ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 4, 2016

KWA HERI MOHAMMED ALI AFARIKI DUNIA




🐯 Hii namba ilikuwa inawachapa sana kinowmerNowmer wenzake ila kuna pambano moja tu ambalo alishinda kwa zilizo la mentali, ndio ni pambano lililofanyika mwaka 1975 jijini manilla Liliitwa Thrilla in Manila. Alipambana na mwanaume mwingine aitwae Hayati Joe Frieza(Joe smoker), Hili ndilo pambano gumu zaidi kwa Mohammed Ali, Walipambana kama wanauwana, ilikuwa hatari sana ila Ilipofika raundi kama mbili za mwisho, Joe Frieza hakurudi ulingoni, Mohammed akatangazwa mshindi, alipohojiwa baada ya ushindi akasema, Hata mm kama Joe angerudi ulingoni nisingeweza kuendelea. Na mpaka Leo hii Hayati Joe Frieza anaaminika kuwa mwanadamu aliyemfanya Mohammed Ali azitolee jasho hela zake... RIP The greatest king of all time Muhammad Ali. 👑.... 📌

Friday, June 3, 2016

MREMBO GIGY MONEY AMCHANA LAIVU RAPA NAY WA MITEGO ASEMA HAYA

KUTOKA BONGO FIVE
Video vixen machachari, Gigy Money amedai ni muda wa rapper Nay wa Mitego kubadilika kwasababu anachokisikia kwenye nyimbo zake ni taarab na sio hip hop ya ukweli.

Gigy ambaye hapo awali amewahi kuzinguana na hitmaker huyo wa ‘Nasaka Pesa’ baada ya kutumika kwenye video ya Shika Adabu Yako ya rapper huyo na kutolipwa ujira wake, amemuambia mtangazaji wa Jembe FM ya Mwanza, JJ kuwa hip hop ya Nay imejaa uswahili mwingi.

“Inabidi abadilishe uimbaji wake uwe wa kisasa zaidi. Nay anaimba hip hop as taarab, imekuwa ni lugha ya mafumbo wakati hip hop ni zamani ilikuwa inatritiwa nyimbo sexy ambazo anasikiliza mtu akiwa ametulia,maneno unayasikia,” amesema Gigy. “Lakini yeye anataka kuimba vitu vingi katika muda mmoja halafu anaponda, so he is bad to me kwa asilimia 00.0.”

Kwa upande mwingine Gigy amesema msanii wa hip hop anayemkubali Tanzania ni Joh Makini.
“Anajielewa, hana skendo, yaani ana nyota yake kali, msafi,” amesisitiza.
“Anaimba vizuri, unamsikia hata kama ni M-Arusha, yaani R na L zinatofautiana.”

SITAKI UPITWE NA HILI LA BARCLAYS KUTOA MSAADA WA MADAWATI HANDENI

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto) akipokea sehemu ya madawati 70  kutoka kwa  Meneja Masoko  wa Benki ya B arclays Tanzania  (BBT) Nasikiwa Berya  yaliyotolewa ba benki hiyo kusaidia  Shule ya Sekondari Handeni kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga hivi karibuni.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto), akikabidhi madawati hay kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Handeni wilayani humo hivi karibuni. 
 Meneja Masoko  wa Benki ya B arclays Tanzania  (BBT) Nasikiwa Berya (watatu kushoto), akikabidhi sehemu ya  msaada wa madawati 70 kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari handeni, Amani Mmbaga, yaliyotolewa na benki kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga .  
 Mmoja wa maofisa wa Benki ya Barclays Tanzania, Raymond Bunyinyiga (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.  
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakibeba madawati tayari kuyakabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Tanga kusaidia shule za sekondari wilayani Handeni.
Mchezaji wa timu ya soka ya Benki ya Barclays iitwayo ‘Blue Eagle’ Edwin Makata, akichuana na Issa Silaji (kulia) wa timu ya soka ya Shule ya Sekondari Handeni, katika mchezo wa kirafiki mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati 70 yaliyotolewa na timu hiyo.

