ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 14, 2019

WAZIRI UMMY AKANUSHA KUWEPO MGONJWA WA EBOLA NCHINI.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu, ametoa tahadhari na kuwataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na kudhibiti ili ugonjwa wa Ebola usiingie hapa nchini.

Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo wakati akitoa taarifa za uvumi wa uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini na kuwatoa hofu wananchi kuwa hakuna dalili za ugonjwa huo kuwepo licha ya kuripotiwa katika nchi jirani.

''Naomba niwatoe hofu wananchi, hadi sasa hakuna mgonjwa yoyote wa Ebola aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo'', amesema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amezitaja dalili za ugonjwa wa Ebola ambazo ni homa kali, kuumwa kichwa, kutapika na kuharisha, viungo vya mwili kuuma pamoja na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili.

Waziri Ummy ameongeza kuwa licha ya watanzania kuwa na utamaduni wa kupeana mikono ni vyema ukawekewa tahadhari ya kunawa mikono mara kwa mara.

YANGA YASHIDWA KUTAMBA NYUMBANI

 Klabu ya Yanga imetoka sare ya 1-1 na Zesco United katika mshindano ya Ligi ya Mabingwa mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

FT: Yanga SC 1-1 Zesco United

Friday, September 13, 2019

WAZIRI LUGOLA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI JIJINI DODOMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisikiliza maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kutoka kwa Mhandisi David Pallangyo (kulia), wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akikagua Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza baada ya Ukaguzi wa  Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Ramadhani Kailima.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka kukagua Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na Wahandisi wa Mradi  wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.Picha ZOTE na Wizara ya Mambo ya  Ndani ya  Nchi

WALIMU 10 MBARONI KWA WIZI WA MITIHANI KAGERA.



Na Clavery Christian, Kagera.

Jeshi la polisi mkoani Kagera linawashikilia walimu watano na wasimamizi watano wa mtihani wa darasa la saba wilayani Ngara mkoani Kagera kwa wizi wa mtihani wa darasa la

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa tukio hilo limetokea jana septemba 12/2019 majira ya saa 4:40 asubuhi katika shule ya msingi Kumunazi iliyopo katika tarafa ya Nyamihaga wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambapo majira hayo kamati yamitihani ya wilaya ilipata taarifa kuwa baadhi ya walimu wa shule hiyo wamejifungia katika nyumba moja ya mwalimu wa shule hiyo na wameiba mtihani wa sayansi na wanajaribu kuufanya kwaajiri ya kuandaa majibu ili waweze kuwapa wanafunzi wa shule hiyo ambapo kamati hiyo ilifika na kuwakuta walimu hao wakiwa na mtihani huo.

Kamanda Malimi amesema kuwa katika shule hiyo kulikuwa na mikondo mitano ambayo kila mkondo ulikuwa na msimazi ambapo jumla ya wasimamizi watano wamekamatwa na walimu watano wa shule hiyo ambao walikuwa wakijaribu kuiba mtihani huo.

Aidha kamanda malimi amesema kuwa idadi ya wanafunzi waliokuwa wameandaliwa kwa ajiri ya kupewa majibu hayo wanahifadhiwa majina yao na idadi yao kwa ajiri ya kulinda haki za watoto.

Kamanda Malimi amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na baada ya kukamilisha uchunguzi watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

FAIDA ZA KUCHEKA MARA KWA MARA KUNATIBU MENGI KWA BINADAMU


Kama wengi wetu tujuavyo, kiwango cha miaka ya kuishi hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu kimepungua sana nyakati hizi, hivyo kila tunaposherekea mwaka mpya tunasherekea pia uzee na utimilifu wa miaka yetu ya kufa, lakini hilo lisitupe hofu kwani wataalam wamegundua maajabu yapatikanayo kwa mtu kucheka.

Kwa kutambua umuhimu wa maajabu hayo nimeona ni vema nikaelezea faida za mtu kucheka. Ifahamike kuwa watafiti mbalimbali duniani wamebaini kuwa mtu anaweza kujikinga, kujiponya na magonjwa hatari ya kansa, moyo na kisukari kwa kucheka na isitoshe achekaye anatajwa kuufanya mwili wake usionekane umezeeka hata kama atakuwa na umri mkubwa.

Kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kijamii, ugumu wa maisha unaoleta msongo wa mawazo ndiyo unaotajwa kuchangia vifo vya wanadamu wengi sambamba na kufupisha umri wa kuishi. Wanasema mtu mwenye kutingwa na sononi kila mara huchoma seli nyingi muhimu katika mwili wake, hivyo kumfanya awe katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa niliyoyataja hapo juu.

