ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 23, 2016

GAZETI LA MTANZANIA LAPEWA SIKU 3 KUKANUSHA TAARIFA ZA TAMVU KUMWOMBA MAGUFULI KUMFUKUZA KAZI MKUU WA MKOA WA MWANZA.

Muungano wa wapiga kura Tanzania TAMVU umekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti ka Mtanzania juu ya ombi la kufukuzwa kazi mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Rais wa muungano huo Milton Rutabana akizungumza na Jembe Fm amesema taarifa hizo si za kweli na kuwa hakutoa taarifa yoyote ya kwamba Rais amfukuze kazi mkuu huyo.

Kufuatia hali hiyo Bwana Milton amesema tayari amekwisha tuma barua kwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo kukanusha taarifa hizo. BOFYA PLAY KUSIKILIZA


Bwana Lutabana ametoa siku 3 kwa gazeti hilo kuomba radhi kupitia kurasa zake za mbele za gazeti sanjari na kukanusha taarifa hiyo vinginevyo atalichukulia hatua za kisheria.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari iliyoandikwa na Muungano huo inasema Gazeti la Mtanzania lilichapisha taarifa tarehe 19 January 2015 ikisema Muungano huo umemwomba Rais Magufuli kumfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa mulongo kutokana na kukosa sifa za kuongoza mkoa huo.

BASI LA BM LAPATA AJALI.

AJALI: Basi la BM linalofanya safari zake Dar-Morogoro, limepata ajali eneo Mikese Morogoro
Watu wawili wamefariki na wengine 43 wamejeruhiwa. Chanzo ni mwendo kasi. Sababu kuna gari lilikuwa limeharibika limeegeshwa pembeni. Kukawa kuna semi trailer inatoka Moro uelekeo DSM ikawa inalipita hilo gari lililoharibika. Kabla halijamalizika kulipita, BM ikawa imefika hapo ndio ikaingia katikati ya trailer.
Kwa mujibu wa mpenyezaji wa taarifa hii amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana (usiku kuamkia leo) majira ya saa nne usiku.
TUTAENDELEA KUPENYEZA TAARIFA ZAIDI.

SIRI YA KUAHIRISHA UCHAGUZI WA MEYA DAR.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya mwamvuli wa Ukawa kimetaja mambo matatu  ambayo ndiyo yamechangia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliokuwa umepangwa kufanyika leo.

Taarifa ya Halmashauri ya Jiji iliyotolewa jana haikueleza sababu za kuahirisha uchaguzi huo zaidi ya kusema kuwa utafanyika katika siku itakayotangazwa baadaye.

Msemaji wa jiji, Gatson Makwembe hakutaka kuzungumzia sababu za kuahirisha uchaguzi huo.

“Siwezi kuzungumza mengi kwa sasa, ila ninachoomba wakazi wa Dar es Salaam wavute subira hadi tutakapotangaza siku ya kufanyika uchaguzi huu,” alisema Makwembe.

Juzi, Makwembe aliliambia gazeti hili kuwa walishapewa maelekezo  kutoka ngazi za juu yaliyowataka kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika Januari 23. Kwa mujibu wa katibu wa Chadema wa Kanda, Henry Kilewo, mambo hayo ni CCM kutaka kujipanga kuwarejesha wajumbe wake waliotimuliwa kwenye uchaguzi wa meya wa Ilala na Kinondoni, kuhofia upinzani kushinda kutokana na idadi yao, na hofu kuwa meya kutoka upinzani atafichua uozo unaotokana na jiji kuwa chini ya utawala wa CCM kwa muda mrefu.

“Mambo hayo matatu ndiyo ambayo yanawapa hofu CCM na kutumia nafasi yake ya chama tawala kuagiza jiji kuahirisha uchaguzi,” alisema Kilewo.

“Wakithubutu kuwaingiza wajumbe hao, na sisi tutafanya hivyohivyo. Waache wamwage ugali Ukawa tutamwaga mboga.”

