ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 7, 2020

TCRA YATOA DARASA ZITO KWA WANAFUNZI CBE MWANZA ILI WASIJEINGIA MATATANI.


Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa tabia ya kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, kusambaza picha chafu au ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp na mitandao mingine kutoka kwenye simu ya mtu binafsi, vitendo ambavyo vinatajwa kufanywa zaidi na vijana ambao mara kadhaa wamekuwa wakijikuta wakiingia matatani hata kuharibu uelekeo na malengo yao ya baadaye na familia kwa ujumla. Kwa kuliona hiyo Wadau wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wameamua kuweka kambi katika Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mwanza na kutoa elimu kwa wanafunzi wa chuo hicho.Yote hayo yamefanyika ikiwa ni matayarisho kuelekea maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni Duniani ambayo hufanyika kila Jumanne ya Pili ya Mwezi Februari, ambayo mwaka huu itakuwa tarehe 11 Feb, 2020, ikiwa na ujumbe mahususi PAMOJA KWA MTANDAO SALAMA' Kulingana na ujumbe huo Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA ikaona vyema kwenda kwa wadau wake kwaajili ya kuwaelimisha namna bora ya kutumia mtandao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.