ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 4, 2019

KISIWA KILICHOKUMBWA NA TUKIO LA AJALI YA MV NYERERE CHAANGUKIWA NA NEEMA HII


WAKAZI wa Bwisya wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wamemshukuru rais JOHN MAGUFULI kwa kuboresha kituo cha afya BWISYA kilichopo katika kisiwa cha UKARA wilayani UKEREWE mkoani MWANZA.

Wakazi hao hao wametoa shukrani hizo wakati wa ziara ya kikazi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELA amabaye ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani UKEREWE.

 Zikijadiliwa changamoto zilizomo kwenye mradi, ni ana kwa ana, hapa ni maswali na majibu mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, injinia wa mradi (mwenye shati jeupe) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Boniphace Maghembe (kushoto) na Mkurugenzi wa wilaya hiyo Bi. Ester Chaula.
 Mazingira ya mmoja kati ya ward zilizojengwa.
 Hatua kwa hatua.
 Jengo moja wapo kwaajili ya huduma za afya.
 Moja kati ya majengo yaliyojengwa kwenye kituo hiki cha Afya Bwisya.
 Tanki kubwa la maji limejengwa hapa.
 Jengo la Mochari..


Hivi ndivyo sehemu tu ya mazingira kwa kituo cha afya Bwisya kinavyoonekana kwa sasa.

SUDAN: VYAMA VYA UPINZANI NA CHAMA TAWALA VYAAFIKIANA.


Chama tawala na vyama vya upinzani nchini Sudan, vimekubaliana kujipa muda wa miezi sita ili viweze kuunda serikali ya pamoja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jumuiya ya ushirikiano wa maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki na pembe ya Afrika IGAD makubaliano hayo yaliyofanyika siku ya Ijumaa ni sehemu ya mazungumzo ya amani yaliyotiwa sahihi mwezi Septemba mwaka jana.

Jumuiya hiyo ambayo imekuwa ikisaidia kusimamia mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili imesema makubaliano mapya yatawasilishwa kwenye baraza la mawaziri huko Juba wiki ijayo.

MSIBA TENA KATIKA RHUMBA.




Mwanamuziki maarufu nchini DR Congo, Mose Fan Fan amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo akiwa nyumbani kwake. Mose mwenye umri wa miaka 75 ambaye ni mtunzi wa wimbo wa Papa Lolo, tangu 2015 alikuwa akishirikiana na bendi ya Ketebul Music na tabu Osus.

PICHA: WAZIRI MKUCHIKA AWATEMBELEA WAJANE WA HAYATI SOKOINE.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akiongozana na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine na baadhi ya wanafamilia kuelekea kwenye kaburi la Hayati Sokoine alipoitembelea familia hiyo nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akisali na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine na baadhi ya wanafamilia kwenye kaburi la Hayati Sokoine alipoitembelea familia hiyo nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akimkabidhi kadi ya bima ya afya mjane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Nakiteto Sokoine alipowatembelea wajane wa Hayati Sokoine nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake

Friday, May 3, 2019

UDHANIAYE NDIYE KUMBE ..... MLEVI AMTWANGA MONGELLA SWALI KUNTU



WAHENGA wanamsemo wao 'Umdhaniaye ndiye kumbe siye' hapa wakimaanisha kuwa wengi iwe ndani ama nje ya jamii yetu huwa na tabia ya kuhukumu kwa kutazama muonekano wa nje ya mtu kwamba eti unatafsiri ubora wa mawazo ya mtu, laa hasha, hata walio dhoofu katika suala la muonekano wanaouwezo wa kuibua masuala yaliyo muhimu katika safari ya utatuzi wa changamoto.

