ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 13, 2019

WALIMU 10 MBARONI KWA WIZI WA MITIHANI KAGERA.



Na Clavery Christian, Kagera.

Jeshi la polisi mkoani Kagera linawashikilia walimu watano na wasimamizi watano wa mtihani wa darasa la saba wilayani Ngara mkoani Kagera kwa wizi wa mtihani wa darasa la

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa tukio hilo limetokea jana septemba 12/2019 majira ya saa 4:40 asubuhi katika shule ya msingi Kumunazi iliyopo katika tarafa ya Nyamihaga wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambapo majira hayo kamati yamitihani ya wilaya ilipata taarifa kuwa baadhi ya walimu wa shule hiyo wamejifungia katika nyumba moja ya mwalimu wa shule hiyo na wameiba mtihani wa sayansi na wanajaribu kuufanya kwaajiri ya kuandaa majibu ili waweze kuwapa wanafunzi wa shule hiyo ambapo kamati hiyo ilifika na kuwakuta walimu hao wakiwa na mtihani huo.

Kamanda Malimi amesema kuwa katika shule hiyo kulikuwa na mikondo mitano ambayo kila mkondo ulikuwa na msimazi ambapo jumla ya wasimamizi watano wamekamatwa na walimu watano wa shule hiyo ambao walikuwa wakijaribu kuiba mtihani huo.

Aidha kamanda malimi amesema kuwa idadi ya wanafunzi waliokuwa wameandaliwa kwa ajiri ya kupewa majibu hayo wanahifadhiwa majina yao na idadi yao kwa ajiri ya kulinda haki za watoto.

Kamanda Malimi amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na baada ya kukamilisha uchunguzi watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.