BANC ABC YAANZISHA HUDUMA YA KUKUZA BIASHARA AFRIKA.

 Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John Kazimoto, Jones Mwalemba, naJohn Du Toit.
 Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akibadikishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo, John Du Toit katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni  BancABC Tanzania, Khalifa Zidadu (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa Superdoll, Sateesh Babu Desu na Prasanthar Govinder pia wa Superdoll.

 Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akifafanua jambo mbele ya baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani), katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Bank ABC imeanzisha huduma mpya kwa wafanyabishara wakubwa kuhamisha and kuingiza mitaji yao ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya elektroniki.Akizungumza katika hafla iliyofanyika Jumatano hii, Mkuu wa kundi la Benki hiyo katika ukanda wa Afrika, Dk. Mabouba Diagne alisema wametenga Dola za Kimarekani milioni 20 (zaidi ya Sh billion 40) kwa ajili ya mpango huo unaolenga kuimarisha biashara miungoni mwa nchi za Afrika.

“Tumeanzisha huduma hii mpya kwa ajili ya kurahisisha na kukuza biashara miungoni mwa wafanyabishara wakubwa barani Afrika. Tunataka wafanyabiashara waweze kufungua milango yenye fursa nyingi za kibishara barani Afrika,” Dk. Diagne alisema.Alisema Banc ABC imezimia kuwawezesha Watanzania kutumia teknolojia mpya ya kuhamisha mitaji na fedha nyingi si ndani ya nchi tu bali nje ambako kuna fursa nyingi za biashara zisizotumika.

“Mara nyingi wafanyabishara wengi wa hapa nchini wanaofanyabishara nan chi jirani wamekuwa wakilalamika kukosekana kwa huduma bora za kuhamisha fedha kwa wingi. Sasa jawabu limepatikana kwa Banc ABC kuanzisha huduma za kisasa za kuhamisha mitaji,” alisema.

Alisema watu wanaweza kuhamisha mitaji hata fedha nyingi nchi za nje kwa kutumia simu za mkononi bila kuathiri biashara.“Tumeanzisha huduma hii kwa sababu biashara baina ya nchi za Afrika ni jambo muhimu la kuwezesha nchi na wafanyabishara waweze kutumia fursa nyingi zilizomo barani Afrika kutokana na bara hili kuwa na rasilimali nyingi asilia,” alisema kiongozi huyo msomi mwenye shahada ya juu ya uzamili ya hisabati.

Alisema suala la kubadilishana na kuhamisha mitaji ni biashara kubwa duniani kwa sababu mitaji ni bidhaa muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu.Mapema mkurugenzi wa Banc ABC Tanzania, Bw Dana Botha alisema tayari benki hiyo imeanzisha mtandao wa matawi 100 hapa nchini na kuwa miungoni mwa benki imara.Naye Mtendaji Mkuu wa kundi la benki hiyo Dk. Blessings Mudavanhu alisema kuwa benki hiyo ambayo imesajiliwa katika soko la fedha la London, ilizindua aina ya bidhaa yake mpya na kujitanua kimataifa baada ya kuungana na Atlas Mara.

“Tutatumia jamvia la teknolojia ya habari na mawasiliano. Tunataka watu waanchane na kuandika cheki nyingi na kutumia gharama kubwa za miamala ya katatazi badala yake watumie simu za mkononi,” alisema Dk Madavanhu.Alisema benki hiyo ambayo inaendesha biashara katika nchi za Tanzania, Nigeria, Afrika kusini, Botswana Zimbabwe, Rwanda, Burundi na Zambia imedhamiria kuwa benk kubwa inayokuza biashara miungoni mwa nchi za Afrika.

Katika hafla hiyo kampuni kadhaa kubwa zilishiriki na kuvutiwa na huduma hiyo mpya itakayotolewa na benki hiyo ya kimataifa. Kampuni hizo ni; Statoil, Mount Meru (T) Ltd, Lake Oil. Superdoll na Puma Energy.