Katika tafiti za hivi karibuni ukiwemo ule uliyoendeshwa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Amerika Cardiology, imebainika kuwa uhaba wa furaha hasa fursa ya watu kupata muda wa kucheka kwa siku ni moja kati ya sababu kubwa zinazochangia magonjwa hatari miongoni mwa watu wengi. Wanasema watu wengi wamechipusha vimelea vya magonjwa si kutokana na bakteria halisi bali mfadhaiko wa mioyo yao.

Kwa maana hiyo wataalam hao wameibuka na ushauri kuwa ni bora watu wakajibidisha kutafuta furaha katika maisha yao kuliko kudumu katika uhangaikia tiba ghali za dawa zinazotolewa na vituo vya afya na hospitali, ilhali mzizi wa magonjwa yao unatokana na wao wenyewe kuishi bila kicheko ambacho kinatafsiri furaha aliyonayo mtu husika (kumbuka sizungumzii kicheko cha kebehi).

Kwa mujibu wa wasomi hao imegundulika kuwa kicheko ni tiba na kinga bora ya magonjwa yanayomkabili mwanadamu yakiwemo magonjwa ya moyo ambayo ni hatari sana kwa uhai. Mtu ambaye anaweza kutumia dakika 20 kwa siku kwa kucheka, anaweza kutibu maradhi yake hata bila kumeza vidonge.


TUKUTANE JB BELMONT HOTEL TAREHE 29 SEPT 2019 TUKAPATE TIBA.

Wednesday, September 11, 2019

ALY CHOKI AFANYA JINGINE HILI.


Aly Choki Ft King Kikii & Mulemule Fbi - 2 Way Traffic

Tuesday, September 10, 2019

CWT YAWATAKA WALIMU KUTOJIHUSISHA NA UDANGANYIFU MTIHANI DARASA LA 7.

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amewataka walimu kutokujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mitihani ya Darasa la saba inayotarajiwa kuanza siku ya hapo kesho ili kuendelea kulinda hadhi ya walimu Nchi.

Mtihanin wa Darasa la Saba umepangwa kufanyika kwa kipindi cha siku mbili Septemba 11 na 12 mwaka huu kote nchini ambapo hii leo Katibu Mkuu CWT,Mwalimu Seif amezungumza na waandishi wa habari na kuwaomba waalimu kuwa waaminifu katika kipindi chote cha Mitihani.

"Tunajua moja ya kazi kubwa ya Chama cha waalimu ni utetezi,na moja ya sehemu ya utetezi ni matatizo ya ufujaji wa mitihani  ambao kimsingi wasimamizi ni walimu,sasa mimi naomba niwaambie walimu wangu kuwa kazi ya kufundisha wameimaliza wiki iliyopita,sasa hivi waache watoto wafanye mitihani,nawaomba wawe waaminifu kwenye zoezi la kusimamia mitihani"Alisema.

Aidha kufuatia baadhi ya shule za binafsi kuhusishwa katika tuhuma za kuiba mitihani Mwalimu seif ametoa wito kwa Viongozi na waalimu wa shule hizo

"Pamoja na kuwa tuna idadi ndogo ya wanachama kutoka shule za Private,niwaase tu wawe waaminifu kwani kama wakiendelea kutuhumiwa watashusha hadhi yao kwa wateja wao"Alisema.

Mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Chemba ilifutiwa matokeo ya mtihani wa Darasa la saba kwa makosa ya kufanya udanganyifu,kwa mwaka huu Kituo hiki kimezungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Semistatus Mashimba ambaye yeye amesema kuwa kwa mwaka huu wamejipanga vyema.

JAFO: UGATUAJI WA MADARAKA NI MUHIMU KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema ili Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kujiendesha lazima kuwepo na demokrasia  ambapo ugatuaji wa madaraka ni muhimu  katika  Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Ameyasema hayo leo wakati akifungua Kikao kazi  kati ya Menejimenti ya  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa na Idara maalum ya Zanznibar  kilichofanyika katika  Ofisi za OR-TAMISEMI Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema katika kuhakikisha wananchi wanapata viongozi bora katika jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI husimamia viongozi wa vijiji wasiopungua 12,000, viongozi wa Mitaa ambao wao wanapatikana katika Majiji, Manispaa na Halmashauri za Mijiambao ni zaidi ya 4000 na viongozi wa vitongoji zaidi ya elfu 64.

