ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 23, 2023

RC PWANI AWAFUNDA VIONGOZI WA KIBAHA TC KUITENDEA HAKI HATI SAFI WALIYOIPATA

 

Na Victor Masangu,Kibaha 


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge amewataka viongozi wa halmashauri ya mji Kibaha licha ya kupata hati ya ukaguzi iliyoridhisha (Hati safi) wasibweteke na badala yake wanapaswa kutatua kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Kunenge ametoa kauli hiyo wakati wa Baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya Kibaha mji lilioandaliwa kwa ajili ya kujadili taarifa ya utekelezaji wa hoja ya ukaguzi na taarifa ya hati ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka wa fedha 2021/2022.


Katika kikao hicho ambacho kilihudhuliwa na na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) wakuu wa idara,watendaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa,wakaguzi wa hesabu,pamoja na Mkuu wa Mkoa ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

Kunenge alisema kuwa upatikanaji wa kupata hati safi ni hatua nzuri lakini inapaswa iendane na kwenda sambamba na kuwahudumia wananchi kwa vitendo katika Mambo mbali mbali ikiwemo upatikanaji wa huduma ya maji safi na salamà,kuboresha hali ya elimu,afya pamoja na maeneo mengine ili kulete tija zaidi.


"Nimeona taarifa yenu ya kupata hati safi katika halmashauri ya mji kibaha,mimi nawapongeza sana kwa hatua hii lakini hatuwezi kufurahia kupata tu hati safi wakati wananchi wetu katika maeneo mbali mbali bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ni vema viongozi na watendaji tufurahie kupata hati lakini tutatue na kero za wananchi wetu waweze kupata huduma zinazostahili,"alisema Kunenge.


Kadhalika aliwawataka viongozi wote wa halmashauri kuweka mipango mikakati mizuri ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kujibu hoja zote zilizotolewa katika taarifa ya utekelezaji ili kuweza kuzifunga kwa wakati ili kuondokana na dosari zilikuwepo.


Aliongeza kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi wote katika ngazi zote kwa lengo la kuweza kuufanya Mkoa wa Pwani uweze kuendekea kuwa kinara zaidi katika suala zima la  uwekezaji  wa ujenzi wa  viwanda na kwamba kunatakiwa kuachana kabisa na kuwepo kwa migogoro ya ardhi.


"Hivi karibuni Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan alitupongeza kwa dhati katika Mkoa wetu wa Pwani kuwa kinara katika uwekezaji wa viwanda kwa hiyo sisi tunapaswa kuweka mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji ikiwemo kuhakikisha tunatatua migogoro ya ardhi katika maeneo yetu,"alisema Kunenge.

Awali kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha mji Mhandisi Mshamu Munde alibainisha kwamba kwa kipindi kinachoishia juni mwaka 2021 halmashauri ilikuwa na mapendejezo ya hoja zipatazo 39.

Pia alibainisha kuwa taarifa ya hati ya ukaguzi wa hesabu za halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 imeweza kupata hati inayoridhisha (hati safi) ambayo imetokana baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kina katika maeneo mbali mbali.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji Mwajuma Nyamka aliipongeza halmashauri hiyo kwa kufanikiwa kupata hati safi mfululizo na kuwahimiza viongozi licha ya kupata hati hiyo wasikilize changamoto zinazowakabili wananchi ili waweze kuzitafutia ufumbuzi katka sekta tofauti.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushauri na kuahidi kuyayanyia kazi maelekezo na maagizo yote yaliyotolewa kwa ajili ya Kuhakikisha baadhi ya hoja zinafanyiwa kazi mapema na ili ziweze kufungwa.


Halmashauri ya mji Kibaha iliyopo Mkoa wa Pwani imeweza kufanikiwa kupata hati inayoridhisha (Hati safi) kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 baada ya kupokea  taarifa ya ukaguzi ya hesabu  kutolewa.

MTOTO HUYU HATARI ANACHEZA NA NYOKA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Katikati ya maonesho ya mabaharia katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza wakati burudani mbalimbali zikiwa zimetawala mioyo ya watu inatikiswa, vinweleo vinasisimshwa na kijana mdogo anayefungulia nyoka toka kwenye box la mbao na kucheza nayo ngoma, kundi laitwa Buyegu toka Kisesa wialayani Magu.

KITUO CHA STERM PARK CHATUMIA WIKI YA SAYANSI AFRIKA KUTOA MAFUNZO YA HISABATI,TEKNOLOJIA N UHANDISI KWA WANAFUNZI 350 JIJINI TANGA

 

Meneja wa Kituo cha Sayansi cha Sterm Park Max George akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani

Wanafunzi wa shule za Msingi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini mafunzo mbalimbali.

