Shangwe za awali Christian Ronaldo akisherehekea goli lake la mapemaaaa. |
Mabingwa wa mara tisa wa michuano ya kombe la Klabu bingwa barani Ulaya,Real Madrid licha ya kufungwa mabao 3-2 na Galatasaray ya Uturuki,wamefanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya na kuandika rekodi ya kuwa timu iliyofika mara nyingi hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Madrid ambayo hii ni mara yao ya 24 kutinga hatua ya nusu fainali,walianza kwa kupata bao la kuongoza ugenini kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga bao hilo dakika ya saba ya mchezo na kumfanya kuwa na magoli kumi kwenye michuano hiyo msimu hu.
Galatasaray walisawazisha bao hilo kipindi cha pili kunako dakika ya 58 kupitia kwa beki wa kimataifa wa Ivory Cost,Emmanuel Eboue aliyemalizia pasi ya Wesley Sneijder na kufungwa bao maridadi kwa shuti la kiufundi
Didier Drogba alidhihirisha umwamba wake wa kuzifumania nyavu kwa kutupia. |
Huku Gala wakiwa wanaendelea kulisakama lango la Madrid, beki mkongwe wa timu Hispania na Real Madrid, Alvaro Arbeloa alizadiwa kadi nyekundu kwa kutumia lugha isiyo ya kiungwana baada ya kucheza ndivyo sivyo.
WE'RE RON TO A GOOD THING Ni bao la pili sasa lililoivusha Real Madrid. |
Hadi mchezo unamalizika Galatasaray 3-2 Real Madrid,lakini Madrid wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-3 baada ya ushindi wa 3-0 nyumbani wiki iliyopita.
Jose Mourinho akimfariji memba mwenzake enzi za Chelsea Didier Drogba. |
Katika Mchezo mwingine, Borussia Dortmund ya Ujerumani nayo imetangulia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa 3-2 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Signal Iduna Park dhidi ya Malaga ya Hispania.
Mchezo huo ambao ulikuwa na kila aina burudani,ulikumbusha mechi ya fainali ya Manchester United na Bayern Munich mwaka 1999 kwa kupatikana mabao mawili ya haraka ndani ya dakika nne za nyongeza kabla ya mchezo kumalizika.
Dortmund walianza kufungwa bao la mapema dakika ya 25 lakini walizinduka na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Roberto Lewandowski kunako dakika ya 40 ya mchezo.
Malaga walipata bao la pili dakika ya 82 kupitia kwa Eliseu Pereira Dos Santo na kuwafanya mashabiki wa Dortmund kuwa wanyonge hasa wakiwa na kumbukumbu ya kulipoteza kombe la ligi kuu ya Ujerumani wikiendi iliyopita kwa kushuudia Bayern Munich wakitawazwa kuwa mabingwa wapya.
Dakika tatu kabla ya Mchezo kumalizika wakiwa kwenye muda wa nyongeza, Dortmund walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Marko Reus na baadaye ikiwa imesalia dakika moja Mbrazil Felipe Augusto Santana aliipatia bao la tatu na la ushindi Borussia Dortmund,goli ambalo liliwafanya wachezaji na mashabiki wa Malaga wasiamini kilichotokea.
Mechi nyingine za leo usiku za hatua ya robo fainal,Juventus watawakaribisha mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich huku Barcelona wakiwa nyumbani kucheza na PSG ya Ufaransa.
Tupe maoni yako
Excellent goods from you, man. I have understand your stuff previous
ReplyDeleteto and you're just extremely great. I actually like what you have acquired here, really like what you're stating and the
way in which you say it. You make it entertaining and you still care for to
keep it sensible. I can't wait to read far more from you. This is really a terrific website.
My web blog ... trading binary options