ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 1, 2009

WASHIRIKI MISS LAKE SOZE WATAPATA HUDUMA HAPA


KATIKA KUBORESHA MWONEKANO NA KUJISWAFI WATU MATAIFA MBALIMBALI HIFIKA CLARA SALON ILIYOPO NYERERE ROAD KTK KITUO CHA MAFUTA MOIL JIJINI MWANZA AMBAMO NDIMO HUDUMA ZATOLEWA KWA KIWANGO.

MAMBO YA CLARA SALONEH BANA EEH MWISHONI MWA WIKI NILIPATA OFA YA HUDUMA TATU NDANI YA CLARA SALON (samahani ntaziandika kivyangu pliz soma kiswahili) MASAJI", MANIKYUA'' NA PEDIKYUA" TEHEE!! EH BWANAAAA! NILITOKA NATABASAMU......!
pichani baadhi ya wateja wakijiswafi ndani ya

NANI KATI YA HAWA KUTWAA TAJI LA MISS LAKE ZONE?


HAWA NI WASHIRIKI WA MIKOA YA MARA, MWANZA SHINYANGA NA KAGERA AMBAO WAKO KAMBINI KATIKA HATUA ZA MWISHO HATIMAYE IJUMAA YA TAREHE 7 AGUST 2009 KTK UKUMBI WA YATCH CLUB WATAPANDA KATIKA JUKWAA MOJA KONESHA ZAO "SKILLZ" NA MISS LAKE ZONE TUMTAMBUE!!

Friday, July 31, 2009

USAFI JADI YETU

WAKIWA NA VIFAA TOSHA WADAU WA USAFI WA JIJI LA MWANZA (hapa wakiwa wamefika eneo la benki kuu) WAKISAFISHA MITARO YA BARABARA YA NYERERE.

NDO MANA KILA KUKICHA TUZO INAKWENDA MWANZA

NI BARABARA YA UHURU SAA 9:30 HOTEL DELUX PEMBEZONI JAPO FLOO YA CHINI PANA SUPU HAPO MUDA WOTE SIUNAONA PARKING WALIOCHELEWA WAKIPATA LUCH WALIO SHUGHULINI KUIFUKUZIA JIONI NA KUFUNGA VITABU.

MOJA KATI YA MAJENGO MAPYA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA PICHA HII NI KATIKA BARABARA YA UHURU.
SAWA NI JENGO ZURI LAKI.....

KUNA HAJA ZAIDI KUTIA MSISITIZO

HUU NI UJENZI UNAOENDELEA KATIKA BARABARA YA NYERERE NDANI YA ROCK CITY.
KATIKA KUBORESHA NA KUPANUA JIJI LA MWANZA SERIKALI MIAKA IMIWILI ILIYOPITA ILIAZIMIA MAJENGO YOTE YALIYOPO KATIKATI YA JIJI KUWA YA GHOROFA KUANZIA NANE NA KUENDELEA HIVYO IKATOA MUDA MAALUM KWA WAMILIKI WENYE NYUMBA ZA KAWAIDA AU ZA KIWANGO CHINI YA HAPO KUHAKIKISHA KUWA WANAKWENDA SAMBAMBA NA AGIZO HILO. ''UKISHINDWA UZA ENEO KWA WAWEKEZAJI WENGINE''. SWALI NI JE! KUNA MIKAKATI GANI ILIYOWEKWA KUHAKIKISHA KUWA MAJENGO YANAYOJENGWA YANAKWENDA NA WAKATI?

Thursday, July 30, 2009

JIJI LA MWANZA LINAKUWA NA KATIKA USAFI HATUKO NYUMA

IKUMBUKWE KWAMBA JIJI LA MWANZA NDILO LINALOONGOZA KWA USAFI NA HIVI KARIBUNI KAMPUNI YA MAWASILIANO TIGO ILITIA CHANGAMOTO KUUNGA MKONO SHUGHULI YA USAFI ILIYOANZISHWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MH. LAWRANCE MASHA SAMBAMBA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA BW. ABASS KANDORO. USAFI ULIKWENDA VIZURI NA NAFURAHI KWAMBA NDANI YAKE MAPUNGUFU YALIIBULIWA NA KUWEKWA HADHARANI HIVYO KUTIA CHANGAMOTO YA USAFI HALISI UNAOTAKIKANA. NENDA USWAZI SASA......NIBARAA.

