ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 27, 2018

ALLIANCE YAISULUBU PAMBA 2 0


Timu ya Alliance Fc ya jijini hapa imeendelea kujiweka mahala pazuri kutinga Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, baada ya kuwafunga "TP lindanda Wanakawekamo'  Pamba Fc pia ya Mwanza, mabao mawili kwa nunge, katika mchezo wa Ligi Soka Daraja la Kwanza Tanzania Bara, uliopigwa ijumaa ya tarehe 26 mwezi January kwenye dimba la Nyamagana.

DKT. MWANJELWA AISHUKURU CHINA KWA KUONYESHA NIA YA KUISAIDIA TANZANIA KWENYE MAENDELEO YA TAFITI ZA KILIMO CHA MINAZI NA MIHOGO

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA
Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt. Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia wadudu marafiki

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.

Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.

Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.

Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.

Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.

Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.

Friday, January 26, 2018

LUKUVI AFUNGUKA KILE KITAKACHO WAKUTA WAMILIKI ARDHI WAKAIDI MKOANI MWANZAWaziri wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi ametangaza kiama kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kutoa muda hadi kufikia APRIL 30 mwaka huu kuhakikisha kuwa wanalipa kodi hiyo ambayo ipo kisheria na watakaoshindwa watafikishwa mahakamani ifikapo mwezi MAY mwaka huu.

MWANAUME ATUHUMIWA KUMUUA MKE NA MTOTO WAKE WILAYANI CHATO


Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo ambalo kumetokea tukio.

Jirani wa Familia ambapo kumetokea mauaji Bi,Mariam Shija akizungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko juu ya tukio hilo.
Diwani wa Kata  Minkoto   , Bw Geroge Magezi akiwasisitiza wananchi kushiriana na jeshi la Polisi kwenye suala la ulinzi na usalama.

Dk Masanja Mchanganya anayetokea kituo cha afya cha Bwanga akielezea namna ambavyo wamebaini mwili wa marehemu majeraha yaliyopo baada ya kufanya uchunguzi.


Na,Joel Maduka,Chato.

Mkazi wa kijiji cha Minkoto Wilaya ya Chato Mkoani Geita Bw Hoja Kasumbakabo ( 25) anatuhumiwa kumuua mke wake Spensioza Petro (22) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali mwilini na kisha kumnyonga mtoto Brison Hoja mwenye umri wa miezi mitatu kisha   kutokomea kusikojulikana.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Leo Nkwabi amesema tukio hilo limetokea tarehe 24 mwezi januari kuamkia tarehe 25 kwenye kijiji hicho ambapo ilibainika miili kuonekana chini ya Sakafu ndani ya chumba walichokuwa wanaishi huku mwili wa mwanamke huyo ukiwa na majeraha sehemu ya kooni, mgongoni na tumboni huku utumbo ukiwa nje.

Mzazi wa marehemu Mzee Petro Lusaga ameelezea kusikitisha na tukio hilo na kwamba hakuwahai kuwaona marehemu na mumewe wakiwa na ugomvi kwani kwa kipindi chote walikuwa wakiishi  kwa amani bila ya kuwa na malumbano wala kelele zozote ndani ya familia yao.

Bi,Judy Masanja ambaye ni jirani wa karibu wa familia hiyo alisema na yeye ameshangazwa na kifo hicho kwani hawakuwai kuwa na ugomvi na siku hiyo walikuwa wamekaa nje na walikuwa wakizungumza vizuri tu hivyo hata  yeye kifo kimekuacha na maswali mengi ya kujiuliza.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Bw Geroge Magezi amewataka wananchi  kuimarisha ulinzi na kuisaidia serikali kumtafuta mtuhumiwa huku akisisitiza wanaume kuacha mauaji ya namna hiyo.

Dr Masanja Mchanganya anayetokea kituo cha afya cha Bwanga amethibitisha tukio hilo ambapo katika uchunguzi walioufanya wamegundua kuwa marehemu alikuwa na majerahaa matatu makubwa 


KATIBU WA CCM KATA YA BUHALAHALA ATUHUMIWA KUTAFUNA KIASI CHA SH MILIONI 20

Ofisi za  kikundi cha wajasiliamali (KIWAGE) zilizopo mtaa wa Shilabela Mjini Geita  zikiwa zimefungwa .