Madiwani 161 kutoka halmashauri hizo wanatarajiwa kupiga kura kumchagua meya mpya atakayemrithi Didas Masaburi, ambaye alihamishia harakati zake za kisiasa kwenye ubunge wa Ubungo, lakini hakufanikiwa.

Kati ya madiwani hao, 87 wanatoka Ukawa, wakati 74 wanatoka CCM. Kwa maana hiyo CCM imezidiwa wajumbe 13 na vyama vya Chadema na CUF ambavyo vimeshinda viti vingi vya udiwani wilayani Ilala na Kinondoni.

Kilewo alisema wajumbe wa CCM ni wachache ukilingalisha na Ukawa, hivyo wamelazimika kufanya hivyo wakisubiri wajumbe ambao ni mawaziri  wamalize vikao vya Bunge ndipo wahudhurie.

Kilewo alikitaka chama hicho tawala kujiandaa  kisaikolojia kwani kuna maisha baada ya uongozi.

“Wanajua muziki wa Ukawa tukilishika jiji hili, tutakwenda kufumua uozo wao wote walikuwa wameuficha na kuwakosesha ulaji baadhi ya viongozi wao,” alisema Kilewo.

Kwa upande wake, Katibu Uenezi wa CCM mkoani Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadaffi’ alisema CCM haihusiki na kuingiza wajumbe katika baraza la madiwani, bali Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ndiyo yenye mamlaka hayo.

“Tatizo lao hawa wapinzani kila kitu wanapinga, hata wajumbe walioteuliwa na Rais kisheria hawataki washiriki katika baraza, halafu ndiyo wanasema wanafuata sheria?” alihoji Gadaffi.

Alisema CCM ni chama makini na kinafanya maamuzi ya busara, kwa kuwa kimemteua mgombea wa umeya aanayekubalika na kila mtu, tofauti na  mshindani wake.

“Usishangae hata huu uchaguzi wa meya wa jiji wajumbe wa upinzani wakatupigia kura kama walivyofanya kule Temeke, kwa sababu ya umakini wa CCM ya kuweka mtu anayekubalika,” alisema Gadaffi.

MAGAZETI YA LEO:- MARUDIO UCHAGUZI ZANZIBAR SASA NI MARCH 20.

Marudio uchaguzi Zanzibar Machi 20. Magufuli atinga ngome ya Lowassa kijeshi. Wasomi walaumiwa sakata la Zanzibar.

NIYONZIMA AANZA KAZI..

Nionzima aanza kazi na vigogo wa msimbazi viroho kwatu pata dondoo za magazeti hapa.

Friday, January 22, 2016

RIPOTI YA TATHMINI YA MAZINGIRA YA KISHERIA KATIKA MWITIKIO WA UKIMWI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA ZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (katikati), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa ripoti ya tahmini ya mazingira ya kisheria katika mwitikio wa ukimwi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Makao Makuu ya Tacaids Dar es Salaam leo asubuhi.
 Viongozi hao wakiwaonesha wageni waalikwa na wadau mbalimbali ripoti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tacaids, Elizabeth Kaganda na kilia ni Dk.Bwijo Bwijo kutoka UNDP.
 Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina, akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (kushoto), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (katikati) wakimpongeza Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina baada ya kuhutubia.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wakiwa katika uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na viongozi.
Wasanii wa Hisia Threatel Group kutoka Sandali Temeke jijini Dar es Salaam wakionesha igizo linalohusu ukimwi katika uzinduzi huo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

MKUTANO WA 32 WA SERIKALI ZA MITAA.

Yajue mengi kutoka kwa Katibu mkuu wa jumuiya za serikali za mitaa akikujuza kuhusu Kuelekea mkutano wa 32 wa serikali za mitaa:

DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI RAIS MWENYE VIPAJI VINGI.

 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juu
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

WAZIRI WA AFYA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI MWANZA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza jana ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada  ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD, Profesa Idrisa Mtulia.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa MSD wakati wa uzinduzi wa duka hilo.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. UmyMwalimu amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni.

Katika hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, ameipongeza MSD kwa hatua hiyo nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na kuitaka MSD kukamilisha ufunguzi wa maduka mengine mawili yaliyosalia katika mikoa ya Arusha naMbeya, kwani hicho ni moja ya kipaumbele katika uongozi waserikali ya awamu yaTano.

