KUBWA ARUSHA HALIJAPATA KUTOKEA

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, ameongoza wakazi wa mkoa huo kushiriki Matembezi na Maombi ya kuuombea mkoa na taifa kwa heshima ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo, Desemba 09, 2024.

Matembezi hayo yalianzia Mzunguko wa Impala kupitia Clock Tower, Barabara ya Sokoine (Uhuru Road) hadi Mnara wa Mwenge (Azimio la Arusha), ambapo maombi maalumu yamepangwa kufanyika. Kauli Mbiu: "Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara; Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu." #Miaka63YaUhuru #ArushaMatembezi #TanzaniaBara

NGORONGORO WATHIBITISHA KUACHANA NA KUNI INAWEZEKANA

📌Wajitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya gesi ya ruzuku

Wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha wameitikia wito wa kutumia Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya na kutunza mazingira.

Hayo yamedhihirika Desemba 8,2024 Wilayani Ngorongoro wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo.

Akizungumza wakati wa zoezi la usambazaji na uuzwaji wa majiko hayo ya ruzuku wilayani humo, Msimamizi wa Mradi wa REA Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro na Arusha), Mhandisi Gift Kombe aliwasisitiza wananchi kuzingatia elimu inayotolewa ya matumizi sahihi ya majiko hayo ili yaweze kuleta tija inayokusudiwa ikiwa na kuendelea kujaza mitungi hiyo pindi inapoisha.

Wananchi wilayani humo kwa nyakati tofauti walishukuru kwa kufikiwa na mradi na waliahidi kuwa mabalozi kwa wananchi wengine ambao hawakupata fursa ya kufika kupata huduma.

"Kwakweli hili ni jambo jema ila bahati mbaya si wananchi wote wameweza kufika hapa; tutaendelea kuhamasishana katika matumizi ya nishati safi ya kupikia," alisema Samwel Maganila mkazi wa Wasso Mashariki, Ngorongoro.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.

Sunday, December 8, 2024

YANGA YACHAPWA 2-0 TENA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

WENYEJI, MC Alger wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa Jumamosi Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria.

Mabao ya MC Alger yamefungwa na beki Ayoub Abdellaoui dakika ya 64 na mshambuliaji Soufiane Bayazid dakika ya 90'+5.

Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Yanga ambayo ilianza michuano hiyo vibaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Hilal nyumbani, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wakati MC Alger inapata ushindi wa kwanza kufuatia isare ya bila mabao ugenini na TP Mazembe Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mchezo mwingine wa Kundi A utafuatia Jumapili usiku, Al Hilal Omdurman watakuwa wenyeji wa TP Mazembe kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Cheikha Ould Boidiya Jijini Nouakchott, Mauritania.​