ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 13, 2013

MH. LOWASSA ATOA MCHANGO WA SHILINGI MIL 5 KWA BARAZA LA MISIKITI TANZANIA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Sheikh Salum Sung'he kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati wa kukabidhi msaada wa sh. mil 5 kwa Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzana,katika makabidhiano yaliyofanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe (kushoto) na Sheikh Salum Sung'he waliofika ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam kupokea msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.

Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati akitoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.

Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akikabidhi kwa Mh. Lowassa barua ya shukrani kutoka Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA).Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.

KASSAM DHALLA GRAND OPENING SPECIAL

KASSAM DHALLA & SONS LTD
Grand Opening Special
8th April - 13th May 2013
+255 22 2113422 | +255 716 048 747 | +255 784 391 622

BALOZI WA CHINA NCHINI AAHIDI KUSAIDIA KILIMO CHA MAHINDI SONGEA


Mwenyekiti wa CCM Oddo Mwisho akimpa zawadi ya kinyago balozi wa China anaye shuhudia kulia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Joseph Mkirikiti. 

   
 Mwenyekiti wa Halmashauli ya Songea vijijini Rajabu Mtiula akimpa Kapu  Balozi wa China,Katikati Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama. 
 

Mzee wa kimilila amabaye jina lake halikufahamika mara moja akimvesha mgorori balozi wa China Nchini Tanzania Lu Younqing. 
 
Afisa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Revocatus Kasimba akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga Kulia.
    
............................................................................................................................

BALOZI wa china nchini Tanzania Lu Younqing ambaye yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku tatu ameahidi kuleta wawekezaji zaidi na watalaamu wengi katika sekta ya kilimo cha mahindi ili kulifanya zao hilo liwe  la kibiashara linalozalishwa kwa njia ya kilimo cha kisasa zaidi na kuwafanya wakulima wa zao hilo kujikwamua zaidi kichumi   .
 
Ahadi hiyo aliitoa wakati wa siku ya kwanza ya   ziara yake alipokuwa akikagua mashamba mbalimbali ya kilimo cha mahindi ambacho kinachofanywa na wakulima wa zao hilo latika jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma .
 
Katika ziara hiyo ya balozi Lu Younqing alitoa misaada mbalimbali kwenye vikundi vya kijamii na wakulima vilivyopo katika jimbo la Peramiho ikiwemo shule ya sekondari ya Namihoro iliyopo katika kijiji cha peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma.
 
Vikundi hivyo vilivyopata msaada huo ikiwemo  sekondari ya Namihoro iliyopewa shilingi milioni 10 ili kuendeleza elimu katika shule hiyo ,kikundi cha wakina mama wajasiriamali kilipewa  vyerehani 20 ili wajikwamue kiuchumi na baiskeli 20 kwa viongozi wa jumuiya ya vijana wa CCM wa kata zote za jimbo hilo la Peramiho.
 
 Aidha balozi huyo kabla ya kuhitimisha ziara yake hiyo ya siku tatu atatembelea pia mashamba ya kilimo cha kahawa yaliyopo katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ili kubaini changamoto zinazokabili kilimo hicho na kuwa akielekea wilaya ya Mbinga amepita kwenye barabara ya kiwango cha lami iliojegwa na nchi ya China kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.
 
 Ziara hiyo ya balozi wa China kutembelea mkoa wa Ruvuma umekuwa ni mwaliko rasmi wa mbunge wa jimbo la Peramiho kwa tiketi ya chama cha mapinduzi  Jenista Mhagama ambaye aliwataka wananchi wa jimbo hilo kutumia fursa hiyo ya ujio wa balozi huyo kwa kufanya kazi zaidi katika kilimo kwa sababu balozi huyo ameahidi kulifanya zao la mahindi kuwa zao la kibiashara.
 
 Alisema kuwa kilimo cha kisasa ndicho kinachoweza kuwakwamua zaidi kuichumi na kuondokana na wimbi la umasikini linalowakabili pia aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo na misaada iliyotolewa kwao na balozi huyo kama changamoto kwao katika kujikwamua kiuchumi na kupambana na umasikini uliopo.