Waziri huyo ameeleza kuwa Wizara yake imejiwekea malengo ya upatikanaji wa dawa nchini kutoka asilimia 70 kwa sasa kufika hadi asilimia 95.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema maduka mawili ya Arusha naMbeya yamemekamilika, na yanatarajia kufunguliwa hivi karibuni, na kwamba kwa  mikoa mingine wameshafanya  mawasiliano  na kwamba tayari MSD imefanya mazungumzo na viongozi wa mikoa Ruvuma, Rukwa, Singida, Dodoma, Geita, Kagera na Iringa kufungua maduka yao ya dawa ambapo MSD itawauzia dawa.

“Tutakachofanya, sisi (MSD) utawapa  utaalamu na  kuwawezesha utaalamu wa uendeshaji maduka hayo” alieleza Bwanakunu.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

ZIARA YA RAIS MAGUFULI ARUSHA.

Rais John Magufuli awaagiza wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi kusimamia vilivyo fedha zinazopelekwa katika shule zote nchini

RAIS DKT MAGUFULI AKIWASALIMIA WANANCHI JIJINI ARUSHA WAKATI AKIELEKEA WILAYANI MONDULI KIKAZI.


Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
Baadhi ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo asubuhi.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO na KISONGO. 
PICHA NA MICHUZI JR.

Thursday, January 21, 2016

MSUKULE ULIOKUTWA NDANI YA CHEMBA YA MAJI MACHAFU JIJINI DAR.

Tukio hilo bado lina maswali mengi ndani yake.!. Baadhi ya wataalamu wa mambo wanasema kama angelikuwa msukule angekatwa ulimi, pia angekuwa na taahira ya akili kwa ufupi hajitambui wala hawezi kujifahamu yeye ni nani. 

Lakini kuna wengine wakasema kuwa suala la kukatwa ulimi ni hatua ya mbele mara baada ya mtu kutekwa msukule.

Lakini bado watu wanahoji wasipate majibu ya chapchap!! Kwa nini yuko humo shimoni? Nani aliyemuweka humo na kisha kumfunika kabisa asilione jua, na kwanini alikuwa uchi....?

"KAMA ULIKOSA SPORTS RIPOTI BASI HUYU NDIYE ROGER MILLA"

**SPORTS RIPOTI** YA JEMBE FM 93.7 KIPINDI KINACHOROKA KILA SIKU SAA 3 USIKU HADI SAA 4, JANA ILIKUSHUSHIA HISTORIA YA NGULI WA SOKA ULIMWENGUNI ANAYETOKEA AFRIKA, ROGER MILLA. KAMA ULIIKOSA 
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

ABBY SOLO AJA NA UNDELA

Mwanamuziki wa JJ Band Abby Solo akimkabidhi zawadi mtangazaji wa kipindi cha Drive Mixx cha kituo cha radio  Jembe Fm Mwanza, CD ya wimbo wake mpya uliotoka rasmi hivi majuzi uitwao Undela.
CD ya wimbo iki namna hii.....

BOFYA PLAY KUISIKILIZA. (SAUTI KUWAJIA PUNDE)

AIRTEL YAZINDUA DUKA KARIAKOO MSIMBAZI

Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba,  akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam, akishuhudia ni wakala mkuu wa Airtel kutoka Celnet, Bwana Kalpesh Bandar
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati),  akiangalia simu aina ya Bravo Z10  wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam.  Akitoa maelezo kuhusu simu hiyo ni Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) , akishuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel, James Moilo
Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) akitoa maelezo  kuhusu simu mbalimbali za smartphone  zinazopatikana katika duka jipya la Airtel Express Kariakoo wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya  lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Pichani ni Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati) akiwa na wateja pamoja na wafanyakazi wa Airtel


AIRTEL YAZINDUA DUKA KARIAKOO MSIMBAZI
·        Airtel yafungua milango kwa wafanya biashara Kariakoo.

