Watawala wa kijeshi nchini Sudan wamepata makubaliano na viongozi wa upinzani juu ya kuundwa kwa baraza la mpito linalojumuisha wanajeshi na raia, Mitaani maandamano yameendelea kulishinikiza jeshi kukabidhi madaraka.
Baraza la kijeshi lililochukua madaraka baada ya kuuangusha utawala wa muda mrefu wa Rais Omar al-Bashir pamoja na muungano wa upinzani, walifanikiwa Jumamosi kupata muafaka juu ya kuundwa kwa baraza la uongozi wa mpito, lenye wajumbe kutoka jeshi na upinzani wa kiraia.
Baraza hilo la kijeshi lenye wajumbe 10 lilikuwa limejitwisha majukumu ya kuongoza kipindi cha mpito cha miaka miwili, baada ya kumuondoa madarakani al-Bashir Aprili 11 kufuatia wimbi kubwa la maandamano ya umma kupinga utawala wake wa miongo mitatu.
Muungano wa upinzani ujulikanao kama 'Azimio la Uhuru na Mabadiliko' ambao unaongozwa na chama cha wanataaluma nchini Sudan ulianzisha mandamano makubwa yaliyotaka utawala wa nchi uwekwe mikononi mwa raia, na kushinikiza kurejeshwa kwa demokrasia nchini mwao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.