MTANDAO WA PR HABARI WAPATA MKOKO WAKE


Gari ya Mtandao wa kijamii wa http://prhabari.blogspot.com/  unaongozwa na mwenyekiti Spear Patrick unatarajia kuzindua hivi karibuni  Gari la mtandao huo ambao litakuwa na matangazo mbalimbali ya kazi za kampuni hiyoo


Mwenyekiti wa  Mtandao wa kijamii wa http://prhabari.blogspot.com/  Spear Patrick akionesha moja ya upande uliokua na matangazo hayo


Mafundi wakiendelea kuiremba gari hiyo


Mwenyekiti wa  Mtandao wa kijamii wa http://prhabari.blogspot.com/  Spear Patrickakiwa amepozi


MKOKO WA Mtandao wa kijamii wa http://prhabari.blogspot.com/

Friday, April 12, 2013

POLISI WA INTERPOL KUTUMIKA KUWASAKA WATUHUMIWA WA KANDA ZA UCHOCHEZI WA KIDINI WALIOTOROKA MWANZA

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu

POLISI wa Kimataifa (Interpol Police) kutumika kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa wawili wa Kanda za uchochezi wa Kidini waliotorokea katika Mataifa ya India na Amerika wanaosakwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza .

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu ametoa tamko hilo hii leo ofisini kwake.

Amesema kwamba tayari jeshi hilo limetoa taarifa kwa Askari wa Interpol na Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es salaam  ili kusaidia kuwakamata na kuwarejesha watuhumiwa wawili ambao ni viongozi wa Kidini wanatuhumiwa kwa kutoa Kanda (DVD na CD) zilizo na maudhui ya uchochezi wa kiimani kwa madhehebu ya Kidini nchini.
  (ZAIDI OFYA PLAY MSIKILIZE)

“Tangu mwezi wa Februari mwaka huu tulitoa rai ya kuwatafuta watu watatu ambao ni viongozi wa kidini kwa tuhuma hizi za uchochezi lakini hadi sasa tumefanikiwa kumkamata mmoja wao aitwaye Imamu Hamza Omary na kumfungulia mashitaka huku yukiwa tayari tumeisha mfikisha katika mahakama ya Wilaya kuendelea na kesi”alisema Kamanda.

Kamanda Mangu amewataja watuhumiwa wengine wanaotafutwa na jeshi hilo na wanaodaiwa kutoroka nchini kwa ni Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kiongozi wa Taasisi ya kidini ya Thaqeeb iliyopo Kata ya Nyamanoro Wilayani Ilemela na Askofu Augustine Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field Evangelist na Mkurugenzi anayemiliki kituo cha Redio Kwa Neema FM cha Jijini Mwanza ambacho kimefungiwa na TCRA miezi sita kwa ukiukwaji wa maadili.

“Hawa wawili tumeamua kuwashirikisha polisi wa Interpol ili kuwakamata na kuwarejesha nchini ili kuwaunganisha na kesi tuliyomfungulia mwenzao Imamu Omary na tunasikia kuwepo kwa taarifa kuwa Sheikh Ilunga kuwa yupo nchini India na Askofu Mpemba yupo nchini Marekani wanakodaiwa kutorokea,bado tutahakikisha tunawakamata tu ni vyema wakajisalimisha kabla ya hawajakamatwa ”alisisitiza.

 Kamanda Mangu ametoa muda wa siku nne kwa wafanyabiashara  wanaouza na kusambaza Kanda (DVD na CD) za uchochezi ziliotolewa na watuhumiwa hao  wanaotafutwa na jeshi hilo na zingine zenye maudhui ya uchochezi wa kiimani wa kidini kuzisalimisha kwa ihali yao kwenye vituo vya polisi  kabla ya kuanza opresheni ya kuzisaka Jijini Mwanza na Wilaya zote za Mkoa huo na hata ile ya jirani.


