ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 11, 2017

RC MONGELLA APANGA KUTATUA KERO ZA ARDHI KILA MWEZI.

Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ametenga siku moja kila mwezi kwa ajili ya ziara za kikazi katika wilaya zote saba mkoani hapa kusikiliza na kutatua kero za migogoro ya ardhi zinazowakabili wananchi.
Mongella alisema jana kuwa ziara hizo zitaanza Novemba 20, katika wilaya za Ilemela na Nyamagana.

“Nitaanza na jiji la Mwanza ambalo ni kinara kwa kuwa idadi kubwa ya migogoro ya ardhi ambayo hutokana na utendaji mbovu wa baadhi ya maofisa wa idara ya ardhi,” alisema Mongella.

Alisema mwaka jana 2016, jiji hilo linaloundwa na Manispaa za Ilemela na Nyamagana lilikuwa na migogoro ya ardhi zaidi ya 1, 040 iliripotiwa.

Friday, November 10, 2017

HAMISA MOBETO AKWAA KISIKI KWA DIAMOND.

Dar es salaam, Mwanamitindo Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.

Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.  Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.

Mobeto  anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto  anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto  akidai  gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni  kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

TAKUKURU YAVIONYA VYAMA VYA SIASA KUHUSU RUSHWA.

Arusha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imevionya vyama vya siasa na washirika wao, wakiwemo wagombea katika uchaguzi mdogo wa madiwani kuhusu kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Ofisa wa Takukuru Wilaya ya Arusha, Jacqueline Kapileh ametoa onyo hilo akitoa mada kwenye baraza la madiwani jana Alhamisi 9,2017.

Uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika katika kata 43 nchini Novemba 26,2017 na kati ya hizo nane ni za Mkoa wa Arusha ambazo ziko wazi kutokana na waliokuwa madiwani kujiondoa Chadema na baadhi kujiunga na CCM.

Kapileh amesema hatua za kisheria zitachukua mkondo wake kwa watakaobainika kujihusisha na rushwa na hasa katika kipindi hiki cha kampeni.

"Tutahudhuria mikutano yote ya kampeni na wengine tutaweka makazi sehemu zinazoendeshwa uchaguzi ili kubaini kwa ukaribu vitendo hivi, na hasa wale washirika wa vyama na wagombea wanaowasumbua wananchi na kuwashawishi kuwapatia rushwa kuwachagua," alisema.

Pia, amewaonya wananchi wenye tabia ya kuwashawishi wagombea kuwapatia rushwa ili wawafanyie kampeni au kuwapigia kura.

Amesema Taifa haliwezi kuwa na kiongozi aliyeshinda kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwa wanategemea viongozi wanaopita katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wawe sehemu ya kutekeleza maagizo ya Serikali kwa masilahi ya wananchi ikiwemo kupiga vita rushwa.

Diwani wa Viti Maalumu katika Kata ya Ngarenaro, Happy Challe ameiomba Takukuru kutoa onyo kwa CCM kuondoa picha za wagombea kwenye miradi ya Serikali inayotekelezwa na hasa kwenye kata zenye uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia amesema, "Lengo la uchaguzi ni kupata wawakilishi wa Serikali, hivyo lazima apatikane kwa mapenzi ya wananchi. Nitasimamia utekelezaji na kutokomeza vitendo vyote vitakavyoashiria kuharibu uchaguzi."

Mkazi wa Kata ya Muriet ambako kutafanyika uchaguzi mdogo wa udiwani, Neema Marko ameiomba Serikali kudumisha ulinzi katika eneo lao kutokana na baadhi ya washirika wa vyama kuwasumbua na hasa usiku kuwaomba kura huku wakitoa vitisho kuwa wasipowachagua watacheleweshewa maendeleo.

IIED NA HAKI MADINI YAWAJENGEA UWEZO WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI MKOANI GEITA.

Baadhi ya wadau wa sekta ya madini Nchini na wachimbaji wadogo wakiwa kwenye mjadala ambao umeandaliwa na Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na  maendeleo(IIED )wakishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali  hakimadini,Kampuni ya ushauri(MTL) na kituo cha kimataifa cha utafiti wa mistu(CIFOR) na kufanyika kwenye ukumbi wa hotel ya alphendo Mkoani Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akimkaribisha mgeni Rasmi kwaajili ya kuzungumza na wadau wa sekta ya madini wakati wa Mkutano wa majadiliano juu ya swala la uchimbaji  madini kwa wachimbaji wadogo.

