ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 20, 2024

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI PWANI LAWAFUNDA WANANCHI JUU YA KUJIKINGA NA MAFURIKO NA MAAFA

 


NA VICTOR MASANGU,PWANI 


Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani Katika kukabiliana na majanga mbali mbali yakiwemo ya  moto na mafuriko ya mvua imetoa elimu kwa zaidi ya wananchi 72862 juu ya kujikinga na majanga pindi yanapotokea.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani Mrakibu mwandamizi Jenifa Shirima wakati akizungumzia mipango na mikakati waliyojiwekea katika kupambana na majanga ya aina tofauti.

Kamanda Shirima alisema kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi juu  ya kujikinga na majanga mbali mbali hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

"Sisi kama jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani tumeendelea kutoa elimu kwa wananchi wetu na kwamba tumeshafanikiwa kwa kuwafikia wananchi wapatao 72862 na kimsingi bado tunaendelea,"

"Katika zoezi ili la kutoa elimu kwa wananchi wetu wa Mkoa wa Pwani tangu Julai 2023 hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu tumepiga hatua kubwa ya kutoa elimu hiyo ambayo idadi yake ni 72862,"alisema Kamanda Shirima.

Kadhika Shirima alifafanua kuwa pamoja na kutoa elimu hiyo pia wameweza kupata fursa ya kutoa elimu juu ya tahadhari dhidi ya mafuriko ambayo yanatokea kutokana na mvua.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo alibainisha kuwa wameshapita kutoa elimu katika mikusanyiko ya watu mbali mbali ikiwa sambamba na kuanzisha sehemu maalumu za Fire club ambazo zitasaidia katika kupambana na majanga.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo aliwasisitiza wananchi ambao wamefanikiwa kupatiwa mafunzo hayo kuendelea kuyatumia vizuri ili yaweze kuwa msaada mkubwa katika jamii inayowazunguka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.