Amefafanua kuwa OR-TAMIEMI ni kiungo muhimu katika kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali zinazoandaliwa na Wizara zote nchini hivyo inaposhindwa kutimiza majukumu yake, kunakuwepo na ongezeko kubwa la Malalamiko kwa wananchi.

“Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ni kiungo muhimu katika Sekta zote ambapo isipotimiza wajibu wake kwa weledi haitatimiza lengo la Serikali la kuhakikisha uwepo wa maendeleo katika kila sekta nchini” Amefafanua Jafo.

Amesema kuwa OR-TAMISEMI ni watekelezaji wa Sera na miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara za Kisekta kwa kuwa ndio yenye Halmashauri ambazo hutoa huduma kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji na mtaa lengo likiwa ni kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Amezitaja Taasisi ambazo zipo chini ya OR-TAMISEMI kuwa ni elimu Kibaha ambayo inasimamia masuala ya elimu, Taasisi ya Mabasi ya Mwendokasi, Chuo cha Hombolo ambacho kinaendesha mafunzo kwa ajili ya kutengeneza watumishi watakaosimamia utendaji kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

Mhe. Jafo amesema ugatuaji wa madaraka hufanyika pia katika  Sekta ya Elimu ambapo  kazi ya Wizara ya Elimu ni kutunga Sera na miongozo mbalimbali wakati OR-TAMISEMI kazi yake ni  kusimamia miundombinu ya Elimu  kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa elimu nchini.

Hata hivyo amesema kwa upande wa Sekta ya Afya Serikali imeweza kufanya mabadiliko makubwa ambapo mpaka sasa Hospitali za Wilaya 67 zinajengwa na Vituo vya kutolea huduma 352 vimekarabatiwa na kujengwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.


Amewataka watumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Serikali za Mitaa na Idara maalum kutoka Zanzibar kujifunza kazi zinazofanywa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania Bara ili waweze kufanyia kazi yale ambayo watayapata katika kikao kazi hicho.

Wakati huohuo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewapongeza watumishi hao kwa kuamua kujifunza kuhusu ugatuaji wa madaraka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu katika majukumu ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa  na Idara Maalum  Zanzibar Mhe. Shamata Khamisi amesema kuwa lengo la ujio wao ni kubadilishana uzoefu kwa kuwa Zanzibar imeanza kupeleka majukumu kwa wananchi ikiwa ni ugatuaji wa madaraka.

Amesema kuwa kwa upande wa Zanzibar utekelezaji wa Sera ya ugatuaji wa madaraka inatakribani miaka miwili ambapo yapo mafanikio ambayo yanaonekana hivyo ni wajibu wetu kuja kujifunza zaidi  juu ya ugatuaji wa madaraka ili kuweza kuendelea  kutoa huduma bora kwa jamii.

WAJUMBE WA CCM GANGILONGA WACHANGIA DAMU NA MISAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA IRINGA.

  Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa katika zoezi la kuchangia damu katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuchangia damu
  Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa na wadau wa chama cha mapinduzi wakienda kuwajulia hali wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kuwapa zaidi mbalimbali
Diwani wa kata ya Gangilonga leonard Raphael Mgina akiwa kwenye picha ya pamojana wadau wa kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa mkoani Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRNGA.

WAJUMBE wa chama cha mapinduzi kata ya Gangilonga wamejitokeza kwa kujitolea kuchangia damu na kutoa msaada kwa wagonjwa wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa lengo la kuadhimisha Gangilonga ya kijani

Akizungumza na blog hii diwani wa kata hiyo leonard Raphael Mgina alisema kuwa katika kuadhimisha Gangilonga ya kijani kwa kujitolea damu na kuwaona wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo hapa nchini.

“Tumepita kwenye hodi kumi na tatu kuwaona wagonjwa pamoja kufanya zoezi la kujitolea damu kwa lengo la kusaidia kupunguza upungufu wa damu kwa maana mara kwa mara tumesikia hata kwenye vyombo vya habari kuwa kuna upungufu kwenye benki ya damu” alisema Mgina

Mgina alitoa rai kwa wananchi wengine kuendelea kuchangia damu kwa kuwa hakuna aijua kesho yake hivyoni muhimu kuwa na moyo wa kujitolea kutoa damu ili kupunguza upungufu wa damu uliopo katika benki za damu katika hospitali zetu zote hapa nchini.