Kamishina msaidizi wa madini anayeshughulikia wachimbaji wadogo ambaye pia ni mgeni rasimi , Mhandisi David Mulabwa akifungua majadiliano hayo mapema hii leo kwenye ukumbi wa mikutano wa alphendo hotel.

Bw,Fitsum Weldegiorgis ambaye anatoka Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na  maendeleo(IIED ) akielezea namna ambavyo taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli pamoja na sekta ya madini Nchini.

Rebecca Burton ambaye anatoka taasisi ya Tiffany akizungumza namba ambavyo taasisi yao inafanya kazi wakati wa Mkutano wa majadiliano.

Mtafiti  wa kampuni ya ushauri  Dkt,Willson Mtagwaba,akibainisha changamoto ambazo wamekutana nazo wakati wakifanya tafiti kwa wachimbaji wadogo.

Baadhi ya wadau wa sekta ya madini wakiwa kwenye makundi kwaajili ya kujadili mambo kadha wa kadha.
NA JOEL MADUKA,GEITA



Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na  maendeleo(IIED )wakishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali  hakimadini,Kampuni ya ushauri(MTL) na kituo cha kimataifa cha utafiti wa mistu(CIFOR) imewakutanisha wachimbaji wadogo wa madini lengo likiwa ni kutazama  na kuona sekta ya madini inavyowahusisha wachimbaji wadogo kwenye shughuli za uchimbaji Mkoani Geita.


Kamishina msaidizi wa madini anayeshughulikia wachimbaji wadogo ambaye pia ni mgeni rasimi , Mhandisi David Mulabwa akifungua majadiliano hayo mapema hii leo kwenye ukumbi wa mikutano wa alphendo hotel,alisema  kuwa tatizo ambalo linawakabili wachimbaji wengi ni kutokuwa na mitaji ya kutosha kwaajili ya kufanya shughuli za uchimbaji kwenye maeneo ambayo yanakuwa na wingi wa madini(MASHAPU).


“Sasa ili kupata wingi wa madini ambayo yapo kwenye Mashapu kunaitajika nguvu kubwa ya mitaji sasa wachimbaji wetu wengi awana mitaji ya kutosha na ndio maana unakuta watu wanachimba tu bila ya kuwa na taarifa za mashapu sasa unapokuwa una taarifa za mashapu ujui unatumia shilingi ngapi na utapata shilingi ngapi  kwa hiyo inakuwa shughuli ya kubahatisha sasa ili uchimbaji uwe wa tija tunawaelimisha ni vizuri wakawa wanatafuta namna ya kupata taarifa za mashapu kwenye maeneo yao”Alisema Mulabwa.


Kwa upande wake Mtafiti  wa kampuni ya ushauri  Dkt,Willson Mtagwaba alibainisha kuwa wakati wa shughuli za kuwazungukia wachimbaji wadogo wamebaini tatizo kubwa wengi wao wamekuwa sio rasmi hali ambayo imeendelea kuleta migogoro baina ya wao na wachimbaji wakubwa na jambo jingine ni kutokuwepo kwa mikopo na bei elekezi.


Bi,Mathar Bitwa ambaye ni mchambaji wa madini ameeleza kuwa bado wanawake wanakabiliwa na changamoto katika sekta ya madini kutokana na kutokupewa kipaumbele kwenye shughuli hizo na kuwepo kwa mila na desturi kwa baadhi ya makabila  pamoja na mfumo dume kwenye shughuli hizo za uchimbaji ,huku Bw, Mtalingi Hamza Mohamedi akielezea sababu ambazo zinasababisha kutokupewa mikopo na mabenki ni kutokana na wao kutokujua kile ambacho wanakichimba wakati wa shughuli hizo.


Naye Mkurugenzi wa taasisi ya hakimadini,Bw Amani Muhina alisema kuwa uchimbaji mdogo unatoa fursa sawa kwa  watu kubadilisha maisha yao bila kuwa na ubaguzi wa kipato au Elimu kwasababu uchumi wa nchi unaletwa na watanzania wenyewe.