ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 8, 2020

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AWASILI ZIMAMOTO BAADA YA KUAPISHWA.



 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto) akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo Mbaraka Semwanza wakati alipotembelea Ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi La Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.
 Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza akiwasilisha taarifa ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, wakati alipotembelea Ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akikagua Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakati alipotembelea Ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo leo jijini Dodoma.
 Picha ni sehemu ya Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unavyoendelea katika Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

Friday, February 7, 2020

TCRA YATOA DARASA ZITO KWA WANAFUNZI CBE MWANZA ILI WASIJEINGIA MATATANI.


Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa tabia ya kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, kusambaza picha chafu au ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp na mitandao mingine kutoka kwenye simu ya mtu binafsi, vitendo ambavyo vinatajwa kufanywa zaidi na vijana ambao mara kadhaa wamekuwa wakijikuta wakiingia matatani hata kuharibu uelekeo na malengo yao ya baadaye na familia kwa ujumla. Kwa kuliona hiyo Wadau wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wameamua kuweka kambi katika Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mwanza na kutoa elimu kwa wanafunzi wa chuo hicho.







Yote hayo yamefanyika ikiwa ni matayarisho kuelekea maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni Duniani ambayo hufanyika kila Jumanne ya Pili ya Mwezi Februari, ambayo mwaka huu itakuwa tarehe 11 Feb, 2020, ikiwa na ujumbe mahususi PAMOJA KWA MTANDAO SALAMA' Kulingana na ujumbe huo Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA ikaona vyema kwenda kwa wadau wake kwaajili ya kuwaelimisha namna bora ya kutumia mtandao.

Thursday, February 6, 2020

IDARA YA AFYA MKOANI MWANZA YATANGAZA MKAKATI WA KUKABILIANA NA HOMA YA CORONA.



Wakati mlipuko wa kusambaa kwa virusi vya Corona ulioanzia kule nchini China na kusababisha vifo vya watu wengi ukizidi kuviumiza vichwa vya watu ulimwenguni, nayo Mamlaka ya anga nchini ikikutana na kujadili mbinu za kuzuia ugonjwa huo usije ukaingia nchini kwa kupatia usafiri wa anga, tayari Mkoa wa Mwanza umetangaza mkakati madhubuti wa kudhibiti ugonjwa huo maeneo yote ya vivuko, bandari pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Mwanza, kwa wageni wote wanaoingia kutoka nje ya nchi kuwafanyia vipimo ili kubaini kama wameathirika na homa ya mafua makali yanayo sababishwa na virusi hivyo. Samson Masalu ni Afisa Afya mkoa wa Mwanza anapata wasaa wa kuzungumzia mikakati ya mkoa kuhusu hilo katika kikao cha kujadili masuala ya lishe, afya ya uzazi hususani mama na mtoto pamoja na tahadhali ya magonjwa ya homa ya manjano, kilichofanyika ukumbi wa mikutano Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Kwa upande wake mratibu wa huduma ya mama na mtoto mkoa wa Mwanza CECILIA MREMA, amesema kwa mwaka jana mama wajawazito waliopoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi pamoja na kifafa cha mimba wakati wa kujifungua walifikia asilimia arobaini hivyo wameweka mkakati wa kumaliza tatizo hilo. Awali akifungua kikao hicho kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Dkt Emmanuel Kipole, amesema umasikini wa kipato, mkanganyiko wa wanasiasa na sera zisizo tambua umuhimu wa lishe ndiyo chanzo kikubwa cha jamii kuwa na lishe duni.

Wednesday, February 5, 2020

MWANZA YAIANZA SAFARI YA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAHAKAMA KWA MSASA WA WAKUU WILAYA NA WATENDAJI MKOA



Tanzania iko katika wiki ya Sheria ambayo imezinduliwa kitaifa mkoani Dodoma ambapo kilele chake kitakuwa Jijini Dodoma tarehe 9 February 2020. Katika kuiboresha wiki hiyo Ofisi ya Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Mwanza imekutana na viongozi wa kamati ya maadili ya mahakama ngazi za wilaya na mkoa ili kufanya uboreshaji wa kuwajengea uwezo zaidi na uelewa zaidi watendaji hao kujua majukumu yao. "Wanahabari hawakatazwi kuripoti mambo yanayojitokeza mahakamani lakini pale mahakama inapokuwa ikiendelea wanahabari hawaruhusiwi kupiga picha wala kurekodi mwenendo wa shauri kwani ni ikinyume cha sheria ....... Lakini upo mjadala unaoendelea wanahabari wakidai kuwa sheria hiyo inawanyima haki ya kupata habari, wakiwa na hoja kwamba mbona kwingineko wanafanya.... tuko kwenye mchakato...." ni sehemu ya kauli yake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Joachim Kiganga wakati akiwasilisha mada.