Naye katibu wa chama cha mapinduzi kata ya hiyo Likotiko Kenyatta alisemalengo ni kuhakikisha wajumbe na wadau wa chama cha mapinduzi nikurudisha fadhila kwa jamii kama ambavyo wamefanya katika siku ya Gangilonga ya kijani.

“Leo tumekuja kufanya shughuli za kijamii, kugawa misaada pamoja nakutoa damu kwa lengo la lakukihusisha chama cha mapinduzi katika shughuli zote za kijamii na kuifanya kata ya Gangilonga kuonekana ya kijani kweli kweli” alisema Kenyatta

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa chama cha mapinduzi wa kata hiyo wamempongeza diwani wa kata hiyo kwa kuendelea kuing’alisha Gangilonga ya kijani.

VIDEO:- NAPE MNAUYE AMUOMBA MSAMAHA RAIS MAGUFULI.


Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia kuhusika kwake katika mazungumzo yasiyofaa dhidi ya Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Nape Nnauye amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo, Mhe. Nape amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kukutana nae na kumsikiliza, na pia kumsamehe kwa makosa aliyoyafanya kufuatia taharuki iliyoibuka baada ya kuvuja kwa sauti za mawasiliano yake na wanasiasa wengine wakimsema Mhe. Rais Magufuli.

“Kwa hiyo baada ya kupata fursa nimekuja nimemuona, na mle ambamo nilimkosea kama Baba yangu nimeongea nae na Baba amenielewa, ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri ambao nitaufanyia kazi na naamini baada ya hapa mambo yatakwenda vizuri, na kwa kweli kwa dhati ya moyo wangu nimshukuru sana sana, amenipa fursa kubwa, ndefu na ameongea maneno mengi kwangu na ushauri wake nimeuchukua” amesema Mhe. Nape Nnauye.

Kuhusu maendeleo, Mhe. Nape Nnauye amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema ana matumaini kuwa CCM itapata ushindi katika chaguzi kutokana na kazi hiyo.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Magufuli amesema Mhe. Nape amekuwa akiomba kukutana nae mara nyingi na tangu siku nyingi kupitia kwa watu mbalimbali wakiwemo wasaidizi wake, viongozi wastaafu na viongozi wa CCM, na kwamba baada ya kukutana nae na kumuomba radhi ameamua kumsahehe.

Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mhe. Nape Nnauye kwenda kufanya kazi za kuhudumia wananchi wa Jimbo lake la Mtama na kukitumikia vyema chama chake cha CCM.

“Yote nimesamehe, huyu bado ni kijana mdogo, ana matarajio makubwa katika maisha yake, mimi nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu kwanza ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu na tumefundishwa katika maandiko yote tusamehe saba mara sabini, kwa hiyo nimemsamehe na Mungu amsaidie katika shughuli zake akafanye kazi zake vizuri, akalee Mke wake na familia yake, akakitumikie chama, akawatumikie wananchi wa Jimbo lake vizuri, mimi nimemsamehe, labda kama yeye atakengeuka hiyo itakuwa ni juu yake, lakini mimi kutoka moyoni mwangu nimeshamsamehe na nimemsaheme kweli. Nape nenda ukafanye kazi, Mungu akujaalie” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

TANZANIA YAWEKEZEA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WATOTO NA WANAWAKE

 Dr Naftari Ng'ondi kamishina wa ustawi wa jamii nchini Tanzania  amesema serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia
 Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Tanzania waliowakilisha mkutano wa msaada wa kisaikolojoa kwa watoto uliofanyika nchi Namibia

Tumaini Godwin,Namibia.

 Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kutokomeza  ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Mtakua) ili kumaliza tatizo hilo ifikapo mwaka 2021.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Tanzania, Dk Naftari Ng'ondi amesema hayo  wakati akiwasilisha mkakati huo kwenye mkutano wa kimataifa wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto(PSS FORUM) unaofanyika Windhoek nchini Namibia.

Dk Ng'ondi amesema mkakati huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2016  umetamka wazi kuwa pamoja na mambo yote, tatizo la mimba na ndoa za utotoni linapaswa kushughulikiwa.

"Mimba za utotoni maana yake kuna ubakaji umefanyika na  kwa Tanzania hilo ni kosa la jinai, tumeimarisha sheria ya mtoto na yeyote anayekutwa na kosa la kumpa mimba mwanafunzi anafungwa jela miaka 30," amesema Kamishna huyo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Amesema mbali na sheria, wanatekeleza mkakati huo kwa kuikarisha kamati za ulinzi wa mtoto kwenye kata kwa kuzipatia nguvu ya kupokea, kuchunguza na kuchukua ikiwa ni pamoja na kufungua kesi.

