MWANA CHADEMA AKISOMESHA MKUTANONI.
HATIMAYE MKUTANO WA KAMPENI CHADEMA MWANZA UMEFANYIKA JANA JIONI KWA AMANI KATIKA UWANJA WA MAGOMENI KIRUMBA MARA BAADA YA JUHUDI ZA MKUTANO HUO KUFANYIKA KATIKA UWANJA MKUBWA ZAIDI WA FURAHISHA KUSHINDIKANA.
WANANCHI WAKITAABIKA KUONA TUKIO KUTOKANA NA UWANJA HUO KUJAA KUPITA KIASI.
KABLA YA MKUTANO HUU KUFANYIKA KATIKA VIWANJA HIVI KAMATI YA MAANDALIZI CHADEMA ILIFIKA KATIKA UWANJA WA FURAHISHA KUANDAA JUKWAA, DAKIKA KADHAA WATU WA INJILI NAO WAKAFIKA KIWANJANI PALE NAO KUANZA KUANDAA JUKWAA LAO WAKIDAI NDIO WENYE KIBALI KUTUMIA UWANJA HUO TENA KIBALI CHA WIKI YOTE HADI KUFIKIA JUMAPILI. WAKATI HAYO YAKIFANYIKA WANAINJILI HAO WAKAWASILIANA NA JESHI LA POLISI AMBALO KWAO HAIKUCHUKUWA MUDA KUWASILI ENEO LA TUKIO. MSIMAMIZI WA UCHAGUZI AKATOA TAARIFA MKUTANO USIFANYIKE FURAHISHA, MAJIBIZANO YA MANENO YA HAPA NA PALE YAKATAWALA HATIMAYE PURUKUSHANI ZILIZO LITIKISA ENEO NA KUTISHIA AMANI LAKINI MWISHO WA SIKU CHADEMA WAKAHAMIA UWANJA HUU WA MAGOMENI NA MKUTANO UKAFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU HUKU JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LIKILINDA PANDE ZOTE ZA ENEO LA MKUTANO KWA KUKAA MITA 100.
PAA LA CHOO CHA VIWANJA HIVYO VYA MAGOMENI LINAPOGEUKA KUWA JUKWAA LA WANANCHI.
HAIKUTOSHA HADI NGUZO ZA MAGOLI.
UCHAGUZI MKUU TANZANIA KUFANYIKA OCTOBER 31 MWAKA HUU 2010.
Tupe maoni yako
tuombe mungu uchakachuaji wa kura usiwepo
ReplyDeletekitakachotusaidia kuondokana na udhaifu wa cmm ni kuanza kuandaa wabunge kila wilaya ila wasomi wa vyuo vikuu tunatakiwa kuwaunga mkono chadema ili kuokoa ndugu zetu vijiji kwani ukweli tunajua.
ReplyDeletefrom monduli,hakuna aliye na afadhali