Ni katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella aliyoifanya wilayani Kwimba kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwemo Afya, Elimu, Maji, Barabara, Viwanda, Uchumi na Biashara akiwa katika mkutano kwenye eneo la Hungumalwa anakutana na jamaa huyo aliyekuwa ameutupika nzwii aka kalewa (haikujulikana ni pombe gani) na kumpa kipaza sauti ili kuwasilisha hoja yake........kwani alionekana kupaza sauti kila mara kama mwenye shauku ya kutaka ufafanuzi wa jambo.

Katika ziara hiyo Mongella alikuwa ameandamana na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansour, Katibu Tawala wa Mkoa, Wataalamu wa idara mbalimbali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa.

Thursday, May 2, 2019

'TANZANIA IMEPATA PIGO SEKTA YA UWEKEZAJI' ASEMA MONGELLA


Wadau wengi wakiwemo viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wanayo mengi ya kuzungumza juu ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Dr. Reginald Mengi aliyefariki dunia alfajiri ya kuamkia siku ya Jumatano ya tarehe 2 Mei 2019.

Akiwa kwenye ziara yake ya kikazi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoa ni kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John V.K Mongella anamzungumzia marehemu Mzee Mengi.....

HISTORIA YA MENGI KWA UFUPI

Dr. Mengi alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Nkuu huko Machame, Kilimanjaro, Tanzania. Baba yake Mr. Abhraham Mengi alizaliwa Marangu, Kilimanjaro, Tanzania lakini baada ya babu yake kufariki ilitokea mivutano juu ya urithi hasa kwenye masuala ya ardhi alilazimika kuhamia Machame ambapo napo licha ya kukutana na changamoto nyingi lakini aliweza kukaa akatulia. Baba yake Mzee Abraham Mengi na mama yake Ndeekyo walibarikiwa watoto saba yeye Dr. Mengi akiwa kama mtoto wa tano kuzaliwa ambao ni Apaanisa, Elitira, Asanterabi, Karileni, Dr. Mengi mwenyewe, Evaresta na Benjamin.

Dr. Mengi alianza shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School. Katika maisha yake ya shule tukio kubwa analolikumbuka ni wakati shule yao ya Old Moshi ilipohamishwa kutoka Old Moshi, Kolila na kuhamia Moshi mjini.

Baada kumaliza shule ya sekondari alipata ufadhili wa KNCU(Kilimanjaro Native Cooperative Union), alikwenda Uingereza kuchukua masomo ya uhasibu. Dr. Reginald Mengi ni moja kati ya watanzania wa mwanzo kabisa kusoma UK, Scotland na kufanikiwa kuwa Mhasibu anayetambulika na Taasisi ya Wahasibu ya Uingereza na Walesi

Mwaka 1971 Reginald mengi alirudi Tanzania na kuajiriwa kwenye kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ambayo kwa sasa inajulikana kama Prince water house Cooper. Baada ya kufanya kazi muda mrefu kwenye kampuni hiyo akiwa kama chairman and partner mwaka 1989 aliondoka kwenye kampuni hiyo na kwenda kuanzisha kampuni yake. Dr. Reginald Abraham Mengi ni mwanzilishi, mmiliki na Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Limited na Taasisi ya teknolojia na ugunduzi ya IPP(IPP Institute of Technology and Innovation).

Kupitia kampuni yake hiyo Reginald Mengi aliweza kumiliki vyombo mbalimbali vya habari mfano kwa upande wa TV alimiliki ITV, EATV na Capital Tv na kwa upande wa Radio anamiliki Radio one, Capital radio na EATV radio. Dr. Reginald Mengi alimiliki magazeti kadhaa, mfano wa magazeti hayo ni Nipashe, kulikoni, Taifa letu , The Guardian , Financial time na Sunday observer.

Mwaka 1992 Dr. Mengi alianzisha makampuni mengi zaidi yaliyokuwa yanazalisha bidhaa mbalimbali za kawaida ambazo zilikuwa ni adimu sana kwa wakati huo. Alikuwa tayari anamiliki biashara kadhaa ambazo ni;- Tanzania Kalamu Company Limited, Anche-Mwedu Limited, Tanpack Industries Limited, Industrial Chemicals Limited ambacho baadaye ilibadili jina na kuitwa Bodycare Limited pamoja na Bonite Bottlers Limited.