MWAKYEMBE AWAPA SIKU TATU BMT KUMPA MAJIBU.



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amelitaka Baraza la Michezo (BMT) kumpa majibu ya malalamiko ya maamuzi katika ligi mbalimbali nchini ndani ya siku tatu kuanzia kesho Februari 6, 2020.


Tuesday, February 4, 2020

DC KATAMBI: WAPINZANI WANASUMBULIWA NA HOFU YA KUSHINDWA VIBAYA UCHAGUZI MKUU UJAO.


Quran Tukufu na Biblia Takatifu zote zinatambua Mamlaka kuu mbili ya Kwanza ni moja tu na kuu kuliko zote ni ya Mwenyezi Mungu Ahera Peponi/Mbinguni na ya Pili ni Mamlaka za Kaisari /Duniani.

Kwa Wanafalsafa wenzangu tungeenda mbali zaidi katika Physical World and the World of Idea ila kwa tija ya uelewa na kufupisha hoja niongelee PW.

Montevideo Convention- laws of State 1933 inatambua nchi kuwa huru kujiamlia mambo yake "Sovereign". Sheria pia inaruhusu ushirika na mahusiano ya kitaifa, kikanda na kimataifa (Domestic,Municipal and International diplomatic and consular relations) Sheria zinatokana na jamii na jamii huzaa sheria "Ubi societus ibi ius..."

Mfumo wetu wa Kiongozi unazaliwa na STKMMB zitokanazo na Katiba yetu ya JMT' 1977  inatambua dini ila Serikali hafungamani na dini,Inatoa haki mfumo wa Vyama vingi, Demokrasia,Uhuru wa mawazo, Uhuru wa mihimili (Separation of power.

Mada ndefu pana na kinzani hutegemea mazingira ya nchi mfano Tanzania na nchi nyingi Afrika,Ulaya na Marekani hatuna 100% Institutional Separation, Functional Separation, Personnel Separation kama Montesque alivyokusudia na badae kina John Lock, Jean Jacque Rossoue nk).

Hivyo dhana kwamba  kila kitu lazima kiamliwe Bungeni au Mahakamani sio sahihi sana ni kukariri theory Mhe. Kaka yangu Zitto Kabwe than impe-fact's in issue n' practice inategemea ni jambo gani, mazingira (season and reason 'racio desdent')ulali wa necessity mfano kwa uchache economic intelligence and sabotage na viability to Public interest etc may surpass and prevail the later. Ref.

Upanuzii wa eneo la Ujenzi wa Ikulu ya Urusi, Viwanja vya ndege Ujerumani baada ya Vita ya kwanza, WED nk.

Plato mwanafunzi wa Socrates aliwahisema "Every human was born free but always bound in chains" Kwa dibaji hiyo fupi ni vema tukajua tunahaki za Binadamu Ibara ya 12-29 na password yake ni Ibara ya 30.

Sio sahihi kutafsiri haki za Binadamu bila kuisoma sambamba na Ibara inayotoa mipaka ya Uhuru, Haki na wajibu wako kabla ya kuzifurahia ni upotoshaji mkubwa. Bakuna Uhuru usio na mipaka Duniani wala Mbinguni.

Nichukizo sana kwa Mabepari na Vibaraka wao kuona hata bila wao Taifa letu tumeweza kushinda mengi; Vita dhidi ya Ujinga,Umasikini, Maradhi,Utegemezi, Rushwa, Ushoga,Maadili utumishi, Madawa ya kulevya, Uhujumu Uchumi nk. imepiganwa kwa ufanisi hodari 4yrs only tumeshuhudia Maendeleo makubwa kila sekta.
Mtasikia mengi, Wapingaji wanatafuta nongwa, Kiki na Agenda za Uchaguzi 2020 mchana kweupe tena kwa tochi.

