ZEPHANIA MANDIA, MWANZA
JESHI la Polisi mkoani hapa, limemkamata mfanyabiashara wa spear za magari, Kasim Hemed na dawa za kulevya yanayozaniwa kuwa ni aina ya Heroine kiasi cha kete 240, huku kiasi kingine kikikamatwa kikiwa kimehifadhiwa kwenye chombo aina ya Ndonga.
Akizungumza na wanahabari mkoani hapa, Kamanda wa polisi Mwanza, Ahmed Msangi alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 6 usiku katika Mtaa wa Kanyerere Kata ya Butimba Wilaya ya Nyamagana.
Alisema polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo, kuwa anajishughulisha na biashara ya dawa za kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusu tuhuma hizo.
“Wakati askari wakiendeea na pelelezi dhidi ya tuhuma za mfanyabiashara huyo, jana polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa ameingiza mzigo mkubwa wa dawa hizo kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza,”alisema Msangi.
Alisema polisi walivyopata taarifa walianza kufuatilia na ndipo walipo zingira nyumba yake na kumuona kupitia dirishani akiendelea kufunga dawa hizo kwenye kete ndogo ndogo na kwamba askari walipo ingia ndani mtuhumiwa alikimbiza dawa hizo chooni ili kupoteza ushahidi.
“Baadhi ya askari waliingia ndani na kufanikiwa kukuta kete 240 zikiwa chooni zikiwa bado hazikwenda na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la choo. Asakri waliyokuwa nje walikwenda kuziba bomba la choo na kufanikiwa kukuta ndonga 2,”alisema Msangi.
Alisema kwa sasa polisi wanaendelea na mahojinao na mtuhumiwa ili kujua mtandao wake na watu wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.