-Mwaka 1981 Dr. Mengi alianzisha kampuni kubwa ya uwekezaji iliyokwenda kwa jina la Mengi Associates Limited ambayo mwaka 1988 ilibadili jina na kuitwa Industrial Projects Promotion Limited na baadaye IPP Limited. IPP Limited kwa sasa ni jina linalojulikana sana Tanzania. Dr. Mengi anasema karibia fedha yote anayotumia kuanzisha makampuni haya inatokana na faida inayopatikana katika kampuni zilizopo.

-Dr. Mengi alikuwa anasita sana kuwekeza katika vyombo vya habari kutokana na uhalisia wa mazingira ya kitanzania kisiasa lakini kufikia mwaka 1993 aliamua kuingia huko kwa kuanzisha Radio One, Itv kisha magazeti kama vile Nipashe, The Guardian n.k.

Reginald Mengi alimiliki viwanda baadhi ambavyo vinazalisha vinywaji mbalimbali hapa Tanzania. Alimiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji, Bonite Bottlers inayoongoza kwa kinywaji cha Coca-Cola na maji ya chupa ya Kilimanjaro. Dr. Mengi pia amewekeza katika madini, mafuta, gesi, gesi asilia, madawa, kilimo cha mboga mboga katika maeneo makubwa, magari(kuunganisha magari ya umeme), saruji na mambo mengine zaidi katika sekta ya utengenezaji(manufacturing sector).

Dr. Mengi amewahi pia kuwa katika nafasi kadhaa za uongozi wa umma ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa magazeti Tanzania(Chairperson of Tanzania Standard Newpapers); Kamishna wa kamati inayoshughulikia mishahara(Commissioner of Salary Review Commission); Mwenyekiti wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania(NBAA); Mwenyekiti wa Baraza la Taifa La Mazingira Tanzania(National Environmental Council of Tanzania (NEMC); Mwenyekiti wa Vyombo vya habari vya Jumuia ya Madola Tanzania(Chairman of the Tanzania Chapter Commonwealth Press Union(CPU)); Mkurugenzi wa bodi ya LEAD(Leadership for Environment and Development International); Kamishna wa kamati ya Ukimwi Tanzania (Commissioner of Tanzania Commission for AIDS(TACAIDS); Mwenyekiti wa Muungano wa viwanda Tanzania(Chairman of the Confederation of Tanzania Industries(CTI); Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki(Chairman of the East African Business Council); Mwenyekiti wa ICC Tanzania (a National Committee of the Intenational Chamber of Commerce); Na Mkurugenzi wa Bodi Ya Baraza la Biashara la Jumuiya ya Madola(Director of the Board of Commonwealth

Kuanzia mwaka 1987 Dr. Mengi amekuwa akisaidia upandaji miti kuzunguka mlima Kilimanjaro kwa sababu amekuwa akiona msitu ukipungua katika mlima Kilimanjaro. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2014 zaidi ya miti milioni 24 ilikuwa imepandw. Kwa mchango huu katika mazingira, Rais Mkapa alimchagua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la kusimamia Mazingira Tanzania(NEMC)National Environmental Management Council licha ya kwamba anatokea katika sekta binafsi.

Dr. Mengi hadi mauti unamkuta alikuwa ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania(Chairman of the Media Owners Association of Tanzania(MOAT) na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania(the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)

Dr. Mengi alikuwa mtu anayejulikana sana kwa kutoa sana misaada ya kijamii(philanthropist). Amepewa tuzo mbalimbali kitaifa, kikanda na kimataifa akitambulika sana kwa kazi yake ya kujitolea kwa watu. Amepewa tuzo ya “The Order of the United Republic of Tanzania” mwaka 1994 na “The Order of The Arusha Declaration of the First Class” zilizotolewa na Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania mwaka 1995. Amepewa tuzo ya “The Martin Luther King Jr. Drum Major for Justice iliyotolewa na Marekani mwaka 2008. Amepewa tuzo ya “The International Order of the Lions Club iliyotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Lions Club mwaka 2014; na “The 2012 Business For Peace Award” iliyotolewa na Taasisi ya Oslo Sweden ya “Business for Peace Foundation” baada ya kupendekezwa na kamati inayotoa tuzo za Nobeli.

