...

...

Saturday, April 19, 2014

KARIBU CLUB JEMBE NI ZAIDI YA UTALII MWANZA

Samaki fresh toka ziwa Victoria wakuchoma, wakubanika, wakukaanga, na vyakula vya kila aina lipate jibu ndani  ya kiota kipya cha kitalii cha gharama nafuu mpaka ushangae Jembe ni Jembe aka Skylight Beach Resort Malimbe Mwanza.
Ni muda wa kupiga picha na samaki.
"This is Jembe Club" says Peter Fabian.
Crew ya vijana wa mjini ikiongozwa na mkurugenzi wa Lakairo Investment Co.Ltd Danny Lameck (kulia) ishatia timu hapa.
G akipata bupepo.....
'Represent'
Bustanini....na kaunta yenye full service.
Kama una karanga njoo kuna jiwe la kale la kusagia.
You see?
Jembe ni Jembe. 
On the top.
Vimiminwa vya kila aina.
Nyakati za usiku huu ndiyo muonekano.
Kama ni kuwochi football au matukio mbalimbali basi kaunta kuna bo-bo-booooonge la skrini!!!!!
Kwa mbaaali utaona......
Engo nyingine adimu....
Wenye boti zao kuna shortcut kutoka Malimbe Nyegezi hadi Mwanza town ni mwendo wa dakika 15 tu amini usiamini.
Kwa heriiiii....
Waleeeeeeee!!!!!
Matukio mawili makubwa kufanyika:-
JUMAMOSI :- Tarehe 19 April 2014 Fool Moon Party wasanii Joh Makini, Nikki wa Pili, G. Nako wanaounda kundi la Weusi kukisanukisha na yule mkali mwingine anayetamba na ngoma inayoitwa Kerewa namzugumzia Sheta, kiingilio ni shilingi 10,000/= tu!!

JUMAPILI :-Tarehe 20 April 2014 Easter Bonanza tutakuwa na Skylight Band, mchana watoto sh 3,000/=  wakubwa sh 10,000/= kisha badae usiku tena tukiwa na Skylight Band Part la Nguvu tu kiingilio sh 10,000/=.
nANI aTABaki hOmU?   

Friday, April 18, 2014

ULINZI WAIMARISHWA SIKUKUU YA PASAKA MWANZA.

KAMANDA wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jijini hapa (hawapo pichani), kuelezea jinsi jeshi lake lilivyo jipanga kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linazingatiwa na kuimarishwa katika kipindi chote cha sherehe za sikukuu ya Pasaka mkoa wa Mwanza.

Pia Kamanda Mlowola alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kwa kutoa ushirikiano. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)

Thursday, April 17, 2014

UMESHAWAHI KULIWA KARATA TATU?

 Siku moja nilisimama hapo kwa interest ya kujua kinachoendelea nikajagundua ni wizi mtupu na ushirikina pia kwani muda wote ni udi ubani,baadaye nikatoka pembeni nikauliza vijana wauza karanga hapo njiani nikawaambia mbona Kama kinachofanyika hapo ni wizi? wakaniambia ndo hivyo tunashangaa hata we ulikuwa umeingia mkenge,kwa Hali hiyo ni kwamba jamii inajua kinachoendelea hapo ni wizi kulikoni jeshi letu la polisi wenye jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao?
Hali tete kwa washirika!!
"Twende mbere" sauti zilisikika. Picha na 
Chigiro Jchigiro

FAN CITY YAJIPANGA KUTOA BURUDANI YA KIPEKEE KWA WATANZANIA PASAKA

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY Bw. Hasan Rizvi akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine za michezo mbali mbali itakayotolewa kipindi cha sikukuu ya Pasaka wakati wa mkutano alioufanya katika eneo la Fun City Kigamboni jijini Dar es Salaam. Pia aliongeza kuwa kwa sasa kampuni yake imeeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.
Mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo la Fun City ambayo itawawezesha wananchi kupata burudani kabambe zenye ubora wa kimataifa kwani hakuna mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo.
Mawimbi yanayotengenezwa kwa mitambo ya kisasa katika bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fun City,
Moja ya Bwawa la kuongelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi  akionyesha vigari vya mchezo.
Bembea za kutosha.
Bembea za watoto.
Mapokezi ya Fun City.
Eneo la Fun City linasehemu ya Ibada. 
 Sehemu ya huduma ya kwanza nayo inapatikana hapa.
Sehemu ya moja ya sehemu ya bembea za magari ikiongesha madhari nzuri za kiota cha burudani cha Fun City.
Vigari vya umeme vinavyopita ndani ya maji.
*YAFUNGA MITAMBO YA KISASA KWA AJILI YA MICHEZO YA KWENYE MAJI
Na Mwandishi Wetu, Dares salaam
Wakati Watanzania wakiwa kwenye maandalizi ya sikukuu ya Pasaka kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY limeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.