Na Oscar Assenga,TANGA

KITUO cha Sayansi cha Sterm Park cha  Jijini Tanga kimetumia wiki ya Sayansi Afrika kutoa mafunzo ya Hisabati ,Teknolojia na uhandisi kwa wanafunzi 350 wa shule mbalimbali za msingi zilizopo jijini hapa yakilenga  kuongeza ari kwa wanafunzi kupenda kujifunza masomo ya sayansi kwa malengo yao ya baadaye na kuja kulisaidia Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Sterm Park Max George amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho kimeweza kusaidia na kuongeza ari kwa wanafunzi wengi kupenda kujifunza masomo ya sayansi na hisabati hatua ambayo inaleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla juu ya kile kinachoelezwa kuwa masomo hayo ni magumu.

Alisema kuwa wanafunzi hao wa shule za msingi ambao wamejitokeza na kupata bahati ya kujifunza technologia, uhandisi pamoja na hisabati ni mwanzo wa Juni 26 hadi 30 mwaka huu ambapo kutakuwa na wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa mbalimbali ambao watajifunza teknologia ya juu kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo imekuwa ikipelekea na adha mbalimbali.

“Tumesherehekea wiki ya sayansi kwa Afrika na watoto 350 kutoka shule mbalimbali za msingi wanaopatikana hapa jijini Tanga wamejifunza juu ya maswala ya hisabati , uhandisi na techolojia kwa vitendo na katika mwendelezo wa kuhakikisha vijana wanedelea kujifunza kwa vitendo zaidi tarehe 26 hadi 30 tutakuwa na vijana wa sekondari kutoka mikoa tofauti toafauti ya Tanzanzia na wao watatengeneza projekti ambayo itakwenda kutatua changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.” Alisema Max.

Awali akizungumza Dkt. Isaya Ipiana ambaye ni balozi wa Next Einstein Forum ambao ni waandaaji wa makongamano ya sayansi Afrika kwa wakishirikiana na Sperm Parka katika mkoa wa Tanga amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika sekta ya elimu ikiwemo miundombinu na mabadiliko ya sera ambapo ameiomba serikali kuzidi kuboresha sekta hiyo kwa kuongeza vifaa vya kujifunza na kujifunzi ili iwe rahisi kwa wanafunzi kuelewa zaidi.

Aidha alisema wanaipongeza serikali kwa kuwa imekuwa ikifanya mabadiliko katika sera mbalimbali za elimu lakini imekuwa inaruhusu wadau wanohusika na masuala ya elimu kufanya kazi katika mazingira mazuri hivyo wao kama wadau wataendelea kuhakikisha wanasonga mbele

Kituo hicho cha Sterm Park kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Tanga june 23 imeandaa tuzo maalum ambazo watatrunukiwa walimu wa kike wanaofanya vizuri katika masomo ya hesabu pamoja na sayansi hii ikilenga hasa kuongeza hamasa kwa walimu kuongeza molari ya kufanya kazi na wanafunzi kupenda na kuwa mabalozi kwa wengine juu ya masomo ya sayansi na hisabati .

Thursday, June 22, 2023

ONYO KWA WANAOPOTOSHA NENO 'UBAHARIA'

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Jamii imeaswa kujiepusha na matumizi mabaya kwa neno 'Baharia', rai hiyo imetolewa hii leo na Waziri wa Ujenzi na uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe.Suleiman Masoud Makame wakati akifungua wiki ya Maonesho ya Siku ya Mabaharia Duniani kitaifa inayofanyika katika Viwanja vya Furahisha vilivyopo Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza. #mwanza #samiasuluhuhassan #kaziiendelee #SikuYaMabahariaDuniani

















KIJANA ALIYEMWIGIZA HAYATI MAGUFULI UZINDUZI SIKU YA MABAHARIA DUNIANI ATIKISA MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Akiigiza kwa ufundi sauti za baadhi ya viongozi wakuu waliopita katika awamu mbalimbali za uongozi nchini Tanzania, kijana Amran Mzalendo amesisimua adhira iliyohudhuria maonesho ya siku ya Mabaharia Duniani yanayoendelea katika Viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza yakitarajiwa kuhitimishwa Jumapili ya Tarehe 25 Juni 2023. Sikiliza ufundi wake kisha twambie wampa asilimia ngapi!!