Kwa kutambua juhudi zake za kupambana na rushwa na ufisadi nchini mwaka 2008 serikali ya Marekani ilimpatia tuzo ya “Martin Luther King Jr. Drum Major Award”

Mwaka 2014 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alimpatia Dr. Mengi tuzo ya taifa katika mambo ya kuisaida na kuiwezesha jamii hasa katika ujasiriamali wa kijamii “The National Philanthropy Award” katika sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mengi amefariki dunia akiwa kwenye matibabu Dubai, U.A.E, usiku wa kuamkia leo. Ameacha mke (Jacqueline Ntuabaliwe) na watoto watano ambao ni Regina, Rodnay, Abdiel, Jayde na Ryan. Watoto hao amezaa na Mercy Mengi pamoja Jackline Mengi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dk Mengi aliandika Aprili 10 kuwa yupo nchini India kwa ajili ya kupandikiza vinasaba (stem cell and genetic engineering), huku akiomba watu kumuombea ili kuweza kufanikisha matibabu hayo.

Dk Mengi alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa barani Afrika, ambapo sehemu ya utajiri wake aliuelekeza kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2014, utajiri wa bilionea huyo ulitajwa kuwa ni TZS trilioni 1.3 ($560 milioni).

Enzi za uwahi wake na katika shughuli zake aliweza kushinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa, pamoa na kuandika kitabu chake cha I Can, I Must, I will.

Kifo cha Dk Mengi kimetokea ikiwa ni miezi 6 tangu mke wake wa kwanza, afariki

Wananchi watakiwa kujitokeza kuchangia damu kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani



Na Thabit Hamidu, Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wanachi ndani ya Mkoa huo kuwa tayari kujitokeza katika Zoezi la Uchangiaji wa damu Salama linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

RC Ayoub alisema Zoezi hilo lina lengo la kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji Damu kutokana na maradhi mbalimbali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Vuga Mjini Magharib Unguja Ayoub alisema imekuwa utaratibu ambao umezoeleka kila ifikapo karibia na mwezi mtukufu wa Ramadhan  wananchi ndani ya Mkoa huo kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa vifo vitokanavyo na mahitaji ya Damu.

Pia aliongeza kuwa ukusanyaji wa damu salama una lengo la kuwasaidia wananchi katika kipindi cha kuelekea mwezi mtukufu wa mfungo wa ramadhani hasa kwa akina mama wanaojifungua na watoto ambao asilimia kubwa ndio wanaohitaji damu hiyo.

Alieleza kuwa katika kipindi cha mfungo huo wa ramadhani mara nyingi si vyema watu kuchangia damu kutokana na hali ya kiafya ambapo katika kipindi hicho cha mwezi mzima kumekuwa na mahitaji makubwa kwa kitengo cha damu salama ambapo kinahitaji ujazo wa unit 1700.

Katika hatua nyengine Mkuu wa Mkoa alisema kitengo hicho cha damu salama kimesha kusanya unit 1400 katika kipindi hichi kwa ajili ya kuelekea mfungo wa ramadhani na kwamba wameshatumia unit 400 kwa muda wiki mbili zilizopita hivyo bado kunahitajika kuchangia damu hiyo ili kufikia malengo hayo.

