ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 20, 2014

WALIOACHISHWA MASOMO KWA KUPATA MIMBA ZA UTOTONI WAPEWA MSAADA WA VIFAA YA UJASILIAMALI SBC

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akimkabidhi mmoja kati ya akinamama wadogo, kitorori vidogo kwaajili ya kufanyia biashara ndogondogo katika makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya PEPSI Igoma jijini Mwanza. 
WASICHANA 45 walioacha shule na kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali Jijini Mwanza ikiweo kujifungua wakiwa na umri mdogo na kuwa mama wadogo wamewezeshwa vifaa vya ujasiriamali na Kampuni ya Pepsi (SBC) ili kumudu majukumu ya kulea na kujikwamua kiuchumi na familia zao.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa.
Akizungumza jana kabla ya kugawa vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wasicha kuacha kujitumbukiza na kujiingiza katika makundi na kufanya vitendo vingine visivyofaa katika umri mdogo na jamii kwani baadhi vimekuwa vikiwafanya akina mama  wadogo bila kutarajia.

“Nipongeze Shirika lisilo la kiserikali  la Education For Better Living (EBLI) nchini chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake Benard Makatya kwa uthubutu wa kuanzisha mpango unaolenga kuwajengea uwezo watoto wa kike walioacha shule ili kuwapatia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya Kompyuta , Ujasiriamali na Biashara,”alisema.

Balozi wa Habari wa PEPSI, Albert G. Sengo akitoa taarifa ya utangulizi ambapo pia alielezea kazi shirika la Education for better Living Organisation (EBLI) ambalo ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi na vijana hususani wasichana katika shule za sekondari jijini Mwanza na Tanzania kwa ujumla. 
Shirika hili liko kwa malengo ya kupunguza idadi ya wasichana waaoachishwa shule kutokana na kubebeshwa mimba, kuwawezesha kiuchumi wasichana wadogo na kuwafundisha mbinu za ujasiliamali pamoja na masoko. 
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, Meneja wa SBC Mwanza Nicolaus Coetz na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akizungumza na umma uliofika kwenye hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi kwa akinamama wajasiliamali jijini Mwanza.
Meneja wa Kampuni ya SBC Mwanza watengenezaji wa vinywaji jamii ya PEPSI akitoa neno la ufafanuzi kuhusu kampuni yake ilivyojipanga katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.
Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya ELBI Benard Makachia (katikati) akiwa na mwanzilishi wa mradi wa Biashara ya vikundi kwa akinamama Mr. Michael Leen.ambaye ni mmisionari toka Maryknoll Lay nchini Marekani.(kulia)
Wakifurahia jambo kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, Meneja wa SBC Mwanza Nicolaus Coetz na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula.
Ndikilo alisema mradi huu umeonyesha kufanikiwa na unakuwa chachu ya kuwapatia mabinti nafasi nyingine (Second chance) hasa baada ya kuwa wamepoteza nafasi ya kupata elimu ya kawaida kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni.

Aidha katika kutekeleza mpango wenu wa “Kijana chagua Maisha” unaotekelezwa katika shule 10 za Jiji la Mwanza utasaidia kuwaelimisha vijana wa kike ili waweze kuepukana na mimba za utotoni na kusaidia kuendelea vyema na masomo shuleni.

“Mpango huu niupongeze mnaoufanya kwa ushirikiano baina ya EBLI na Kampuni ya SBC uliolenga kuwawezesha wamama wadogo (Young Mothers) waweze kujitegemea  na kufanya biashara ili kupata kipato na kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na utunzaji mazingira ya Jiji letu linaloshikiria rekodi bora ya ushindi wa usafi na mazingira kwa mara ya tisa sasa,”alisema.
Awali Mkurugenzi mwanzilishi wa Shirika la EBLI Mmissional kutoka Maryknoll Lay Marekani, Michael Leen, alisema Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya EBLI ilisajiliwa mwaka 2009 nchini na kuweka malengo ya kuisaidia jamii kwa kuanzisha mradi wa kwanza wa biashara ya vikundi unaolenga kuwafundisha au kutoa elimu ya mbinu mbalimbali za biashara na ujasiriamali.