Kanda zilizopigwa marufuku ni pamoja na Unafiki katika SensaBakwata tawi la Kanisa,Mauaji ya Sheikh Abdu Rogo wa Mombasa na Mwisilamu rudisha Imani zilitolewa na Sheikh Ilunga, Ndege wote walie akilia Bundi Uchuro ya Imamu Omary na Inuka chinja ule iliyotolewa na kusambazwa na Askofu Mpemba.

Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri kwa jeshi hilo ili kuweza kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na watu wanaoendelea kusambaza na kuziuza kanda hizo kwa usiri ili kuwafikisha katika chombo cha sheria kutokana na kueneza uchochezi wa kiimani ka madhehebu ya kidini jambo ambalo linahatarisha amani ya nchi na huweza kusababisha machafuko zaidi ya kidini. 

THE BEAT TONIGHT

THE BEAT FESTIVAL FEATURING 100% live music: Friday 12. April 2013 - 20.00 - 01.00 - Venue: Triniti - Msasani Rd. 26, Oysterbay DSM

HII HAPA VIDEO MPYA YA KINGKAPITA "KUNA TATIZO KWANI"


HIT MAKER KINGKAPITA TOKA TANZANIA TENA NA TENA KATIKA UJIO MPYA WIMBO ALIOFANYA NA GODZILLA KUTOKA STUDIO YA DEFATALITY PALE KWA MESSEN SELEKTA

NYIMBO INAITWA "KUNATATIZO KWANI"
HII SASA NDO VIDEO YAKE AMBAYO INAPATIKANA YOUTUBE KWA SASA KWA LINK HII

http://youtu.be/NaJDR38AKE4

IKIWA IMEBEBA LINE KALI ZA KUELIMISHA NA KUBURUDISHA JAMII KAMA :
"BABA JAMBAZI MAMA CHANGUDOA MTOTO KAZALIWA KONDA OTEA NINI KITAFATIIA//"
//HII BAHATI HAIZIMWI KWA MIDOMO FORM SIX ALIPATA ZIRO NA LEO NDO BOSS WAO//
                              
     "KUNATATIZO KWANI"
HAPO NI KATIKA KUWAPA MOYO WOTE WALIOPATA MATATIZO KWENYE KUTAFUTA WAKA FAIL WASIKATE TAMAA NA MAISHA BADO YANAWEZEKANA PIA KUNA LINE KAMA
       //MI MKRISTO WEWE MWISLAM HAIJALISHI DINI GANI TUDUMISHE HII AMANI//
                                    "KUNATATIZO KWANI"
 HAPO NIKIWA NAELEZEA KUHUSU MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

KINGKAPITA ANA NYIMBO HIT NYINGINE NYINGI KAMA:
1.MTOTO MLITO
2.MTOTO WA FISADI
3.SHIKAMOO PESA
NA SASA NAOMBA MSIKILIZE 4. KUNATATIZO KWANI IKIWA KAMA MSEMO MPYA KATIKA JAMII ETI KUNATATIZO KWANI???

TAMASHA AIRTEL YATOSHA KUAMIA CHALINZE JUMAMOSI NA JUMAPILI HII.


Tamasha la Airtel Yatosha lenye lengo la kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo huduma mpya ya Airtel Yatosha linalofanyika katika mikoa mbalimbali nchini mwishoni mwa wiki hii litafanyika katika mkoa wa Pwani.

Shangwe za Airtel yatosha litajumuisha wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Ney wa Mitego, sir Juma Nature, kikundi cha Tip top connection kikiongozwa na madii,  msanii wakizazi kipya Roma Mkatoliki pamoja na burudani nyingi toka kwa wasanii chipukizi na burudani za dansi na acrobatic kutoka katika kikundi cha vinoko.

