ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 10, 2017

STORI TANO ZILIZO BAMBA LEO MITANDAONI.

NO.1 Mbowe akataa wito wa Makonda.
 NO. 2 Dogo shabiki wa Sunderland Bradley Lowery mwenye umri wa miaka mitano, anayesumbuliwa na ugonjwa wa kansa kachagua kufa mikononi mwa Defoe, nae amekubali kuwepo muda wote pale akihitajika na huyo mtoto.

High risk neuroblastoma, a form of cancer which attacks the nervous system, has up to an 80 per cent relapse rate. But there is no available relapse treatment in the UK.

NO. 3 Zitto Kabwe ampiga tafu Mhe. Mbowe baada ya kuhusishwa na sakata la madawa ya kulevya kwa madai kuwa hizo ni hujuma tu za kuchafua majina ya watetezi wa wananchi..

NO. 4 Samatta afanya yake ndani ya klabu yake ya KRC Genk, atupia na kuipa ushindi timu yake hiyo.
NO. 5 Ni dhahiri kuwa taarifa hii itakuwa mwiba mwingine kwa mashabiki wa Arsenal, baada ya kocha Wenger kusaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo hadi 2019.
NA G.SENGO JEMBE FM.

MACHAFUKO YAEDELEA KUTIKISA PARIS BAADA YA POLISI KUMDHALILISHA MWAFRIKA.


Ghasia na machafuko yameendelea kuukumba mji mkuu wa Ufaransa, Paris kwa siku kadhaa baada ya kuenea ripoti kuwa maafisa wa polisi ya nchi hiyo wamempiga vibaya na baadaye kumnajisi kwa kijiti mwanaume mwenye asili ya Afrika katika viunga vya mji wa Paris.
Walalamikaji wamechoma moto shule ya chekechea, magari na mapipa ya jalala na kuvunja viyoo vya nyumba za eneo hilo.
Ripoti zinasema waandamanaji waliokuwa wanejifunga vitambaa usoni waliharibu na kuchoma moto madazeni ya magari ya watu binafsi.
Hadi kufikia jana ghasia na machafuko hayo yalikuwa yameenea katika vitongoji kadhaa vya Paris karibu na eneo la Aulnay-sous-Bois ambako inasemekana maafisa wa polisi ya Ufaransa alimpiga na kumnajisi kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyetajwa kwa jina moja tu la Theo hapo tahere 2 mwezi huu wa Februari.
Kijana huyo ambaye amejeruhiwa vibaya amelazwa hospitalini ambako amefanyiwa upasuaji. 
Ghasia na machafuko yanaendelea Paris.
Ukatili na unyama huo wa polisi ya Ufaransa umesababisha maandamano na machafuko kwa usiku kadhaa sasa kaskazini mwa Paris na viunga vyake. Waandamanaji mbali na kulaani vikali ukatili wa polisi na namna wanavyotumia vibaya mamlaka yao, wametaka uadilifu utendeke. 
Kijana Theo aliyenajisiwa na polisi ya Ufaransa akiwa hospitalini.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bruno Le Roux amesema maafisa hao wanne wa polisi wamefunguliwa mashtaka ya kufanya mashambulizi makali na kunajisi.

MFANYABIASHARA MWANZA MBARONI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA.

Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mfanyabiashara wa vipuri vya magari jijini Mwanza Kassim Hemed Hamad kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya heroine kiasi cha pinchi 240.
ZEPHANIA MANDIA, MWANZA
JESHI  la Polisi mkoani hapa, limemkamata mfanyabiashara wa spear za magari, Kasim Hemed na dawa za kulevya yanayozaniwa kuwa ni aina ya  Heroine kiasi cha kete 240, huku kiasi kingine kikikamatwa  kikiwa kimehifadhiwa kwenye chombo aina ya Ndonga.

Akizungumza na wanahabari mkoani hapa, Kamanda wa polisi Mwanza, Ahmed Msangi alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 6 usiku katika Mtaa wa Kanyerere Kata ya Butimba Wilaya ya Nyamagana.

Alisema polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo, kuwa anajishughulisha na biashara ya dawa za kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusu  tuhuma hizo.

“Wakati askari wakiendeea na pelelezi  dhidi ya tuhuma za mfanyabiashara huyo, jana polisi walipokea taarifa  kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa ameingiza mzigo mkubwa wa dawa hizo kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza,”alisema Msangi.





Alisema polisi walivyopata taarifa walianza kufuatilia  na ndipo walipo zingira nyumba yake na kumuona kupitia dirishani akiendelea kufunga dawa hizo kwenye kete ndogo ndogo na kwamba askari walipo ingia ndani mtuhumiwa alikimbiza dawa hizo chooni ili kupoteza ushahidi.