Zoezi hilo la Uchangiaji wa Damu Salama linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

HUU SIO UBINADAMU, MNAHATARISHA AFYA ZA WATOTO- RC MWANGELA

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akitazama makazi ya wananchi wa Mtaa wa Shule ulioko jirani na Shule ya Msingi Mlowo, Wilayani Mbozi ambapo takataka zimemwaga katikati ya makazi ya wananchi kabla ya kuagiza kufungwa kwa dampo hilo.
  Wananchi wa Mtaa wa Shule wakitazama takataka zilizomwagwa jirani na makazi yao mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela kupita mtaani hapo na kuagiza dampo hilo lifungwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ameagiza kushikiliwa na polisi kwa masaa 24 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo Seriadi Mbugi kutokana na kurundika takataka jirani na makazi ya wananchi pamoja na shule ya Msingi Mlowo na hivyo kuhatarisha maisha yao.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela amefikia uamuzi huo mapema leo wakati akifanya ukaguzi wa hali ya usafi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo na kukuta takataka zimemwagwa katikati ya makazi ya wananchi ikiwa ni siku saba tangu amuelekeze Kaimu Mkurugenzi huyo kuhakikisha mji huo unakuwa Msafi.
“Nilifanya Mkutano na wananchi wa Mji wa Mlowo na malalamiko yao makubwa yalikuwa mrundikano wa takataka na madampo katikati ya miji yao, nilimuagiza na kumpa siku saba Mkurugenzi wa Mji mdogo wa Mlowo kuhakikisha anausafisha mji huu lakini leo siku saba zimepita ninakagua na kukuta takataka zimemwaga katikati ya makazi ya watu, naambiwa watoto wanacheza na kuokota taka hapa, huu sio ubinadamu”, amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela
Ameongeza kuwa Mkurugenzi huyo amekiuka agizo lake na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi hao kwa kuwawekea takakata wananchi katikati ya makazi yao kinyume na taratibu za kiafya zinavyoelekeza.
“Huu sio utendaji wa serikali kabisa, licha ya Kaimu Mkurugenzi wa Mji Mdogo kukaa ndani, namuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha ndani ya masaa manne takataka hizo ziwe zimetolewa na dampo hilo lifutwe”, amesisitiza Brig. Jen. (Mst) Mwangela
Kwa upande wake mkazi wa mtaa wa shule Bi Salehemu Filimon Mwaihojo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea eneo hilo na kutatua kero hiyo kwakuwa wamekuwa wakipata hofu ya magonjwa kutokana na uwepo wa takataka hizo
“Hii ni wiki ya pili wanamwaga matakataka hapa, watoto wanachezea na kuokota makopo wanachota maji machafu na kunywa kwenye makopo hayo machafu wengine unakuta wanaokota kondomu zinazomwaga hapa wanapuliza wao wanajua mipira, kwakweli tulikuwa na hali mbaya, kwakuwa tuliona wametumwagia magonjwa hapa”, amesema Mwaihojo
Ameongeza kuwa dampo hilo lipo pia jirani na Shule ya Msingi Mlowo na hivyo wanafunzi hupita na kuchezea hapo hali ambayo wangeweza kudhuriwa na vipande vya chupa na taka ngumu zinazo mwagwa hapo huku wengine wakiokota na kula mabaki ya vyakula yanayotupwa hapo na hivyo kuhatarisha afya zao.

Tuesday, April 30, 2019

MADUDU YA MHANDISI YASABABISHA MONGELLA KUGOMA KUFUNGUA MRADI.


MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongella amekataa kata kata kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa mradi wa maji ulioko kata ya Maligisu, Tarafa ya Ibindo wilayani Kwimba mkoani hapa, akidai kuwa hataki kushikishwa mradi huo ambao ujenzi wake umekuwa wakusuasua huku ukigubikwa na mianya ya upigaji.