Mtambo huo wa aina yake utaongeza hamasa kwa waogeleaji kuhisi kama wapo baharini.
Akizungumzia mtambo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi amesema, lengo la kuoberesha michezo hiyo ni kuwawezesha watanzania kufurahia michezo hiyo pamoja na familia zao wakati huu wa Pasaka.

Ameongeza kuwa mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo lake itawawezesha wananchi kupata burudani kabambe yenye ubora wa kimataifa kwani hakuna mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo inapatikana.

“Tumefunga mtambo huu ambao utakua ukitengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fan City, lengo letu nikutoa burudani zaidi kwa watu wanaotembelea hapa”.Alisema Rizvi.

“Tumefanya uwekezaji wa mashine za kisasa za michezo mbalimbali kwenye eneo letu ili kutoa burudani nzuri na za kipekee kwa wananchi wanaotembelea eneo hili na hasa wakati huu wa Pasaka”. Alisisitiza Rizvi. Fan City iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Fun City imekuwa ikitoa burudani safi ya michezo mbalimbali kwa familia na katika kipindi hiki cha Pasaka imeandaa michezo kama Sarakasi, Mazingaombwe na zawadi kemkem kwa watakaotembelea eneo hilo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog

SHUGHULI ZA USAFI ZAWAUMBUA WENYE MADANGURO NA GESTI BUBU STENDI YA BASI NYEGEZI MWANZA .

Mstahiki Meya wa Jiji laMwanza Stanslaus Mabula (kulia) akitoa maelekezo na amri ya kukusanya magodoro yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye baadhi ya majengo ya chakula kwa wasafiri katika kituo cha Stendi Nyegezi jijini Mwanza ambapo magodoro hayo nyakati za usiku hutumika kama gesti bubu na madanguro.
Ni shehena ya magodoro imehifadhiwa katika kila stoo na kona zilizojificha kituoni hapa.
Nyakati za usiku baadhi ya mapango la mabanda haya ya kuuzia vyakula hugeuka kuwa danguro na watu huja hapa kumaliza haja zao.
Lundo la vitendea kazi limenaswa kituoni hapa.
Kugundulika kwa madanguro na gesti hizo bubu ndani ya majengo hayo ya huduma za chakula kulikuja mara baada ya kuzuka mtafaruku kwa baadhi ya makundi ya vijana wanaodaiwa kuwa ni wapiga debe pamoja na makuli waliokuwa wakipiga kelele wakijibishana wakidai kuwa kuna watu wamegeuza stendi hiyo kuwa madanguro na gesti bubu kwaajili ya watu kumaliza haja zao.
Seleka, kasheshe, mbinde.
Hifadhi ya vitendea kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akitoa maelekezo ya utekelezaji wa zoezi la usafi kwa Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wapili kutoka kushoto), Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (wa tatu) na Mkurugenzi Alfa Hassan Hida pamoja na Afisa Habari wa Jiji Joseph Mlinzi.
Ni baadhi ya mabanda yaliyo jengwa kinyume cha utaratibu pembezoni mwa majengo ya stendi ya Nyegezi na hapa maafisa usalama pamoja na kamati ya usafi wakishiriki kuyaondoa katika zoezi hili linalotajwa kuwa litakuwa la kudumu.
Mkuu wa mkoa Ndikilo kikazi zaidi.
Meya Mabula kikazi zaidi.
Mkurugenzi wa jiji kikazi zaidi.
Wananchi wameitikia kwa dhati mpango huu wa usafi.
Kikazi zaidi.
Harambee.
Vijana nao wako mbele kufanikisha.
Zoezi lilikamilika kwa uchomaji wa taka hizo.
HABARI KAMILI.
MPANGO wa usafi umefumua gesti bubu na madangulo katika stendi ya Nyegezi jijini Mwanza.  

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa juma lililopita wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, Mkurugenzi wa Jiji Alfa Hassan Hida na Diwani Dismas Masunu (Butimba) walikuwa katika zoezi la usafi jamii shirikishi katika maeneo ya Stendi hiyo.

Kufumuliwa kwa gesti hizo bubu katika majengo ya wasafiri, na katika baadhi ya majengo yanayotumiwa na mama lishe, maduka na maofisi yaliyopo maeneo hayo kunafatia uchafu uliokuwa umekithili na kusababisha Meya Mabula kuagiza wafanyabiashara katika stendi hiyo kufunga kwanza biashara zao ili kushiriki katika zoezi hilo la usafi wa mazingira.