MASHAUZI, SNURA, ROMA MKATOLIKI NA WAZEE WA SINGELI KUISHIKA DAR LIVE JUMAMOSI HII


Jumamosi hii ya Juni 4 mbona ‘kitanuka’ Dar Live! Ni usiku wa nani mkali kutoka kwa mastaa wataarab, bongo fleva na singeli. Ni onyesho kubwa la na mwisho kabla kuelekea mapumziko ya mwezi mtufu wa Ramadhan ambapo Isha Mashauzi akiwa na kundi zima la Mashauzi Classic ataumanajukwaanaSnura, Roma Mkatoliki, Sholo Mwamba na Man Fongo. Msemaji wa ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo amesema onyesho hilo la kipekee limezingatia muziki wakila nyanja ilikuleta ladha isiyochuja mwanzo hadi mwisho wa show. 

Mbizo amesema kupitia onyesho hilo mashabiki watajionea wenyewe nimzuki upi wenye nguvu zaidi kati ya taarab, bongo fleva, singeli na hata rumba kutokana na ukweli kuwa Isha Mashauzi mbali na taarab lakini pia anangoma zake kali zamuziki wa rumba.

Naye Isha Mashauzi amesema atalitendea haki onyesho hilo hasa kutokana na ukweli kuwa hajapanda jukwaa la Dar Live kwa takriban miaka miwili na hivyo hiyo ni nafasi pekee ya kuka ta kiu ya mashabiki wake watakaofika kwenye ukumbi huo mkubwa zaidi wa burudani ulioko maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wednesday, June 1, 2016

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA TAMKO KUKEMEA WIMBI LA VITENDO VYA MAUAJI VILIVYOANZA KUSHAMIRI NCHINI.


TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa kupokea taarifa za vitendo vya mauaji ya kikatili vinavyoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali nchini, hususani kanda ya Ziwa, Mkoa wa Pwani, na Dar es Salaam.

Wimbi hili la matukio ya vitendo vya mauaji na ukatili uliojitokeza kwa kufuatana mwezi Mei 2016 yanavunja haki ya kuishi ambayo ndio msingi wa haki zote za binadamu kwa ujumla wake.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya yote na matendo yote ya kikatili dhidi ya mwanadamu yanapotokea popote nchini.

Baadhi ya matukio hayo kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Tume yametokea usiku wa Mei 11, 2016 katika kitongoji cha Nyigumba, Kijiji cha Sima Wilayani Sengerema, Mwanza, ambako watu watano (5) wa familia moja waliuwawa kwa kukatwa mapanga; Mei 18 watu watatu (3) pia waliuwawa kwa kukatwa mapanga wakiwa katika nyumba ya ibada, Msikiti wa Rahman, eneo la Ibanda relini, mtaa wa Utemini, Kata ya Mkolani,Wilaya ya Nyamagana, Mwanza; Usiku wa Mei 25, mwanamume mmoja na mkewe waliuwawa kwa kukatwa mapanga kijijini Manzavi, Wilayani Butiama, Mara.

Aidha, mnamo Mei 22, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bulale, Kata ya Buhongwa, Mwanza, Bwana Alphonce Musanyenzi aliuawa. Mauaji mengine yametokea Mei 18, Mkoani Pwani, Askari Polisi, Sajenti Ally Salum Kinyogoli alipouwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika. Mei 23, jijini Dar es Salaam, eneo la Kiwalani, watu wanne (4) waliuawa kwa kuchomwa moto wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao; Mei 26, Bi. Anathe Msuya aliuawa kwa kuchinjwa akiwa nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Matukio haya ya ukatili yanakiuka haki ya kuishi iliyoainishwa katika ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria za nchi, matamko na mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ya kikanda na kimataifa.

