ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 28, 2014

WAY BACK CONCERT KUFANYIKA LEO CCM KIRUMBA MWANZA.

Inspector Haroon aka Babu (L) akiwa na Soggy Doggy Hunter (R) jana usiku kwenye stage la Villa Park wakiwakaribisha wakazi wa jiji la Mwanza kwenye Tamasha la Burudani ya Bongo fleva za kale litakalofanyika leo Jumamosi ya tarehe  28 juni 2014 katika uwanja wa CCM Kirumba. 

'SIKILIZA MPANGO MZIMA'
Inspector Haroon aka Babu akiwa sambamba na Jay Moo, Juma Nature, Suma G, Soggy Doggy Hunter na Afande Sele wakiwa chini ya usimamizi wa Dj Choka wanategemea kufanya show leo kuanzia saa 11 jioni hii katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ambapo kiingilio ni shilingi 3,000/= Vinywaji, vyakula, kuwepo.
Utambulisho jana usiku.
yep...
We are in..

Friday, June 27, 2014

HAPPY BIRTHDAY YA CUTHBERT.

Birthday Boy Cuthbert Albert G. Sengo katika pozi
Wwwoooopp!! Leo ni mshumaa wa sita...
Kata keki tule...kata keki tule"
Kwasababu ni hivi majuzi tu kaka yake Cuthbert, namzungumzia Cedrick alikuwa naye ana sherehekea Birthday yake basi kuona hivyo mamayao aliwazawadia kwa pamoja game kwaajili ya burudani.
Yes!!
Cuthbert akimlisha keki kaka yake Cedrick.
Cedrick akilishwa keki na mama yake.
Cedrick akimlisha keki dada yake.
Cuthbert with his Daddy baada ya kumlisha keki.
Zawadi aliyozawadiwa from his mom.
ChiaZzZz!!!

KIDUMU AKIFANYA SOUND CHECK KWA SHOW YA LEO VUNJA JUNGU VILLA PARK.

Mhandisi wa Sauti (Sound Eng) wa Club Villa Park ya jijini Mwanza, Dj Chris akidadisi usikivu wa sauti ya muziki toka kwenye jukwaa la shughuli ya Vunja Jungu ndani ya Villa Park Mwanza jioni ya leo ambapo Kidumu na Bendi yake walikuwa wakifanya majaribio kabla ya kupanda jukwaani katika Mkali nani baina yao na Malaika Band ya Cristian Bella.  
Kidumu na wanamuziki wa kundi la Bodaboda Band wakiwa kwenye jukwaa kwa majaribio ya muziki jioni ya leo.
Mzigo utapigwa hapa usiku wa leo, je uko tayari kukosa?

MALAIKA BAND WAWASILI MWANZA TAYARI KUVUNJA JUNGU LEO DHIDI YA KIDUMU.

Mwanamuziki ambaye pia ni repa hatari wa kundi la Malaika band Totoo Ze bingwa akiwasili katika uwanja wa Airport Mwanza kwaajili ya kujumuika na wenzake kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza hii leo katika Usiku wa Vunja Jungu Villa Park ambapo kundi hilo litapambanishwa na Bodaboda Band ya mwanamuziki Kidumu.
 Msikilize Cristian Bella.


Akisalimiana na Meneja wa Villa Park Mwanza ambaye ni mwenyeji wao pichani kulia ni Mwanamuziki mpiga kinanda wa kundi la Malaika band Andrew Sekedia akiwasili katika uwanja wa Airport Mwanza kwaajili ya kujumuika na wenzake kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza hii leo katika Usiku wa Vunja Jungu Villa Park.
Andrew Sekedia (L) akiwa na mtangazaji wa Star Tv Abdalah Tilata katika uwanja wa Airport Mwanza alipowasili leo asubuhi akiwa yeye na wanamuziki wengine wote wa Malaika Band.
Hawa hapa Malaika Band wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Villa Park Mr. Ramma.
Totoo Ze Bingwa (L) akiwa na mpiga bass wa Malaika Band uwanja wa ndege wa Mwanza walipowasili leo asubuhi.
The angle.

Thursday, June 26, 2014

LUIS SUAREZ AFUNGIWA NA FIFA.

