ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 7, 2013

SERENGETI FIESTA 2013 JIJI LA MBEYA USPIME

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisi jukwaani huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine.
Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu.

 Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya
 Mama wa miduara ya Kibongofleva,Shilole akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
 Sehemu ya umati wa watu.
Mkali mwingine wa hip hop (bongofleva),Ney wa Mitego akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine,mjini Mbeya.
 Wakazi wa jiji la Mbeya wakitoa heshima kwa baadhi ya wasanii waliotangulia mbele za haki, kwa kuwasha tochi za simu zao usiku huu.
 Rich Mavoko na skwadi lake wakilishambulia jukwaa. 
 Shilole akiimba jukwaani.
Wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop,Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine usiku huu.
 Ni shangwe tu kwa wakazi wa jiji la Mbeya usiku huu ndani ya uwanja wa Sokoine. 
Mmoja wa sanii mahati wa kizazi kipya,Ommy Dimpo akiwaimbia mashabiki wake singo yake mpya iitwayo Tupogo usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
 MKali wa kukamua mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwarusha maelfu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wanaondelea kumiminika kwenye uwanja wa Sokoine usiku huu.
Msanii aliyewahi kulwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu,pichani akitumbuiza mbele ya mashabiki wake.
Baadhi ya watu wakifuatilia yanayojiri usiku huu kwenye tamasha la Seremgeto Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Mkali wa Mahaba,a.k.a tajiri wa Mahapa kutoka mwambao wa Pwani,Cassi Mganga akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine mkoanni Mbeya.Picha na Michuzi Media Group-Mbeya.

JAKAYA AZINDUA KITUO CHA AFYA LUGEYE WILAYANI MAGU - APATA MAPOKEZI YA NGUVU

Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye helkopta ya jeshi la polisi kufanya ziara yake wilayani Magu ambapo alipata mapokezi ya kutosha wilayani humo kuanzia kata hii ya Lugeye..

Rais Kikwete akiwa na wenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt Anthony Diallo (mbele) na Mkuu wa  Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (kushoto).

Maelfu ya wananchi wamefurika kwenye kiwanja hiki kumpokea Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipokewa na ngoma za asili kwenye uwanja wa eneo la Zahanati ya Lugeye ambayo alifika kuifunguwa. 

Burudani zaidi.

Wengi walimuona.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la Zahanati ya Lugeye iliyoko wilayani Magu mkoani Mwanza.

Na sasa utepe kwaajili ya kuruhusu rasmi huduma kuendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akikaguwa wodi mbalimbali za Zahanati ya Lugeye.

Moja ya Vitanda. 

Hatua kwa hatua ndani ya Zahanati hii ya Lugeye.

Jk amesema kuwa sera ya Afya nchini inasema kuwa Serikali itahakikisha kuwa kila kijiji na kata inakuwa na Zahanati yake na hizi ni hatua. "Tutaendelea kukihudumia kituo hiki cha afya kwa kukipatia X-Ray pamoja na gari la wagonjwa kwa huduma za rufaa.

Hapa kulikuwa na jambo la furaha zaidi...

Mara baada ya kuzindua kituo hiki Mhe. Rais alisalimiana ana kwa ana na wananchi wake.

Hatua kuelekea majukumu mengine ya ziara.

Maandari ya kata ya Lugeye.

SAMSUNG YALETA UHAKIKA NA MFUMO WA “E-WARRANTY”.

