Saturday, January 22, 2011
BANGO
FBG; wanahiphop toka chuga chuga wafungua mwaka na concious joint kuelezea hali halisi ya taifa le2 na maisha ya mtaa yanavotupelekesha huku viongozi wanafuja fedha ya mlipa kodi,Ngoma hi inakwenda kwa jina "inaniuma kwa roho" na imerekodiwa pande za noizmekah s2dio arachuga na harakati za kushoot video yake zilikwama kutokana na fujo kuzuka mjini arusha siku hiyo hiyo ilopangwa kushoot...FBG wanamalizia tape yao itayotolewa "FREE" na itakwenda kwa jina "codemixxing",collection hiyo itajumuisha pia wimbo huu na nyinginezo kibaona mwezi wa tatu mashabiki wategemee vibe za kumwaga
Thursday, January 20, 2011
HABARI
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Saidi Mwema kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, wametoa jumla ya shilingi milioni 3200000/= kwa askari 31 walioshiriki katika tukio la kupambana na majambazi lililotokea desemba 29 mwaka jana katika kijiji cha kanyama wilaya ya Magu mkoani hapa.Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro akikabidhi cheti na pesa taslimu kwa mmoja wa polisi walioshiriki zoezi la kupambana na majambazi wezi wa magari, mapambano yaliyotokea katika Kijiji cha Kanyama, Kata ya Kisesa wilayani Magu, mkoani Mwanza.
Sherehe fupi ya kuwapongeza Askari hao iliyokwenda sanjari na kuwakabidhi fedha na kuwatunuku vyeti imefanyika leo asubuhi katika uwanja wa polisi mabatini jijini Mwanza na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za wilaya na mkoa.
"Jeshi la polisi ngazi ya mkoa tulipanga kutoa kiasi hicho cha fedha nilichokitaja lakini mkuu wetu wa kazi IGP Mwema kwa kutambua kazi nzuri waliyo ifanya vijana hawa akaongeza sh, 50,000/= kwa kila mmoja, vivyo leo tutawakabidhi shilingi lakimoja kila mmoja na kwa wale majeruhi wawili watakabidhiwa shilingi lakimoja na elfu hamsini kila mmoja" Kaimu kamanda wa pilisi mkoa wa Mwanza Nonosius Komba Akiongea wakati wa kumkaribisha mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Kamanda Komba amesema hali za majeruhi wote wawili zinaendelea vizuri ambapo PC Erasto aliyejeruhiwa kwa risasi katika paja na mkono wake wa kulia ameruhusiwa kutoka hospitalini wakati CPL jumanne aliyepigwa risasi mbili begani katika mkono wake wa kushoto anaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya BugandoGwaride la jeshi la polisi.
Wakati mgeni rasmi akihutubia, askari huyu aliyekuwa yummoja kati ya waliokuwa wamesimama wima ktk rigwaride wakisikiliza hotuba alianguka ghafla, Pichani akipelekwa eneo la huduma ya kwanza.
Aidha mkuu wa mkoa wa Mwanza amewataka wananchi kuheshimu utawala wa sheria kwa vile nchi inaongozwa kwa misingi ya kanuni na taratibu za utawala bora, wananchi waachane na dhana mbaya ya kuchukuwa sheria mkononi bali wanapomtuhumu au kumkamata mhalifu ni vyema wakamkabidhi mikononi mwa polisi ili sheria zichukuwe mkondo wake.
Picha ya pamoja askari waliotunukiwa na kaimu kamanda wa polisi.
Picha ya pamoja viongozi wa serikali pamoja na askari waliotunukiwa.
Pichani kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa TBL, David Minja pamoja na Katibu Mkuu wa BASATA, Gonche Materego wakizindua rasmi tuzo za kilimanjaro Tanzania music Award 2011 mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia hafla hiyo. Wanaoshuhudia kulia ni Mratibu wa tuzo hizo kutoka BASATA, Angelo Luhala pamoja na Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro, George Kavishe.
HABARI ZAIDI TEMBELEA BLOGU YA JIACHIE
Wednesday, January 19, 2011
HABARI
Kamanda wa jeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameshutumiwa kwa kuongoza ubakaji wa wanawake takriban 50 uliofanyika hivi karibuni.Kumekuwa na ripoti nyingi za ubakaji huko Congo lakini tukio hili linaaminiwa kuwa la kwanza kwa idadi kubwa ya wanawake kubakwa likihusishwa jeshi. Mmoja wa waliobakwa, pamoja na vyanzo vilivyonukuliwa katika ripoti ya umoja wa mataifa, wote wanamshutumu Lt Col Kibibi Mutware kwa kuhusika na ubakaji huo uliofanyika mwaka mpya mjini Fizi.
