Kama wengi wetu tujuavyo, kiwango cha miaka ya kuishi hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu kimepungua sana nyakati hizi, hivyo kila tunaposherekea mwaka mpya tunasherekea pia uzee na utimilifu wa miaka yetu ya kufa, lakini hilo lisitupe hofu kwani wataalam wamegundua maajabu yapatikanayo kwa mtu kucheka.
Kwa kutambua umuhimu wa maajabu hayo nimeona ni vema nikaelezea faida za mtu kucheka. Ifahamike kuwa watafiti mbalimbali duniani wamebaini kuwa mtu anaweza kujikinga, kujiponya na magonjwa hatari ya kansa, moyo na kisukari kwa kucheka na isitoshe achekaye anatajwa kuufanya mwili wake usionekane umezeeka hata kama atakuwa na umri mkubwa.
Kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kijamii, ugumu wa maisha unaoleta msongo wa mawazo ndiyo unaotajwa kuchangia vifo vya wanadamu wengi sambamba na kufupisha umri wa kuishi. Wanasema mtu mwenye kutingwa na sononi kila mara huchoma seli nyingi muhimu katika mwili wake, hivyo kumfanya awe katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa niliyoyataja hapo juu.
Katika tafiti za hivi karibuni ukiwemo ule uliyoendeshwa na wasomi wa Chuo Kikuu cha Amerika Cardiology, imebainika kuwa uhaba wa furaha hasa fursa ya watu kupata muda wa kucheka kwa siku ni moja kati ya sababu kubwa zinazochangia magonjwa hatari miongoni mwa watu wengi. Wanasema watu wengi wamechipusha vimelea vya magonjwa si kutokana na bakteria halisi bali mfadhaiko wa mioyo yao.
Kwa maana hiyo wataalam hao wameibuka na ushauri kuwa ni bora watu wakajibidisha kutafuta furaha katika maisha yao kuliko kudumu katika uhangaikia tiba ghali za dawa zinazotolewa na vituo vya afya na hospitali, ilhali mzizi wa magonjwa yao unatokana na wao wenyewe kuishi bila kicheko ambacho kinatafsiri furaha aliyonayo mtu husika (kumbuka sizungumzii kicheko cha kebehi).
Kwa mujibu wa wasomi hao imegundulika kuwa kicheko ni tiba na kinga bora ya magonjwa yanayomkabili mwanadamu yakiwemo magonjwa ya moyo ambayo ni hatari sana kwa uhai. Mtu ambaye anaweza kutumia dakika 20 kwa siku kwa kucheka, anaweza kutibu maradhi yake hata bila kumeza vidonge.
TUKUTANE JB BELMONT HOTEL TAREHE 29 SEPT 2019 TUKAPATE TIBA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.