Tunawakaribisha watanzania na wakazi wa mkoa wa pwani kuhudhuria tamasha ili siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 13 na 14 mwenzi wa 4,  katika viwanja vya sokoni chalinze, kuanzia saa tatu mpaka saa kumi na mbili jioni.
Kiingilio ni BURE, njoo na kitambulisho chako usajili namba yako na kuunganishwa na huduma poa ya Airtel yatosha na kupata ofa kibao kutoka Airtel.

Airtel itaendelea na burdani hizi za shangwe katika mikoa mingine katika kuitambulisha kwa wateja wake na watanzania huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.  Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99# 

AIRTEL GHANA WINS TWO AWARDS AT THE 1ST PUBLIC RELATIONS EXCELLENCE AWARDS


AIRTEL GHANA WINS TWO AWARDS AT THE 1ST PUBLIC RELATIONS EXCELLENCE AWARDSAirtel Ghana has been recognized with two awards for Corporate Social Responsibility interventions. 
IPR Award.jpg
The awards, Public Relations Campaign of the year and Best Community Relations Programme of the year were handed to Airtel at the 1st Public Relations Excellence Awards Ceremony organized by the Institute of Public Relations Ghana at a ceremony in Accra over the weekend.

The first award was in recognition of Airtel’s comprehensive and widely acclaimed public relations effort before, during and after the company went to the rescue of the Odumase Krobo Presby School in Odumase.

The second award was for Airtel Ghana’s biggest social intervention programme, Touching Lives, which has already received several awards in recognition of its massive impact on a wide section of the Ghanaian society.

Airtel is committed to increase sustainability in the educations sector, reaching the grassroots of societies across Africa. Among its largest projects is the ADOPT A SCHOOL program where the most impoverished public primary schools are adopted by AIRTEL and provided with facilities including classrooms, desks text books, scholastic materials, uniforms and ICT learning facilities.

 Similar to Ghana, AIRTEL Tanzania has thus far implemented this project for Kiromo Primary school in Bagamoyo.

Thursday, April 11, 2013

KOSHA MACHO ROCK CITY.

Ze uJumbE.

Mwanza wa ujenzi Barabara za mawe Rock City. 

Ngazi za mawe mwanzo mwisho.

Karibu.

Chuma kile ziwani..

Kitu juu ya kitu.

 Rock City.

Wednesday, April 10, 2013

LIGI YA MABINGWA IMEFIKIA PATAMU


Shangwe za awali Christian Ronaldo akisherehekea goli lake la mapemaaaa.