Dr Faise Chacha, mkuu wa hospitali ya Fizi ameeleza, " Askari mmoja aliuawa hapa karibu kabisa na hospitali hii." "Hiyo ilisababisha wasiwasi na wagonjwa wetu wote wakakimbia. Tulirudi siku ya pili asubuhi na tukaanza kuwapokea watu waliokuwa wamepigwa kisu na wengine- wanawake- waliobakwa." Dr huyo na shirika la kitabibu la kutoa msaada Medecins Sans Frontieres wamewatibu waathirika 51 waliobakwa mpaka sasa.
Kama ilivyo kwa matukio ya awali huko Congo, wengi wanatarajiwa kuficha yaliyowasibu kuepuka kuachwa na waume na familia zao. Wawili miongoni mwa wanawake hao walikubali kuzungumza na BBC ilimradi tu wasitajwe majina yao.
Mmoja aliiambia BBC, " Nilibakwa mbele ya watoto wangu wanne." "Ninaona aibu, ninaona aibu sana. Nikikutana na watu wawili au watatu ambao wanajadili jambo, naanza kuhisi tu kuwa wananizungumzia mimi, hata kama si kuhusu mie."
Mwanamke huyo mwengine alifanikiwa kumtambua aliyembaka. "Ilikuwa jioni na walionibaka walikuwa wanajeshi," alisema kwa sauti ndogo, mwili wake ukiwa umefunikwa na khanga yenye rangi za kuvutia. nakuongeza kwa kusema " Walikuwa wanne- Kibibi na walinzi wake. Wameiba vitu vyetu vyote pamoja na pesa."
HISANI YA BBC SWAHILI.
Wednesday, January 19, 2011
BANGO
(a)
(b)Mambo vipi mdau? hope uko poa kabisa mashine hii inauzwa ni mpya imo kwenye box lake, Naiweka hewani kwa atakayekuwa tayari kununua tafadhali anaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi, 0756-162161 or 0762-854444 au kwa maelezo na details zote zaidi wanaweza kutembelea jojosssfashions.blogspot.com
Asante sana nakutakia kazi njema na kila la kheri.
Wednesday, January 19, 2011
BANGO
Tuesday, January 18, 2011
HABARI
Polisi mkoani Mwanza, imewakamata watu wawili akiwamo afisa wa wanyama pori, Allchraus Jacob (31),na Kasika John (44) ambaye ni mkuluma wa wilayani Bunda, wakijaribu kuuza pembe za kifaru maarufu kwa jina la George (12) akifahamika kama faru wa Rais Jakaya Kikwete, aliyeuawa na majangili, Desemba mwaka jana. Jeshi hilo limekamata Vipusa vya Faru vikitembezwa sokoni kutafuta Mteja, Inasemekana kuwa pembe hizi za faru (Vipusa) hutumika kutengenezea dawa ya kuongeza nguvu za Kiume huko katika nchi za Falme za Kiarabu, Japan, Korea na hata china ambako vinasoko kubwa sana.
#####WAKATI HUO HUO jeshi la polisi mkoani mwanza lanawashikilia watu wanne, wawili kati yao wakiwa na bunduki aina ya SMG na risasi 64 ambazo zilikuwa zimefichwa ndani ya begi la nguo zikisafirishwa kwenda wilayani Geita..Kaimu wa polisi amesema kuwa watuhumiwa ambao walikamatwa na begi hilo la silaha walijitambulisha kama mke na mume na kwamba walikuwa wakielekea katika kijiji cha Bukondo wilayani Geita.
Ndani ya begi hilo kulikuwa na viatu vya kike, panga moja na shoka ambavyo vilikuwa vimefungwa katika mfuko wa sandarusi pamoja na vikaratasi vidogovidogo vilivyokuwa vimefungwa dawa mbalimbali za mitishamba ambavyo walidai kuwa ni hirizi za dawa za kusaidia wakati wa matukio ya ujambazi.
