ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 7, 2013

JAKAYA AZINDUA KITUO CHA AFYA LUGEYE WILAYANI MAGU - APATA MAPOKEZI YA NGUVU

Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye helkopta ya jeshi la polisi kufanya ziara yake wilayani Magu ambapo alipata mapokezi ya kutosha wilayani humo kuanzia kata hii ya Lugeye..

Rais Kikwete akiwa na wenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt Anthony Diallo (mbele) na Mkuu wa  Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (kushoto).

Maelfu ya wananchi wamefurika kwenye kiwanja hiki kumpokea Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipokewa na ngoma za asili kwenye uwanja wa eneo la Zahanati ya Lugeye ambayo alifika kuifunguwa. 

Burudani zaidi.

Wengi walimuona.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la Zahanati ya Lugeye iliyoko wilayani Magu mkoani Mwanza.

Na sasa utepe kwaajili ya kuruhusu rasmi huduma kuendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akikaguwa wodi mbalimbali za Zahanati ya Lugeye.

Moja ya Vitanda. 

Hatua kwa hatua ndani ya Zahanati hii ya Lugeye.

Jk amesema kuwa sera ya Afya nchini inasema kuwa Serikali itahakikisha kuwa kila kijiji na kata inakuwa na Zahanati yake na hizi ni hatua. "Tutaendelea kukihudumia kituo hiki cha afya kwa kukipatia X-Ray pamoja na gari la wagonjwa kwa huduma za rufaa.

Hapa kulikuwa na jambo la furaha zaidi...

Mara baada ya kuzindua kituo hiki Mhe. Rais alisalimiana ana kwa ana na wananchi wake.

Hatua kuelekea majukumu mengine ya ziara.

Maandari ya kata ya Lugeye.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.