Friday, October 28, 2022
SHIRIKA LA DSIK Tanzania LAKABIDHI MAHITAJI YA SHULE KWA WANAFUNZI JIJINI MWANZA.
DC MOYO ATOA MWEZI MMOJA KWA IDARA YA MIPANGO MIJI KUMALIZA MGOGORO WA KIUMAKI NA WANANCHI MKIMBIZI.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa maagizo kwa idara ya mipango mijikumaliza mgogoro wa ardhi katika mlima Igereke
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa maagizo kwa idara ya mipango mijikumaliza mgogoro wa ardhi katika mlima Igereke
Fausta Timoth Kitindi ni bibi anayekadiliwa kuwa na zaidi ya miaka miaka 70 akitoa malalamiko yake kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuhusu madai yake ya kudhurumiwa ardhi
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametoa mwezi mmoja idara ya mipango miji kuhakikisha wanatatua mgogoro ya mipaka katika eneo la mlima Igeleke uliopo kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa baina ya wananchi na kikundi cha uhifadhi wa mazingira KIUMAKI.
Akizungumza
kwenye Mkutano wa hadhara,mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa idara ya mipango
miji inatakiwa kufanya kazi haraka ya kuitambua mipaka ya mlima Igeleke na
maeneo ya wananchi.
Moyo alisema kuwa amegundua kuwa kuna mapungufu waliyoyabaini katika nakala ya mkataba uliowapa mamlaka KIUMAKI kujihusisha na uhifadhi katika eneo hilo hivyo ni muhimu ukapitiwa ili kujiridhisha.
Alisema kuwa kufuatia mapungufu ya kimkataba ikiwemo kuwepo kwa Mashaka ya uhalali wa mkataba huo baina ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na KIUMAKI na kuamuru mkataba huo kuwasilishwa katika ofisi mapema kesho asubuhi Ili uweze kupitia na kamati ya Ulinzi
Lakini pia mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliamuru kukamatwa Kwa Mtu yeyote atakayebainika kufanya shughuli za kibinaadam katika hifadhi ya Igeleke wakati huu serikali ikishughulikia Mgogoro baina ya Wananchi na kikundi Cha uhifadhi Cha KIUMAKI.
Moyo alimazia kwa kuwaomba wananchi wa mtaa wa Kihesa Kilolo A na B kuwa na subira wakati serikali ya wilaya ikiwa inautafutia ufumbuzi mgogoro huo.
Kwa upande wa wananchi wa Kihesa Kilolo A na B walisema kuwa kikundi cha KIUMAKI kimepora ardhi ya eneo hilo kwa kutumia mabavu kwa madai kuwa kikundi hicho kinachojihusisha na utunzaji wa Mazingira katika Mlima Igeleke yalipo makumbusho ya michoro ya kale.
Fausta Timoth Kitindi ni bibi anayekadiliwa kuwa na zaidi ya miaka miaka 70 alisema kuwa Amekuwa akikumbana na bughudha ya Mgogoro huu huku eneo aliloachiwa na wazazi wake pamoja sehemu kaburi kutajwa na kikundi hicho kuwa ni eneo lililo chini ya Hifadhi.
Awali Katibu wa KIUMAKI Filipo Mkwama alisema walichukuwa maeneo hayo na kuanza kuyaifadhi kwa kufuata taratibu na sheria za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na kuingia mkataba baina ya kikundi hicho na uongo wa Manispaa ya Iringa.
Hata hivyo Kaimu Afisa Ardhi wa Manispaa ya Iringa Priscus Shirima ameshauri baadhi ya masuala muhimu kufanyika huku akitoa hakikisho la kuanishwa Kwa mipaka ya eneo hilo.
MBUNGE KOKA AAHIDI KUWAPIGA JEKI UVCCM KIBAHA MJI KATIKA MIRADIYA MAENDELEO.
Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka wa katikati akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa UVccm Kibaha mji Ramadhani Kazembe wa kulia na kushoto kwake ni Katibu wa Uvccm.
Na Victor Masangu,Pwani
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewaasa vijana kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo iliwemo kubuni miradi mbali mbali ambayo itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kiuchumi.
Koka ametoa kauli hiyo wakati wakati wa kufungua mkutano wa kwanza wa Baraza la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini (UVVCCM) na kuhudhiliwa na viongozi mbali mbali wa chama.
Aidha koka aliongeza kwamba vijana wanapaswa kubadilika na kuaangalia namna ya kuweza kujiunga kwa pamoja katika vikundi ili waweze kuwezeshwa kupata fursa ya mikopo ambayo inatolewa na halmashauri.
