ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 8, 2011

YANGA USO KWA USO NA WATANI ZAO SIMBA KATIKA FAINALI KAGAME CASTLE CUP 2011

Baada ya Simba ya Dar es Salaam, kufanikiwa kufika katika hatua ya fainali ya Kombe la Kagame kwenye michuano hiyo inayoendelea jijini Dar, baada ya kuwaondosha El-Mereikh ya Sudan jana kwa mikwaju ya penati kufuatia kumalizika kwa dakika 90 huku timu hizo zikiwa sare ya 1-1. Leo tena ndani ya muda kama wa jana hatua za mikwaju ya penati hatimaye mtani wake wa Jadi Yanga ambaye alikutana na timu ya St. George ya Ethiopia wamefanikiwa nao kutinga fainali kwa style hiyohiyo katika mchezo wao wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa kushinda penati 5-4. Ndani ya dakika 120 timu hizo zilitoka 0-0.

Fainali inayokutanisha watani hao itakuwa siku ya Jumapili ya tarehe 10july, ambapo kabla mchezo kati ya St. George v/s El-Mereikh utapigwa kumtafuta mshindi wa tatu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mh. Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro.

VIONGOZI MWANZA CHANZO CHA VURUGU

Vurugu za wamachinga na mgambo zilizotokea juzi jijini hapa, zimedaiwa kusababishwa na mvutano baina ya ofisi ya Meya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.Zima moto shughulini.
Madai hayo yalitolewa jana na Meya wa Jiji, Josephat Manyerere (Chadema), wakati akizungumza wa waandishi wa habari ambapo alidai kwamba ofisi yake haikupewa taarifa ya operesheni ya kuondoa wamachinga katika maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara katika mtaa wa Makoroboi.

Alipofuatilia, alibaini kuwa hata ofisi ya Mbunge wa Nyamagana, haikuwa na taarifa ya operesheni hiyo, ambayo imesababisha watu saba kujeruhiwa na kwamba habari zilizoenezwa kuwa Chadema walihusika na vurugu hizo kwa sababu halmashauri
inayoongozwa na chama hicho ni ya uchochezi.


Amesema kwa kuwa operesheni hiyo ni batili, amewataka wamachinga waendelee kufanya biashara katika maeneo ya Makoroboi, hadi suala lao litakapopelekwa kwenye Baraza la Madiwani, ili kutafutiwa utaratibu na maeneo yasiyo na bughudha. Mvutano huo wa kiuhusiano, umesababisha ofisi ya Mkurugenzi kutotoa ushirikiano kwa ofisi ya Meya na kutolea mfano wa uuzwaji wa viwanja katika eneo la Kiseke bila ofisi yake kujulishwa.

Aidha, ametoa wito kwa wamachinga kujitahidi kupanga bidhaa zao vizuri, ili watu wapate njia ya kupita na pia wasitumie vipaza sauti kutangaza bidhaa zao na kuhakikisha maeneo ya biashara yanabaki safi na wafanye biashara hizo kuanzia saa 10 jioni.

Amewaomba wenye misikiti na shule katika mtaa wa Makoroboi waendelee kuwavumilia hadi ufumbuzi wa kudumu utakapopatikana kutokana na kwamba kulegalega kwa uhusiano wa kikazi kumesababisha vurugu zilizotokea juzi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alisema watu 49 kati ya 131 waliokamatwa juzi kwenye vurugu watafikishwa mahakamani leo baada ya uchunguzi kukamilika.

Jamani vita haina macho, binti huyu alishambuliwa akiwa anakwenda Sokoni alikotumwa na Mama yake.
Sirro amesema hali jijini hapa ni shwari na majeruhi watatu wameonekana kuwa na majeraha ya risasi za Shot gun na uchunguzi unafanywa kubaini walipigwa na nani kama ni mgambo au kwenye maduka waliyovamia.

Magari yaliyochomwa moto.
Wenje amesema kuwa yuko tayari kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) The Hague, Uholanzi katika suala la kutetea haki za wamachinga kufanya biashara katikati ya Jiji.

Hata hivyo, Mbunge huyo amemwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda Tume ya kuchunguza chanzo cha mgambo kupiga watu risasi kutokana na majeruhi wengi wa vurugu hizo kuwa na majeraha ya risasi za bunduki ambazo hazimilikiwi na Polisi.

TIGO YAZINDUA KAMPENI YA 'TIGO TUCHANGE' KUSAIDIA ELIMU TANZANIA


Meneja Habari Elimu na Mawasiliano, Sylivia Lupembe Gumza akiwapongeza Tigo kwa huduma yao ya "Tigo Tuchange" ambayo ni kwaajili ya kusaidia elimu kwa watoto Tanzania ambayo itafanyika 9 Julai 2011. Meneja Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando (kulia) amesema zoezi hili litaanza saa 9:00 asubuhi mpaka 10:00 asubuhi ambapo kama utanunua vocha zaidi ya 500/-ndani ya saa moja utapata mara mbili ya kile kiwango umeweka na hapo utakuwa umechangia elimu Tanzania. Pesa itakusanywa kununua vitabu vya wanafunzi wa shule ya msingi.

