Polisi mkoani Mwanza, imewakamata watu wawili akiwamo afisa wa wanyama pori, Allchraus Jacob (31),na Kasika John (44) ambaye ni mkuluma wa wilayani Bunda, wakijaribu kuuza pembe za kifaru maarufu kwa jina la George (12) akifahamika kama faru wa Rais Jakaya Kikwete, aliyeuawa na majangili, Desemba mwaka jana. Jeshi hilo limekamata Vipusa vya Faru vikitembezwa sokoni kutafuta Mteja, Inasemekana kuwa pembe hizi za faru (Vipusa) hutumika kutengenezea dawa ya kuongeza nguvu za Kiume huko katika nchi za Falme za Kiarabu, Japan, Korea na hata china ambako vinasoko kubwa sana.
#####WAKATI HUO HUO jeshi la polisi mkoani mwanza lanawashikilia watu wanne, wawili kati yao wakiwa na bunduki aina ya SMG na risasi 64 ambazo zilikuwa zimefichwa ndani ya begi la nguo zikisafirishwa kwenda wilayani Geita..Kaimu wa polisi amesema kuwa watuhumiwa ambao walikamatwa na begi hilo la silaha walijitambulisha kama mke na mume na kwamba walikuwa wakielekea katika kijiji cha Bukondo wilayani Geita.
Ndani ya begi hilo kulikuwa na viatu vya kike, panga moja na shoka ambavyo vilikuwa vimefungwa katika mfuko wa sandarusi pamoja na vikaratasi vidogovidogo vilivyokuwa vimefungwa dawa mbalimbali za mitishamba ambavyo walidai kuwa ni hirizi za dawa za kusaidia wakati wa matukio ya ujambazi. Baada ya kuwakamata watu hao waliweza kuwataja wenzao ambao walikuwa bado hawajaondoka Mwanza kuungana nao katika shughuli zao za uharamia, ambao nao waliweza kukamatwa eneo la Nyegezi wakiwa na mkakati wa safari kuelekea ambako walipanga kufanya uhalifu mwingine..
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.