"Vijana wa uvccm ni lazima kuanzisha na kubuni miradi mbali mbali kwa fursa ni nyingi za kuweza kujikwamua na uchumi na mm nitakuwa na nyinyi bega kwa bega katika kuwasaidia katika suala la maendeleo,"alisema Koka.
Pia alisema lengo lake kubwa kuwasaidia vijana hao endapo wakijiunga katika majukwaa na kuanzisha vikundi mbali mbali ili aweze kuvisapoti kwa Hali na Mali.
Pia aliwashauri viongozi kuwaunganisha vijana wa kada mbalimbali katika kila kata ili wajiunge na UVCCM na waweze kunufaika na fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata fursa za mikopo na ajira kwa wenye vigezo.
"Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana hao hivyo kuna umuhimu wa vijana kuwaunganisha kwa pamoja na kujiunga na Uvccm ili wanufaike na fursa zilizopo katika maeneo yao,"alisema Koka.
Kwa Upande wake mwenyekiti wa Uvccm Kibaha mjini Ramadhan Kazembe pamoja na mambo mengine amemuomba mbunge huyo kusaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu wa ccm
Kazembe alishidi kushirikiana bega kwa bega katika kuboresha maisha ya vijana na kuimalisha mahuziano mazuri ambayo yatasaidia kuleta chachu ya maendeleo.
Kadhali aliongeza kuwa ataweka mipango madhubuti ya kusimamia shughuli mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo sambamba na suala la kujenga amani.
Baraza hilo la UVCCM limehusisha uchaguzi wa kamati ya utekelezaji wajumbe watu pamoja na katibu wa hamasa mmoja na kufanya kamati hiyo kuwa na idadi ya wajumbe nane.
Thursday, October 27, 2022
MASHAIRI YA WIMBO JEEPS, LEX COUPS, MIMAZ & BENZ - LOST BOYZ
[Intro: Mr. Cheeks]
Yeah
LB fam finally up in this piece
Got my mans that put me on, you know what I'm sayin'
Want a shout out to the Uptown, know what I'm sayin'
Word up
MCA, this is how we do everyday
Me and Freaky Tah, hah
Pretty Lou, my man, Spigg Nice
We be getting down representing
So this is how we go
Let me let you know
How it be
In da, G-H-E, double T-O
Rhyme name ho
They be runnin' shit down the line
Hey, if you hear a mistake - rewind
[Verse: ]
Who's the best, who's the worst in this here rap game
For those who claim to be the best
I tear them out the frame
I'm representin' puttin' Queens on the map (you wear)
Devil's Springs, with some baggy jeans when I rap
Come up with a style that they call versatile
Don't treat me like no lame, I've been in this game for a while
I've seen alot a-come, I've seen alot a-go
I've seen a lot a-break, I've seen alot a-blow
A yo, it's a trip to see a nigga slip
Get a grip nigga, nigga get a grip, geta
You don't even know the half of my crew
To be talking, but you're talking and you act like you knew
Yo set it, you fuckin' crossed the line and hit the border
LB fam start attacking some attacking outa order
Put on your leather gloves, and hats and get your picture mats
And get the gats just in case you take it to the stacks
[Chorus: Lost Boyz]
Shout out to the Jeeps
It's the Lex Coups, Bimas and the Benz (and the Benz)
To all my ladies and my men (my men)
To all my peoples in the pen' (in the pen')
Keep your head up
And to the hoods (the hoods)
East coast, West coast and world wide (world wide)
Ain't nothing wrong with puffin' on la (on la)
And if you're with me let me hear you say "Ri-ght"
Verse Two:
Nowa- Now- Nowadays
Niggas' fronting like they ill (like they' ill)
Now bustin' caps ain't got a muthafucking thing to do with showing skill
Recognize
Nigga, what' you fronting for?
I know your style
You've never hit a blunt before
Oh, you're just another in the race (man you betta stop)
Fakin' gats, takin' up space
To me you're nothing but a needle in a hay stack
Listen kid, I've been doing this since way back
In the day, Ace Deuce Tre, at the best
Up to Zimbabwe, hey, who's the best?