Mwenyekiti wa Mtaa wa Shilabela   Bw,Elias  Mtoni akielezea suala la vikundi ambavyo vimeonekana kuwa na dhana ya utapeli juu ya fedha za wajalisiamali .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akizungumza juu ya uwepo wa taarifa za kiongozi ambaye analalamikiwa kutokomea na fedha za wajasiliamali.
Na,Joel Maduka,Geita...


Katibu wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Buhalahala mjini Geita Lazaro Kagoma  anatuhumiwa kutafuna kiasi cha zaidi ya milioni 20 ambazo  zilitolewa na halmashauri ya mji wa Geita kwa kikundi cha wajasiliamali Geita (KIWAGE)walipatiwa na halmashauri ya mji wa Geita.


Kagoma ambaye ni Katibu wa Kikundi hicho cha KIWAGE anadaiwa kuwazunguka wanachama wenzake na kutafuna   fedha walizopatiwa  kwa ajili ya manufaa ya kufanya shughuli za ujasiliamali inadaiwa badala yake alizifanyia matumizi yake binafsi kinyume na matarajio ya kikundi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shilabela  Bw,Elias Mtoni  alisema  kikundi hicho kimeonekana kuwa na  ujanja  mwingi kutokana na udanganyifu ambao wameweza kuufanya wa kuidanganya halmashauri  ya mji wa Geita na mwisho wa siku kupatiwa fedha  kiasi cha  Milioni 45.

Shida Mpondi ambaye ni mkazi wa Geita,ameitaka serikali kufanya uhakiki kabla ya kutoa mikopo kwenye vikundi kwa maana ya kujildhihirisha na kujua shughuli ambazo vikundi vinafanya kazi za ujasiriamali ili kuepukana na utapeli wa namna kama hiyo iliyojitokeza.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola amekiri kupokea malalamiko dhidi ya kikundi hicho huku akisema kwamba Katibu wa Kiwage amekuwa akiwatishia wanakikundi wenzake wanapohoji fedha walizokopeshwa.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti amejibu  tuhuma za kuhusihwa na kikundi hicho kuwa ni mmoja wa watu aliyekipigia chepuo ili kurudisha fadhila katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015 jambo ambalo amesema sio sahihi kwani fedha hizo wamekuwa wakikopesha kwa vijana na vikundi ambavyo vimekidhi vigezo pasipo kubagua itikadi ya vyama vya siasa.


Hata hivyo mtandao huu  umewatafuta wahusika akiwemo mwenyekiti na Katibu wa kikundi hicho kwa njia ya simu na simu zilikuwa zikiita bila majibu  huku ofisi za kiwage zikiwa zimefungwa kwa takribani miezi mitano sasa. 

MWILI WA MAREHEMU LULU SYLVESTER MATTUNDA LEMA WAWASILI KIJIJINI NRONGA KWA MAZISHI

Waombolezaji wakiwa wamebeba  jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro  Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018.

 Marehemu Lulu  Sylvester Mattunda Lema.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


 Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Bararara ya Tanga


 
Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo
 Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo  Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo

 Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza  jambo baada ya mwili wa  marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema ulipowasili katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro  Januari 25, 2018 kwa taratibu za mazishi yanayofanyika leo  Ijumaa Januari 26, 2018 saa Nane Mchana, katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema, "Katika mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyotamka ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha mimi na wewe Lulu,hivyo ahadi hiyo umeitimiza.

 "Profesa Lema pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa maisha yake yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana.

Wapendwa niseme nivile tunauona msiba tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu wanashughulika kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa hali na mali.

Na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka ndani na nje ya nchi naomba 

kuwashukuru sana kwaniaba ya ushirika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani pasipo amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali  afya imetoweka na huu mwaka nimzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.

ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA YA MWAKA 2017


Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) akiongea na Waandishi wa habari wa radio Times Fm wakati akitoa taarifa ya Mafanikio ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2017, kabla ya kukabidhiwa Tuzo na Cheti cha heshima kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo, Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akitoa pongezi na shukrani kwa Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo na cheti cha heshima kwa kutambua utendaji kazi wa jeshi hilo (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.

Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko akipokea Tuzo ya heshima toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa kutokana na utendaji kazi wa Jeshi hilo kwa jamii na Taifa kwa ujumla (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Picha ya Pamoja, Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (wa nne kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kulia kwake) na (kushoto kwake) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

LUKUVI AJA NA MAAMUZI HAYA JIJINI MWANZA

WANANCHI wanaomiliki nyumba 664 katika mitaa ya Kigoto na Kabuhoro katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.