Baada ya kuwakamata watu hao waliweza kuwataja wenzao ambao walikuwa bado hawajaondoka Mwanza kuungana nao katika shughuli zao za uharamia, ambao nao waliweza kukamatwa eneo la Nyegezi wakiwa na mkakati wa safari kuelekea ambako walipanga kufanya uhalifu mwingine..
Monday, January 17, 2011
BANGO
Ni mtangazaji wa The no One Radio Station in Southern Highland...87.8...88.2 & 94.7 EBONY fm.
Vwalaa! MARAFIKI WA UKWELI MTAFUTENI MDAU WENU WA UKWELI MKAMTUNUKISHE UVUMBA pia na MANEMANE.
Happy borzei braza.
Monday, January 17, 2011
HABARI
Hatimaye waziri Mkuu wa Tanzania mh. Mizengo Pinda amesuluhisha mgogoro uliokuwepo baina ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na wahadhiri wa chuo hicho, kuhusu maslahi yao na wamekubali kuingia madarasani kuanzia leo Jumatatu, Januari 17, 2011.“Nimeongea na viongozi wa UDOMASA na kuwaahidi kuwa madai yenu ya posho yanaweza kukamilika mwezi wa Februari, nilitaka yaishe mwezi huu lakini kwa taratibu za HAZINA sasa hivi wameshaanza kushughulikia mishahara ya mwezi wa Januari kwa hiyo marekebisho yenu hayawezi kuwahi…wameniahidi mwezi ujao yatakamilika”, alisema huku akishangiliwa na wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA).
Amesema amemwita Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua taarifa za mahesabu ya chuo hicho ili kubaini tuhuma zilizojitokeza za watu kulipwa hundi mbili za mishahara, walioacha kazi kuendelea kuwemo kwenye payroll ya mishahara, na wengine kukosekana kabisa kwenye payroll.
Kuhusu madai ya wanafunzi ya matatizo ya maji, Waziri Mkuu alisema amemwagiza Naibu Katibu Mkuu (Fedha) Bw. John Haule, afuatilie uhamisho wa ndani wa fedha katika Wizara ya Maji ili zipatikane sh. bilioni 1.66 zinazohitajiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dodoma (DUWASA) kuchimba visima maeneo ya Ng’ong’ona na Ihumwa ikiwa ni pamoja na kutandaza mabomba hadi chuoni ili kupunguza shida ya maji haraka iwezekanavyo.
Pia alisema katika mipango ya muda mrefu, DUWASA pia wanataraji kupata dola za Marekani milioni 26 ambazo zitatumika kuchimba visima vingine na kujenga matanki yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 12 za maji na hivyo kuondoa kabisa tatizo la maji chuoni hapo. Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimweleza Bw Pinda, mahitaji halisi ya maji chuoni hapo ni lita milioni 3.5 kwa siku ambazo kati ya hizo, lita milioni 1.5 ni kwa matumizi ya wanafunzi peke yao na lita nyingine milioni mbili ni kwa matumizi ya ujenzi wa majengo unaoendelea chuoni hapo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Bw. Idd Mwerange alimwahidi Waziri Mkuu watarudi madarasani wakati wakisubiri madai yao yakamilishwe bali aliomba kuwe na uwakilishi wa UDOMASA katika timu ya watu watakaonana na CAG.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Monday, January 17, 2011
HABARI
Habari zimetapakaa kutoka Johannesburg nchini Afrika kusini zikidokeza kuwa , uvumi umezagaa jijini humo kuwa Raisi wa zamani wa nchi hiyo Mzee Nelson Mandela yu taabani anaumwa na hali yake ni majaaliwa.Msemaji wa mfuko wa Nelson Mandela Sello Hatang amekanusha taarifa hizo siku ya jumamosi na kusema Mzee Mandela mwenye miaka 92 alikuwa katika mapumziko na mkewe Graca Machel na kwamba walikokwenda na wanachokifanya ni siri yao wawili na ni haki ya faragha kwa kila mwanadamu nayo inapaswa kuheshimiwa.
Hata hivyo kuna habari kuwa hali ya mzee huyo imezorota mno na wengine wamekuwa wakiwasiliana wakisema kuwa amekufa jambo ambalo limekanushwa vikali na watu wake wa karibu.
Hata hiyo vyanzo vya uhakika vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimeonyesha kuanza kukubaliana na uvumi huo.
Source wa habari: www.news24.com/SouthAfrica