Dk Ng'ondi amesema nguvu kubwa imewekwa katika kutoka  elimu kwa Jamii na vijana kupitia kampeni mbalimbali.

"Na sasa hivi tunaendesha kampeni inayoitwa Twende pamoja, tokomeza ukatili," amesema.

Awali Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Mpango wa kutokomeza mimba za utotoni, Nyaradzayi Gumbonzvanda alisema nchi za Afrika zinapaswa kufanya kampeni ya kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni linaisha.

Amesema nchi nyingi za Afrika zinakutana na changamoto ya mimba za utotoni huku umaskini ukichangia tatizo hilo.

"Tuandae mkakati ya kumalizaa tatizo,inawezekana," amesema Gumbonzvanda.

Mkutano huo unaoendeshwa na Shirika la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) umezikutanisha zaidi ya nchi 24 kutoka kusini mwa Afrika.

Monday, September 9, 2019

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ASEMA HASHTUSHWIN NA WABUNGE KUMPINGA.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema leo kwamba hashtushwi na jaribio la wabunge la kutaka kupinga mpango wake wa kuitoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano.

Kauli hiyo ya Boris ilizua mzozo bungeni baada ya kupitishwa sheria inayomtaka acheleweshe mchakato wa Brexit au atafute makubaliano mapya na Umoja wa Ulaya.

Johnson anatarajiwa kusimamisha shughuli za bunge kwa mwezi mzima kuanzia leo, baada ya pendekezo lake la kuitisha uchaguzi wa mapema kupigiwa kura ambayo huenda ikapingwa.

Brexit, mchakato wa kijiografia muhimu zaidi katika kipindi cha miongo kadhaa nchini Uingereza, bado hauna suluhisho ikiwa ni miaka mitatu tangu raia wa nchi hiyo walipopiga kura ya maoni mwaka 2016 ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

PSS FORUM YAWEKA MIKAKATI YA ULINZI KWA WATOTO AFRIKA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REPPSI Lynette Mudekunye na Mwenyekiti wa Bodi ya REPPSI Tanzania wakiwa kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia. 

Mkurugenzi Mkazi wa REPPSI Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia
 wadau na viongozi wakiwa kwenye kwenye kongamano kujadili jinsi ya kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia

 Tumaini Godwin, Namibia

 Nchi za Afrika ikiwamo Tanzania zinaweza kumaliza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ikiwa zitafanikiwa kuweka nguvu kubwa kwenye  ulinzi wao kuanzia ngazi ya familia.

Profesa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Hosea Rwegoshola amesema hayo wakati akiwasilisha utafiti wake kuhusu kuimarisha malezi mbadala ya watoto, katika mkutano wa kimataifa wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto (PSS FORUM) unaofanyika Windhoek nchini Namibia.

Profesa Rwegoshola amesema kupitia utafiti alioufanyia katika kata ya Chanika jijini Dar es Salaam, watoto wanaweza kuwa salama ikiwa ulinzi wao utaanza kuimarishwa kuanzia ngazi ya familia.

"Kwa hiyo matokeo ya utafiti wangu ni kwamba familia mbadala zinaweza kusaidia malezi ya watoto, na hizi zikiimarishwa tatizo la watoto mitaani linaweza kupungua, ukatili majumbani utakoma," amesema.

Ametaja familia mbadala kuwa ni pamoja na ndugu wa ukoo kulea watoto, walezi wakujitolewa na wale wanaorithi watoto kisheria.

Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF)nchini Namibia Rachel Odede amesema mazingira bora ya mtoto kukua ni kwenye familia.

"Mamilioni ya watoto wameachwa nyuma kwenye malezi na takwimu zinaonyesha kuwa mmoja kati ya watano analelewa bila familia, mtoto anatakuwa kukua kwa furaha," amesema Odede.

Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) Tanzania Edwick Mapalala amesema ulinzi wa mtoto unapaswa kuanzia ngazi ya familia.

'CCM SI CHAMA CHA UCHAGUZI BALI CHA KUHANGAIKA NA MAENDELEO YA WATU'



NA BALTAZAR MASHAKA, MISUNGWI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kimesema si Chama cha uchaguzi, kinahangaika na maendeleo ya wananchi na hata wasiokipigia kura wanayahitaji hivyo  Makatibu wa Kata na Matawi wajipange kupata wagombea wanaoguswa na maendeleo .

