MBUNGE
wa Jimbo la Myamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ameutaka uongozi wa
Halmashauri ya Jiji la Mwanza kusitisha tamko na zoezi la kuwaondoa na kufanya
shughuli zao wafanyabiashara wa mbogambonga, matunda, majisafi, juisi na
mamalishe jijini humo kwa madai kuwepo ugonjwa wa kipindupindu na badala yake
kuwaelimisha kufuata kanuni bora za afya.
Mbunge Mabula
amesema hayo akiwa Mjini Dodoma kwenye shughuli za Bunge zinazoendelea baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo waliompigia simu kumpatia taarifa ili awasaidie juu ya tamko na zoezi linalofanywa na Halmashauri
kupitia Idara ya Afya ya Jiji hilo kuwazuia kufanya biashara katika maeneo
mbalimbali ya mitaa ya Kata 18 kutokana na tishio la kutokea kwa mlipuko wa
ugonjwa wa kipindupindu jambo ambalo wamedai
linawaathili katika kujitafutia kipato.
Mabula
akizungumza na Blog hii ameutaka uongozi wa Jiji hilo chini ya Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Tito Mahinya, kusitisha tamko na zuio hilo la na badala
yake wawaelimishe kwanza wananchi kupitia Idara yake ya Afya kwa kuwaeleza
wafanyabiashara wa mbogamboga, matunda, maji juisi na vyakula vingine kuepuka
kupanga dhidhaa zao sehemu zilizo safi na mamalishe watoe huduma ya chakula
katika mazingira bora na yaliyo safi kwa
kufuata kanuni bora za afya zilizopo.
“Wananchi
hao wanatakiwa kupewa elimu na kuelimishwa juu ya madhala ya ugonjwa wa
kipindupindu uliolikumba jiji letu kwa wiki tatu ambapo taarifa zilieleza watu saba walipatwa na ugonjwa
huo na walitibiwa na jana wameruhusiwa baada ya kuthibitika kuwa wamepona,
jambo hili likifanyika kwa kuwaeleza wananchi kutaondosha dhana na madai ya
kuonewa ikiwemo kuondolewa katika maeneo yao ya kufanyia shughuli zao za
kujiingizia kipato,”alisema.
Mabula
alieleza kwamba kufatia hali hiyo amewasiliana na Kaimu Mkurugenzi Mahinya kusitisha zoezi haraka na badala yake kupitia
Idara ya Afya kupita na kutangaza kwa wananchi kanuni bora za kuepuka mlipuko
wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoa elimu kwa wananchi hao jinsi ya kuzifuata
ikiwa ni kuuza matunda, mbogamboga, vyakula sehemu zilizo safi na wasipange
kwenye majimaji na mazingira safi.
“Mamalishe
ambao
wanahangaika kujitafutia kipato waelimishwe kwani wamekopa fedha za
mitaji na kuanzisha biashara zao ni vyema wakapewa elimu kuzifuata
kanuni bora za usafi katika
mazingira ya tishio la kipindupindu kwa kutengeneza chakula na kukiuza
kwa
wateja wao katika mazingira safi na salama ikiwemo kuhakikisha vyakula
saa zote
vinakuwa vya moto, kuwepo na jiko lenye sufuria la maji ya moto ambapo
ndani
yake kutawekwa sahani, vijiko na vikombe ambavyo mamalishe watavitumia
kuwapatia wateja wao chakula na siyo kuwaeleza wasitishe na kuondoka
kama
ilivyotangazwa ,”alisema.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi, Mahinya alieleza kuwa kutokana na kubainika
kuwepo ugonjwa wa kipindupimdu na watu saba kugundulika kupata ugonjwa huo
waliochukua hatua za kuwazuia wananchi hasa wafanyabiashara wa matunda,
mbogamboga na vyakula kupanga bidhaa zao chini sehemu zenye majimaji, lakini
pia kuwazuia mamalishe kuendelea kuuza chakula kwenye vibanda na masoko ya jioni yaliyo kwenye
mazingira machafu.
“Tumezungumza
na Mbunge Mabula baada ya kupigiwa simu na kupewa taarifa na wananchi kuwa
uongozi wa Halmashauri umewazuia kufanya biashara, lakini nimemuelewesha na
tumekubaliana kuwa tutatumia gari la matangazo kupita tena kuwaeleza wananchi jinsi
ya kufuata kanuni bora za mamalishe kutoa huduma ya chakula kwa wateja ili
kuepuka kuambukizwa ugonjwa wa kipimdupimdu na wauzaji wengine kufanya usafi na
kuacha kupanda vyakula chini kwenye
majimaji,”alisema.
Mahinya
amewataka wananchi kuzingatia taratibu na kanuni za afya ili kuepuka kupatwa na
ugonjwa wa mlipuko pia wadumishe utamaduni wa kufanya usafi na utunzaji
mazingira ili kuendelea kuliweka jiji katika taswila ma muonekano wa usafi
badala ya kukimbilia kulalamikia Halmashauri inapochukua hatua za kusitishwa
utolewawaji huduma kwenye mazingira hatarishi na yasiyo salama kwa wateja na
watumiaji kwenye baadhi ya maeneo ya masoko na vibanda vinavyotumiwa na mamalishe.