Mwanamke mwenye umri wa miaka 76, kutoka Ecuado amefariki dunia wiki moja baada ya kutangazwa kufufuka siku ya maziko yake.
Katika tukio hilo, Bella Montoya
alishangaza jamaa zake waliokuwa wanamuomboleza kwa kugonga jeneza lake
mwenyewe wakati wa ibada yake ya mazishi.
Baada ya kufungua jeneza, waombolezaji
walishangazwa kuona kwamba mama huyo mzee bado yuko hai na haraka wakamrudisha
hospitalini.
Walakini, hali yake ilikuwa bado mbaya.
Wiki moja baada ya kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi, Wizara ya Afya
ya Ecuador ilitangaza muuguzi huyo mstaafu aliyefufuia alifariki kutokana na
kiharusi.
"Wakati huu, mama yangu alikufa
kweli. Maisha yangu hayatakuwa kama zamani," alisema Gilbert Barbera,
mtoto wake Montoya, kama alivyonukuliwa na BBC.
Tukio hilo la kushangaza limesababisha
serikali kufanya uchunguzi kuhusu hospitali iliyohusika, likiibua maswali
kuhusu taratibu za matibabu na usahihi wa vyeti vya kifo.
Kamati ya kiufundi ilibuniwa kuchunguza
jinsi hospitali inavyotoa vyeti vya kifo, ilisema taarifa kutoka wizara hiyo.
Montoya alikuwa amelazwa hospitalini
tarehe Ijumaa, Juni 9, kwa uwezekano wa kupatwa na kiharusi na kusimama kwa
moyo na mapafu, na baada ya kushindwa kujibu jitihada za kumrejesha kwenye hali
ya uhai, daktari aliye kuwajibika alitangaza kifo chake, ilisema wizara hiyo.
Baadaye, familia ilimpeleka katika chumba cha
kuhifadhia maiti na ilikuwa ikifanya shughuli za mazishi wakati walipoanza
kusikia sauti za ajabu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.