Pia wahakikishe wanazingatia mabadiliko ya Katiba ya CCM na kanuni  zake pamoja na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwaeleza wananchi mazuri yaliyofanywa  na serikali  ya CCM, kufanya hivyo wataisaidia kuibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Hayo yalielezwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli, alipozungumza na makatibu hao wa kata na matawi wa tarafa za Misasi na Mbarika, katika Wilaya  Misungwi jana akisema CCM si chama cha kusubiri uchaguzi bali kinahangaika na maendeleo ya wananchi na kujenga uchumi.

Alisema mabadiliko makubwa ya Katiba ya CCM yaliyofanywa mwaka 2017 na kanuni zake yaliathiri mambo mengi na hivyo kipimo na majaribio yake yatafanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani ili kurejesha vijiji na vitongoji vilivyoangukia kwa wapinzani wilayani Misungwi.

Alisema makatibu wa kata na matawi waielewe katiba na kanuni katika mchakato wa kupitisha wagombea,wajipange kupata  wagombea wenye sifa wanaotokana na CCM wasio na makunyanzi, wanaokubalika ambao itakuwa rahisi kuwanadi na si kupitisha wagombea mizigo.

“Kwenye uchaguzi huu tujiongeze tusije kuletewa wagombea mizigo ya ajabu bali wanaokubalika kwa sifa zao, viongozi waliochokwa na wananchi wasirejeshwe kuwania nafasi yoyote vinginevyo itakuwa tatizo.Pia watafutwe mameneja kampeni watakaoeleza kazi zilizotekelezwa na serikali ya CCM maana viongozi tunaowatafuta  wengine hawajui lolote kwenye ilani,”alisema Kalli.

Alisema kuwa siasa ni sayansi na ushindi kwenye uchaguzi ni namba na kutahadharisha kuwa licha ya  Rais John Magufuli kufanya mengi mazuri mengine nje ya ilani unaweza kushangaa kwa sababu tu imekosekana tafsiri ya yaliyofanyika, hivyo wananchi wakumbushwe hayo ili kuongeza mtaji wa kura.

Aidha, Kalli alieleza kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu wagombea wa ajabu ajabu wasipitishwe ambao wananchi na wana CCM hawajawahi kuwaona, hivyo vikao vya uteuzi vizingatie haki kwa sababu Rais Magufuli ana mambo mengi ya kujenga uchumi wan chi na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aliongeza kuwa yapo mambo watendaji wa Chama hawayafanyi ya kutatua kero za wananchi na wala hawaishi na matatizo yao, hivyo akawataka wakaishi na shida za wananchi,wakatatue kero na migogoro na wakiyafanya hayo na kutimiza wajibu wao CCM itakuwa kimbilio la wanyonge watakuwa wanamsaidia Rais.

Pia katibu huyo wa CCM Mkoa wa Mwanza alikemea makundi ya uchaguzi na kuhimiza uhusiano baina ya watendaji wa Chama na watumishi wa serikali kuhakikisha ilani ya uchaguzi imetekelezwa na wananchi kupata mrejesho wa shughuli na miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali yao.

Picha
Katibu wa CCM MKoa wa Mwanza, salum Kalli akizungumza na makatibu wa kata na matawi wa kata za Mbarika na Misiasi wilayani Misungwi (hawapo pichani).

NAIBU KATIBU MKUU WAZAZI ATOA SOMO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Kija Magoma akivishwa skafu na vijana wa Green gurd alipowasili wilayani Nyamagana kwenye kongamano la elimu, afya,maadili, siasa, uchumi na mazingira lililoandaliwa na Wazazi ya Nyamagana kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Kija Magoma amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilipoteza baadhi ya vijiji, vitongoji,mitaa, kata na majimbo kwa fitna na uzembe wa wanachama wake na kuwataka wasirudie makosa kwenye chaguzi zijazo.

Pia kimeonya wana CCM wanaojipitisha kwenye majimbo na kata  wakifanya kampeni za siri na kuanza kuchafuana na kuagiza majina yao yaorodheshwe ili washughulikie kwa sababu wanakichafua Chama.

Magoma alitoa kauli hiyo jana jijini Mwanza, kwenye kongamano la elimu, maadili,afya,mazingira, siasa na uchumi lililoandaliwa na Wazazi Wilaya ya Nyamagana, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Alisema mwaka 2014 na 2015 CCM ilishindwa kwenye baadhi ya maeneo kwa sababu ya fitna, majungu, kusemana vibaya (kuchafuana)  na uzembe wa wanachama wake pindi uchaguzi unapokaribia, hivyo uchaguzi wa mwaka huu wasirudie makosa hayo.

“Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu ni wa kuonyesha dira ya 2020.Chama kwanza, mtu baadaye na tuache majungu, fitna,kuchafuana na kutukanana, ikitokea hivyo hao tunaowachafua tukawapitisha itakuwa fimbo ya kutuadhibu itakayotumiwa na wapinzani,”alisema Magoma.

Alisema wapo wana CCM kote nchini wanajipitisha kabla ya wakati wakifanya kampeni za siri ili wapitishwe kugombea uongozi na kuonya muda huo haujafika na wanaofanya hivyo wasidhani wako salama,wataanza kuchukuliwa hatua wilayani  kwa sababu wanaichafua CCM.

“Angalizo, serikali ya Rais John Magufuli si ya mchezo, wanaofanya kampeni za ubunge na udiwani kabla ya wakati wanafahamika na taarifa zao zipo mezani,na safari hii hakuna ujinga wa CCM kushindwa.Hapa Nyamagana kuna watu wanamvuruga mbunge ili kumuondoa, muda bado haujaisha.Wabunge na madiwani waheshimiwe ,waachwe wafanye kazi,”alisistiza Magoma.

Akizungumzia utaekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi alisema imetekelezwa ndani ya miaka mitatu na nusu ya uongozi wa Rais Magufuli kutokana na ualidifu na uzalendo wake wa kuhakikisha nchi inapata maendeleo ya kweli aliyoahidi wakati wa kampeni.

Alisema Rais Dk. Magufuli kwa aliyoyafanya ni dhahiri ameshaifanyia CCM kampeni kwa asilimia 80 hata kabla ya uchaguzi, hivyo ni jukumu la wana CCM kutafuta takwimu na kuwaeleza wananchi yaliyofanyika kwa sababu hakuna mwingine wa kuyasema lakini wakikaa kimya ni kutomtendea haki.

“JPM anastahili pongezi kwa namna alivyotekeleza ilani ya CCM katika muda mchache,amejenga miundombinu ya barabara km 12,885, fly over na Ubongo Interchange kwa bilioni 247,litajengwa daraja la Kigongo-Busisi (Milioni 700),amenunua ndege sita tayari,amelipa madeni ya watumishi sh. bilioni 595.2,”alisema Magoma.

Aliongeza kuwa amefanikiwa kujenga vituo vya afya 118, zahanati 522, hospitali 67 za wilaya ambapo 34 zimekamilika,ujenzi wa majengo ya ukaguzi wa elimu kote nchini kwa bilioni 15.2, umeme umeunganishwa kwenye vijiji 7,100, ujenzi wa mradi wa umeme Stiglers kwa Trilioni 6.5, Reli ya kisasa (SGR) kwa Trilioni 7 kwa fedha za ndani.

“Anataka Tanzania iwe nchi ya mfano ambapo bajeti ya mwaka huu ni Trilioni 33.11 kati ya hizo trilioni 12.15 za maendeleo, mikopo trilioni 2.52, bajeti ya dawa sh. milioni 415 (2019/2020) na elimu bilioni 450,”alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wazazi na kuhoji ,tulichelewa wapi kumpata Rais wa aina hii mwenye maono makubwa na nchi, uchumi unapanda.sssss

