Kutoka juu ni Uwanja wa Nyamagana mahala ambako fainali ya Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 kati ya Mkolani Fc v/s Mirongo utachezwa. |
Wadau wa Michezo waliofurika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kushuhudia mchezo wa nusu fainali kati ya Mkolani v/s Mnadani Fc. |
Pepsi Kombe la Meya ni michuano iliyoasisiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula, ikisimamiwa na Kampuni ya May way Entertainment. |
Mashabiki . |
Wanahabari dimbani. |
Diwani wa kata ya Mirongo Mhe. Mkama (mwenye tracksuit ya blue) na shangwe za kutinga fainali ambapo timu ya mirongo itashuka dimbani kukiputa na Mkolani jumamosi hii.(20/09/2014) |
Waamuzi toka kituo cha elimu na michezo Alliance Academy Mwanza ndiyo wanaosimamia michuano hii ya Pepsi kombe la Meya 2014. |
Nahodha wa Mkolani Fc akizungumza na vyombo vya habari. |
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Imeshafahamika kwamba timu ya soka ya Mkolani fc na Mirongo ndizo zitakazo kutana katika fainali ya kutafuta bingwa wa Michuano ya PEPSI Kombe la Meya 2014 Mkoa wa Mwanza, mchezo unaotaraji kutimua vumbi jumamosi hii ya tarehe 20 sept katika uwanja wa Nyamagana jijini humo.
Mchezo huo wa fainali utatanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baina ya Mnadani Fc na Sokoni. (ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA)
ZAWADI KWA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO:-
- Mfungaji bora wa mashindano kuondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
- Timu yenye nidhamu itaondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
- Refa bora wa mashindano shilingi laki mbili, ile hali mshindi wa tatu atalitwaa kombe, medali ya shaba na kitita cha shilingi milioni moja.
- Mshindi wa pili wa michuano hiyo ataondoka na kombe, medali ya fedha na kitita cha shilingi milioni mbili.
- Bingwa atakabidhiwa Kombe, medali ya dhahabu na bajaji ya kisasa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba pia watu wanne yenye thamani ya shilingi milioni 4.5,
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.