Hofu ya kushindwa vibaya uchaguzi imetanda CHADEMA na ACT, ndio maana ya Vilio hivi vya Kitoto, Uzushi, Uchochezi Waraka na Barua; hata  kabla haijamfikia mlengwa na kuisoma,  inasomwa hadharani (Via Social Media)na kuanza kumtisha Mhe. Rais wetu na kutishia Watanzania kwa kauli nanukuu "Kutakuwa na machafuko, kabla,wakati na baada ya Uchaguzi".

"Tunawahakikishia hii Nchi haitakuwa salama"..."...Kunampasuko mkubwa" nk sioni Busara (Ne' Ubelima fides/NoUt-most good faith)ya kufunga mjadala kabla mlengwa hajaisoma na kuijibu Barua hiyo, zaidi inaonekana nia ovu na maandalizi ya kudai kwa nguvu hoja hizo dhaifu zisizo na ushahidi zijibiwe na Rais wetu alie-busy kutatua kero za Wananchi wake waliomchagua (It's an overt act and preparation to disruption of Public order, peace and tranquility).

Ni dhahiri Upinzani umekosa Agenda za kisiasa zinazoigusa jamii ya Watanzania ili iwaamini na kuwapigia kura kutokana na Siasa biashara,maslahi na za ki Yuda na Ukigeugeu, hawana Wagombea makini, wana poor Organization Vyama vipo mjini tu na hawana ofisi na anuani mpaka vijijini waliko wapiga kura wengi.

Hakuna maendeleo waliyowafanyia Wananchi kama alama (No tangible Legacy) hawana Rasilimali pesa wamekula ruzuku na misaada ovyo kwa maslahi binafsi na kiu ya madaraka, wanatumia mbinu ya kusaka huruma ya kisiasa(Appeal to Political Sympathy) kwa Wafadhiri na Wananchi kwa kuzusha visingizio bingo kabla ya kushindwa uchaguzi (pre-emption medhod), Uchaguzi mdogo waliususia bila kutafakari madhara(Un-presumed/un-calculated), leo wanaomba tena urudiwe? (Afterthought).

 Demokrasia kwao haipo ila Serikali ya CCM ilikubari kushindwa, wakatangazwa na Tume huru ya Uchaguzi(leo wanaiponda),  imewapa heshima zote za Kibunge na kutii haki,Kinga na madaraka yao, inawalipa ruzuku kila mwezi, imewapa kwa kutii sheria na demokrasia KUB, Unadhimu na front benches kwa vyama, Ukamishina, Ubunge uwakilishiEAC, PAP nk bado eti wanadai hakuna Demokrasia wala Tume huru ya Uchaguzi; Kama kweli why hawajiuzulu Ubunge kama walitangazwa na Tume isiyohuru na haramu?

Wameacha Uongozi na kuwa watunga sinema zakujiteka na kujizushia kukamatwa, hatujasahau walizusha uongo wa Trillion 1.5, Bombedier zinazonunuliwa Sio mpya ni used,  leo wao ndio abiria hahaaa ukistaajabu ya Mhe. Mbowe utayaona ya Mhe. Zitto Kabwe ni ngonjera za Hon. Lissu /Fatma 2017 na Mhe. Maalim Wagombea urais Watarajiwa Tz Bara na Visiwani 2020.

Wamepoteana hawaelewani wamevurugwa kama wajenzi wa Mnara wa Babeli kila mtu anapambana na Hali yake.
Kwa Uongozi wa CCM na Dr. JPM,  Uvccm walinzi wa Taifa,Chama na Viongozi Nchi iko salama tuko vizuri hatutetereki mbele ya Ulinzi wa Mungu, Sheria na Haki. Mhe. Rais JPM, VP Mama Samia, PM Majaliwa, MMK Mangula, KM Bashiru, Comred Kheri na Watanzania wote tusonge mbele Msiogope... Joshua 1:8-9.

"MRADI MUNGU ANATUMIKIWA NA ANAHESHIMIWA NA WATU WAKE, MANENO  YA MAADUI WA TAIFA YASIWAHANGAISHE WALA KUWATISHA" MT. Vicent wa Paulo.
 Mungu atazidi kuwaumbua na kuwaaibisha MAADUI wa Tanzania huru kila leo". Amina!

Wacha maneno chapa kazi kwa maendeleo ya Watanzania-Tukutane October '20 Wananchi wataongea.