“Baadhi ya askari waliingia  ndani na kufanikiwa kukuta kete 240 zikiwa chooni zikiwa bado hazikwenda na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la choo. Asakri waliyokuwa nje walikwenda kuziba bomba la choo na kufanikiwa kukuta ndonga 2,”alisema Msangi.

Alisema kwa sasa polisi wanaendelea na mahojinao na mtuhumiwa ili kujua mtandao wake  na watu wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya Mwanza.

MBOWE AKANUSHA TUHUMA ZA HUKUSIKA KUUZA AMA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akanusha tuhuma za kuhusika kuuza ama kutumia dawa za kulevya.

TADB YAANZA KUTEKELEZA MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA MOROCCO


 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAD, Bw. Francis Assenga (Katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru (Watatu kushoto) wakiwa na wenyeji wao Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM).
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga (wa pili toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit Agricole) Bw. Jamal Eddine Wl Jamali (Katikati). Wengine ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB  Bw. Albert Ngusaru na Wakurugenzi wawili wa Benki ya Credit Agricole Bi. Dkhil Mariem (Kushoto) na Bi Leila Akhmisse (Kulia).

 Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ukipatiwa maelezo juu ya miradi ya kilimo inavyoendeshwa nchini Morocco wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga (Mwenye Kaunda Suti) na Bw. Albert Ngusaru Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha (Mwanye Daftari) walipotembelea Morocco wiki hii kuanza utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya TADB na GCAM.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw. Francis Assenga (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Credit Agricole na Tamwil El Fellah wakati walipokagua miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji katika vijiji vya mji wa Khemisset nchini Morocco jana. Kulia kabisa ni Bw. Albert Ngusaru ambaye ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB.

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit Agricole) Bw. Jamal Eddine W. Jamali (Katikati). Kulia ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB  Bw. Albert Ngusaru.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB  Bw. Albert Ngusaru (Kulia) walipotembelea Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit Agricole).



Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeanza kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Morocco wakati wa Ziara ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI alipotembelea Tanzania kwa mwaliko wa Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mnamo mwezi Oktoba 2016.

Katika kutekeleza makubaliano hayo, ujumbe wa TADB ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Francis Assenga na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru upo nchini Morocco, pamoja na mambo mengine kuainisha maeneo ambayo Benki hiyo itashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM) na kuwekeana mikakati ya utekelezaji.

Kwa mujibu wa Bw. Assenga, pamoja na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua miradi kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo Tanzania inaweza kuianzisha kwa mafanikio.

TADB imeanzishwa kwa malengo makuu ya Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

KITUO CHA RADIO SENGEREMA CHAKABIDHIWA KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA

NA OSCAR
JEMBE FM
SENGEREMA
Mkuu wa wilaya ya sengerema mh Emanueli Kipole jana amekabidhi kituo cha radio Sengererma kwa almashauri ya wilaya ya Sengerema kuratibu kituo hicho ambacho ni mali ya serikali kupitia wananchi wa wilaya hiyo.
.
Tendo hilo limefanyika katika ukumbi wa almashauri ya wilaya ya sengerema  katika kikao cha madiwani wa almashauri hiyo  kilichokaa ili kupanga bajeti ya almashauri hiyo.


Mh Kipole amesema kuwa kituo hicho ni mali ya wananchi na kutokana na michango iliyotolewa na almashauri na pia kutika wahisani mbalimbali wakati wa kuanzishwa kituo hicho na serikali haijawahi kukabidhi kituo hicho isipokuwa kuna watu wachache wamejimilikisha kituo hicho.

Inatajwa kuwa umiliki wa kituo hicho tangu mwaka 2005 ulikuwa chini ya kamati ya watu 20 ambao walikuwa wakitumia jina la Halmashauri kuomba misaada toka kwa wahisani na wafadhili mbalimbali wakitengenezamiradi na kujinufaisha ikiwa ni pamoja na kugawana faida wakati Halmashauri haiingizi chochote.

Mhe. Kipole ameunda kamati mpya ya kuiendesha redio hiyo ambapo sasa ofisi zake zinalindwa na jeshi la polisi.

Hata hivyo kikao hicho kimeshindwa kupitisha bajeti hiyo iliyopendekezwa sh 55,466,009,060/= kutokana na kuwa chini ya kiwango cha makusanyo kulingana na vyanzo vya mapato katika almashauri hiyo.