Kufuatia wimbi hili la mauaji linaloonekana kuendelea nchini, Tume inalaani na kukemea vikali vitendo hivyo vya kikatili.

Mbali ya ukiukaji mkubwa wa haki ya msingi ya kuishi, mauaji haya na matukio haya pia ni kinyume na mafundisho ya imani zetu mbalimbali, hivyo yasifumbiwe macho na kuachwa yaendelee, kwani yanaweza kuleta mazoea mabaya ya kuona suala la kuuwa ni jambo la kawaida na hivyo kuhatarisha amani, maisha ya watu na jamii.

Hivyo, Tume inashauri yafuatayo:
1. Serikali kupitia Jeshi la Polisi ichukue hatua mahsusi kuhakikisha ulinzi wa wananchi dhidi ya mauaji na vitendo hivi, kwani jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama wa wananchi ni jukumu la serikali. Jeshi la Polisi lihakikishe watu wote waliohusika kutekeleza mauaji haya wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake.

2. Tume inawataka pia wananchi wahakikishe wanashirikiana na vyombo vya dola kufichua maovu na kubaini uvunjifu wowote wa sheria na haki za binadamu ndani ya jamii, na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuzuia matukio kama haya kujirudia, au kusaidia upelelezi wa mauaji haya na matendo mengineyo ya uvunjifu wa sheria.

3. Jamii ijenge utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.
4. Mamlaka za Serikali za mitaa katika ngazi zote ziwe na mipango madhubuti ya kuhakikisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
5. Tume inatoa rambirambi kwa ndugu, jamaa na wanafamilia waliopoteza wapendwa wao katika matukio haya na pole kwa majeruhi.
Jukumu la ulinzi na utetezi wa haki za binadamu ni letu sote!

 Imetolewa na:
 (SIGNED)
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Mei 31, 2016.

MIJADALA YA BUNGE LEO MJINI DODOMA.


Hii hapa hotuba ya bajeti ya wizara ya fedha na mipango kwa mwaka 2016/2017 iliyowasilishwa bungeni hii leo.  


Mbunge wa Muheza aihoji serikali juu ya ucheleweshaji wa uidhinishaji wa Muheza kuwa halmashauri ya mji ikiwa kuna ongezeko kubwa la watu.  


Mipango ya serikali kutatua kero ya wananchi walio na kaya masikini kutopata fedha za TASAF hususani katika mkoa wa Kigoma.  


Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Gasia ahoji serikali juu ya ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Mtwara.  

KATIKA TELEVISHENI MAGAZETI YA LEO> MBOWE TUPO TAYARI KUTIMULIWA WOTE BUNGENI. MAALIM SEIF AHOJIWA SAA 3.DPP ASIMAMIAMWENYEWE RUFAA DHIDI YA KINA KITILYA.


Magufuli awamwagia neema wawekezaji viwanda vya ndani. 8 wachinjwa Tanga.Wanafunzi UDOM wasaka vibarua kwa mama lishe.


Mbowe: Tupo tayari kutimuliwa wote bungeni. Maalim Seif ahojiwa saa 3. DPP asimamia mwenyewe rufaa dhidi ya kina Kitilya. 


Wanataaluma UDOM wataja kiini cha mgogoro.TBS kusaka vilainishi, matairi feki. JPM amuombea radhi Muhongo. 

WIMBI LA MAUAJI NCHINI TANZANIA LAZIDI KUTIKISA WATU WANANE WAUAWA KIKATILI TANGA.

Watu nane wameuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana katika kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya Amboni mkoani Tanga

Tuesday, May 31, 2016

MAALIM SEIF AHOJIWA MASAA MATATU POLISI.

Jopo kuu la upelelezi la polisi visiwani Zanzibar limefanya mahojiano maalumu na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais visiwani humo Maalim Seif Shariff Hamad

TBL YAIBUKA MSHINDI


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo  kwa mshindi  wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015, kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  wakati wa hafla ya kutoa  tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia)  na kushoto ni Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo


TBL Group yaibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya mzalishaji bora wa mwaka 2015

Kampuni ya  TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo  imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.

Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI nahafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.

Akiongea baada ya hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni  kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.

“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.

Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.

“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.

GARI CHUPUCHUPU KUZAMA BAHARI YA HINDI

 Gari lenye namba za usajili T 709 AYW likiwa limeegeshwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi baada ya kutofuata sheria za vivuko, gari hilo likiwa limesheheni barafu ambapo haikufahamika mara moja ilikuwa ikipelekwa wapi.  Inakadiriwa mnamo  majira ya saa 11: 25 alfajiri, gari hilo likiingia katika kivuko cha MV Lami mapema leo hii lilinasa kwenye mlango wa kivuko  hicho kwa kile kinachodaiwa ni kuzidisha mzigo mkubwa na kusababisha kunasa katika mlango huo na kusababisha MV Lami kusukumwa na gari hilo na ikabidi barafu hiyo kupakuliwa kisha gari hilo kuvutwa na na gari lingine lenye namba za usajili T 661 AXB na kupelekwa   Kituo cha Polisi cha Kigamboni Jijini  Dar es Salaam   


(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

MADAKTARI WAPATA MAFUNZO YA KUREKEBISHA MIGUU ILIYOPINDA

 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa Dk.Richald Gellman  kutoka Califonia - San Fransisco Marekani (kushoto), akiwaonesha kifaa Chuma, maalumu kinacho tumika kufanya marekebisho ya mifupa iliyo pinda baada ya kuunga vibaya au kutounga kabisa,   madaktari  mbalimbali kutoka nchi mbalimbali , Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia, DRC Congo, Nigeri, Zimbabwe na wenyeji wao Madaktari wa Taasisi hiyo  wamehudhuria Mkutano huo utakaomalizika Juni 3, 2016 , unaendelea katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mifupa ya Fahamu Muhimbili (MOI) 
Dar es Salaam leo. 
 Pichani ni baadhi ni vifaa
Vifaa mifano na mifananisho.
Vifaa mwili wa mwanadamu wakati mwingine ni kama motokaa.
Vifaa na vitendea kazi kwaajili ya tiba za mifupa.
Darasani zaidi.
 Madaktari Bingwa wakiwa katika chumba cha mikutano katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Moi

Mmoja wa Maktari Bingwa wa Taasisi hiyo mwenye miwani mbele Dk. Moonlight Mnyenye akiandika jambo wakati wa mkutano huo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

HIVI NDIVYO MWANZA ILIVYOJIPANGA KUVUNJA JUNGU.





🎧Jumamosi hii 4 June 2016 tumenuia kuifanya Villa Park Resort igeuke kwa muda kuwa mji wa burudani.... Pale sebuleni Super Kamanyola kuwakaribisha tena na tena wakali wa town wa kukushika JJ BAND🎸na Le King 'chumvi ya warembo' Zarry Edosha @zarryedosha 🎤Ma-MC wako with 'Giant Voices' toka Jembe Fm @mbabavc + @bonzbalaa kusimamia show la Villa Night Club ambamo Jembe dJZ wakuitwa @chrissthedj na @deejaykflip wamepewa dhamana ya kuki-hapenisha. Kiingilio buku 3 sebuleni na ukitaka kuzama chumbani Disco buku 7. 📌

BOFYA PLAY KUUPATA MPANGO MZIMA.

RAYMOND:- 'KILA KITU KWANGU DILI KIWE KIBAYA AU KIZURI' ALIZOMEWA JUKWAANI NA KUGEUZA MZOMEO WA MASHABIKI 'BUUUU' KUWA CHORUS. HAO HAO WALIOMZOMEA NDIYO WALIO MSHANGILIA.

