ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 20, 2015

MACHIMBO YA NYANGARATA YAFUNGWA KWA MUDA

Na Emmanuel Mlelekwa,
Novemba 19,2015.
KAHAMA
Wizara ya Nishati na madini imesitisha shughuli za uchimbaji katika machimbo ya Nyangarata yaliyopo wilayani kahama hadi hapo serikali itakaporuhusu shughuli za uchimbaji kuendelea.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Kamishina wa Madini Nchini Mhandisi Ally Samage katika kikao  cha tahmini baada ya kuopoa maiti ya mtu mmoja aliyekuwa amefukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyangarata.

Amesema serikali imelazimika kufanya hivyo ili kufanya upembuzi wa namna ya kuendesha machimbo baada ya mtu mmoja kufariki na wengine 15 kuopolewa kwa nyakati tofauti tangu kutitia kwake Oktoba 6 mwaka huu.

Insert…..Kamishina 1

Aidha amesema serikali imekuwa ikishirikiana na wachimbaji hivyo kutokana na majanga ya namna kama ilivyotokea katika machimbo ya Nyangarata yanatakiwa kuepukika kwa kuzingatia usalama wa shughuli za uchimbaji.

Insert……Kamishina 2

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo Vita Kawawa amesema tayari kamati yake imefanikiwa kuuopoa mwili wa marehemu aliyefarikina kuukabidhi kwa ndugu zake.

Hata hivyo amesema kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha afya za wahanga zinaimarika na zirejee katika hali zao za awali na kupata uwezo wa kufanya kazi ili kuendeleza familia zao,jamii na taifa kwa ujumla.
 Insert….DC



KAHAMA

Mahakama ya Mwanzo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imewahukumu Watu wawili Vifungo vya miezi 6 baada ya kukutwa na makosa ya wizi wa Beteri za minara mali ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya HALOTEL

Katika hukumu ya kwanza  hiyo iliyotolewa Novemba 17 mwaka huu, Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo  Herman Byalugaba amesema mahakama imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao ni Kampuni ya Halotel 

Awali mwendesha mashitaka kutoka kampuni hiyo Bw.Stephen Chacha  amemtaja mshitakiwa kuwa ni  Emmanuel Charles ambaye  amekutwa na hatia ya wizi wa Betri 3 zenye thamani ya shilingi milioni mbili laki saba katika kosa hilo lililotendeka Oktoba 30 mwaka huu

Hukumu ya pili imetolewa na  Hakimu Leah Kyomushula dhidi ya mtuhumiwa Humphrey Silvesta kifungo cha nje miezi 6baada ya kukutwa na hatia ya wizi wa betri 4 zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki saba uliofanyika Oktoba 30 mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.