ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 22, 2010

ULINZI IMARA NA MAZINGIRA TULIVU NI MUHIMU KUFANIKISHA ZOEZI LA KUPIGA KURA.

MWONGOZO KWA WAPIGA KURA WENZANGU.
OCTOBER 31 KUWAKILISHA NDIYO HOJA. KATIKA KIPINDI HIKI TUKIELEKEA KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI, WATANZANIA WENGI TUMEKUWA NA WOGA HASA PALE TUNAPOKUTANA NA MAGARI MAPYA PAMOJA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKIWA NA NYENZO MPYA ZA KISASA KWA AJILI YA ULINZI NA USALAMA.

MENGI YAMEZUNGUMZWA MIONGONI MWETU LAKINI BLOG HII INAUNGANA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUWAONDOA HOFU WATANZANIA KUWA YOTE HAYA YANAFANYIKA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAKE, NA TEKNOLOJIA HII NDIYO INAYOTUMIKA KATIKA DUNIA YA SASA. AU TULIPENDA WALINZI WETU HAWA WABAKI NA VITENDEA KAZI VYA KARNE ILIYOPITA KWA KULINDA BILA VIZUIZI, ILE HALI WAVAMIZI NA MAJAMBAZI WAKIZAMA MASKANI ZETU KWA SILAHA ZA MOTO NA MITUTU YA HATARI?

KWA NYENZO KAMA HIZI HATA YULE MFANYA FUJO HATOKUWA NA JEURI KAMA VILE ASKARI ANGEMFUATA MFANYA FUJO HUYO AKA MHALIFU BILA NYENZO YAANI KAVUKAVU.

JESHI LA POLISI NI RAFIKI WA RAIA TUSHIRIKIANE NALO KUKOMESHA UHALIFU, HIVYO HATUNA HAJA YA KUOGOPA TUJITOKEZE KWA WINGI OCTOBER 31 2010 KUKAPIGA KURA.

Thursday, October 21, 2010

AFA USINGIZINI KWEUPEE!

MTU MMOJA (PICHANI) ANAYE SADIKIKA KUWA NI MLEMAVU WA AKILI ALIYEKUWA NA MAZOEA YA KUZURURA MITAA YA MWANZA AKIOKOTA OKOTA AMEKUTWA AMEKUFA PEMBEZONI MWA BUSTANI YA JIJI KARIBU NA KITUO CHA MAFUTA GAPCO MKOANI MWANZA.

NILIPITA MAENEO HAYA MAJIRA YA SAA 2:30 ASUBUHI NA KISHA BAADAE SAA 4 MTU HUYU AKIWA AMELALA MAHALA HAPA AKIWA ANAHEMA, LAKINI MUDA HUU WA JIONI SAA 10:10 NIKAJIULIZA HUYU BWANA MASAA YOTE HAYA BADO KALALA NDIPO JAMAA WALIO KARIBU NA ENEO HILI WAKANAMBIA TAYARI KESHAKUFA MASAA MENGI YAMEPITA, POLISI WANATAARIFA LAKINI CHA AJABU HAWAJAJA KUMTOA.

PICHANI WANANCHI WAKIUANGALIA MWILI WA MTU HUYO.
KATIKA ZAMA HIZI VIJANA WENGI AMBAO NI NGUVU KAZI YA TAIFA WAMEKUWA WAKIPOTEA KWA STYLE KAMA HII KWA KUKATA TAMAA YA MAISHA PINDI PALE WANAPO KUTANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA AJIRA NA UGUMU WA MAISHA HALI INAYOSABABISHA WENGINE KUTAFUTA NJIA ZA MKATO KWA KUJITUMBUKIZA KTK VITENDO VYA UHALIFU ILIJIPATIA MALI. TATIZO ZAIDI NI PALE WANAPOSHINDWA KUFANIKISHA MALENGO YAO KUPITIA HIZO NJIA HATARI ZA MKATO.
LAZIMA UPATE UCHIZI.

PAMOJA NA KULA MABOMU NA KUCHEZEA VIRUNGU, CHADEMA YAFANYA KAMPENI MWANZA.

NI MKUTANO ULIOANZA KWA SHAKASHAKA NA KUMALIZIKA KWA AMANI. MKUTANO ULIOTOA FURSA KWA MGOMBEA URAIS TIKETI YA CHADEMA DR. W.SLAA KUZINADI SERA ZA CHAMA HICHO NA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA UBUNGE WILAYA ZA NYAMAGANA NA ILEMELA SAMBAMBA NA WAGOMBEA UDIWANI KWA WILAYA ZOTE HIZO MBILI.

MWANA CHADEMA AKISOMESHA MKUTANONI.