Leen alisema mradi wa pili ni uanzishwaji na uendeshaji wa biashara za vikundi na utekelezaji wake kitumia kwa ambapo utekelezaji wake utashuhudia wanawake 25 wakipatiwa vifaa aina ya Push Carts na wanawake 20 kupatiwa Ice box, meza na viti vyake  ili kuboresha biashara na kuongeza tija katika uendeshaji wa shughuli zao.
“Vifaa hivi pia vitawasaidia kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi na vitumike pia katika maeneo yaliyokusudiwa ili visiwe chanzo cha uchafuzi wa mazingira ya Jiji letu hivyo mtatakiwa watunzaji wazuri wa mazingira mkizingatia rai iliyotolewa kwenu na Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikilo kwenu kabla ya kuwakabidhi vifaa hivi leo,”alisisitiza.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya SBC, Niclous Coetz, inashirikiana na jamii na kwa kuzingatia hilo imekuwa ikirudisha kwa jamii faida inayopata kupitia bidhaa zake za Pepsi ambapo mbali na kutoa vifaa hivyo itachangia gharama za utoaji elimu na uainishaji wa fursa za biashara na nyanja mbalimbali kwa kushirikiana na EBLI nchini.

Wito wangu kwa wananchi kuendelea kutupatia ushirikiano na kutuunga mkono kwa kununua na kutumia vinywaji vya Pepsi ili Kampuni ya SBC nayo iweze kurejesha faida yake kwa jamii kwa kuchangia miradi na shughuli mbalimbali ya maendeleo na kutoa msaada wa vifaa na kughramia wataalamu wa kutoa elimu ili kuwasaidia wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Friday, September 19, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI WA MAFUNZO, JIJINI DAR LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kama ishala ya kuzindua rasmi mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Kazi, na Ajira, Gaudensia Kabaka (kushoto) ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Shukuru Kawambwa. Pich na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa kuzindua rasmi mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Baadhi ya wahitimu wa Mafunzo hayo kutoka Chuo cha VETA, wakisubiri kutunikiwa vyeti na mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo. Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Charles Gwambassa, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali. Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Baadhi washiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi washiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi  wa VETA na washiriki na wadau waliohudhuria uzinduzi huo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo katika Chuo cha VETA na wakufunzi wao baada ya uzinduzi huo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wawakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani ILO  waliohudhuria uzinduzi huo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Kazi, na Ajira, Gaudensia Kabaka, wakati akiondoka katika Hoteli ya Kunduchi Beach baada ya uzinduzi huo wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo. Picha na OMR

UNAAMBIWA HIVIII, UKITAKA RAHA NA BURUDANI YA MUZIKI MZURI BASI NI SKYLIGHT BAND PEKEE LEO NDANI YA THAI VILLAGE

9
Majembe ya kazi wakiwajibika jukwaaani ili kutoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wao ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai Village Kutoka kushoto ni Joniko Flower akifuatiwa na Sony Masamba (katikati) pamoja na Sam Mapenzi a.k.a asali ya warembo. Mwambie yule na yule na wale tukutane pale kati kwa uchakavu wa Tshs 5,000 tu getini.
8
Skylight Band Divas wakishirikiana kwa pamoja kutoa vocal tamuuuuuuu ndani ya kiota cha maraha Thai Village. Wa kwanza kushoto ni Mary Luvcos, Digna Mbepera (katikati) pamoja na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0439
Na hivi ndio vile mashabiki wa Skylight Band wanavyofurikaga kwenye kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0345
Na hivi ndio vile inakuwaga kila Ijumaa ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar... Karibu sana....!!
 