Ni ushamba, Usaliti/ Judaism na Sio uungwana kuchafua Nchi yetu Ughaibuni kutafta Kick za kisiasa hata wao wanawaona wajinga, na tunajua mko 60% ya kupata Uraia wa Ujerumani na Ubelgiji kwa jina la ukimbizi wa Kisiasa, mnatafta Justification tu ili mkubaliwe kwa kuichokonoa na kuichafuaa Serikali mvuruge Amani ya Nchi yetu kwa kuwa mna pa kukimbilia.

Endeleeni kuchezea Amani yetumtauona mkono wake Bwana Mungu wetu alie mbinguni. Atatuokoa dhidi ya taama zenu ovu kwa Taifa!

HARMONIZE AIACHIA KICHUPA CHA - Hainistui (Official Video)


Goma jipya la mkali wa wakali nchini Tanzania, Harmonize linalokwenda kwa jina la Hainistui sasa limeshuka You Tube Bofya PLAY kusikiliza.

VIFO VYA CORONA VYAFIKIA 427



Corona Virus vimeua Watu 427 kufikia leo huku Watu 20,627 wakiathirika Duniani. Vifo viwili na waathirika 190 wametokea nje ya China.

Nje ya China, Mataifa 25 yamekumbwa na CoronaVirus huku Japan (20), Thailand (19) na Singapore (18) yakiwa na Waathirika zaidi.

Monday, February 3, 2020

HAFLA YA UAPISHO WA VIONGOZI WATEULE - IKULU DSM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 03 Febuari, 2020 anawaapisha viongozi wateule wafuatao A. MAKATIBU WAKUU 1. Bi. MARY GASPER MAKONDO - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mary Gasper Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Anachukua nafasi ya Bi. Doroth Mwanyika ambaye amestaafu. 2. Dkt. HASSAN ABBAS - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Anachukua nafasi ya Bi. Suzan Mlawi ambaye amestaafu. 3. Prof. RIZIKI SILAS SHEMDOE - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huo Prof. Riziki Silas Shemdoe alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Prof. Joseph Buchweishaija ambaye amestaafu. 4. Bi. ZENA AHMED SAID - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bi. Zena Ahmed Said alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga. Anachukua nafasi ya Dkt. Hamis Mwinyimvua ambaye amestaafu. 5.Bw. CHRISTOPHER KADIO - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Christopher Kadio alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Mej. Jen Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. B. NAIBU KATIBU MKUU 6. Bw. LEONARD MASANJA - kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bw. Leonard R. Masanja alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala. C. MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 7. Bi. JUDICA HAIKASE OMARI - kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga. 8. Bw. STEPHEN MASHAURI - kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. 9. Bw. EMMANUEL MPAWE TURUBA - kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Majeshi. D. WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA 10. Brig. Jen. SULEMAN MUNGIYA MZEE - kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee anachukua nafasi ya Phaustine Kasike ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. 11. Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) JOHN WILLIAM MASUNGA - kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. DCP John William Hasunga anachukua nafasi ya Thobias Andengenye ambaye uteuzi wake umetenguliwa. E. KAMISHNA WA ARDHI 12. Bw. NATHANIEL MATHEW NHONGE - kuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Nathaniel Mathew Nhonge alikuwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam na Pwani. F. MSAJILI WA MAHAKAMA 13. Bw. WILBERT CHUMA - kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama. 14. Bw. KELVIN MHINA - kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. 15. Bi. SHAMIRA SARWAT - kuwa Msajili wa Mahakama Kuu. G. MAKAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA 16. Mhe. Jaji Dkt. GERALD NDIKA - kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama 17. Wakili JULIUS KALOLO BUNDALA - kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa 18. Wakili GENOVEVA KATO - kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Tukio linalofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

Sunday, February 2, 2020

POLISI YATHIBITISHA VIFO VYA WATU 20 KWENYE IBADA MKOANI KILIMANJARO/ WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NAYE AZUNGUMZA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi George Simbachawene amesema Nabii na Mtume, Boniphace Mwamposa alikaidi taratibu za kibali kilichomtaka afanye huduma mpaka saa 12 jioni, huduma aliyoitoa hadi saa 2 usiku na kuwaamuru waumini wakanyage mafuta kabla ya maafa hayo kutokea.

Simbachawene ameyasema hayo Jijini Dodoma leo Jumapili Februari 2, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema baada ya Mwamposa kuona maafa hayo yametokea, alitoroka ili kukwepa polisi na kurudi jijini Dar es Salaam usiku huohuo.