JOHN BARNES WA LIVERPOOL KUTUA NCHINI KUANGALIA KOMBE LA STANDARD CHARTERED

  Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (katikati) akiwa ameambatana na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (kulia) pamoja na Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba wakiwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumzia tukio adhimu la Benki ya Standard Chartered, Tanzania Limited kutimiza miaka 100 tangu ilipofungua milango yake nchini Tanzania kabla ya kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Sanjay Rughani kutoa risala katika sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa iadara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said (wa pili kushoto) akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa mchezaji aliyewika wa timu ya Liverpool, John Barnes ambapo wateja wa Benki hiyo watapata fursa ya kukutana na mchezaji huyo.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (wa pili kulia) akitoa baraka zake kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine (kulia) akitoa salamu za TFF kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. 
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine (kulia) akimkabidhi bendera ya TFF Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (wa pili kulia) na Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (kulia) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool akitoa uchambuzi wa timu hiyo barabara ya kuelekea Anfield wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (katikati) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (wa pili kulia) huku wengine wakishuhudia tukio hilo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine, Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said (kushoto) na Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (kulia) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool (wa pili kushoto).
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (katikati)akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine (kulia) kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (wa tano kulia) akimkabidhi zawadi Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (wa tatu kushoto) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool katika sherehe za uzinduzi huo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (kushoto) akibadilishana mawazo na Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool kabla ya kuanza kwa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi katika picha ya pamoja na timu A na B na waamuzi wa mechi hiyo ya ufunguzi wa wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi akisalimiana na vikosi vya timu A na B kabla ya kuanza kwa mechi hiyo ya ufunguzi wa wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi akibutua mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Kapteni wa timu A Majuto Omary wa gazeti la Mwananchi akiwatoka wachezaji wa timu B ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani wakati wa mechi ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mpiga picha wa Azam TV akimtoka Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani wakati wa mechi ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga akikabidhi zawadi kwa wachezaji wa timu A baada ya kuichapa bao 1-0 timu B kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi
  Kapteni wa timu A Majuto Omary kutoka  gazeti la Mwananchi akifurahia zawadi yake baada ya timu yake kuibuka kidedea dhidi ya timu B kwa bao 1-0 wakati wa mechi ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja timu A iliyoibuka kidedea dhidi ya timu B kwa bao 1-0 kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. 

Thursday, February 9, 2017

UJENZI WA JENGO JIPYA LA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (TERMINAL 3) BAADA YA AGIZO LA JPM





Shughuli za Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3) ukiendelea mbele ya Jengo jipya la Abiria kama inavyoonekana pichani kufatia ziara ya kushtukiza  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyofanya hapo jana na kutoa Maagizo kwa Mkandarasi wa Uwanja huo kuanza kazi mara moja kuanzia leo.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Moja ya nguzo katika jengo hilo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).

Sehemu ya mbele ya jengo hilo la Abiria kama linavyoonekana.

SHAMRASHAMRA ZA UZINDUZI WA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Tamasha la Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Mabalozi wa Norway na Uswisi kulia kwa Mhe Simai ni Balozi wa Uswisi Tanzania Balozi Florence Tinguely na Balozi wa Norway Tanzania Balozi Hanne Marie wakiangalia wakiangalia vikundi vya Utamaduni wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisongo leo wakiangalia burudani hizo.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni kutoka Nchini Burundi wakitowa burudani kwa Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Zanzibar kabla ya kuaza kwa maandamano ya Uzinduzi huo yalioazia katika viwanja hivyo hadi katika viwanja vya bustani ya forodhani.
Wasanii kutoka burundi wakionesha umahiri wao wa kupiga ngoma za utamaduni wa Kwao. 


Wananchi waliofika katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani wakifuatilia burudani za wasanii mbalimbali kabla ya kuaza kwa maandamano ya ufunguzi wa Tamasha la Busara Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar akitowa maelezo kwa Mabalozi wa Uswisi na Norway walipokuwa katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu wakipata maelezo ya Mnara huo

Kikundi cha Six Unity wakionesha umahiri wao wa kujenza Dance wakati wa uzinduzi huo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani.
Wasanii wakitowa Burudani katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisonge.
Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi Jangombe wakicheza ngoma ya Bomo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu kabla ya kuaza kwa maandamano ya Uzinduzi wa Tamasha la Busara Zanzibar.


Wananchi wakifuatilia burudani zilikuwa zikitolewa  na Vikundi mbalimbali vya Utamaduni vinavyoshiriki Tamasha la Busara Zanzibar.
Imeandaliwa na OthmanMapara.
Zanzinews.com.
othmanmaulid@gmail.com.