Chekshia video ya wimbo 'Pasua Twende' ~ Skylight Band

MILEMBE INSURANCE KUNOGESHA TAMASHA LA KWANZA LA MAGARI LA ‘AUTOMOBILE CLINIC' JIJINI DAR

Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Septemba 27 na 28, 2014 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Ambapo alisema kuwa tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari. Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo na Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo.
Na Mwandishi Wetu. Kampuni ya Jast Tanzania Limited kwa kushirikiana na Jossekazi Auto Garage and General supplier wameandaa tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari.
Akizungumza na vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa habari Maelezo, Joseph Mgaya mmiliki wa Jossekazi Auto garage amesema tamasha hili lina lengo kuwakutanisha mafundi stadi na wenye magari, kwa gharama nafuu sana ya shillingi elfu ishirini tu.
Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo akielezea machache juu ya tamasha hilo.
Mgaya alisema huduma hizo ambazo zilipaswa kugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa kwa wenye magari, kitatolewa kwa bei nafuu ili kwa makusudi tu ya kukutanisha mafundi hao na wenye magari,.
Alisema pamoja na Wateja kutengenezewa Air condition na kujaziwa gesi, kufanyiwa Electronical scan diagnosis, Kuchekiwa Matairi, kuchekiwa Battery, na kupata ushauri wa kiufundi kuhusu gari zao, pia tamasha hilo litakuwa ni sehemu ya kukutanisha watu na kupata burudani.
Mgaya alisema, Mafundi wapatao 50 waliobobea katika fani ya ufundi magari, wamepatikana baada ya kufanyiwa usaili wa kina na kupitia mchujo na semina elekezi ili kuweza kuhudumia magari yanayokadiriwa kufika zaidi ya 6000 kwa siku hizo mbili.
Pamoja na hayo, Mgaya alisema “ Tumeandaa warsha maalum kwa kina dada, tunatambua kuwa asilimia kubwa ya waendesha magari barabarani hivi sasa ni kina dada, tunataka waelewe ni nini cha kufanya pindi atakapopatwa na hitilafu kwenye gari mabarabarani. “
Elimu hii ambayo wameiita ‘Auto First Aid’, alisema itasaidia kupunguza uharibifu zaidi kwenye magari yao, alisema wakati mwingine kwenye dashboard ya gari kuna kuwa na alama za hatari, lakini kwa kuwa gari inatembea wanawake wengi wamekua wakipuuzia alama hizo na matokeo yake wanasababisha hasara kubwa zaidi.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Milembe Insurance, Dioniz Diocles (wa kwanza kulia) akiongea mbele ya waandishi wa habari kuelezea jinsi walivyoona umuhimu wa kudhamini tamasha hilo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo, Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha, Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
“Pamoja na kuwafundisha alama za hatari na nini cha kufanya pindi waonapo alama hizo pia Tutawafundisha kubadilisha matairi, na nini chakufanya na kuwa nacho ikitokea gari limewaharibikia njiani. “ alisema Mgaya.
Mgaya ambaye amefanikiwa sana katika ufundi wa AC za magari, Ndege, na Meli, aliongeza kuwa fani ya ufundi makenika ni kazi ya kuheshimika kama zilivyo kazi nyingine, na kuongeza kuwa anaiona fursa kubwa kwa vijana wanaomaliza elimu ya juu.
“Siku hizi magari yote kuanzia Mwaka 2005 kwenda juu yanatumia vifaa maalum vya computer na internet, pamoja na kuwa maelezo yanakuja kwa lugha ya kingereza, ufundi spana wa kurithishwa hivi sasa hauna nafasi,”alisema.
“Tofauti na zamani ukifeli form 4, unapelekwa kwenye ufundi hali hivi sasa imebadiliilka fani hii inahitaji wasomi na watu wanaoweza kubadilika na kurudi shuleni kila mara, kama computer matoleo ya magari kila mwaka yanakuja na vitu tofauti, hivi sasa break hazina annoying sound, break zikiisha utaona kwenye dashboard, kutengeneza lazima useme user manual ya kingereza na u download soft ware kwenye internet,” alisema Mgaya na kusistiza vijana waingie kwenye fani hii.
Aidha Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo walisema kuwa, Automobile Clinic litakuwa zaidi ya Tamasha.
“Katika kuhakikisha tunautumia muda wa wateja wetu vizuri, wakati gari inafanyiwa ufundi, kutakuwa na huduma nyingine za ziada zitakazo patikana siku hizo mbili, kutakuwa na vinywaji, vyakula kama nyama choma, na michezo ya watoto, kutakuwa na huduma ya kulipia ya kuoshewa magari, kusafishiwa taa, na baadhi ya vifaa kama Fire extinguisher, manukato ya gari, Triangle na kadhalika vitauzwa hapo uwanjani,”
Jahu alisema Tiketi zitauza kabla, na kwamba tiketi hizo zitakuwa katika mfano wa sticker ya kubandika kwenye magari, na zitapatikana katika vituo vyote vya kuweka mafuta vya TSN, Supermarket zote za TSN, Kwenye ofisi za Millembe insurance, Bon to shine, BM hair cutting salon, na Mlimani City.
“Hakutakuwa na Kiingilio kwa watu, lakini badala yake kwa magari, magari yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia na kupata huduma hizo, tunashauri wenye kununua sticker wafike mapema kwani watakao fika kwanza ndio watakao hudumiwa,”
Jahu alisema katika kurudisha kwa jamamii, mafundi hao hamsini baada ya Tamasha watatembelea kwenye hospitali ya CCBRT kusaidia wakina mama wenye matatizo ya fistula.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Milembe insurance, Wambi lube oil distributor, TSN, Binslum tires company Limited, I view, Cocacola, Dreams Limited, Hugo Domingo, Olduvai Bay Wash, 0-60 autogarage, Meku Auto spear part, Dick Sound, Brand Tiger, Clouds FM, Auto Beats, Neh Catering, Pamoja na Lim Painting and decorating.