Mabingwa wa mara tisa wa michuano ya kombe la Klabu bingwa barani Ulaya,Real Madrid licha ya kufungwa mabao 3-2 na Galatasaray ya Uturuki,wamefanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya na kuandika rekodi ya kuwa timu iliyofika mara nyingi hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Madrid ambayo hii ni mara yao ya 24 kutinga hatua ya nusu fainali,walianza kwa kupata bao la kuongoza ugenini kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga bao hilo dakika ya saba ya mchezo na kumfanya kuwa na magoli kumi kwenye michuano hiyo msimu hu.
Galatasaray walisawazisha bao hilo kipindi cha pili kunako dakika ya 58 kupitia kwa beki wa kimataifa wa Ivory Cost,Emmanuel Eboue aliyemalizia pasi ya Wesley Sneijder na kufungwa bao maridadi kwa shuti la kiufundi
Didier Drogba alidhihirisha umwamba wake wa kuzifumania nyavu kwa kutupia.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya vijana wa Jose Mourinho kwani,dakika ya 70 na 72 walijikuta wakifungwa mabao mawili ndani ya dakika mbili mfululizo,mabao yaliyofungwa na kiungo wa zamani wa Inter Milan aliyehamia Galatasaray msimu huu Wesley Sneijder na Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na nahodha wa timu ya taifa Ivory Cost,Didier Drogba.
Huku Gala wakiwa wanaendelea kulisakama lango la Madrid, beki mkongwe wa timu Hispania na Real Madrid, Alvaro Arbeloa alizadiwa kadi nyekundu kwa kutumia lugha isiyo ya kiungwana baada ya kucheza ndivyo sivyo.
WE'RE RON TO A GOOD THING  Ni bao la pili sasa lililoivusha Real Madrid.
Pamoja na kucheza pungufu,Madrid waliendelea kumudu mchezo huo na ikiwa imebakia dakika moja mchezo kumalizika Cristiano Ronaldo aliipatia timu yake bao la pili na bao lake la 11 kwenye michuano hiyo msimu huu na pia goli lake la 21 kwenye michezo 20 ya klabu bingwa toka msimu wa 2011/12.
Hadi mchezo unamalizika Galatasaray 3-2 Real Madrid,lakini Madrid wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-3 baada ya ushindi wa 3-0 nyumbani wiki iliyopita.
Jose Mourinho akimfariji memba mwenzake enzi za Chelsea Didier Drogba.
Matokeo hayo yanawafanya Madrid kutangulia katika nusu fainal ya Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ambapo kuna uwezekano kocha wake Jose Mourinho akaandika rekodi ya kipekee kuwa kocha wa kwanza kushinda mataji matatu ya Klabu barani Ulaya na vilabu vitatu tofauti baada ya kufanya hivyo akiwa na FC Porto ya Ureno mwaka 2004 baada ya kuwafunga AS Monaco kwa mabao 3-0 na kisha baadaye mwaka 2010 alipokuwa kocha wa Inter Milan ya Italia katika mchezo ambao Inter iliwafunga 2-0 Bayern Munich ya Ujerumani.
Katika Mchezo mwingine, Borussia Dortmund ya Ujerumani nayo imetangulia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa 3-2 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Signal Iduna Park dhidi ya Malaga ya Hispania.
Mchezo huo ambao ulikuwa na kila aina burudani,ulikumbusha mechi ya fainali ya Manchester United na Bayern Munich mwaka 1999 kwa kupatikana mabao mawili ya haraka ndani ya dakika nne za nyongeza kabla ya mchezo kumalizika.
Dortmund walianza kufungwa bao la mapema dakika ya 25 lakini walizinduka na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Roberto Lewandowski kunako dakika ya 40 ya mchezo.
Malaga walipata bao la pili dakika ya 82 kupitia kwa Eliseu Pereira Dos Santo na kuwafanya mashabiki wa Dortmund kuwa wanyonge hasa wakiwa na kumbukumbu ya kulipoteza kombe la ligi kuu ya Ujerumani wikiendi iliyopita kwa kushuudia Bayern Munich wakitawazwa kuwa mabingwa wapya.
Dakika tatu kabla ya Mchezo kumalizika wakiwa kwenye muda wa nyongeza, Dortmund walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Marko Reus na baadaye ikiwa imesalia dakika moja Mbrazil Felipe Augusto Santana aliipatia bao la tatu na la ushindi Borussia Dortmund,goli ambalo liliwafanya wachezaji na mashabiki wa Malaga wasiamini kilichotokea.
Mechi nyingine za leo usiku za hatua ya robo fainal,Juventus watawakaribisha mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich huku Barcelona wakiwa nyumbani kucheza na PSG ya Ufaransa.

MILIPUKO YA JUMAPILI YANGU...

Bony Mwaitege na vijana wake.

Mineso jukwaani.

Sarakasi nazo zilikuwemo.

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi katika muziki wa injili Nesta Sanga (katikati) akiwa na watumishi wenzake.

Ni faraja Mtaboba.

Upendo Nkone alipata fursa kumtambulisha mumewe (aliye katikati).

Solomon Mkubwa.

Rose Muhando ni mmoja kati ya waliohudumu.

Msisimko.

Raha.

Upendo Kilahilo akisalimia mashabiki wake..

Safu ya ufundi.

Jukwaa jingine la uimbaji hili hapa.

Waumini.

Kutoka kushoto ni Meneja Ramma wa Villa Park Resort, Kaka na Mkurugenzi wa COSU Entertainment Fabian Fanuel.

Umoja na ushirikiano katika kuliombea taifa.