Ujenzi wa mradi huo umeanza tangu mwaka 2013 ambapo hadi hii leo hali ni tete.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TEMEKE LAZINDUA KAMPENI YA NINACHO, NAJUA KUKITUMIA


 Kamanda wa Viwanja vya Ndege wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini (ACF) Maria Kulaya, akisalimiana na Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete (kulia), alipowasili katika viwanja vya Mwembe Yanga, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia, iliyofanyika katika viwanja hivyo Temeke Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 30/04/2019  
 Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete akitoa hotuba kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam, mapema leo asubuhi tarehe 30/04/2019 
 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Temeke (ASF) Puyo Nzalayaimisi, akihutubia wananchi na wakazi wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 30/04/2019  
 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya akitoa salamu kwa niamba ya Makamanda wa Mikoa na Kumkaribisha Mgenia Rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 30/04/2019 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete (kulia) akimsikiliza Sajini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lugendo Rashidi (kushoto), alipotembelea Banda la kutolea elimu, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam, mapema leo asubuhi tarehe 30/04/2019
(Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji Makao Makuu)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MAKAO MAKUU

MAKOSA YASIRUDIWE UJENZI WA HOSPITALI YA ILEJE- RC MWANGELA

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akiwa amebeba tofali kabla ya kulipigiza chini ili kujua ubora wake, matofali hayo yatatumika katika Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ileje ambapo serikali imetoa shilingi bilioni 1.5 na wananchi wanachangia nguvu kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akikagua ujenzi wa mabweni katika shule ya sekondari ya Ileje ambapo serikali imetoa shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, madarasa na vyoo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ameutaka uongozi na watendaji wa Wilaya ya Ileje kusimamia ubora katika ujenzi wa Hospitali ya Ileje ili makosa yaliyojitokeza awali katika ujenzi wa hospitali hiyo, yasijirudie.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela ameyasema hapo mapema jana mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo serikali ilitoa shilingi bilioni 1.5 mwezi Disemba 2018 huku majengo yaliyo anza kujengwa yakionekana kuwa na hitilafu za baadhi ya nguzo kupinda na kuwa na nyufa.
“Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Madiwani na watendaji wote, jengo lilioanza kujengwa na kuwa na nyufa na kupinda pinda liwe funzo kwetu tuhakikishe makosa hayo yasirudie tena katika ujenzi unao endelea sasa, pia wataalamu wote msimamie taaluma zenu na hatutawavumilia endapo mtafanya tofauti” amesisitiza Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Ameongeza kuwa Wananchi wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wa kujitolea kwa ajili ya kujiletea maendeleo hivyo basi watendaji wasiwaangushe.
“Serikali imeleta fedha na wananchi wametoa nguvu zao, halafu sisi wataalamu tuiharibu kazi, mimi siko tayari kuona kazi inaharibika, kila mtalaamu atimize wajibu wake, wataalamu wa hospitali wasimamie ujenzi uendane na mahitaji ya hospitali lakini wahandisi wasimamie ubora wa majengo hayo”, ameelekeza Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema licha ya ujenzi wa Hospitali hiyo kuchelwa kuanza kwakuwa serikali ilitoa fedha mwezi Disemba 2018, ujenzi huo ufanyike kwa haraka na kwa viwango ili uwe na ubora unaotakiwa na sio kufanya haraka bila kuzingatia ubora huku akiahidi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara

Amewataka viongozi wa hospitali waliopewa fedha za ujenzi wa hospitali hiyo wawe waaminifu huku akiwataka madiwani kusimamia na kuhoji kwa kufuata taratibu ili waweze kufahamu kila senti ya fedha hizo imetumikaje pia viongozi hao watoe taarifa kwa madiwani kwani ndio wawakilishi wa wananchi ili kuepusha malalamiko kutokana na wananchi kutokuwa na taarifa sahihi.
Aidha Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema kuwa imefikia kipindi cha mavuno hivyo basi madiwani na watendaji wa halmashauri washirikiane katika kukusanya mapato kwani hali ya ukusanyaji mapato sio nzuri
Amewashauri wananchi wachukue tahadhari ya kutouza sana mazao yao kwakuwa si mikoa yote imevuna vizuri hiyvo bei ya mazao inaweza kuwa nzuri zaidi hapo mbeleni hivyo wasifanye haraka kuuza chakula chao na kusisitza kuwa hilo sio katazo kwa wananchi ushauri wa kuchukua tahadhari.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela  amewataka Madiwani wasikae na kero na malalamiko ya wananchi bali wawafikishie Wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ili kero hivo ziweze kutafutiwa ufumbuzi na pia wawahimize wananchi kujitokeza na kueleza kero, maoni na malalamiko yao.