Dar es Salaam, 20 Januari 2016, Airtel Tanzania imezingua duka la Airtel Xpress mtaa wa msimbazi, Kariakoo Dar es Salaam ikiwa ni moja ya mipango yake ya kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja wake.
Kuzinduliwa kwa duka la kariakoo Airtel Xpress inaongeza idadi ya maduka kuongezeka kufatia uzinduzi wa dula jipya la kisasa lililoko Morocco Dar es salaam ulifanyika wiki iliyopita.
Katika uzinduzi wa duka la Airtel XPress  kariakoo mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba alisema, kufunguliwa kwa duka la Airtel Xpress kariakoo itawawezesha wateja wa Airtel na wafanya biashara wa Kariakoo, Ilala, Magomeni kupata huduma zetu kwa ukaribu zaidi kama kujipatia simu za kisasa na kwa bei nafuu. Tunaimani kufunguliwa kwa duka hili hapa kutatasaidia kupata huduma kwa uharaka na ubora zaidi.
“Airtel tumejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wetu zaidi ya milioni 10 nchi nzima. Kipaumbele chetu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kiurahisi zaidi na kwa ufanisi wakati wote na hili limejidhihirisha leo kwa kufungua duka la Airtel Xpress”, aliongezea Adriana
Baadhi ya huduma zitakazotolewa kwenye duka la Kariakoo ni pamoja na Airtel Money, kusajili laini, huduma za internet na huduma zetu nyinginezo.

Pamoja na duka jipya lililozinduliwa kariakoo pia Airtel inamaduka sehemu mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam kama Airtel Morroco, Mlimani City, J Mall, Buguruni Airtel inatarajia kufungua maduka zaidi ifikapo Juni 2016 yatakayotoa huduma sambamba na mawakala wake Zaidi ya 80,000 nchi nzima

TAFAKURI KUHUSU UCHAGUZI MKUU 2015.


Kongamano La Tafakuri Kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015
Msikilize Dkt. Ayoub Ryoba akikujuza kuhusu kongamano litakalofanyika kwa ajili ya tafakuri ya uchaguzi mkuu wa October 2015:

Wednesday, January 20, 2016

RADI YAUWA WAWILI KATAVI.

Radi yauwa wawili na kujeruhi watatu  Katavi  waliokuwa wakijihifadhi chini ya mti kutokana na mvua kubwa zinazonyesha wilayani humo.

SIZONJE - NEW SONG 2016 MRISHO MPOTO

 Pata nafasi kuusikiliza hapa BOFYA PLAY KUUSIKILIZA.
Baada ya "kutoka" kwa wimbo na mashairi ya 'Mjomba' ,kisha baada ya hapo akaja na kitu Samahani wanangu, Waite, Njoo uichukuwe, Chochea kuni na nyingine nyingi msanii malenga Mrisho Mpoto anayeendelea kupata mafanikio siku hadi siku kwa kuweza sasa kumiliki bandi yake aliyoipa jina la Mjomba Band, akiajiri vijana zaidi ya 10 na kuendeleza libeneke kwa nguvu zake zote ni safari nyingine sasa kwako kufaidi ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Sizonje, hapa akimshirikisha mkali mwingine Banana Zorro. Cheki mzigo mzima hapo juu.

DAKTARI FEKI ANASWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA.

Daktari feki kakamatwa mchana kweupeeee Hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekeutoure..... jamaa amekuwa hospitalini hapo kimtindo akipiga mzigo zaidi ya mwezi mzima, huku akitoa huduma zake feki za uigizaji bila kustukiwa na akijimix na madaktari wa ukweli hospitalini hapo. 

Kwamujibu wa wagonjwa na ndugu waliokuwa wakifika hospitali wanasema 'Jamaa amekuwa akiwatoza fedha wagonjwa kwa kuwaahidi kuwafanyia operation au kuwaharakishia oparesheni wakati sio mwanataaluma. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)


ILI KUPATA HABARI ZAIDI SIKILIZA JEMBE HABARI kila siku saa moja asubuhi (07:00), kumi kamili (16:00) na saa moja jioni (19:00) ukiwa na @harith_jaha / @elikanamathias na @mustafakinkulah Tupate popote ulimwenguni kupitia Google play store kwa kusachi JEMBE Fm kisha sikiliza LIVE kupitia simu yako ya mkononi.

