Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu akiteta jambo na Wastara Juma mara baada ya mkutano huo. |
Wastara Juma akihojiwa na Timzoo Karugira wa Azam TV. Picha na Cathbert Angelo wa Kajunason Blog. |
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WASANII tasnia ya filamu Tanzania ambao wanaunda umoja unaofahamikakama Bongo Movie wameomba kutohusishwa na masuala ya kisiasa katika shughuli zao.
Hayo yalisemwa na Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere kutokana na hsia za kuhusishwa kwao katika mambo ya siasa mara baada ya kushiriki katika uzinduzi wa filamu ya “I love Mwanza” ambayo ilizinduliwa na wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Waziri wa Utalii, Lazaro Nyalandu.
Steve alisema kuwa wao kama wakuu wa tasnia ya Filamu nchini, hawana mamlaka ya kumtenga mtukatika shughuli zao zaidi ya kumshirikisha mtu yoyote awe mkulima, mfanyabiashara, mwanasiasi bila kujali wa chama gani.
“Membe na Nyalandu wameshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, wewe subiri uzinduzi mwingine kama utapata nafasi ya kualikwa, lengo letu kubwa ni kuenea sanaa ambayo imezoeleka zaidi mkoani Dar es Salaam, ni mafanikio kwetu,” alisema Steve.
Alisema kuwa kitendo cha kuinadi filamu hiyo mbele ya halaiki ya watu kwenye siku ya uzinduzi wake kilikuwa ni cha kawaida tu kwa sababu hata katika katika nyumba za ibada mambo haya hufanyika, tulifanya wazi bila kificho kwa sababu halikua jambo la haramu ukizingatia ni jambo lililokuwa lina lengo la kusaidia maendeleo y asana nchini katika kukuza kipato cha wasanii wa nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Wasanii wa Filam Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura alisema kuwa Membe hakuwa na shughuli nyingine tofauti na zaidi ya uzinduzi wa filamu.
“Ukweli ni huu katika uzinduzi wa filamu ya Ilove Mwanza ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Bernad Membe ndiyo alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Membe ametokea kuisapoti Bongo Movie siyo dhambi hivyo viongozi wengine wajitokeze kusapoti wasanii kama jinsi alivyo Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, alisema Anitha.
“Tume sikitishwa sana na kusingiziwa mambo ya uongo ambayo hayana ukweli ndani yake na kuhusishwa na masuala ya kisiasa,” alifafanua.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.