Thursday, September 18, 2014

FAINALI YA KOMBE LA MEYA 2014 NYAMAGANA JUMAMOSI HII HAPATOSHI

Kutoka juu ni Uwanja wa Nyamagana mahala ambako fainali ya Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 kati ya Mkolani Fc v/s Mirongo utachezwa.
Kikosi cha Mkolani Fc kilichoshuka dimbani jana kukiputa na Mnadani Fc, matokeo kikaibuka na ushindi wa bao 2-1, hivyo kusonga mbele katika hatua ya fainali ya Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, itakayochezwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Kikosi cha Mnadani Fc, kilichoshuka dimbani jana kucheza na Mkolani Fc matokeo kikakamuliwa bao 2-1, hivyo kucheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Sokoni katika Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, mchezo utakaochezwa kabla mchana kabla ya fainali jumamosi hii kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Wadau wa Michezo waliofurika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kushuhudia mchezo wa nusu fainali kati ya Mkolani v/s Mnadani Fc.
Pepsi Kombe la Meya ni michuano iliyoasisiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula, ikisimamiwa na Kampuni ya May way Entertainment.
Mashabiki .
Diwani wa kata ya Mirongo Mhe. Mkama (mwenye tracksuit ya blue) juzi alikuwepo uwanja wa Nyamagana pindi timu toka kata yake Mirongo Fc iliposhuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Sokoni, ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 2-1.
Wanahabari dimbani.
Diwani wa kata ya Mirongo Mhe. Mkama (mwenye tracksuit ya blue) juzi alikuwepo uwanja wa Nyamagana pindi timu toka kata yake Mirongo Fc iliposhuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Sokoni, ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 2-1. hapa akishangilia ushindi.
Diwani wa kata ya Mirongo Mhe. Mkama (mwenye tracksuit ya blue) na shangwe za kutinga fainali ambapo timu ya mirongo itashuka dimbani kukiputa na Mkolani jumamosi hii.(20/09/2014)
Waamuzi toka kituo cha elimu na michezo Alliance Academy Mwanza ndiyo wanaosimamia michuano  hii ya Pepsi kombe la Meya 2014.
Nahodha wa Mkolani Fc akizungumza na vyombo vya habari.
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Imeshafahamika kwamba timu ya soka ya Mkolani fc na Mirongo ndizo zitakazo kutana katika fainali ya kutafuta bingwa wa Michuano ya PEPSI Kombe la Meya 2014 Mkoa wa Mwanza, mchezo unaotaraji kutimua vumbi jumamosi hii ya tarehe 20 sept katika uwanja wa Nyamagana jijini humo.

Mchezo huo wa fainali utatanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baina ya Mnadani Fc na Sokoni. (ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA)


ZAWADI KWA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO:-
- Mfungaji bora wa mashindano kuondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
- Timu yenye nidhamu itaondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
- Refa bora wa mashindano shilingi laki mbili, ile hali mshindi wa tatu atalitwaa kombe, medali ya shaba na kitita cha shilingi milioni moja. 
- Mshindi wa pili wa michuano hiyo ataondoka na kombe, medali ya fedha na kitita cha shilingi milioni mbili.
- Bingwa atakabidhiwa Kombe, medali ya dhahabu na bajaji ya kisasa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba pia watu wanne yenye thamani ya shilingi milioni 4.5, 

MABINGWA WA SAFARI POOL 2014 WALIVYOPOKEWA.

Mabingwa wa mchezo wa Safari Pool 2014, Klabu ya Topland ya Mkoa wa Kimichezo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakipokelewa kwa shangwe na mashabiki mara baada ya kuwasili klabuni kwao Magomeni wakitokea mkoani Kilimanjaro jana.
Mabingwa wa mchezo wa Safari Pool wa Klabu ya Topland ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni Dar es Salaam wakishangilia kwa kucheza mara baada ya kuwasili klabuni kwao  Magomeni wakitokea Mkoani Kilimanjaro jana.
Meneja wa timu ya Topland, Isiaka Afande(kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Pool wa Mkoa wa kimichezo Kinondoni(KIPA), Goodluck Mmari mara baada ya kurejea na ubingwa wa fainali za mashindano ya Safari Pool 2014.
Mwenyekiti wa Chama cha Pool wa Mkoa wa kimichezo Kinondoni(KIPA), Goodluck Mmari (kulia) akimkabidhi mkurugenzi wa klabu ya Topland,Fredrick Kiando kikombe mara baada ya timu ya Topland ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Pool Taifa 2014 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Kilimanjaro