MWAKYEMBE ANOGESHA MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE ZA BETHEL MISSION UBUNGO NA MSAKUZI,AAHIDI WIZARA YAKE KUIPIGA JEKI YA SH. MILIONI 5 UJENZI BWALO LA WANAFUNZI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Abdulkadri Shayo, wakati wa Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, leo, Septemba 8, 2019. Katika Mahafali hayo Wanafunzi 33 wa Bethel School Ubungo na 19 wa Msakuzi walikabidhiwa vyeti. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote Jumatano ijayo. Wapili kulia ni Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (Wapili kulia) akimpatia maelezo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe (kushoto) baada ya kumpokea ofisini kwake, Waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba  ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana. Katika Mahafali hayo Wanafunzi 33 wa Bethel School Ubungo na 19 wa Msakuzi walikabidhiwa vyeti. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote, Jumatano ijayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo Justine Sangu.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana. akimpa kitabu cha wageni Waziri Dk. Harison Mwakyembe kwa ajili ya kusaini baada ya kuwasili.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio, baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya  Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na wenzao wa darasa hilo nchini kote, Jumatano ijayo.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio, baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya  Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (Kulia) akimpatia maelezo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kabla ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akizindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana .Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akizungumza baada ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa Bwalo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana .Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akitazama eneo ambalo ujenzi wa Bwalo hilo la chakula la Wanafunzi wa Bethel International School unafanyika, waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio la sherehe za mahafali, , baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana (kulia) akimwongoza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenda eneo la tukio la sherehe za mahafali, , baada ya kumpokea waziri huyo alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana "Hawa ndiyo wahitimu wenyewe?" Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akiuliza alipowaona wanafunzi wa darasa la saba alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana  "Watoto hamjambo?" Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe akiwasalimia wanafunzi haoWanafunzi wa darasa la saba na chekechea wakimlaki kwa nyimbo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana Wanafunzi wa darasa la saba na Chekechea wakimlaki kwa nyimbo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harison Mwakyembe alipowasili kwenye Mahafali ya 15 ya darasa la saba ya Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Mahafali ya kwanza ya darasa hilo shule ya Bethel Mission Mbezi Msakuzi, yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, jana  Waziri Dk. Mwakyembe akifuatana na Ndugu Mshana wakati akiwasili eneo la shughuli ya mahafali hayo. Kulia ni Ndugu Sangu. Wazazi na wageni waalikwa wakishangilia wakati Waziri Dk. Mwakyembe akiwasili eneo la shughuli ya Mahafali. Wazazi na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati Waziri Dk. Mwakyembe akiwasili eneo la shughuli ya Mahafali.Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakiingia ukumbini tayari kwa shughuli za mahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana. Waziri Dk. Mwakyembe akiwa amesimama pamoja na meza kuu kuwalaki ukumbini wanafunzi hao.
Waziri Dk. Mwakyembe akishiriki kuimba wimbo wa Taifa mwanzoni wa shughuli za mahafali hayo.Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akimsikiliza kwa makini Waziri Dk. Mwakyembe wakati akielezwa jambo wakati wa mahafali hayo. Baadhi ya Wazazi wakiwa kwenye mahafali hayoWanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,janaWanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana akizungumzaWanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam,jana  Wawakilishi wa wanafunzi wa darasa la saba wakisoma risala wakati wa mahafali hayo. Wanafunzi hao wakimkabidhi risala yao waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuisoma.Wanafunzi wa darasa la saba Shule za Bethel Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, janaWaziri Dk. Mwakyembe na viongozi wa meza kuu wakishangilia bada ya kuvutiwa na namna wahitimu wa tarajiwa wa darasa la saba Shule za Bethel  Mission ya Ubungo Makuburi na Bethel Mission Mbezi Msakuzi, walivyokuwa wakitoa burudani ya wimbo wakati wamahafali yao yaliyofanyika kwa pamoja kwenye Shule ya Bethel Mission Ubungo Makuburi, Dar es Salaam, janaMeneja wa Bethel Mission School akitoa hotuba wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Waziri Dk. Mwakyembe na kulia ni Mtunza hazina wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Kanda ya Afrika Mchungaji Perminar Shirima.Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue akimkaribisha Dk. Mwakyembe kuzungumza.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Mwakyembe akihyutubia kwenye mahafali hayo. Dk. Mwakyembe alionyesha kuvutiwa na wanafunzi wa darasa la saba kwa namna walivyoonyesha vipaji na weledi mkubwa katika kuzungumza kiingereza. Aliipongeza shule hiyo kwa kazi nzuri ya kueleimisha watoto huku ikijikita pia katika kuwalea vizuri kimaadili. Kutokana na kukunwa na shule hiyo aliahidi Wizara yake kutoa sh. milioni 5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Bwalo la wanafunzi kwenye shule ya Bethel Mission Ubungo.Waziri Dk. Mwakyembge akishauriana jambo na Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue 

KUKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU⇓













Waziri Dk. Mwakyembe akionyesha zawaidi baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakyembe akipokea zawaidi ya shati baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bethel Mission School Emmanuel Mshana wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakyembe akipokea zawaidi ya kitabu cha tiba kutoka kwa Kiongozi wa Kanisa la International Mission Society of Seventy Adventist Church Mchungaji Bright Fue Waziri Dk. Mwakenye na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Chekechea wa Bethel Mission School Ubungo wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakenye na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu watarajiwa wa Darasa la saba wa Bethel Mission School Ubungo na Mbezi Msakuzi, wakati wa mahafali hayoWaziri Dk. Mwakenye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bethel Mission School na baadhi ya wageni waalikwa mwishoni wa shughuli za mahafali hayo.