“Haiwezekani leo viongozi tuje kufanya usafi ninyi mmekaa na kuendelea na shughuli zenu wakati nyinyi ndo mnaozalisha takataka hizi, lakini hamna hata chembe ya aibu kuona Mkuu wa Mkoa Ndikilo anafagia na kuzoa takataka hata bila kushituka mnaendelea kusonga ugali na kupanga vitu maeneo yasiyoruhusiwa.

Kufuatia Hatua hiyo Mkurugenzi Hida alimuamuru Mtendaji wa Kata Hiyo kuwataka wafanyabiashara wenye vibanda ndani ya stendi hiyo kufunga mara moja na vingine kuondolewa kupisha usafi kufanyika ili kuweka mazingira safi yanayolidhisha na kuwepo uhalisia wa stendi ya mabasi na abiria wanaosubiria usafiri.

Aidha kutolewa kwa amri hiyo kulizua mtafaruku kwa baadhi ya makundi ya vijana wanaodaiwa ni wapiga debe na makuli wa kubeba mizigo kudai kwa kupaza sauti kuwa kuna watu wamegeuza stendi kuwa madanguro na gesti bubu ndani ya majengo ya huduma za chakula na humo ndani kuna magodoro mengi kwaajili ya watu kumaliza haja zao.

Baada ya makelele hayo Mkurugenzi Hida, Meya Mabula, Diwani Masunu, Mtendaji , Afisa Afya wa Jiji Kamenya kuingia ndani ya majengo ya stendi kushuhudiwa kilichokuwa kikilalamikiwa na vijana hao jambo ambalo lilimshangaza kila kiongozi na wananchi wakiwemo wanafunzi wa chuo kikuu cha St. Agustine (SAUT) walioshiriki zoezi la usafi wa mazingira maeneo ya stendi ya Nyegezi ambapo ni kutekeleza mpango kabambe wa usafi kila jumamosi ya kwanza ya mwanzo wa mwezi.

Akizungumza na wananchi, wapiga debe wa stendi na wafanyabiashara wa maeneo ya stendi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndikilo, aliwaagiza Mkuu wa Wilaya Konisaga, Meya Mabula, Mkurugenzi wa Jiji Hida, Diwani wa Kata hiyo na Afisa afya kufanya uwajibikaji na kurudi kuchunguza tuhuma zilizoelekezwa kwa watendaji wa serikali waliopo eneo la stendi.

“Hapa kuna tatizo haiwezekani mambo haya yanafanyika Mtendaji, Meneja wa stendi, Afisa afya wa Kata, Mkuu wa Kituo cha Stendi hawatambui haya, hili haliwezekani naagiza chukueni hatua kwa watendaji hawa na inawezekana stendi hii na mambo haya kuachwa kufanyika ni mradi wa mtu na wanaficha wanajuwa” alisema

Aliongeza kwa kusema kuwa "Nawapa wiki moja kuhakikisha hali ya usafi inarejea na kuhakikisha vibanda vyote vilivyo kinyume cha utaratibu na sheria vinaondolewa na kuhakikisha haya tuliyoyashuhudia leo yanakomeshwa na kutojirudia ikiwemo kuwachukulia hatua kali viongozi watakashindwa kutekeleza majukumu yao"

Mhandisi Ndikilo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali kushiriki katika usafi na mazingira katika maeneo yao ili kuendeleza juhudi zilizoanzishwa na uongozi wa Jiji hilo la usafi ili kuhakikisha linaendelea kuwa safi na kuendela kushinda na kunyakua tuzo ya usafi kwa mara ya tisa mfurulizo ikiwa ni kama utamaduni.

“Tujitokeze kutekeleza mpango huu kwa vitendo na usafi iwe ni tabia na tuchukie uchafu kwani huleta magonjwa ya kuambukiza kuharibu mazingira hivyo ni vyema tukaanza kuchukua hatua za kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaofanya uharibifu wa mazingira kwa kutumia sheria ndogo za Jiji zilizopo kudhibiti hali hii” alisisitiza Mkuu huyo.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Hida Hassan, tayari amewatangazia wafanyabiashara waliopo katika maeneo hayo ya stendi kuondoa mabanda yaliyo kinyume cha utaratibu na sheria za mipango miji kwani kuachwa wakifanya biashara kiholela kutasababisha kuendeleza uchafu kuzagaa kila kona hivyo kupoteza sifa na hadhi ya stendi.