WABUNGE CCM WAMGEUKIA MAGUFULI:- MAGAZETI JAN 20 STAR TV.

Ekari 3000 zaleta kizaazaa Kigamboni. Serikali ya tano yajipanga kupambana na mdudu rushwa, Wenye shule binafsi waibana NECTA.

ASKARI POLISI ALIYEKEJELI PASPORT YA LIONEL MESSI KUPITIA SNAPCHAT AFIKISHWA MAHAKAMANI.

Askari Polisi aliye mkejeli Lionel Messi kupitia Snapchat video hiyo akiwa  na passport halisi ya Messi na kuigiza kwenye video hiyo akiuliza watazanaji "Je! Niichome hii passport ya Messi au niirudishe" 

Habari zinasema askari huyo hii leo kasimamishwa mahakamani, moja ya majarida ya Abu Dhabi yameripoti taarifa hiyo that the policeman appeared in Dubai's Court of Misdemeanours over posting the video to pals in December. 

The newspaper said the clip included the caption: "Shall I burn the passport or just put it back!" Albert Sengo 8:57pm The cop, identified as J.M., admitting breaching the five-time Ballon d'Or winner's privacy - but said it was just a joke. 

He claimed he had tried to get a photo with the Barca superstar only to be told he was too tired after arriving in Dubai airport's private jet area. 

The cop also claimed he had the permission of Messi's bodyguard to hold the document. He said: "I went to the passport control desk and noticed that Messi's passport had been left there, so I picked it up and shot a video of myself while holding it.

Tuesday, January 19, 2016

POLISI DAR WAVURUGA MTANDAO WA BIASHARA DAWA ZA KULEVYA

Polisi kanda maalum Dar es Salaam yavuruga mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya baada ya kuwanasa vinara wawili wa biashara hiyo.

MUUJIZA WA KUPANDIKIZWA KWA UBOHO (BONE MARROW) ULIVYOBADILISHA MAISHA

The founder and Chairman of Apollo Hospitals Dr. Prathap .C. Reddy.

Mara nyingi watu kutoka nchi zilizoendelea waishio na tatizo la damu na upungufu wa kinga mwilini huishi, tofauti na nchi zinazoendelea ambazo zinakumbana na uhaba wa huduma ya kupandikiza uboho.

Huduma za kisasa na bora za kupandikiza uboho katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ni tatizo; kusubiria huduma bora katika nchi hizi zinazoendelea, inaendelea kuhusiana na hali mbaya ya kiafya na vifo. Hii ni kutokana na ripoti mpya za kiafya. Kutokana na takwimu za mwaka 2012, ni nchi tatu tu za kiafrika ambazo ni Misri, Afrika kusini na Nigeria ambazo zina hospitali zenye uwezo wa kupandikiza uboho.

Upandikizi wa uboho ni njia mpya ya kisayansi na udaktari katika kutibu matatizo na maradhi kama Leukimia, kuvimba kwa seli (Lymphoma), saratani katika seli nyeupe (Multiple myeloma), sicko seli anaemia, kuharibika kwa uboho (Aplastic anaemia), Thalassemia, ukosefu wa seli nyeupe (Congenital neutropenia), na upungufu wa kinga za mwili. Matatizo maalum kama ya uvimbe na ulemavu wa kurithi kama Thalassemia pia umepatiwa ufumbuzi mzuri kupitia matibabu haya.

Upandikizwaji wa uboho na seli za mfumo wa kati wa damu ni mfumo unaorudisha seli katika shina la mfupa zilizoharibiwa kwa matumizi makubwa ya mionzi ya kuulia saratani na mionzi mingine pia. Baada ya kupatiwa tiba kwa dozi yenye nguvu ya dawa za saratani na mionzi, mgonjwa huwa anatengeneza shina bora la seli, zinazo safiri kwenye uboho na kuanza kutengeneza seli mpya za damu.