I want the best to come test me
So I can release some stress from my chest, G
Is you down to go pound for pound
Toe to toe, blow for blow, round for round
I'm wonderin' 'cause I bring the thunder and the rain
Causing confusion to your brain
[Chorus: ]
Shout out to the Jeeps
It's the Lex Coups, Bimas and the Benz (and the Benz)
To all my ladies and my men (my men)
To all my peoples in the pen' (in the pen')
Keep your head up
And to the hoods (the hoods)
East coast, West coast and world wide (world wide)
Ain't nothing wrong with puffin' on la (on la)
And if you're with me let me hear you say "ri-ght"
[Verse: ]
Keep the shit live for the year Nine Five
I got more niggas in my tribe
Than theres beez in the bee hive
LB Fam everyday stay high
Mr. Cheeks, everyday high
Concentrate to get my shit straight, make us wait
Before it's too fuckin' late
The Lost Boyz, yeah that's who I be'z wit
That's who I runs wit
Who I smoke Treez wit
Pack your bags, head outta town
I'll be back around so be gone before sundown
From Jamaica comes a nigga named Cheeks
With techniques of the streets
Over rough neck beats
This room is going bounce about the Cheeks can't remember
I'm the muthafucker choppin' crews like a chainsaw
Talk what you what ta
Do what you gotta
Well let me tell you something man you can't do me nadda
[Chorus: Lost Boyz]
Shout out to the Jeeps
It's the Lex Coups, Bimas and the Benz (and the Benz)
To all my ladies and my men (my men)
To all my peoples in the pen' (in the pen')
Keep your head up
And to the hoods (the hoods)
East coast, West coast and world wide (world wide)
Ain't nothing wrong with puffin' on la (on la)
And if you're with me let me hear you say "ri-ght"
[Outro: ]
Now, if you listen to my album
You'll see we only deal
With the real deal street life
MSIKILIZE SHABIKI HUYU
NA ALBERT G. SENGO
TAREHE 25 October 2021 katu haitoweza kutoka vichwani mwa wapenzi wa burudani jijini Mwanza, kwani ni siku ambayo kiwanda chao tegemewa kinachozalisha burudani na chenye misosi havvy ya kila aina, The Cask Bar & Grill kiliungua na kuteketea kabisa kwa moto.
Ni mwaka mmoja sasa tangu kutokea kwa tukio hilo ambapo tarehe 29 itakuwa kilele, zawadi za kurejesha shukurani kwa wateja wake na burudani full kiwangu kushushwa kwa stage. Pata simulizi kabla ya siku yenyewe toka kwa shabiki.WATANZANIA YAPASWA KUOMBE MVUA
SWALA YA KUOMBA MVUA
Kila ugonjwa una tiba yake, ardhi ikiwa kavu na kupatikana ukame. Uislamu umeweka ibaada Maluum nayo ni (Swalatul IstisQai) ni Swala ya kumuomba Mwenyezi Mungu kuteremsha mvua. Leo Swala hii imesahulika kabisa katika Umma wa kislamu. Waislamu wakipata matatizo ya uhaba wa Mvua, moja kwa moja wanaelekea kuomba majini na mashetani. Mafundisho ya Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam yako wazi kabisa kuwaelekeza Waislamu katika njia ya Allah Subhaanahu wa Taala)wakati wowote na hali yoyote sawa wakati wa raha au shida. Kumtii Mwenyezi Mungu ndio mambo yote. Amesema Mwenyzi Mungu(Subhaanahu wa Taala:
{وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ}
“Na lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.” [Al-Maaida:66]
Na Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ} {الأعراف:96}
“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma” [Al-A’raaf:96]
Kumuasi Mwenyezi Mungu ndio sababu ya kuleta shari na kuondoka kwa baraka.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{ وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ} آل عمران:135
“Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao – na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua.” [Al-Imraan:135]
Ametaja Ibn Qayyim (R.A) baadhi ya maafa yanayoletwa na maasi; huleta udhalifu, huharibu akili, huwaondosha haya, hudhoofisha moyo, huondosha neema, hutia maradhi moyo, huleta nuksi, hupotosha ya moyo, hufanya moyo kuwa mdogo, huondosha karama, pia Baraka, na kulaumiwa, kutishika, huondosha hima ya kumcha Mwenyezi Mungu.
Ukame ni alama ya kuwa watu mbali na twaa ya Mwenyezi Mungu, na ishara ya kuzidi maasi. Hali ya anga inabadilika kutokana na maasi.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ} الروم:41
“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.“ [Al-Ruum:41]
Na anasema Anas bin Malik: (R.A.) Upepo ukiwa mkali hujulikana hilo kwa uso wa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam.
Amepokea Abu Huraira (R.A) hadithi: kutoka kwa Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)akisema: [Hakisimami Qiyama mpaka iondoke ilimu, na kuzidi Zilzaal, na zahama kuwa karibu, na kudhihiri fitna, na kuzidi mauaji, mpaka itakua kwenu mali nyingi]. Ufupisho ni kujirudi nafsi, na kuomba msamaha kwa Allah pamoja na kufuata sheria za Allah(Subhaanahu wa Taala).