Meneja wa mauzo na usambazaji wa kampuni ya Samsung , Silvester Manyara,  Bakari Maggid toka bodi ya michezo ya kubahatisha na meneja mwakilishi wa Samsung nchini Kishor Kumar wakiwa wameshika baaadhi ya bidhaa za kampuni hiyo zinazotolewa kwa washindi wa droo inayofanyika kila mwezi.
Mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Bakari  Maggid (kushoto) akifurahia jambo na Meneja wa mauzo na usambazaji wa kampuni ya Samsung , Silvester Manyara na meneja mwakilishi wa Samsung nchini, Kishor Kumar wakati wa droo ya mshindi bidhaa za Samsung iliyochezeshwa jana katika duka la kampuni hiyo lililopo Uchumi Plaza, barabara ya Nyerere. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Toleo La leo;

SAMSUNG YALETA UHAKIKA NA MFUMO WA “E-WARRANTY”.
 “Mfumo wa E-Warranty yawasaidia wateja wa Samsung kishinda zawadi mabalimali”

Alhamisi, Septemba 5  2013;

Dar es SalaamKwa mara nyingine tena Kampuni ya Samsung Tanzania imechezesha droo ya mfumo wake wa “E-Warranty”, washindi walitangazwa katika hafla iliyoandaliwa katika Ofisi zao katika Barabara ya Pugu. Mfumo huu wa “E-Warranty ni mbinu inayotumiwa na Kampuni ya Samsung kama jinsi ya kukumbana na bidhaa feki zinazopatikana kwenye soko la Tanzania.

Mfumo huo wa e-warranty unawasaidia wateja kujua kama simu ya Samsung ni halali au ni feki. Wateja wanapaswa kusajali simu zao pale wanapozinunua na hivyo kupata dhamana ya miezi 24.
Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Bwana Kishor Kumar akizungumuza na waandishi wa habari alisema “Mfumo wa E-Warranty imeonyesha kwamba ni mbinu bora zaidi dhidi ya kukumbana na bidhaa feki kwani wateja wengi wanasajili simu zao. Tunawahimiza wateja wetu  waendele kutuunga mkono kwa kununu bidhaa bora na kuzisajili na hivyo kupata nafasi ya kujishindia bidhaa kabambe za Samsung katika droo zetu”.

Washindi wanaweza kushinda zawadi 1 kati ya hizi 10: Televisheni 1 aina ya LED ya inchi 32, laptop 1, Kamera 3, home theatre 3 na simu 2 aina ya Galaxy Grand.

Bwana Kumar aliendelea kusema “ Licha na kujua kama simu mteja anayotaka kununua ni bora au feki, mfumo wa e-warranty unawasiadia wateja kujua kama simu hiyo inadhama ya miezi 24, kama simu hiyo inatafutwa au imeibiwa na kama simu hiyo ni mpya au imeshatumika”.

Kujua kama simu ni halali, mteja anatakiwa kufuta maelekezo yafuatayo: Tuma ujumbe na neno ‘Check’ ikifuatiwa na alama ya nyota(*) kisha namba ya IMEI, ikifuatiwa na alama ya reli (#) na kutuma kwa namba ‘15685’. Ujumbe unatumwa moja kwa moja kuelezea hadhi ya simu hiyo ya Samsung.

“Mfumo huu wa e-warranty ulianzishwa haswa kukabiliana na changamoto moto inayoikumba soko la simu za mkononi huku Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo kuna simu nyingi ni za bandia, za wizi, zilizotumika na simu ambazo hazina dhamana”, alisema Bwana, Kumar.

Bwana Kumar alimaliza kwa kusema ‘ili kuboresha huduma zetu za mfumo wa e-warranty, wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy S 4 (iliyozinduliwa mwezi huu jijini Dar es Salaam), watapata huduma mpya inayoitwa ADH. ADH (Accidental Damage from Handling), ni huduma inayoilinda simu hiyo ya S 4 kutoka uharibifu kutokana na matumizi ya kawaida’.

Ilikujiunga na huduma ya ADH, wateja wanatakiwa kujisajili na mfumo wa e-warranty na usajili untakiwa kufanywa ndani ya siku 30 tangu kununuliwa kwa simu. Athari ya kutokujiunga na mfumo wa e-warranty kwa muda unaotakikana ni kwamba simu hiyo ya S4 haitaweza kutengenezwa kwa bure pale ambapo itaharibika.