Sunday, April 28, 2019

MONGELLA ATEMBEZA KUKU KUFANIKISHA HARAMBEE ALIYOMWAKILISHA MHE PINDA


Siku zote maamuzi magumu na kujitolea ndio hutupa matokeo makubwa yenye tija, sisi Binadamu tunakitu kinachoitwa woga, ni kitu kibaya sana kwani ndiyo chanzo cha wengi kushindwa kuyafikia mafanikio.

Wahenga walisema uoga wako ndiyo umaskini wako. 

Kwa kulijua hilo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella jumamosi Aprili 27, 2019 amemwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana wilayani Sengerema ambapo alilazimika kutembea kiti baada ya kiti, meza baada ya meza akimnadi kuku aliyetolewa na mmoja wa waalikwa na hata kufanikiwa kumuuza kuku huyo kwa kiasi cha shilingi laki 3 na elfu 8 na mia tatu hamsini (Tshs 308,350/=) suala lililokuwa gumzo kwenye kusanyiko hilo.
Harambee hiyo imelenga kukusanya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya kwaya ya “New Life” ya kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji Leonard Giligwa pamoja na gari kwa ajili ya Parishi ya Bomani wilayani humo ambapo zaidi ya shilingi milioni 20 zimepatikana ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi

RAIS MAGUFULI AWEKA HAMASA KWA SHULE ALIYOWAHI KUFUNDISHA


Katika moja ya hotuba alizotoa mwaka 1981, Mwalimu Julius Nyerere alisema watu waliopata fursa ya elimu wana wajibu wa kulipa fadhila kwa kile ambacho wengine wamewafanyia.

Alisema watu hao ni sawa na wale waliopewa akiba yote ya chakula ili wapate nguvu na kwenda kutafuta kingi zaidi wawaletee wenzao.

Alisema kuwa, watu hao wasipotimiza wajibu huo, watahesabika kuwa ni wasaliti.

Tofauti na alichosema Nyerere, leo Tanzania ina watu wengi waliopata elimu na mafanikio ya kimaisha, lakini wameshindwa kurudi katika jamii zao kuzisaidia au japo kuzipa mwongozo kuelekea kwenye mafanikio.

Moja ya sehemu muhimu katika jamii ni asasi za elimu, hususan shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na Serikali.

Licha ya shule hizi kuwa mhimili mkubwa uliojenga maisha ya watu wengi wenye mafanikio, watu hao wameshindwa kurudi kuzisaidia.

Shule nyingi za Serikali na za umma zina hali mbaya. Majengo yamechoka, taaluma imeporomoka. Serikali nayo inadai imeelemewa. Hakuna wa kuzinusuru shule hizi isipokuwa wale waliopitia katika shule hizo. Cha kusikitisha nao wamezipa kisogo.

Nyerere aliyasema haya kupitia mfano wa kisa kifupi cha kijiji ambacho kilitoa hazina yote kwa ajili ya kuwapa wachache wapate nguvu ya kwenda kutafuta ili warudi kuwasaidia walio wengi.

Zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mtihani wa Taifa wa kidato cha sita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli ametoa motisha ya ng’ombe watano na kilo 500 za mchele kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Sengerema, ili kuamsha ari ya uwezo wao wa kufikiri katika mitihani hiyo. 
"TH 1 ni nyumba aliyoishi Rais Magufuli wakati akifundisha Shule ya Sekondari Sengerema" 

Mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye aliye mwakilisha Mhe. Magufuli kuwasilisha hamasa yake kwa wanafunzi wa moja kati ya shule alizopata kuhudumu  Kanda ya Ziwa.