Pia wamezuiwa kujenga nyumba nyingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.

Akizungumza na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.

 Amesema serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza) majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa fidia.

“Nimekuja kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema Lukuvi.

Waziri huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi hiyo ya serikali.

Lukuvi alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha Polisi wanamaji, nyumba za askari, gati la boti na meli za doria zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba za hoovyo hovyo.

“Miaka 70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?

Aidha akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde eneo lake.

Pia alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo na uheshimiwe.

Thursday, January 25, 2018

JEMBEKA NA KILIMO.VIJANA 6 wilayani #igunga wanaolima kwa kikundi huku wakicheza ngoma, wanapiga mzigo balaa. 

Baada ya mahojiano na #KAZINANGOMA niliwauliza, "kundi lenu linaitwaje....!!?" Wakasema ingawa wako kipindi kirefu katika kilimo wakilima mashamba ya wananchi kwa malipo ambayo kwayo wametengeneza ajira, lakini bado kundi lao hawajalipa jina....... Nikawaambia "Hamuwezi kwenda hivi hivi bila ya kuwa na jina la kundi watu watawatambuaje..!" Na ndipo wakanipa fursa niwachagulie jina.

Bila ajizi nikawabatiza kwa MAJI YA MOTO kundi lao nikalipa jina JEMBEKA NA KILIMO (ikiwa na maana 'fanya kilimo kama burudani ingawa inatupa pesa'. 

Wao wanafurahia sana kazi hii, kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tisa wanauwezo wa kulima hekari 4, na kwa kila hekari moja gharama ya kulima au kupalilia ni shilingi elfu 15,000/= top... Haina mjadala. .

Hivyo wana uhakika wa kutoka na Tsh 45,000/= kwa siku. .

Jeh huoni kuwa hii itahamasisha vijana wengi kuwekeza kwenye ajira za kilimo kuliko kubanana na ajira za maofisini?..........
CC:- @jembenijembe @paulmakonda @eddievied @gijegije @mansourjumanne @deejaykflip @prince_nzwalla @johnjackson_jj @djmike_beatz @chrissthedj @djscopion @deejay_jacko @mustafakinkulah @johangasa4 @harith_jaha

DC MJEMA, AKAGUA UKARABATI MAJENGO SHULE ZA JANGWANI NA AZANIA, LEO. WALIMU NA WANAFUNZI WAMSHUKURU RAIS DK. MAGUFULI, WASEMA AKIAHIDI ANATEKELEZA