Wednesday, June 21, 2023

DC MOYO AONDOA SINTOFAHAMU KATIKA MLIMA CHILALO

 

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mbute juu ya sintofahamu ya uchimbaji wa madini katika mlima Chilalo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwasikiliza wananchi wa Kijiji cha Mbute wakati wa kuondoa hofu kuwa Mlima Chilalo upo wilaya ya Ruangwa

Na Fredy Mgunda, Nachingwea

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amefanikiwa kuondoka sintofahamu kwa wananchi wa Kijiji cha Mbute iliyokuwa imetanda juu ya uchimbaji wa madini ya Graphite  katika mlima Chilalo.

Akizungumza wakati alipofanya ziara katika Kijiji hicho baada kusambaa Kwa video ikionyesha malalamiko ya wananchi juu mlima na msitu wa akiba wa Chilalo kuonekana upo katika wilaya ya Ruangwa na sio Nachingwea.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo aliwaeleza wananchi kuwa Mlima Chilalo upo wilaya ya Nachingwea na kila shughuli inayofanywa kwenye Mlima huo mapato yote yatakuwa ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea.

Moyo aliwatoa hofu hiyo kwa kuwaambia suala la mipaka linashughulikiwa na serikali ya mkoa wa Lindi kwa ofisi ya wilaya ya Nachingwea ilifanya kazi mgogoro huo ila bado upande wa mkoa na kuhaidi hivi karibuni wataalam kutoka TAMISEMI na ofisi mkoa watafika eneo hilo kutatua mgogoro huo.

Kwa upande wake Afisa madini mkazi mkoa wa Lindi Eng Dickson Joram alisema kuwa leseni iliyotelewa katika eneo la Mlima Chilalo ni leseni ya utafiti na sio ya kuchimbwa kwa madini ya Graphite katika eneo hilo.

Eng Joram alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuondoa hofu kuwa eneo hilo limeanza kuchimbwa madini wakati sio kweli.

Nao baadhi ya wananchi walisema kuwa wanampongeza mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo Kwa kuwapeleka wataalam na kutoa ufafanuzi juu ya uchimbaji wa madini ya Graphite katika mlima Chilalo

"Tumepata ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite  Mlima Chilalo ambao umetulea hofu iliyokuwa imetanda Kwa wananchi"walisema

TANESCO KINONDONI YAWAONDOSHA WAFANYABIASHARA MLANDIZI WALIOPO CHINI YA UMEME MKUBWA

 

Na Victor Masangu,Kibaha 

Kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo kuamua kufanyia biashara zao chini ya nyaya kubwa za umeme hali ambayo inahararisha zaidi usalama wa maisha yao kwani kufanya hivyo ni kinyume kabisa na sheria na taratibu zilizowekwa.

Katika kuliona hilo na kulitafutia ufumbuzi suala hilo Shirika la umeme (Tanesco) Mkoa wa Kinondoni kusini limefanya ziara maalumu ya kutoa elimu na kuwataka  baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la mlandizi na maeneo mengine Wilayani Kibaha kuondoa biashara zao ambazo wanazifanyia chini ya miundombinu ya Tanesco.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Kinondoni Kusini Lilian William wakati wa zoezi la kuwaondoa baadhi wafanyabiashara wa eneo la mlandizi sokoni ambao wamekuwa wakiendesha shughuli zao chini line kubwa za umeme.

"Tupo katika zoezi la kuwaondosha baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hili la mlandizi sokoni kwani wanafanya makosa kutokana na kufanya biashara chini ya miundombinu ya line kubwa ya umeme kwa hiyo hii ni hatare sana kwa usalama wao kwani nyaya zinaweza kukatika,"alisema Lilian.

Aidha afisa huyo alibainisha kwamba wafanyabiashara hao wanapaswa kutambua kuendesha shughuli zao chini ya line kubwa ya umeme wanaweza kusababisha madhara makubwa pindi litakapokuja tatizo la nyanya kukatika hivyo ni vizuri wakahama na kutafuta maeneo mengine.

"Sisi kama Tanesco tutaendelea kuwaelimisha wafanyabiashara kuachana kabisa na kufanya biashara zao na pia tutawaondosha wote maana hii line yetu kubwa ya umeme kutokea Dar es Salaam hadi morogoro tumebaini kuwepo kwa maeneo watu wanavunja sheria ya kupanga hata bidhaa zao,"alifafanua Lilian.