WADAU SI KITUO CHA DALADALA HIKI NI MTAA

WADAU OFISI YA MKURUGENZI JIJI LA MWANZA HEBU TUAMBIENI! ULE UTARATIBU WA NJIA NDEFU UMEISHIA WAPI AU TUITE ILIKUWA NI OPARESHENI PITISHA MUDA AKA SINGLE? UTARATIBU ULIKUWA MZURI KWANI EXPRESS KATIKATI YA JIJI ZILIKUWA ZINA PITA TU HAZIWEKI KITUO ZAIDI YA KUPAKIA ABIRIA NA KU GO, KITUO KILIKUWA MWANZO WA SAFARI NA MWISHO WA SAFARI EITHER NYEGEZI AU IGOMA KUTOKANA NA RUTI. PICHANI NI MTAA WA SOKONI WENYE BARABARA YA ONE WAY AMBAO UMEGEUKA KUWA KITUO CHA EXPRESS. MITAANI ATUHEMI NI MBANANO MWANZO MWISHO.
HATA ZILE EXPRESS ZILIZOKO KITUONI NI MWENDO KUCHOMEKEANA LASIVYO ENEO HALITOSHI

MAONESHO YA NNE YA BIASHARA KUFANYIKA MWANZA

MAONESHO YA NNE YA BIASHARA NA KILIMO JIJINI MWANZA 2009 YANATEGEMEWA KUANZA KUFANYIKA KUANZIA TRH 14 AUGUST 2009 HADI 23 AUGUST 2009 KATIKA VIWANJA VYA SABASABA ILEMELA ROCK CITY.
LENGO LIKIWA NI;- KUTOA NAFASI KWA MAKAMPUNI KUZITANGAZA BIDHAA ZAO AFRIKA MASHARIKI.
;- KUPANUA WIGO WA KIBIASHARA KWA MAKAMPUNI.
;- KUTOA FURSA KWA MAKAMPUNI HAPA NCHINI KUBORESHA BIDHAA KUENDANA NA MAPINDUZI YA VIWANDA DUNIANI.
;- KUBORESHA SOKO LA BIDHAA AFRIKA MASHARIKI KWA KUSHINDANISHA BIDHAA KTK CATEGORY TOFAUTI NA NK.
WASHIRIKI 350 WA MASHIRIKA NA MAKAMPUNI YA KISERIKALI NA WATU BINAFSI KUTOKA KENYA, UGANDA, RWANDA, BURUNDI NA TANZANIA WANATEGEMEA KUSHIRIKI MAONESHO. HUKU WATU WALIO TEMBELEA MAONESHO HAYO WANATEGEMEWA KUPANDA KUTOKA 315,000 MWAKA JANA HADI KUFIKIA 400,000.

Wednesday, July 29, 2009

JAMANI WALIO ULIZA MA MC'S WA PAMOJA CONCERT WALIKUWA AKINA NANI?


MC'S WA PAMOJA CONCERT KUTOKA KUSHOTO MC JOB AKA BABA PAROKO and G.SENGO. USINIULIZE ZAIDI.....

TRH 26JULY2009 MWANZA ILITIKISIKA

MH. DIWANI WA NYAMAGANA BHIKU KOTECHA (mbele kushoto mwenye kaunda suti bkack) AKIMSHUHUDIA MGENI RASMI WA PAMOJA CONCERT MH. LUTENI KANALI MSTAAFU SERENGE MRENGO AKIKATA UTEPE KUZINDUA DVD YA ALBUM FURAHA YAKO. NAYE MC AKILA CHABOX.......

WAJUE KIHELYA AUTO TRACTOR PARTS MWANZA

DEALERS IN; SALE TRACTOR AND SPSRE PARTS
P.O. BOX 2074, TEL;+255 (28) 2540602
CELL; +255 754 437242
MWANZA, TANZANIA - EAST AFRICA
Email; lazarokihelya@yahoo.com

ENDELEAAAA!!!!!!

KUILINDA KAULI KILIMO UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU...


MARA BAADA YA KUONA SEKTA YA KILIMO INASUASUA HUKU WANANCHI WAKIKOSA MAZAO YA KUTOSHA KUILISHA NCHI NA HATA KUSHINDWA KUFANYA BIASHARA YA MAZAO NJE, SERIKALI KUPITIA VITENGO VYAKE ILIANZISHA MFUKO WA PEMBEJEO KWA MIKOPO YA RIBA NAFUU. IKIHITAJI WAKALA WA PEMBEJEO ZA KILIMO KWA KILA KANDA KUPITIA MCHAKATO WA KUOMBA TENDA ILIPITISHA WAKALA WAPATAO SITA KTK KANDA TOFAUTI NCHINI TZ. NAO NI -INCAR, NOBLE MOTORS, QUALITY GROUP, TTD, KIHERY AUTO TRACTOR PARTS NA FARM PARTS. PICHANI NI MKURUGENZI WA MOJA KATI YA WAKALA WA UZAJI MATRECTOR NA SPEA ZAKE KANDA YA ZIWA AMBAO NI KIHERY AUTO PARTS BW. LAZARO NGWELEJA AKIFAFANUA JAMBO NILIPOMTEMBELEA LEO KTK OFISI ZAKE ZILIZOPO MITIMIREFU JIJINI MWANZA.