MBEYA WAANZA RASMI FAINALI ZA SAFARI POOL TAIFA

Baadhi ya wachezaji wanaoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye maandamano kuingia ukumbini wakati wa ufunguzi wa fainali hizo zinazofanyika Airport Pub mkoani humo.
Meneja wa matukio wa TBL tawi la Mbeya, Godfrey Mwangulungu (kushoto) akizungumza nawachezaji wa Pool (hawapo pichani) wakati wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa yanayofanyika Airport Pub mkoani humo. Wengine kushoto kwake ni mratibu wa mashindano hayo, Peter Zacharia, Afisa michezo mkoa wa Mbeya George Mbijimana Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Samwel Aron.

Afisa michezo mkoa wa Mbeya George Mbijimana akizungumza na wachezaji wa Pool wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoayanayofanyika Airport Pub mkoani humo. Kulia ni Meneja wa matukio wa TBL tawi la Mbeya Godfrey Mwangulungu, mratibu wa mashindano Peter Zacharia Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Samwel Aron.


Shoot ....ya ufunguzi.
Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya george Mbijimana akipigiwa makofi mara baada ya kufungua rasmi mashindano. 

Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya mchezo wa Pool Taifa zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Safari Lager zimeanza rasmi jana Mkoani mbeya zikishilikisha vilabu tisa vya mkoani humo.

Akifungua fainali hizo Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima aliwaomba wachezaji kuwa na watulivu na kuzingatia nidhamu ya mchezo ili mwisho wa fainali apatikane mshindi atakaebeba bendera ya Mkoa wa mbeya kwenye fainali za kitaifa na arudi na ushindi.

Mbijima alisema taswila ya mchezo wa Pool si nzuri sana miongoni mwa watu kwani unatazamwa kama mchezo wa wahuni na hakuna mtu mwingine wa kubalilisha zaidi ya wachezaji wenyewe, hivyo kuweni na nidhamu ili hata jamii ifike mahala itambue kumbe pool ni mchezo kama michezo mingine.

Mbijima pia aliishukuru TBL, kupitia bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo kwani kwa kufanya hivyo inawafanya vijana kuepuka vitu vingi ikiwemo uhalifu,kukaa vijiweni bila kazi lakini sasa wananufaika  chochote  kutokana na zawadi wanazopata ukizingaatia michezo ni ajira,michezo burudabi na michezo ni kufahamiana.

Nae Meneja matukio wa TBL Mbeya,Godfrey Mwangugulu aliwatakia wachezaji michezo mema na yenye amani mwisho apatikane bingwa wa haki atakaye wakilisha vyema Mkoa wa Mbeya

Mwisho Mwenyekiti  alivitaja vilabu vinavyoshiriki fainali za Safari Pool Mkoa wa Mbeya kuwa ni Tunduma Kontena Klabu,Royal Zambezi Klabu,Royal Glass Klabu,Shooters klabu,Luanch time klabu,Mbeya snukers klabu,Kizota klabu,Makonde klabu na Terminal Stand klabu.

Zawadi  katika fainali hizo upande wa timu,bingwa atajnyakulia fedha taslimu shilingi 700,000/=,mshingi wa pili 350,000/=,wa tatu 200,000/= na wanne 100,000/ na timu nane zitakazoingia robo fainali zitapata kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 50,000/= kila moja.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles), wanaume bingwa atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/=,wa pili 250,000/=,wa tatu 150,000/= na wanne 100,000/= na upande wa kinadada bingwa atajinyakulia fedha taslimu shilingi 250,000/=,wa pili 150,000/=,wa tatu 100,000/= na wanne 50,000/=.

Fainali za mashindano hayo zinatarajiwa kumailizika mwishoni mwa wiki hii ambapo mgeni rasmi atakayefunga anatarajiwa kuwa RPC wa mkoa huo.