Wednesday, July 6, 2011

THE BEAT FESTIVAL

FRI 8TH JULY - 20.00 - 00.00

Venue: Triniti - Msasani rd. 26, Oysterbay, Dar es Salaam, Tanzania.

VURUGU ZA MACHINGA ZASABABISHA MAUAJI MWANZA RISASI ZARINDIMA WATANZANIA WENYE ASILI YA ASIA WAPATA MISUKOSUKO

Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.Kamanda Sirro akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani.

Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.

Friji ikiteketea..
Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market nakisha kuchoma friji ilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuiteketeza.

Kusanyiko la shaka-shaka.

Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza haliiliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa..

Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.

Kona ya kuingia barabara ya Msikiti wa Ijumaa kutokea barabara ya Nyerere risasi zimelia nao wananchi wakikimbia kujihami na mabomu ya machozi.

Market Street hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji.

Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.

Machinga na jiwe lake mkononi tayari kulirusha..Hali imekuwa tete kwa watanzania wenye asili ya kiasia kwani imekuwa wakionekana tu wanafanyiwa kitu mbaya.

Kuvunjwa vioo kwa jengo hili la msikiti wa hindu ni moja kati ya hasara zilizojitokeza.

Mpaka sasa hivi ikiwa ni saa 6:15 barabara ya Nyerere haijatulia kwani kuna umati mkubwa wa watu eneo hili mawe yakirushwa nayo mabomu ya machozi yakisikika mitaa ya Makoroboi, Alhamini, Maketi na Msikiti wa Ijumaa kuwatawanya waandamanaji.

Tuesday, July 5, 2011

ASANTE MUNGU KWA KUMNUSURU MWANANGU OBAMA ALIYEMEZA SARAFU YA SH 50

X-ray ya pili.
Ilikuwa ni asubuhi ya Jumatatu ya tarehe 27juni2011 nikiwa na plani za kuamka saa 3 mara baada ya uchovu wa pilika pilika za siku iliyopita yaani Fiesta Mwanza stimu za usingizi zilikatika ghafla mara baada ya mke wangu kunipa taarifa kuwa my second kid Cuthbert aka Obama(3) kameza sarafu ya shilingi 50.

Huduma ya kwanza ilikuwa nikumuuliza yu hali gani na anajisikiaje:
Jibu: "nimemeza hela kama wali"
Swali: iko wapi?
Jibu: "nimetupa humu.." akielekeza kidole mdomoni
Swali: sasaaa.. huumiii?
Jibu: "mmh-mmh" akimaanisha kukataa

Ndipo pilika zikaanza kutafuta daktari ambaye alishauri kumpeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi. Tulipita hospitali kadhaa bila mafanikio nyingi zikiwa hazitoi huduma ya X-ray kutokana na tatizo la mgao wa umeme linaloendelea nchini.

Huku na huko hatimaye tuakapata huduma ya X-ray katika hospitali binafsi inayoitwa 'Mwananchi' iliyoko wilaya ya Nyamagana mitaa ya Makoroboi nayo ikaonyesha sehemu sarafu hiyo ilipofika, madaktari wakasema kuwa ipo katika eneo lisilo la mashaka sana (kwenye utumbo kifuani) hivyo tumrudishe siku ya pili kama hatakuwa ameitoa kwa njia ya haja kubwa.

Siku ya pili X-ray ikafanyika na kuonyesha kama inavyoonekana pichani juu. Nao madaktari wakasema kuwa ipo kwenye utumbo imeshuka kidogo chini ya mbavu hivyo akatupa siku mbili kurejea kama haitakuwa imetoka. Kweli baada ya siku mbili .... Ikatoka.

Ashukuriwe Mola muumba wa mbingu na nchi.

TBL YAZINDUA KAMPENI YA JIVUNIE UTANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania,Robin Goetzche akizungumza leo katika uzinduzi wa Kampeni ya Jivunie Utanzania inayoendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager ikiwa ni harakati ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Kampeni hii imezinduliwa leo hii katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,katikati ya Jiji la Dar na kuhudhuriwa na wageni mbali mbali.

Suleiman Nyambui akiwaeleza jambo waandishi wa habari.

Wakongwe wa Muziki wa dansi nchini pia walikuwa ni sehemu ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.

Wachezaji wa zamani wa timu za mpira wa miguu wa timu za Yanga na Simba pia walikuwepo.toka kushoto ni Salvatory Edward,Kenneth Mkapa,Mohamed Mwameja na Edbil Jonath Lunyamila.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwa katika mazungumzo na Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Ali Mwaimu.

