ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 19, 2011

TAMKO LA WANA CCM TAWI LA KAMBARAGE SAUT KUHUSU KATIBA: WAMPONGEZA JAKAYA.

Halmashauri ya ccm tawi la kambarage ya chuo cha Mt. Agustino (SAUT) imempongeza Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa hekima na busara katika salamu zake za mwaka mpya alizozitoa tarehe 31dec2010 kwa kuunda tume ya kuratibu mchakato wa katiba mpya."Katika salamu za zake Mh.Rais aliridhia kuanzisha mchakato wa katiba mpya kwa mstakabali mwema na mapenzi ya dhati kwa watanzania kwaajili ya kulinda maslahi ya watanzania. Sisi tawi la ccm chuo kikuu cha mtakatifu Agustino Mwanza tunampongeza mheshimiwa Rais kwa hatua yake hiyo ya hekima na busara" kauli ya Mwenyekiti wa tawi hilo Silvester Yaredi.

SILVESTER YEREDI.Ushauri pia umetolewa kwa watanzania kuwa mchakato wa katiba mpya usije ukawa chanzo cha kuvunjika kwa umoja na amani yetu tuliyojiwekea kwa miaka mingi. Tuepushe hisia zetu za kisiasa, kikabila na kidini kwani katiba mpya ni kwa manufaa ya watanzania wote bila kujali itikadi ya dini, kabila wala rangi.

Vipengere vingine ndani ya salamu hizo za pongezi vinasema:- Tubishane kwa hoja kwa nia ya kujenga taifa letu na si kubomoa. Katiba mpya iwe chachu ya kuleta mabadiliko katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Bila kujali itikadi za vyama wanachuo wa chuo cha SAUT Mwanza kwa hivi sasa wanaendelea na mijadala na makongamano kuijadili katiba ya sasa, kung'amua mapungufu yaliyomo, kuorodhesha mapendekezo, hatimaye pindi itakapo fika wakati wapate kuyawasilisha kunakohusika.

Halmashauri hiyo ya ccm tawi la kambarage SAUT, kwa upande wake imekubali kuwa katiba ya sasa inamapungufu. "Upungufu uko kutokana na wakati" Aidha tawi hilo limeiomba tume itakayoundwa kuratibu mchakato huo wa katiba ifanye kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa ili nchi ipate katiba nzuri inayojali na kukidhi matakwa ya watanzania wote.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.