Hii ni shule ambayo JPM alipata kufundisha kabla ya kuingia kwenye uongozi nyanja mbalimbali za Serikali hatimaye kuwa rais wa nchi, ambayo imepata huduma ya kukarabatiwa kati ya shule nyingi kongwe hapa nchini zilizokarabatiwa kwa fedha za Serikali.

Kwaniaba ya wanafunzi wenzao 543 wa kidato cha 6 wanaotarajia kuanza mitihani yao May 6  mwaka huu kupitia ofa ya kitoweo na ubweche wanasema kati ya ma milioni ya wanafunzi nchi nzima wao ni akina nani mpaka zari hilo la hamasa kuwaangukia? Nao kahawakusita kufunguka yale yaliyomo sakafuni mwa mioyo yao…......

Sehemu ya wanafunzi wa Sjule ya Sekondari Sengerema iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

JESHI NA UPINZANI WAKUBALIANA KUUNDA BARAZA LA MPITO NCHINI SUDAN.


Watawala wa kijeshi nchini Sudan wamepata makubaliano na viongozi wa upinzani juu ya kuundwa kwa baraza la mpito linalojumuisha wanajeshi na raia, Mitaani maandamano yameendelea kulishinikiza jeshi kukabidhi madaraka.

Baraza la kijeshi lililochukua madaraka baada ya kuuangusha utawala wa muda mrefu wa Rais Omar al-Bashir pamoja na muungano wa upinzani, walifanikiwa Jumamosi kupata muafaka juu ya kuundwa kwa baraza la uongozi wa mpito, lenye wajumbe kutoka jeshi na upinzani wa kiraia.

Baraza hilo la kijeshi lenye wajumbe 10 lilikuwa limejitwisha majukumu ya kuongoza kipindi cha mpito cha miaka miwili, baada ya kumuondoa madarakani al-Bashir Aprili 11 kufuatia wimbi kubwa la maandamano ya umma kupinga utawala wake wa miongo mitatu.

Muungano wa upinzani ujulikanao kama 'Azimio la Uhuru na Mabadiliko' ambao unaongozwa na chama cha wanataaluma nchini Sudan ulianzisha mandamano makubwa  yaliyotaka utawala wa nchi uwekwe mikononi mwa raia, na kushinikiza kurejeshwa kwa demokrasia nchini mwao.

YANGA SC WAJA NA MFUMO MPYA.



Klabu ya Yanga SC imeanzisha mfumo mpya ndani ya kikosi chake kwa kutaka wachezaji wake wakutane siku moja kabla ya mechi ikiwa ni mfumo ambao unatumiwa na timu nyingi za mabara mengine likiwemo la Ulaya.

Mfumo huo umeanzishwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kwa kutaka timu hiyo kutokuwa na muda mrefu wa kukaa kambini kwa ajili ya kuepusha gharama kubwa za kambi ambazo wanatumia wanapokaa katika hoteli mbalimbali.

Zahera ambaye ni raia wa DR Congo amesema anataka kikosi chake kiwe na siku chache za kukaa kambini kwa ajili ya kuwapa wachezaji muda wa kupumzika na familia zao lakini pia kuepusha gharama kubwa wanazotumia katika kulipa hoteli na sehemu nyingine wanazoweka kambi.

“Kama itawezekana ndani ya kikosi kwa sasa ninataka tuwe tunakutana siku moja kabla ya mechi au muda mchache tu kabla ya kucheza mechi na kuachana na kambi za muda mrefu.

“Hali hiyo inafanywa na timu nyingi na inawafanya wachezaji wakae na familia zao, lakini pia inasaidia kuepusha fedha nyingi ambazo tunazitumia katika kuweka kambi,” alisema kocha huyo.