🐯 Leo ndani ya #Hitzone ya @jembefm kipindi kinachoruka majira ya mchana saa 7 hadi kumi alisikika mkali wa Wakali kutoka #WCB wasafi.. Mkali wa #Kwetu na Sasa #Anatafutakiki @Rayvanny ndani ya #Celtalk jamaa amefunguka mengi ya kusisimua na kufurahisha, ikiwemo kitendo cha Kuzomewa na Mashabiki uwanja mzima ila akacheza nao kisaikolojia😂🙌, CC:- @nattyebrandy @babajuti @deejay_Jacko🙏🙅📻📻📻📻📻Tell them!.... 📌 Ungana na simulizi kamili kwa njia ya sauti hapa chini kusikia kilichotokea anga la 93.7 Mwanza.

BOFYA PLAY KUSIKILIZA

NEMC IMEKIFUNGIA KIWANDA CHA KUSINDIKA NYAMA YA PUNDA DODOMA.

Baraza la taifa la usimamizi wa mazingira {NEMC} limekifungia kiwanda cha Huwa Cheng Company Limited kilichopo mjini Dodoma na kukitoza faini ya shilingi milioni 200 baada ya kubaini kiwanda hicho kinajihusisha na usindikaji wa nyama ya Punda kinyume na utamaduni wa watanzania huku mazingira yake yakiwa hatarishi kutokana na uchafu unaozalishwa kuzagaa kwenye makazi ya watu.

Mabishano makali baina ya wamiliki wa kiwanda husika ambao ni raia wa uchina na maofisa wa NEMC yaliyochukua muda mrefu kabla ya maofisa hao kutoa tamko la kufungwa kwa kiwanda hicho ambacho mbali na kuzalisha nyama ya Punda ambayo ni kinyume na utamaduni wa watanzania lakini pia mazingira ya uzalishaji wake ni hatarishi kwa afya za wafanyakazi na majirani wa eneo hilo.
 
Kiwanda hicho ambacho kwa siku kinadaiwa kuchinja Punda wasiopungua 200 inaelezwa kuwa mbali na kukiuka utamaduni lakini pia kinaharibu kizazi cha wanyama hao ambao uzao wake unatajwa kuwa ni mdogo hali inayotishia wanyama hao ambao kwa kanda ya kati hutumiwa katika kazi mbalimbali kupungua ama kutoweka kabisa.
 
Mohamed Hamis ni meneja msaidizi wa kiwanda hiki ambaye amezungumza kwa niaba ya raia hao wa uchina anasema nyama hizo za Punda zinasafirishwa kwenda kuuzwa nchini China.
 
Wakazi wa mji wa Dodoma wanatupa lawama kwa mamlaka za mkoa kutobaini kiwanda hicho na kukichukulia hatua huku kukiwa na taarifa ya nyama hizo kuzagaa na kuuzwa katika maeneo mbalimbali ya mji huo hasa kwenye mabaa na migahawa ya chakula.

Monday, May 30, 2016

TWANGA PEPETA YAZINDUA ALBUM YAKE YA 13 'USIOGOPE MAISHA' MBELE YA MKUU WA MKOA WA MWANZA NA KUCHANGIA MADAWATI.

Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwakaribisha wakazi wa Mwanza katika Uzinduzi wa Album ya 13 ya Bendi ya Twanga Pepeta inayojulikana kwa jina la 'Usiyaogope Maisha' uliofanyika Villa Park jumamosi na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki wa burudani ya muziki wa nyumbani akiwemo mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela.
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa album ya 13 ya Bendi ya Twanga Pepeta Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela (kulia) akizungumza na wadau wa burudani ambapo pia ilikuwa fursa ya kufanya harambee fupi ya kuchangia madawati kwa ya manufaa ya shule zenye uhaba, Kushoto ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka mara baada ya kumkaribisha mgeni rasmi, mpango mzima ukifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbiwa Villa Park Resort.
Mikononi mwa mgeni rasmi album 'Usiyaogope Maisha'
Wadau wa burudani  walizichanga kwa njia mbalimbali....
Mkurugenzi wa Semira LTD naye alipata nafasi ya kuchangia katika harambee fupi iliyofanyika ndani ya uzinduzi wa album 'Usiyaogope Maisha' ya Bendi ya Twanga Pepeta.
Afande Abou aka Mzee wa Boma ya Ng'ombe akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela mara baada ya kuchangia harambee ya madawati kwa shule za Mwanza ndani ya uzinduzi wa album Usiyaogope Maisha ya Bendi ya Twanga Pepeta.
Master Plan naye alipata fursa ya kuujazia mfuko wa madawati.
Zamu ya Ashraf.
Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 1.3 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela  zilizochangwa na waakazi wa Mwanza kwenye zoezi la 'Changia elimu papo hapo'   katika Uzinduzi wa Album ya 13 ya Bendi ya Twanga Pepeta uliofanyika Villa Park mwishoni mwa wiki siku ya jumamosi na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki wa burudani ya muziki wa nyumbani.
Shukurani za Mkuu wa Mkoa mara baada ya fedha kukabidhiwa kwa Mr. Matia Levi (kulia) ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa album ya 13 ya Bendi ya Twanga Pepeta Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela (kulia) akibofya rimoti kwaajili ya wadau wa burudani kujionea kwa mara ya kwanza Video ya album mpya ya Twanga Pepeta iitwayo 'Usiyaogope Maisha'  Kushoto ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akishuhudia tukio hilo, mpango mzima ukifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbiwa Villa Park Resort.
Rais wa Bendi ya Twanga Pepeta Ally Choki (kushoto) na Makamu wake Luiza Mbutu (kulia) wakiongoza safu ya mashambulizi jukwaani.
Hapa Kalala Jr, hapa Haji BSS na hapa Luiza Mbutu.
Rogati Hega na sauti yake adimu kwa stage la Twanga.
Makamuzi yaliendelea kwa style yake.
Hatari sana.
Kikazi zaidi.
Mashambulizi ya Twanga.
Mzuka wa bass guitar ulipopanda ilikuwa zaidi ya uchizi.
Zile swaggZ....pale kati.
Shabiki na stage la Twanga Mwanza.
Chekshia.
Keyboardist wa Twanga Pepeta mtamboni huku Luiza Mbutu akichombeza kwa pembe ni balaaa.
Mpigaji wa solo guitar na Twanga Pepeta akifanya mashambulizi.


Kwa hisia zaidi Kalala Jr na Luiza Mbutu.
Twanga Pepeta dadaz....mbeeeeele.
Ally Chiki akiimbisha  mashabiki wake.
Double impact.
Selfie na kamera ya Gsengo.
Drummer boy wa Twanga Pepeta James Kibosho na selfie ya Gsengo blog.
Taswita kutoka juu.
Another selfie.
Meneja wa Villa Park Mwanza Rammadhan akiwa na mkewe Bi Husna.
The last Selfie kwa tukio.
Kama ni nafasi ya kuwaizungumzia Twanga Pepeta ya sasa kauli ninayoweza kuitoa kuhusu onyesho lao la burudani Mwanza , ni kuwa "Onyesho la Jumamosi lilikuwa la aina yake, nidhamu ya jukwaani ilikuwa kubwa kiasi cha kushangaza, uchaguzi wa nyimbo (playlist) ukadhihirisha kuwa Twanga Pepeta ina utajiri wa nyimbo nyingi kali, za zamani hadi za sasa, kwa upande wa ma-vocalisti daah wametulia hawana papara wanajua wanachofanya, wanaimba kwa kupokezana wakipishana kimahesabu sahihi ya muziki....Nashindwa kubaini nani alikuwa nyota wa mchezo kwani hata wanenguaji walikuwa balaaa. 

BIG UP TWANGA PEPETA 'KISIMA CHA BURUDANI' TUTAINUNUA SANA ALBUM YENU 'USIYAOGOPE MAISHA' 
by Gsengo.