Baada ya Simba ya Dar es Salaam, kufanikiwa kufika katika hatua ya fainali ya Kombe la Kagame kwenye michuano hiyo inayoendelea jijini Dar, baada ya kuwaondosha El-Mereikh ya Sudan jana kwa mikwaju ya penati kufuatia kumalizika kwa dakika 90 huku timu hizo zikiwa sare ya 1-1. Leo tena ndani ya muda kama wa jana hatua za mikwaju ya penati hatimaye mtani wake wa Jadi Yanga ambaye alikutana na timu ya St. George ya Ethiopia wamefanikiwa nao kutinga fainali kwa style hiyohiyo katika mchezo wao wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa kushinda penati 5-4. Ndani ya dakika 120 timu hizo zilitoka 0-0.
Fainali inayokutanisha watani hao itakuwa siku ya Jumapili ya tarehe 10july, ambapo kabla mchezo kati ya St. George v/s El-Mereikh utapigwa kumtafuta mshindi wa tatu.
Chukua Mkwanja Wako Mapema Leo
-
HATIMAYE baada ya jana kushuhudia mechi kibao zikipigwa na matokeo mengine
yakiwa yakustaajibisha, leo hii ni zamu tena ya wababe wengine kibao
uwanja...
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.