Luis Suarez akiwa ameshika meno yake huku mlinzi wa ngome ya Italy Giorgio Chiellini akionyesha madhara aliyopata kwenye bega kwa kung'atwa na mchezaji huyo wa Uruguay.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ta mlinzi wa timu ya Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.
Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.
Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.
Kutokana na adhabu hiyo iliyochukuliwa na kamati ya nidhamu ya Fifa Suarez sasa hatashiriki kwenye mechi ya raundi ya pili kati ya Uruguay na Columbia Juni tarehe 28.
Adhabu hiyo pia inamaanisha Suarez hatashiriki kwenye mechi za Uruguay zijazo za kombe la dunia endapo timu itazidi kusonga mbele na zile zijazo za kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia.
Kamati hiyo ya nidhamu ya Fifa imesema Suarez hatakiwi kuingia kwenye uwanja wowote Uruguay inapocheza wakati wa adhabu hiyo ya kutocheza mechi tisa za kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio Sulser amesema:"Hatuwezi kuruhusu tabia duni kama hii uwanjani hasa wakati wa kombe la dunia kwani mamillioni ya mashabiki kote duniani wanafuatilia mashindano haya. Kamati ya Fifa imetilia maanani kila kitu kwenye kitendo hicho kabla ya uamuzi huo.Tayari tumemjulisha mchezaji huyo na shirikisho la kandanda la Uruguay.''
Mashabiki wengi duniani wamemshutumu vikali Suarez kwa kumng'ata mchezaji huyo wa Italia kwani hii ni mara ya tatu anapatikana na hatia hiyo.
Lakini mashabiki, waandishi wa habari wa Uruguay na shirikisho la kandanda nchini humo wamemtetea mchezaji wao,wakisema hizo ni njama za kumuangamiza Suarez ambaye huichezea Liverpool ya England. CHANZO BBC SWAHILI.

'INAVYOKUWAGA' WIKIENDI YETU NDANI YA JEMBE BEACH MWANZA.

Brothers with 'Jembe'....Hatari
"Mpaka watu wanatambaa" Samm Love....
Mzuka...!!
Mizuka ya Doctor na Karaokee Show.
Ushindwe mwenyewe...!!!
Wakiimba ni marafiki toka mbali...
Hawa hapaa...
Sisters ....
Makanda.
Nightmare dizaini.
Dance.
pop corn.

UZINDUZI WA FILAMU YA 'I LOVE MWANZA' HAUKUWA WA KISIASA - BONGO MOVIE

Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya kukanusha uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) na kulia kwake n Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa tarifa ya kukanusha taarifa za uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kuanzia kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) , Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu na kulia kwa Nyerere ni Rais wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura, Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kuanzia kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) , Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu na kulia kwa Nyerere ni Rais wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura, Wastara Juma na Salama "Sandra" Salimin.
Rais wa Bongo Movie Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura (katikati) akizugumza katika mkutanona waandishi wa habari kukanusha taarifa ya uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. 
 Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu akiteta jambo na Wastara Juma mara baada ya mkutano huo.
Wastara Juma akihojiwa na Timzoo Karugira wa Azam TV. Picha na Cathbert Angelo wa Kajunason Blog.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WASANII tasnia ya filamu Tanzania ambao wanaunda umoja unaofahamikakama Bongo Movie wameomba kutohusishwa na masuala ya kisiasa katika shughuli zao.

Hayo yalisemwa na Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere kutokana na hsia za kuhusishwa kwao katika mambo ya siasa mara baada ya kushiriki katika uzinduzi wa filamu ya “I love Mwanza” ambayo ilizinduliwa na wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Waziri wa Utalii, Lazaro Nyalandu.
Steve alisema kuwa wao kama wakuu wa tasnia ya Filamu nchini, hawana mamlaka ya kumtenga mtukatika shughuli zao zaidi ya kumshirikisha mtu yoyote awe mkulima, mfanyabiashara, mwanasiasi bila kujali wa chama gani.

“Membe na Nyalandu wameshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, wewe subiri uzinduzi mwingine kama utapata nafasi ya kualikwa, lengo letu kubwa ni kuenea sanaa ambayo imezoeleka zaidi mkoani Dar es Salaam, ni mafanikio kwetu,” alisema Steve.