"KWA KASI HII.. LIVERPOOL SHIKAMOO"


Goals from Oxlade-Chamberlain, Jordan Henderson and Mohamed Salah help the Reds go 22 points clear at the top of the Premier League.

TMDA WAPONGEZA USAJILI WA MADUKA YA DAWA MUHIMU ZA BINADAMU NJOMBE.


Na Amiri kilagalila-Njombe
Licha ya uwepo wa changamoto katika utoaji na utekekelezaji wa huduma za afya nchini,taarifa ya mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya nyanda za juu kusini inaonyesha utekelezaji mzuri katika usajili wa maduka ya dawa za binadamu mkoani Njombe huku moja pekee likibainika kuto kuwa na usajili.
Taarifa ya matokeo ya ukaguzi  wa mwezi wa 7 mpaka wa 12 mwaka 2019 iliyosomwa katika kikao cha kawaida cha TMDA na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Njombe katika ukumbi wa chuo cha afya Kibena, kwa lengo la kuwaongezea uzoefu,inaonesha maduka matatu huku moja likiwa ni la dawa za binadamu na mawili ni dawa za mifugo hayakuwa na usajili pamoja na vibali vya kuendesha biashara huku wamiliki wakiagizwa kuomba usajili wa vibali ndani ya siku 14.
Aidha Idadi ya majengo ya afya yaliyokaguliwa katika kipindi hicho,kanda ilikagua jumla ya majengo 128 ikiwa hospitali 12,vituo vya afya 13,zahanati 4,famasi 9,maduka ya dawa muhimu 70,maduka ya dawa za mifugo 19 na maabara 1.
Anitha Mshighati ni kaimu meneja wa TMDA  kanda ya nyanda za juu kusini,amasema wataendelea kukumbushana na kutoa elimu ili kuepusha ukiukwaji katika utoaji huduma.
“Tunataka kuhakikisha vile vitu ambavyo tumevisajili vinaendelea kuwepo sokoni na katika ubora ule ule maana sio kila wakati wakaguzi wanakuwepo wakati wa uhishaji wa bidhaa,kwa hiyo tunatakiwa kuhakikisha ubora tulioukubali unaendelea kuwepo katika nchi yetu”alisema Anitha Mshighati
Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Bumi Mwamasage amesema ukaguzi hufanyika kila robo ya mwaka katika maduka yote ya dawa mkoani Njombe licha ya kuwepo kwa changamoto za ukiukwaji wa sheria huku hatua za kisheria zikiendelea kuchukuliwa kwa wanaobainika.
Katalina Revocati ni katibu tawala wa mkoa wa Njombe,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho,ametoa rai kwa wakurugenzi wa halmashauri zote kuendelea kutekeleza majukumu ya udhibiti wa bidhaa za afya ili kulinda afya ya jamii.
“kumekuwa na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikijitokeza ambazo sisi sote tunatakiwa kuwa walinzi maswala haya ni kama vile halmashauri kuto kufanya kaguzi za mara kwa mara katika vituo vya kutolea huduma za afya na maduka ya dawa,kufuatilia dawa na vifaa tiba,hali hiyo inasababisha baadhi ya maduka na vituo vya afya kuendelea kuhifadhi dawa katika mazingira yasiyofaa hivyo kuhatarisha ubora wake”alisema Katalina Revocati
Baadhi ya washiriki katika kikao hicho wamekiri kupokea mafunzo na kwenda kuyatumia kikamilifu ili kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa jamii.
  Kaimu meneja wa TMDA kanda ya nyanda za juu kusini,Anitha Mshighati akiendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu/watendaji wa afya wa halmashauri za mkoa wa Njombe katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha afya Kibena mjini Njombe mkoani humo.
  Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa makini kusikiliza,wakati wa kikao cha afya kilichofanyika mjini Njombe.
 Katalina Revocat katibu tawala wa mkoa wa Njombe aliyekuwa mgeni rasmi akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha wataalamu wa afya na TMDA kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha afya kibena.
Kaimu meneja wa TMDA  kanda ya nyanda za juu kusini, Anitha Mshighati wakati alipokuwa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
 Dkt.Bumi Mwamasage mganga mkuu wa mkoa wa Njombe akizunguzmza na waandishi wa habari mara baada ya hotuba ya mgeni rasmi iliyotolewa kwa wataalamu wa afya na mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya nyanda za juu kusini.