CHUMA KINGINE KWA KILIMO

NI MOJA KATI YA MALI ZINAZOPATIKANA NDANI YA YARD ZA WAKALA HAWA WA PEMBEJEO ZA KILIMO WALIO IDHINISHWA NA SERIKALI KANDA YA ZIWA.

NAFASI YAKO MKULIMA KTK UFANISI


MAMIA YA WAKULIMA WANAMIMINIKA NDANI YA KIHELYA AUTO TRACTOR PART KUJIPATIA ZANA ZA KISASA ZA KILIMO ILI KUJIKWAMUA WAO NA TAIFA LAO NA LINDI LA UMASKINI WEWE JE?

FURAHA YAKO NA FLORA MBASHA

HAIJALISHI UMEKUMBWA NA MASAIBU GANI MAISHANI WALA KAYA YAKO IKOKATIKA KIPINDI KIPI KIGUMU YOTE YALISAHAULIKA KWA WADAU WALIODHURU TAMASHA LA PAMOJA.

MZUKA UKIONGEZWA NA MASHABIKI NIBARRA!

FLORA MBASHA NA KUNDI LAKE HAPA ILIKUWA KATIKA WIMBO "MWANAMKE SIMAMA IMARA" UNAUJUA KAMATA COPY YA ALBUM KISHA NAMBIE TUITE (mchiruku gospel AU gospel mchiriku?). TEHE!

Tuesday, July 28, 2009

TANGAZA SASA!


KWA KARNE YA SASA ILOJAA USHINDANI UKIINGIA KWENYE BIASHARA NI KAMA UMEINGIA VITANI. HIVYO ''BIASHARA BILA MATANGAZO NI KAMA BUNDUKI VITANI BILA RISASI''. PICHANI MMOJA KATI YA WADAU WA UKWELI KITENGO CHA MASOKO CLOUDS FM MWANZA HUMFREY SIMON AKA CHENGE AKIDIZAIN MATANGAZO YA MOJA YA WATEJA WAKE AMBAO TAYARI WANAINGIZA HUDUMA ZAO SOKONI. UKIFANYA NAYE BIASHARA LAZIMA UWIN! HILO NAKUHAKIKISHIA!!

CONTACT NAE KUPITIA - 0784476556
- 0282502553

Monday, July 27, 2009

TRH 26 MWANZA ILITIKISIKA


KILA MMOJA HAKUKUBALI KUHADITHIWA NI MGUU KWA MGUU KUSHUHUDIA PAMOJA CONCERT ILIYOFANYIKA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA SAMBAMBA NA TAMASHA HILO KUSHEHENI KWAYA MBALIMBALI TOKA JIJINI MWANZA, DAR ES SALAAM ILIWAKILISHWA NA FLORA MBASHA NA EDWARD, KENYA ILIWAKILISHWA NA MERCY KENNY, MARY MUTHUI NA PEACE MULU.

WATU SAFI, ENEO SAFI,MUZIKI SAFI!!

"KAMA UNAHITAJI AMANI OMBEA ADUI YAKO" by PEACE MULUMWIMBAJI MAARUFU KUTOKA NCHINI KENYA PEACE MULU ANAYETIKISA NA NYIMBO KAMA OMBEA ADUI YAKO, WAAMBIE WANADAMU NA NYINGINEZO NYINGI ALIPATA SHANGWE ZA KUTOSHA TOKA KWA WATANZANIA HUKU WENGINE WAKIMPOKEA KWA KUIMBA VIPANDE VYA BAADHI YA NYIMBO ZAKE HATA AKAKIRI KUWA AKIRUDI KWAO LAZIMA AKAHADITHIE MAPOKEZI ALOYAPATA.

UTUKUFU JUU MPAKA CHINI

HAKIKA MWANZA HAPASHIKIKI!! TIZAMA NYUSO ZA VIJANA WENYE NGUVU ZA KUTOSHA.

MWONEKANO SMART

KWAYA ZA JIJINI MWANZA ZILIJIANDAA, BILA SHAKA ZILI WEKA KAMBI KWA MAANDALIZI YA PAMOJA CONCERT KWANI KUNA MUDA NILIHISI ARDHI INACHIMBIKA! HENGERA ZANGU CHUKUENI.

FLORA MBASHA PAMOJA CONCERT ILIVYOFANA

EH BANA EEEH! HII NI KONA YA UMATI WA WATU ULIOFURIKA KUPOKEA KAMA SI KUJIZOLEA MIBARAKA YA BWANA KATIKA TAMASHA LA PAMOJA LA UIMBAJI MUZIKI WA INJILI, KULIA NI JAMAA WA VIDEO KAMERA TOKA NCHINI KENYA AKIWA SHUGHULINI.