Kwa mujibu wa daktari mtaalamu wa upasuaji Tanzania Dk. Harrison Chuwa, upandikizwaji wa uboho ni wa muhimu sana kulinganisha na madhara ya kutokufanya hivyo kama kupata magonjwa ya leukaemia, seli kuvimbiana hasa kwa kesi za kupooza kwa viungo vya mwili.

“Upandikizwaji wa uboho ndio tiba ya mwisho kwa wagonjwa wenye saratani ya damu,watanzania wengi huwa wanapewa rufaa ya kwenda kufanya upandikizwaji katika hospitali za Apollo India kwa kudhaminiwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii” Alisema Dk. Chuwa.

Ufanano katika uboho au seli za damu unaokusanywa kutoka kwa wanaojitolea damu kwa wagonjwa wanaohitaji inaweza kuokoa maisha ya wagonjwa zaidi ya asilimia 70.

Wastani wa gharama za kufanya upandikizaji wa uboho kwa nchi zilizoendelea ni kati ya dola za kimarekani 50,000 mpaka dola 1,000,000 kulingana na aina ya hospitali unayofanyia. Kwa nchi kama Singapore, Malaysia, Brazil, Mexico, India, Thailand, Hong Kong gharama ni kati ya dola za kimarekani 20,000 mpaka 60,000 kulingana na aina za hospitali.

Kwa mujibu wa www.patient-help.com, Marekani na Ulaya wanatoa huduma ya gharama zaidi ya upandikizwaji wa uboho kwa dola 200,000 na upandikizwaji kwa kupata mtoaji damu anayefanana na kundi lako ni dola 250,000. Hii ni tofauti na India ambao wanatoa huduma hiyo ya kwanza kwa dola 35,000 na ya pili kwa dola 50,000.

Mbali na kupewa cheti kutoka JCI hospitali za Apollo nchini India zinatoa matibabu bora kabisa kwa kutumia vifaa vya kisasa na kwa bei nafuu kulinganisha na mataifa ya Ulaya na Marekani. Kutokana na uhitaji wa upandikizwaji wa uboho duniani kote, hospitali za Apollo zimezindua huduma maalum ya upandikizwaji wa uboho. Kitendo hicho kimeifanya hospitali hii kuwa kitengo cha kiteknolojia katika afya bora.

Hospitali za Apollo zilifungua milango yake mwaka 1983 na kutambulisha huduma bora za kimataifa nchini India, kwa gharama zilizo chini sana kulinganisha na zile za ulaya. Hii ni mara ya kwanza kwa hospitali za Apollo kuchukua jukumu kubwa hilo la kiafya na kuifanya kuwa hospitali kubwa ya kwanza kutumia teknolijia ya hali ya juu katika matibabu”. Aliyasema hayo mwanzilishi na mwenyekiti wa hospitali za Apollo Dk. Prathap.C. Reddy.

Kituo cha upandikizwaji wa uboho katika hospitali za Apollo, kimefanikiwa kufanya zaidi upandikizaji 700 kwa mafanikio ya hali ya juu. India ni nchi inayosifika kwa upandikizwaji kwa wagonjwa wanaotoka mataifa mbalimbali, kwa sababu sio tu kwa kwamba hospitali hizi zina timu za madaktari bingwa wa upandikizaji bali pia wana njia nyingi bora za kuzuia madhara ya kiafya katika zoezi hilo.

Tanzania ni kati ya nchi iliyonufaika na vituo vya afya kutoka hospitali za Apollo. Katika mahojiano siku za karibuni na mgonjwa aliyetambulika kwa majina ya Dk. Philip Robert Hiza ambaye baada ya kugundulika ana tatizo la seli alipewa rufaa kwenda hospitali za Apollo ambapo alipatiwa matibabu kwa miezi mitano yanayohusisha upandikizwaji wa uboho pia, Dk. Philip Robert Hiza alikiri kuwa upandikizwaji wa uboho umeleta mafanikio makubwa katika maisha yake.