HATIMAYE MKUTANO WA KAMPENI CHADEMA MWANZA UMEFANYIKA JANA JIONI KWA AMANI KATIKA UWANJA WA MAGOMENI KIRUMBA MARA BAADA YA JUHUDI ZA MKUTANO HUO KUFANYIKA KATIKA UWANJA MKUBWA ZAIDI WA FURAHISHA KUSHINDIKANA.
WANANCHI WAKITAABIKA KUONA TUKIO KUTOKANA NA UWANJA HUO KUJAA KUPITA KIASI.

KABLA YA MKUTANO HUU KUFANYIKA KATIKA VIWANJA HIVI KAMATI YA MAANDALIZI CHADEMA ILIFIKA KATIKA UWANJA WA FURAHISHA KUANDAA JUKWAA, DAKIKA KADHAA WATU WA INJILI NAO WAKAFIKA KIWANJANI PALE NAO KUANZA KUANDAA JUKWAA LAO WAKIDAI NDIO WENYE KIBALI KUTUMIA UWANJA HUO TENA KIBALI CHA WIKI YOTE HADI KUFIKIA JUMAPILI. WAKATI HAYO YAKIFANYIKA WANAINJILI HAO WAKAWASILIANA NA JESHI LA POLISI AMBALO KWAO HAIKUCHUKUWA MUDA KUWASILI ENEO LA TUKIO. MSIMAMIZI WA UCHAGUZI AKATOA TAARIFA MKUTANO USIFANYIKE FURAHISHA, MAJIBIZANO YA MANENO YA HAPA NA PALE YAKATAWALA HATIMAYE PURUKUSHANI ZILIZO LITIKISA ENEO NA KUTISHIA AMANI LAKINI MWISHO WA SIKU CHADEMA WAKAHAMIA UWANJA HUU WA MAGOMENI NA MKUTANO UKAFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU HUKU JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LIKILINDA PANDE ZOTE ZA ENEO LA MKUTANO KWA KUKAA MITA 100.

PAA LA CHOO CHA VIWANJA HIVYO VYA MAGOMENI LINAPOGEUKA KUWA JUKWAA LA WANANCHI.

HAIKUTOSHA HADI NGUZO ZA MAGOLI.

UCHAGUZI MKUU TANZANIA KUFANYIKA OCTOBER 31 MWAKA HUU 2010.

Monday, October 18, 2010

SIMBA MWENYEJI APOKEA KICHAPO TOKA KWA MGENI YANGA KUPITIA MZAWA TEGETE.

ILIKUONESHA KUWA ILIKUWA NI UFUNDI, BAADA TU! YA NONG'ONEZO HILI JERRY TEGETE AKAIPATIA TIMU YAKE GOLI LA USHINDI.

MASHABIKI WA YANGA AFRIKA NA SHANGWE ZAO.

SEHEMU YA MASHABIKI WA SIMBA WAKITIA HAMASA.

WATU WALIANZA KUINGIA UWANJANI MAJIRA YA SAA 4 ASUBUHI KWA FOLENI NDEFU BILA YA KUKATA TAMAA ZA KUINGIA UWANJANI KUSHUHUDIA KIPUTE.

MATUKIO YA KISHIRIKINA NAYO NI KAMA KAWA KWA SOKA LA BONGO ZOGO LILIZUKA MARA BAADA YA MASHABIKI WA YANGA KUMNASA SHABIKI MMOJA WA SIMBA AMBAYE ALIKUWA AMEAMBATANA NA MWEZAKE ALIYE TIMKA IKINASEMEKANA KUWA WALIKUWA KTK HARAKATI ZA KINYUNYIZA.

SHABIKI HUYO WA SIMBA ALISHUTUMIWA KUWA ALIPEWA FUKO LA UCHAWI TOKA KWA MGANGA WAKE LIKIWA NA MASHARTI YAKE NA ALIFIKA ENEO HILO AKINYUNYIZA KIMTINDO KWA NIA YA KUPATA USHINDI.

DUH! PEPA LIMELIKI! PICHANI MAELEKEZO YA MGANGA.

MASHABIKI WAKIMCHANIA BENDERA SHABIKI HUYO WA SIMBA TUKIO LILILOTOKEA MAPEMA KABISA MASAA MAWILI KABLA YA MECHI KUANZA.

HATIMAYE ASKARI POLISI WALIFIKA ENEO HILO NA KUMNUSURU SHABIKI HUYO INGAWA ALIACHA FUKO LAKE.

KUTOKA GAZETINI.GAZETI LA MWANASPOTI NALO LILIKUWA NA SHUHUDA WAKE NAYE AKARIPOTI....

SIMBA NA YANGA WALIPAMBANA KWENYE UWANJA WA CCM KIRUMBA JUMAMOSI YA 16.OCT.2010 KATIKA MECHI YA LIGI KUU TANZANIA BARA NA YANGA KUIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 LILILOFUNGWA NA JERRY TEGETE.