Alisema kuwa kitendo cha kuinadi filamu hiyo mbele ya halaiki ya watu kwenye siku ya uzinduzi wake kilikuwa ni cha kawaida tu kwa sababu hata katika katika nyumba za ibada mambo haya hufanyika, tulifanya wazi bila kificho kwa sababu halikua jambo la haramu ukizingatia ni jambo lililokuwa lina lengo la kusaidia maendeleo y asana nchini katika kukuza kipato cha wasanii wa nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Wasanii wa Filam Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura alisema kuwa Membe hakuwa na shughuli nyingine tofauti na zaidi ya uzinduzi wa filamu.

“Ukweli ni huu katika uzinduzi wa filamu ya Ilove Mwanza ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Bernad Membe ndiyo alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Membe ametokea kuisapoti Bongo Movie siyo dhambi hivyo viongozi wengine wajitokeze kusapoti wasanii kama jinsi alivyo Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, alisema Anitha.

“Tume sikitishwa sana na kusingiziwa mambo ya uongo ambayo hayana ukweli ndani yake na kuhusishwa na masuala ya kisiasa,” alifafanua.

FARIDA FOUNDATION YATOA MISAADA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA NA KWA WALEMAVU ENEO LA UBUNGO DARAJANI.

Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi moja ya msaada kwa kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle,Huku wafanyakazi wengine wa Hospitali hiyo wakishuhudia.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle akipoke Ndoo zitakazotumika kwa ajili ya kuhifadhia uchafu katika Hospitali hiyo,ambazo zilitolewa kama Msaada na Farida Foundation
Bi Farida Abdul akimuonyesha kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle Vifaa ambavyo vimeletwa kama msaada kwenye Hospitali hiyo.Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti vya magurudumu vitatu ambavyo vitasaidia kubebea wagonjwa,Bandeji za kufungia vidonda,Ndoo za kuwekea taka,na vinginevyo.
Hivi ni viti Vitatu vya kubebea wagonjwa ambavyo vilitolewa kama msaada kwenye Hospitali ya Palestina(sinza) na Farida Foundation.
 Mkurugenzi wa Farida Foundation Bi Farida Abdul akiongea na vyombo vya habari na kuelezea ni kwanini ameamua kutoa misaada hiyo katika hospitali ya Palestina,Amesema kwamba Serikali peke yake haiwezi kufika kwa kila mgonjwa na hospitali kwa wakati,kwa hiyo inatakiwa kujitoa kwa mashirika kusaidiana na Serikali ili Hospitalietu Ziweze kuwa na Huduma bora.
Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle ameishukuru Taasisi ya Farida Foundation kwa misaada waliyotoa kwani itawasaidia sana kuboresha Huduma zao.
BAADA YA KUTOKA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA FARIDA FOUNDATION WALIELEKEA UBUNGO DARAJANI KWA AJILI YA KUTOA MSAADA KWA MLEMAVU WA MIGUU,AMBAPO WALIMPATIA BAISKELI NA MTAJI WA VITU VYA BIASHARA
Mkurugenzi wa Farida Foundation Bi Faridah Abdul akiongea na mlemavu wa miguu ndugu Marcerine Mayemba eneo la ubungo darajani kabla ya kumkabidhi msaada wa mtaji wa biashara pamoja na baiskeli atakayokuwa anaitumia.
Bi Farida Abdul Akiwa na baiskeli ambayo aliikabidhi kwa mlemavu wa miguu bwana Marceline Mayemba,kwa ajili ya kumsaidia katika matumizi yake ya kila siku.
Mlemavu wa Miguu Bwana Marceline Mayemba Akipanda kwenye Baiskeli yake aliyokabidhhiwa na Farida Foundation
 Mlemavu wa Miguu Bwana Marceline Mayemba Akiendesha Baiskeli yake mara tu baada ya kukabidhiwa na Farida Foundation.
Bi Farida Abdul Akimkabidhi Mlemavu wa miguu bwana Marceline Mayemba Katoni ya Bidhaa ambazo ataanza nazo kama mtaji wa bishara,pia alikabidhiwa katoni tatu za maji,Katoni tatu za Juice na Katoni zingine Vifaa kama pipi,bigijii ili viwe kama kianzio kwa biashara yake.
Bi Farida Abdul Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi Mlemavu mwingine Chakula Pamoja na vinywaji.