Maendeleo haya katika matibabu yamepunguza kiwango ha muda uliokuwa unatumika hospitalini kwa ajili ya mgonjwa kupata nafuu. Na kupata nafuu ndani ya muda mfupi kunapunguza gharama za matibabu pia.

MWILI WA MBUNGE LETICIA NYERERE WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM MAZISHI YAKE KUFANYIKA BUTIHAMA MKOANI MARA KESHO KUTWA

 Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani  kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika keshokutwa.
 Mwili huo ukiingizwa kwenye gari maalumu katika uwanja huo.
 Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
 Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
 Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.

MWANAMUME ASHTAKIWA PICHA ZA WHATSAPP KENYA

Miili
Miili ya Kwanza ya wanajeshi waliouawa Somalia iliwasiki Nairobi Jumatatu.

Mwanamume mmoja nchini Kenya ameshtakiwa kusambaza picha alizodai ni za wanajeshi wa Kenya waliouawa nchini Somalia akitumia WhatsApp.
Eddy Reuben Illah ameshtakiwa kwa kueneza: “Picha zinazodaiwa kuwa za miili ya maafisa wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF), waliodaiwa kushambuliwa na kuuawa eneo la El-Adde nchini Somalia ukijua kwamba ni za uchochezi na zingesababisha hofu na wasiwasi miongoni mwa raia.”
Anadaiwa kusambaza picha hizo kwenye kundi la watumiaji wa WhatsApp kwa jina A young peoples union (Muungano wa vijana).
Bw Illah amekanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mwandamizi wa Kiambu, mji ulio karibu na Nairobi, Bw Justus Mutuku.
Juhudi za wakili wake Bw Edwin Sifuna kutaka aachiliwe huru kwa dhamana huru zimegonga mwamba na akatakiwa kuweka dhamana ya Sh100,000 na mdhamini wa Sh50,000, gazeti la Daily Nation limeripoti.
Kesi hiyo itatajwa Februari 2 na kuanza kusikilizwa Februari 12.
CHANZO BBC SWAHILI.

HADI SASA WATU 100 WAMENUFAIKA NA AIRTEL MKWANJIKA.

Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akikabidhi shilingi 790,000 bw, kwa Elias Makani mshindi wa Airtel Mkwanjika ikiwa ni zawadi yake  aliyojizolea katika boxi la Airtel  Mkwanjika mkoani Dodoma jana, anaeshudia katikati ni Afisa Masoko kanda ya Kati bw, Hendrick Bruno. Promosheni ya Airtel Mkwanjika bado inaendelea ambapo hadi sasa tayari Airtel imeshawanyakua washindi 100 na kuwazawadia pesa taslim kila mmoja.
Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akikabidhi shilingi 910,000 kwa Bi  Devota Fongonyo mshindi wa Airtel Mkwanjika ikiwa ni zawadi yake  aliyojizolea katika boxi la Airtel  Mkwanjika mkoani Dodoma jana, anaeshuhudia kulia ni mtangazaji wa kipindi cha mkwanjika Bw Godfrey Rugalabamu (gala B). Promosheni ya Airtel Mkwanjika bado inaendelea ambapo hadi sasa tayari Airtel im
Toka Kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na mtangazaji wa kipindi cha mkwanjika Bw Godfrey Rugalabamu (gala B) wakwanza kushoto wakisaidiana kuhesabu hela na mshindi wa promosheni ya Airtel Mkwanjika  mkoani Dodoma bw Rioba Matiku ikiwa ni zawadi yake  aliyojizolea katika boxi la Airtel  Mkwanjika mkoani Dodoma jana, Promosheni ya Airtel Mkwanjika bado inaendelea ambapo hadi sasa tayari Airtel imeshawanyakua washindi 100 na kuwazawadia pesa taslim kila mmoja.