Katika hatua nyingine aliwataka kuhakikisha wafanyabiashara wote kuzingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa na kwamba hawatasita kuwachukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwa Upande wake msimamizi wa njia kuu za kusafirishia umeme kanda ya Dar es Salaam Juma Sungura alisema kuwa kwa sasa wamejipanga katika kuilinda miundombinu hiyo ya umeme ili kuepukaba na madhara ambayo yanaweza kujitokeza kwa wananchi.

Nao baadhi ya wananchi wanaoishi katika eneo la  mlandizi Wilayani Kibaha walisema kuwa kufanya biashara chini ya nyaya kubwa za umeme ni hatari kwa maisha yao hivyo wanapaswa kutafutiwa maeneo mengine ambayo yatakuwa ni rafiki zaidi kwa biashara zao.

Monday, June 19, 2023

MWANAMKE ALIYEFUFUKA SIKU YA MAZISHI YAKE AFARIKI DUNIA BAADA YA SIKU 5


Mwanamke mwenye umri wa miaka 76, kutoka Ecuado amefariki dunia wiki moja baada ya kutangazwa kufufuka siku ya maziko yake.

Katika tukio hilo, Bella Montoya alishangaza jamaa zake waliokuwa wanamuomboleza kwa kugonga jeneza lake mwenyewe wakati wa ibada yake ya mazishi.

 

Baada ya kufungua jeneza, waombolezaji walishangazwa kuona kwamba mama huyo mzee bado yuko hai na haraka wakamrudisha hospitalini.

 

Walakini, hali yake ilikuwa bado mbaya. Wiki moja baada ya kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi, Wizara ya Afya ya Ecuador ilitangaza muuguzi huyo mstaafu aliyefufuia alifariki kutokana na kiharusi.

 


"Wakati huu, mama yangu alikufa kweli. Maisha yangu hayatakuwa kama zamani," alisema Gilbert Barbera, mtoto wake Montoya, kama alivyonukuliwa na BBC.

 

Tukio hilo la kushangaza limesababisha serikali kufanya uchunguzi kuhusu hospitali iliyohusika, likiibua maswali kuhusu taratibu za matibabu na usahihi wa vyeti vya kifo.

 

Kamati ya kiufundi ilibuniwa kuchunguza jinsi hospitali inavyotoa vyeti vya kifo, ilisema taarifa kutoka wizara hiyo.

 

Montoya alikuwa amelazwa hospitalini tarehe Ijumaa, Juni 9, kwa uwezekano wa kupatwa na kiharusi na kusimama kwa moyo na mapafu, na baada ya kushindwa kujibu jitihada za kumrejesha kwenye hali ya uhai, daktari aliye kuwajibika alitangaza kifo chake, ilisema wizara hiyo.

 

 Baadaye, familia ilimpeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti na ilikuwa ikifanya shughuli za mazishi wakati walipoanza kusikia sauti za ajabu.

JAMAA AKAMATWA KWA KUMPIGA MBWA NA KUMFANYA KULAZWA KATIKA ICU


Mbwa mwenye umri wa miaka 15 anapigania maisha yake katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) baada ya kushambuliwa kwa ukatili na mtu mwenye umri wa miaka 39, ambaye anaishi mitaani mjini Venice.

 

Katika tukio hilo lililotokea Jumatano, Juni 14, inasemekana Michael Langman alimpiga mbwa, anayejulikana kama Bart, kwa nguvu na kumfanya aruke na kugongana na kucha ya chuma ya trekta ya bobcat ambayo wafanyakazi wa jiji walitumia kurekebisha barabara.

 

mbwa wa kizazi cha Yorkshire Terrier alipoteza fahamu baada ya kupigwa na akarudishwa katika hali ya kuishi na mwanamaji wa zamani ambaye, kwa bahati, alikuwa akitembelea eneo hilo.

Hadi Jumamosi, Juni 17, mbwa huyo alikuwa ameimarishwa lakini hakuweza kusimama mwenyewe.

 

Inaaminiwa kuwa alipata jeraha la ubongo la kutokana na mshtuko. Jirani ya Michele, Laura Rosenfield, mmiliki wa Bart, ameanzisha akaunti ya GoFundMe ili kukusanya fedha za kufadhili matibabu ya mbwa huyo.

 

 Mashahidi walimfuata Langman na kumshikilia mpaka polisi walipofika na kumkamata

 

Polisi wanaochunguza tukio hilo wamepata kamera za usalama zikionyesha mbwa akipigwa, ambazo zitatumika kama ushahidi. Pia, mtu huyo ameshitakiwa kwa kumpiga mtu kichwani na chupa ya glasi.

 

 Kwa sasa, amewekwa rumande bila dhamana