ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 6, 2020

IDARA YA AFYA MKOANI MWANZA YATANGAZA MKAKATI WA KUKABILIANA NA HOMA YA CORONA.



Wakati mlipuko wa kusambaa kwa virusi vya Corona ulioanzia kule nchini China na kusababisha vifo vya watu wengi ukizidi kuviumiza vichwa vya watu ulimwenguni, nayo Mamlaka ya anga nchini ikikutana na kujadili mbinu za kuzuia ugonjwa huo usije ukaingia nchini kwa kupatia usafiri wa anga, tayari Mkoa wa Mwanza umetangaza mkakati madhubuti wa kudhibiti ugonjwa huo maeneo yote ya vivuko, bandari pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Mwanza, kwa wageni wote wanaoingia kutoka nje ya nchi kuwafanyia vipimo ili kubaini kama wameathirika na homa ya mafua makali yanayo sababishwa na virusi hivyo. Samson Masalu ni Afisa Afya mkoa wa Mwanza anapata wasaa wa kuzungumzia mikakati ya mkoa kuhusu hilo katika kikao cha kujadili masuala ya lishe, afya ya uzazi hususani mama na mtoto pamoja na tahadhali ya magonjwa ya homa ya manjano, kilichofanyika ukumbi wa mikutano Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Kwa upande wake mratibu wa huduma ya mama na mtoto mkoa wa Mwanza CECILIA MREMA, amesema kwa mwaka jana mama wajawazito waliopoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi pamoja na kifafa cha mimba wakati wa kujifungua walifikia asilimia arobaini hivyo wameweka mkakati wa kumaliza tatizo hilo. Awali akifungua kikao hicho kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Dkt Emmanuel Kipole, amesema umasikini wa kipato, mkanganyiko wa wanasiasa na sera zisizo tambua umuhimu wa lishe ndiyo chanzo kikubwa cha jamii kuwa na lishe duni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.