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{ يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ} القيامة:13-15
“Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.” [Al-Qiyama:13-15]
Na neno lake Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam akisema: [Tunajilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wa nafsi zetu, na uovu wa matendo yetu].
Imepekewa kwa Masahaba wakisema: Alitusalisha Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)swala ya usubuhi Hudeibiyah kukiwa na mawingu usiku, baada ya hapo akatukabili na kusema: Je mnajua alivyosema Mwenyezi Mungu? Wakajibu maswahaba: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua. Akasema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam: [Baadhi ya waja wangu wamekua waumini ni wale waliosema tumeteremshiwa mvua kutokana na fadhila zake Mwenyezi Mungu, na makafiri tumeteremshiwa mvua kutokana na nyota fulani].
Wednesday, October 26, 2022
SIMULIZI YA BALOZI ALIYESHUHUDIA CASK IKITEKETEA MPAKA MAJIVU.
NA ALBERT G. SENGO
TAREHE 25 October 2021 katu haitoweza kutoka vichwani mwa wapenzi wa burudani jijini Mwanza, kwani ni siku ambayo kiwanda chao tegemewa kinachozalisha burudani na chenye misosi havvy ya kila aina, The Cask Bar & Grill kiliungua na kuteketea kabisa kwa moto.
Ni mwaka mmoja sasa tangu kutokea kwa tukio hilo ambapo tarehe 29 itakuwa kilele, zawadi za kurejesha shukurani kwa wateja wake na burudani full kiwangu kushushwa kwa stage. Pata simulizi kabla ya siku yenyewe.MAGONJWA YA MACHO NA TIBA ZAKE - ST CLARE HOSPITAL MWANZA WAFUNGUKA
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
IDAARA ya macho ina sehemu kuu mbili nazo ni kliniki ya macho na chumba cha upasuaji wa macho. Jeh yapi magonjwa ya macho yanayo wakuta wengi? Vipi kwa wachomeleaji vyoma watumiao moto wenye wmanga mkali? Wako salama kiasi gani? Ungana na madaktari wataalamu wa Hospitali ya St. Clare inayopatikana Nyahingi Mkolani Jijini Mwanza.SERIKALI YATANGAZA VIJIJI VITANO, VITONGOJI 41 KUONDOLEWA HIFADHI YA USANGU
Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta wanaoushughulikia migogoro ya Matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisoma majina ya vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha magwalisi kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilaya ya Mbarali kuhamishwa ili kupisha hifadhi.
SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeeo ya Makazi imetangaza kwamba vijiji vitano na vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha Magwalisi ambacho kipo kwenye Mamlaka ya Mji mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali wananchi wanatakiwa kuhamishwa ili kupisha hifadhi.
Akitangaza uamuzi huo leo Oktoba 25 mwaka 2022 ,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angelina Mabula amesema katika uamuzi huo pia vitongoji vitatu katika kijiji cha Lualaje wilayani Chunya navyo vinatakiwa kuondoka kupisha hifadhi.
Akieleza zaidi mbele ya wananchi wa Ubaruku wilayani Mbarali wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta walipofanya ziara kwenye eneo la Mto Ruaha Mkuu ,Dk.Mabula amesema lengo la uamuzi ni kutunza na kulinda ardhi oevu na vyanzo vya kupokea na kutunza maji yanayotiririka kutoka mito mbalimbali.
Dk.Mabula amevitaja vijiji vitakavyoondoka kwa asilimia 100 ni Madundasi, Luhanga, Iyala, Msanga pamoja na Kalambo yo vina idadi ya wakazi 21,252 na kusisitiza watu wa maeneo hayo wanatakiwa wasiwepo na usajili wa vijiji hivyo kufutwa.
Ameongeza kwamba kwenye mchakato huo wapo ambao watalipwa fidia na wengine ambao hawastahili Kulipwa fidia wataondoka kama walivyokwenda huku akisisitiza lengo la Serikali ni kuwa na urithi wa watu wote."Mnakumbuka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikuja na kuahidi kushughulikia migogoro ya ardhi ,Sasa tumekuka na uamuzi ambao tutaomba."
Pamoja na hayo amesema pia Serikali imeridhia vijiji 15 ambavyo vina ukubwa wa hekta 74, 324.12 na ranchi ya Usangu ya NARCO vitaendelea kubaki wakati vijiji vingine vyote vinavyopakana na hifadhi ya Ruaha kutawekwa mipango mikakati ya mpango wa matumizi ya ardhi.
"Kwenye mapendekezo ya timu ya wataalamu ilipendekeza Ranchi ya Usangu ambalo linalopendekezwa kuondolewa ndani ya hifadhi litumiwe na wafugaji watakaohamishwa kutoka kwenye vijiji na vitongoji vinavyopisha hifadhi, " amesema Dk.Mabula.
Pia ameeleza Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya za Mbarali na Chunya pamoja na wadau wanatakiwa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji vyote vinavyopatikana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Kwa mujibu wa Dk.Mabula TAMISEMI inatakiwa kushirikiana na wadau muhimu wakati wa mchakato wa usajili wa vijiji na vitongoji kwa ajili ya kuondokana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza na kusababisha malumbano yasiyo na tija.
Kuhusu bonde la Uhifadhi wa Bonde la Usangu imeelezwa kwamba ulianza mwaka 1953 na wakati huo kama pori tengefu la Utengule lenye ukubwa wa kilomita za mraba 500 kwa lengo la kuhifadhi bioanuwai katika ardhi oevu ya Ihefu.
kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira na vyanzo vya maji uliofanyika miaka ya 1990 serikali iliamua kupandisha hadhi pori tengefu la utengule na kuwa Pori la Akiba la Usangu likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 4148 kwa tangazo la serikali namba 436A la tarehe 24 julai 1998.
Pamoja na hayo amesema Serikali imekuja na mpango wa kitaifa wa hifadhi ya mazingira ya ardhi oevu na vyanzo vya maji mwaka 2006 na kutaka bonde la Usangu kuwa kati ya maeneo ambayo wafugaji waliovamia mabonde na maeneo ya vyanzo vya maji waondolewe.
Baadi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ubaruku,Mbarali mkoni Mbeya leo Oktoba 24,2022.
Baadi ya Wananchi wakiondokoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ubaruku,Mbarali mkoni Mbeya leo Oktoba 24,2022 ambapo Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wa Wizara nane za Kisekta wanaoushughulikia migogoro ya Matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisoma majina ya vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha magwalisi kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilaya ya Mbarali kuhamishwa ili kupisha hifadhi.
Timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiongozwa na Mwenyekiti wao Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Homela walipokwenda kutazama na kujionea hali halisi ya upungufu mkubwa wa maji katika mto Ruaha Mkuu leo Oktoba 24,2022,Mbarali mkoani Mbeya.
Tuesday, October 25, 2022
RC DR ES SALAAM ATANGAZA HALI YA UKAME KATIKA MTO RUVU.
PPROFESA MKENDA ASEMA WANAFUNZI SABA WALIBADILISHIWA NAMBA ZA MTIHANI.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa ni kweli mwanafunzi wa Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary, Iptisum Slim pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasala saba.
Profesa Mkenda amebainisha hayo leo Jumanne Oktoba 25, 2022 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Uchunguzi uliofanywa na Kamati ya Uendeshaji Mitihani ya Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wataalamu wa maandishi kutoka Jeshi la Polisi (Forensic Bureau) umebainika jumla ya watahiniwa saba walibadilishiwa namba za mtihani katika kituo cha mtihani namba PS1408009 shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic” amesema Profesa Mkenda
Uchunguzi huo ulifanywa baada kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim wa kituo cha mtihani cha shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic akieleza kwamba, alibadilishiwa namba yake ya mtihani wakati akifanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) uliofanyika Oktoba 05 na 06/10/2022.
Profesa Mkenda amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo Serikali kupitia Baraza la Mitihani ilielekeza Kamati ya Uendeshaji Mitihani ya Mkoa wa Pwani kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko ya mtahiniwa na kuwasilisha taarifa Baraza la Mitihani.
Amesema kuwa uchunguzi uliofanyika pia umebaini kuwa mwanafunzi huyo pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasala saba.
“Mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim alifanya masomo matano kwa kutumia namba PS1408009/0040 na somo la sita (mwisho) kwa kutumia namba PS1408009/0039 na Watahiniwa wengine wanne pia walibadilishiwa namba katika somo la sita katika kituo hicho,” amesema.
Profesa Mkenda pia amesema Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary iliyoko mkoani Pwani imefungiwa kuwa kituo cha mtihani kwa muda usiojulikana.
Vilevile, Profesa Mkenda ameagiza watumishi waliohusika na udanganyifu katika mtihani wa darasa la saba Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary kuchukuliwa hatua.
Pia, Profesa Mkenda ameiagiza Necta kumefanya marekebisho ya namba za mitihani za watahiniwa husika ili kila mtahiniwa aweze kutunukiwa matokeo yake halali.
“Nisisitize kuwa shule yoyote itakayobainika kufanya vitendo vya udanganyifu wa mitihani, itafungiwa na hata kufutwa kabisa kuendesha shughuli za elimu nchini,” anasema.