ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 28, 2019

YANGA SC WAJA NA MFUMO MPYA.



Klabu ya Yanga SC imeanzisha mfumo mpya ndani ya kikosi chake kwa kutaka wachezaji wake wakutane siku moja kabla ya mechi ikiwa ni mfumo ambao unatumiwa na timu nyingi za mabara mengine likiwemo la Ulaya.

Mfumo huo umeanzishwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kwa kutaka timu hiyo kutokuwa na muda mrefu wa kukaa kambini kwa ajili ya kuepusha gharama kubwa za kambi ambazo wanatumia wanapokaa katika hoteli mbalimbali.

Zahera ambaye ni raia wa DR Congo amesema anataka kikosi chake kiwe na siku chache za kukaa kambini kwa ajili ya kuwapa wachezaji muda wa kupumzika na familia zao lakini pia kuepusha gharama kubwa wanazotumia katika kulipa hoteli na sehemu nyingine wanazoweka kambi.

“Kama itawezekana ndani ya kikosi kwa sasa ninataka tuwe tunakutana siku moja kabla ya mechi au muda mchache tu kabla ya kucheza mechi na kuachana na kambi za muda mrefu.

“Hali hiyo inafanywa na timu nyingi na inawafanya wachezaji wakae na familia zao, lakini pia inasaidia kuepusha fedha nyingi ambazo tunazitumia katika kuweka kambi,” alisema kocha huyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.