SIMBA YAIBENJUA BUNAMWAYA 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KAGAME CASTLE CUP

Kiungo wa katikati wa timu ya Simba Mohamed Banka akiachia shuti kali kuelekea langoni mwa timu ya Bunamwaya huku Ronard Seku akijaribu kuuzuia mpira huo bila mafanikio. Hadi mwisho Simba 2, Bunamwaya 1. Kwaushindi huo Simba imesonga mbele hatua ya nusu fainali.

Mashabiki wa timu ya Simba wakiwatukana waamuzi wa mchezo huo wakati timu zikienda mapumziko wakilalamikia uchezeshaji kwa madai kuwa ni wa upendeleo.

Picha kwa hisani ya Michuzi.

Monday, July 4, 2011

BINTI MAARUFU WA KIJAPANI ASTUSHA WATU KWA KUJITANGAZA KUWA YEYE NI MVULANA!!!

Mwanamitindo, mtangazaji wa michezo ya kubahatisha na binti anayejipenda sana Bi.Kayo Sato (a.k.a Kayo Police)amewaacha watu vinywa wazi pale aliposema kuwa ana siri kubwa sana moyoni mwake inayohusu jinsia yake.

Kufuatia maneno ya chini chini ya muda mrefu, binti huyo ambaye sasa ana miaka 23 alikwenda kwenye kituo kimoja cha Televisheni na kusema kuwa kwa hakika yeye ni mwanaume na si mwanamke ...ila anapenda kuwa katika muonekano wa kike. Kayo ni maarufu sana nchini Japani kwa kusimamia maonyesho yanayojulikana kama 'The Nico video game show.

Bi. Kayo anasema kuwa aliondoka kwenye mji wa kwao kipindi kidogo, na sio rahisi kwa watu waliokuwa wakimjua awali kujua kuwa ni mwanaume na akaanza kuishi kama mwanamke kwa kutumia majina mengine.

Alijiunga na shirika la wanamitindo na kujizolea umaarufu mkubwa kama mdada modeli wa kutumainiwa na katika kwa kipindi chote cha miaka kadhaa hakuna mtu katika shirika lake aliyewahi kumgutukia.

Anasema wala hajafanyiwa upasuaji wa ngozi na kuwekewa vipande bandia, yeye ana uzuri wa asili na amepata mafanikio makubwa katika kazi yake kwa kutumia vipodozi tu. Bi. Kayo aliandika katika blogi moja nchini Japani kuwa , "Kwa yeyote aliyepokea ujumbe wangu, asante sana kwa maoni yenu, nimetiwa moyo sana na maoni yenu, na kaa nilivyosema kwenye maonyesho yale mie nilizaliwa mvulana,niliona litakuwa jambo jema kumwambia kila mtu juu ya yale yanayonihusu , yaliyopita. Nimefarijika kwa kunipa fursa hii na , nitafanya kazi kama Kayo Sato na kuendelea mbele, na nina furaha sana kuwa watu wengi wamenikubali na kukubali mwanzo wangu huu mpya".

Tangu wakati alipoweka wazi jinsia yake kwenye blogi amekuwa akipokea ujumbe wa kumtia moyo kutoka kwa watu wengi.

Source; webs za kijapani..

SERENGETI FIESTA SHINYANGA ILIVYOKUWA..

Pamoja na kuwa imekuwa chance yake ya kwanza kanda ya ziwa mchizan amekubalika kwa kushuka kiudiferenti zaidi, densi kali, mashairi taiti...yani nowma!.

Huyu ndiye yule Mc ambaye pia ni Prizenta...Eyo Mchomvu! akitupia pale kati kitu cha baba Jonii

Vipaji toka Shy Town pia vilipata nafasi kulikwea jukwaa.

Zamu ya Sajna sasa kulibeng'isha.

Mwasiti...

Wadau wa Shy Town na raha zao.

Mh. Temba akiimbisha..

Hawa jamaa kila walichokuwa wakigusa kiligeuka dhahabu kwa kupata shangwe za kutosha..

Aisee fundi, niongezee tafadhali!

Ndani ya mmimino kitu cha Serengeti....

Mahudhurio.

Moja kati ya watangazaji wa Jahazi Wasiwasi Mwabulambo (wa3 kutoka shoto) akiwa na wadau wa JAHAZI Shy Town.

Engo

Mtangazaji wa Faraja Fm Shinyanga Emmanuel S. Msigwa (shoto) na mshkaji wake.

Peace!! Wasiwasi huyoooo akisepa!

Shughuli iliisha kwa mbinde.. Huku wakiimba 'NGOSHAaaaa!! NGOSHAaaa!!' wakazi wa Shinyanga walikataa kata kata kuondoka eneo la tukio mara baada ya muda kuisha wakilazimisha 'Ngosha The Don' aendelee kutema madini kwenye stage, ilibidi polisi waingilie kati kumwondosha eneo la tukio.