ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 5, 2020

MWANZA YAIANZA SAFARI YA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAHAKAMA KWA MSASA WA WAKUU WILAYA NA WATENDAJI MKOATanzania iko katika wiki ya Sheria ambayo imezinduliwa kitaifa mkoani Dodoma ambapo kilele chake kitakuwa Jijini Dodoma tarehe 9 February 2020. Katika kuiboresha wiki hiyo Ofisi ya Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Mwanza imekutana na viongozi wa kamati ya maadili ya mahakama ngazi za wilaya na mkoa ili kufanya uboreshaji wa kuwajengea uwezo zaidi na uelewa zaidi watendaji hao kujua majukumu yao. "Wanahabari hawakatazwi kuripoti mambo yanayojitokeza mahakamani lakini pale mahakama inapokuwa ikiendelea wanahabari hawaruhusiwi kupiga picha wala kurekodi mwenendo wa shauri kwani ni ikinyume cha sheria ....... Lakini upo mjadala unaoendelea wanahabari wakidai kuwa sheria hiyo inawanyima haki ya kupata habari, wakiwa na hoja kwamba mbona kwingineko wanafanya.... tuko kwenye mchakato...." ni sehemu ya kauli yake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Joachim Kiganga wakati akiwasilisha mada.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.