Mabishano makali baina ya wamiliki wa kiwanda husika ambao ni raia wa
uchina na maofisa wa NEMC yaliyochukua muda mrefu kabla ya maofisa hao
kutoa tamko la kufungwa kwa kiwanda hicho ambacho mbali na kuzalisha
nyama ya Punda ambayo ni kinyume na utamaduni wa watanzania lakini pia
mazingira ya uzalishaji wake ni hatarishi kwa afya za wafanyakazi na
majirani wa eneo hilo.
Kiwanda hicho ambacho kwa siku kinadaiwa kuchinja Punda wasiopungua
200 inaelezwa kuwa mbali na kukiuka utamaduni lakini pia kinaharibu
kizazi cha wanyama hao ambao uzao wake unatajwa kuwa ni mdogo hali
inayotishia wanyama hao ambao kwa kanda ya kati hutumiwa katika kazi
mbalimbali kupungua ama kutoweka kabisa.
Mohamed Hamis ni meneja msaidizi wa kiwanda hiki ambaye amezungumza
kwa niaba ya raia hao wa uchina anasema nyama hizo za Punda
zinasafirishwa kwenda kuuzwa nchini China.
Wakazi wa mji wa Dodoma wanatupa lawama kwa mamlaka za mkoa kutobaini kiwanda hicho na
kukichukulia hatua huku kukiwa na taarifa ya nyama hizo kuzagaa na
kuuzwa katika maeneo mbalimbali ya mji huo hasa kwenye mabaa na migahawa
ya chakula.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.