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Sopphia Mjema akipozi kwenye kitanda alipotembelea Shule ya sekonari ya Jangwani, kukagua maendeleo ya ukarabati wa majengo unaogharamiwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Dk. John Maguduli katika shule hiyo na shule ya Azania, jijini Dar es Salaam, leo. DC Mjema alitumia kitanda hicho wakati akisoma katika shule hiyo miaka zaidi ya 30 iliyopita.
 Mkuu wa shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akimpokea DC Mjema kuka alipowasili kwenye shule hiyo. 
 Mkuu wa Shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akieleza taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo ulipofikia sasa ambapo amesema umekamilika kwa kiasi cha asilimia 90. Kulia ni Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo na katikati DC Mjema
Ofisa wa Wakala wa majengo akimpatia maelezo DC Mjema kuhusu mradi huo wa ukarabati wa vyoo kwenye majengo ya shule ya jangwani. Kulia ni Edward Mpogolo
Moja ya vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema (kushoto) akizunguma alipokuwa akikagua chumba cha darasa kilichokarabatiwa
Mwalimu wa somo la fizikia wa kidato cha nne Felix Sameli akifundisha darasani muda mfupi kabla ya DC Mjema kuingia katika darasa la kidato hicho.
DC Mjema (kulia) akisalimiana na wanafunzinwa Kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Jangwani akiwa katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya ukaranbati wa majengo
DC Mjengwa akiwa na mwanafunzi wa kidato hicho  sabrina Saidi ambaye alikuta anakaa kwenye dawati alilokuwa akitumia wakati wakisoma katika shule ya Jangwani zaidi ya miaka 30 iliyopita.
DC Mjema akiwaonya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Jangwani kutojiingiza katika mambo ya utukutu ikiwemo kupata mimba wakiwa bado masomoni na badala yake wazingatie masomo kwa bidii.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa shule hiyo kukagua mabweni ya wasichana yaliyokarabatiwa.
DC Mjema akihoji jambo alipokagua vyoo ambavyo ukarabati wake unaendelea katika shule hiyo.
"Hivi hii milango metengenezwa kwa mbao aina gani?" DC Mjema akahoji alipokagua ukarabati wa vyoo katika shule hiyo.
DC Mjema akijaribu kuhakikisha kama maji yanatoka kwenye bafu alipokagua ukarabati wa vyoo kwenye eneo la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akionyeshwa sehemu ya wanafunzi kulia chakula ambayo bado ukarabati wake haujakamilika katika shule hiyo ya Jangwani.
baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji maalum wakiwa darasani katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema kabla ya kuondoka akakagua ukarabati wa chumba cha maabara katika shule hiyo
"Sasa chumba kama hiki cha maabara kinatakiwa kuwa na umeme muda wote" akasema DC Mjema.
Ofisa wa wakala wa Majengo akitoa maelezo ya mwisho kabla ya kuondoka DC Mjema kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akizungumza na waandishi wa habari alichoshuhudia na maoni yake baada ya kukagua ukarabati wa majengo kwenye shule hiyo ya Jangwani. " Nimerishwa sana na ukarabati uliofanyika, Walimu, wafanyakazi wa kawaida na wanafunzi hakikisheni mnaitunza miundo mbinu hii ilivyokarabatiwa na kuwa mizuri. namshukuru na kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa uamuzi wake wa kuielekeza serikali kukarabati shule hizi" Alisema DC Mjengwa.
DC Mjengwa akizungumza na wanafunzi aliowakuta wakijisomea kwenye viwanja vya shule ya Jangwani wakati akienda shule ya Azania kuendelea na ukaguzi wa ukarabati wa majengo pia katika shule hiyo.
DC Mjema akizungumza na wanafunzi katika shule ya Azania.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa Shue ya Azania Erasto Gwimile (kushoto), kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya majengo yaliyofanyiwa ukarabati katika shule hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (katikati) akiinama wakati wakienda kukagua ukarabati katika moja ya madarasa ya shule hiyo ya Azania.
DC Mjema akikagua vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shue hiyo ya Azania.
DC Mjema akizungumza wakati akikagua mabweni katika shule hiyi=o ya Azania. Alishauri kuwekwa milango ya dharula kuwezesha wanafunzi kutoka kwa urahisi wakati wa majanga kama ya moto, badala ya kutegemea kutoka katka milango yenye vizuizi vingi kama mageti.
DC Mjema akimpa pole mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Azania Enock Michael ambaye alimkuta amelala bwenini kutokana na kuwa na homa.
Mkuu wa shule ya Azania akitoa maelezo kuhusu ukarabati wa moja ya vyumba vya madarasa.
DC Mjema na msafara wake wakiendelea na ukaguzi
DC Mjema akiwa katika chumba cha darasa kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Azania. Kulia ni Edward Mpologo na kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Erasto Gwamile.
DC Mjema akizungumza nao
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Azania Goodlove Kapufi akizungumzia ukarabati wa majengo ya shule yao. " kwa niaba ya wenzangu tunamshukuru sana Rais Dk Magufuli kwa kuelekeza ukarabati huu ufanyike, tunasema asante sana," alisema. Makamu huyo wa Rais.
Katibu Tawala wa Ilala akimsalimia Makamu huyo wa Rais wa Serikali ya Wafnafunzi wa shule ya Azabia
Mkuu wa Shule ya Azania Erasto Gwimile akisoma taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule, alisema ukarabati ulichelewa kukamilika kwa wakati hivyo kusababisha shule kuhelewa kufunguliwa.
DAS wa Ilala Mpogolo akiwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Azania.
Mkuu wa Shule ya Azania akimshukuru DC Mjema kwa kutembelea shule yao
DC Mjema akizungumza na baadhi ya wanafunzi za shule ya zanaki wakati ameketi nao kwenye dawati

DC Mjema akiagana na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Azania
DC Mjema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi katika msafara wake na baadhi ya viongozi wa shule hiyo ya Azania kabla ya kuondoka mwishoni mwa ziara yake.
DC Mjema akiagana na Mkuu wa Shue ya Azania  Erasto Gwamile baada ya ziara yake ya kukagua ukarabati wa majengo katika shule hiyo leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO