ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 28, 2022

MBUNGE KOKA AAHIDI KUWAPIGA JEKI UVCCM KIBAHA MJI KATIKA MIRADIYA MAENDELEO.

Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka wa katikati akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa UVccm Kibaha mji Ramadhani Kazembe wa kulia na kushoto kwake ni Katibu wa Uvccm. 

Na Victor Masangu,Pwani 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewaasa vijana kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo iliwemo kubuni miradi mbali mbali ambayo itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kiuchumi.


Koka ametoa kauli hiyo wakati wakati wa kufungua mkutano wa kwanza wa Baraza la umoja wa vijana wa chama  cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini (UVVCCM) na kuhudhiliwa na viongozi mbali mbali wa chama.


Aidha koka aliongeza kwamba vijana wanapaswa kubadilika na kuaangalia namna ya kuweza kujiunga kwa pamoja katika vikundi ili waweze kuwezeshwa kupata fursa ya mikopo ambayo inatolewa na halmashauri.


"Vijana wa uvccm ni lazima kuanzisha na kubuni miradi mbali mbali kwa fursa ni nyingi za kuweza kujikwamua na uchumi na mm nitakuwa na nyinyi bega kwa bega katika kuwasaidia katika suala la maendeleo,"alisema Koka.


Pia alisema lengo lake kubwa kuwasaidia vijana hao endapo wakijiunga katika majukwaa na kuanzisha vikundi  mbali mbali ili aweze kuvisapoti kwa Hali na Mali.


Pia aliwashauri viongozi kuwaunganisha  vijana wa kada mbalimbali katika kila kata ili wajiunge na UVCCM na waweze kunufaika na fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata fursa za  mikopo na ajira kwa wenye vigezo.


"Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana hao hivyo kuna umuhimu wa vijana kuwaunganisha kwa pamoja na kujiunga na Uvccm ili wanufaike na fursa zilizopo katika maeneo yao,"alisema Koka.


Kwa Upande wake  mwenyekiti wa Uvccm Kibaha mjini Ramadhan Kazembe pamoja na mambo mengine amemuomba mbunge huyo kusaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu wa ccm


Kazembe alishidi kushirikiana bega kwa bega katika kuboresha maisha ya vijana na kuimalisha mahuziano mazuri ambayo yatasaidia kuleta chachu ya maendeleo.


Kadhali aliongeza kuwa ataweka mipango madhubuti ya kusimamia shughuli mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo sambamba na suala la kujenga amani.


Baraza hilo la UVCCM  limehusisha uchaguzi wa kamati ya utekelezaji  wajumbe watu pamoja na katibu wa hamasa mmoja na kufanya kamati hiyo kuwa na idadi ya wajumbe  nane.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.