AIRTEL MKWANJIKA YAWAZADIA 100 HADI SASA
Airtel Mkwanjika tayari imeshawazawadia jumla ya watanzanzia 100 tangu ilipozinduliwa ambapo jana washindi wengine watatu kati ya saba wa Airtel toka mikoa ya Singida,Dodoma na Tabora, wamevuna fedha katika boxi la promosheni ya 'Airtel Mkwanjika' wakati Boxi la Mkwanjika lilipofika mkoani Dodoma kwa lengo la kuwazawadia washindi wake wa kanda ya Kati.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema hayo katika  droo iliyochezeshwa  mjini Dodoma jana kwa wateja  wa kanda  ya kati ambapo wateja wanne wameshindwa kufika licha ya kuambiwa watagharamikiwa kila kitu ikiwemo nauli, chakula na malazi ili waweze kufika kujizolea fedha lakini wamekuwa hawaamini na kuhofia kuwa inawezekana ni matapeli.

"leo wateja wa Singida,Dodoma na Tabora,  ni zamu yenu kujizolea mapesa ya Airtel Mkwanjika, pia natoa wito kwenu wateja wa airtel mnapopigiwa simu za ushindi kwa namba ya Airtel 0683-442244 kutoa ushirikiano kwakuwa droo hiyo haina tozo ya aina yoyote laisema mmbando”.

Mmbando alisema Airtel imetenga kiasi cha sh.milioni 300 kwaajili ya wateja wa Airtel na kila mmoja anaweza kushinda na mteja anachotakiwa kufanya ni kujiunga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza salio kwa kutumia vocha na kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya siku bila makato yoyote.

Alisema kila siku wateja wanne wa airtel wanavuta mkwanja katika promosheni hiyo na huchezeshwa kila baada ya siku saba za wiki na kutoa washindi 28.

Alibainisha bado zaidi ya wateja 200 kushindaniwa  kwenye bado droo tisa zilizobaki ambazo zitawapa  fursa wateja wanne wa airtel kila siku kushinda kila mmoja hadi sh.milioni moja.

Wakizungumza mara baada ya kujiokotea fedha katika droo hiyo, mshindi wa kwanza mkazi wa Dodoma,James Ryoba matiku, alisema ameweza kujipatia Shilingi laki tisa na elfu kumi ambazo zitamsaidia kuongeza mtaji katika biashara zake za nguo.

Kwa upande wake, Mkazi wa Tabora, Devota Fongonyo, alisema awali alipopigiwa simu ya ushindi hakuamini na kuona kuwa ni matapeli lakini baada ya siku nne alipigiwa tena na akubali kufika Dodoma huku akiwa na hofu.

Alisema katika droo hiyo amejipatia kiasi cha shilingi laki tisa na elfu thelasini ambazo zitamsaidia kulipa ada za watoto wake.

Naye Mkazi wa Kongwa, Elias Makani, alisema amejipatia kiasi cha shilingi laki Saba na elfu tisini ambazo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo.

TINGATINGA LIKISAWAZISHA BONDE LA MKWAJUNI YALIPOKUWA MAKAZI YA WATU CHINI YA ULINZI.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Mtaa wa Ananasifu,  Deogratias Mogela akizungumza na waandishi wa Habari (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Moja ya banda lililochomwa moto na kudaiwa  kuokolewa mtoto Braiton Emanueli (2) ambae mama yake Amina  Selemani humuacha hapo na kwenda kufanya biasha ya kupika uji 



 Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Muongozo Darasa la 6 Faiza Abdallah (11) akizungumza na mama yake ambapo hapo awali walikuwa katika Bonde hilo na sasa amehifadhiwa kwa ndugu Gongolamboto

 Baada ya Tingatinga kutinga eneo la Bonde la Mkwajuni, Mtoto Rozi akihamisha godoro










 Wananchi wakibomoa wenyewe banda lao baada ya kuliona tingatinga kufika katika Bonde la Mkwajuni kwa lengo la kusawazisha eneo hilo
 Mwananchi (kulia) anusurika kipigo toka kwa wananchi waliokuwa wakitoa vifaa vyao katika Bonde la Mkwajuni  alipotaka kuchukuwa chuma cha Tanesco
 Tingatinga likibomoa moja ya vibanda vilivyojengwa kujihifadhi kwa muda wakazi wa Bonde la Mkwajuni, Dar es Salaam ambao nyumba zao zilibomolewa hivi karibuni.