ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 28, 2019

RAIS MAGUFULI AWEKA HAMASA KWA SHULE ALIYOWAHI KUFUNDISHA


Katika moja ya hotuba alizotoa mwaka 1981, Mwalimu Julius Nyerere alisema watu waliopata fursa ya elimu wana wajibu wa kulipa fadhila kwa kile ambacho wengine wamewafanyia.

Alisema watu hao ni sawa na wale waliopewa akiba yote ya chakula ili wapate nguvu na kwenda kutafuta kingi zaidi wawaletee wenzao.

Alisema kuwa, watu hao wasipotimiza wajibu huo, watahesabika kuwa ni wasaliti.

Tofauti na alichosema Nyerere, leo Tanzania ina watu wengi waliopata elimu na mafanikio ya kimaisha, lakini wameshindwa kurudi katika jamii zao kuzisaidia au japo kuzipa mwongozo kuelekea kwenye mafanikio.

Moja ya sehemu muhimu katika jamii ni asasi za elimu, hususan shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na Serikali.

Licha ya shule hizi kuwa mhimili mkubwa uliojenga maisha ya watu wengi wenye mafanikio, watu hao wameshindwa kurudi kuzisaidia.

Shule nyingi za Serikali na za umma zina hali mbaya. Majengo yamechoka, taaluma imeporomoka. Serikali nayo inadai imeelemewa. Hakuna wa kuzinusuru shule hizi isipokuwa wale waliopitia katika shule hizo. Cha kusikitisha nao wamezipa kisogo.

Nyerere aliyasema haya kupitia mfano wa kisa kifupi cha kijiji ambacho kilitoa hazina yote kwa ajili ya kuwapa wachache wapate nguvu ya kwenda kutafuta ili warudi kuwasaidia walio wengi.

Zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mtihani wa Taifa wa kidato cha sita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli ametoa motisha ya ng’ombe watano na kilo 500 za mchele kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Sengerema, ili kuamsha ari ya uwezo wao wa kufikiri katika mitihani hiyo. 
"TH 1 ni nyumba aliyoishi Rais Magufuli wakati akifundisha Shule ya Sekondari Sengerema" 

Mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye aliye mwakilisha Mhe. Magufuli kuwasilisha hamasa yake kwa wanafunzi wa moja kati ya shule alizopata kuhudumu  Kanda ya Ziwa.

Hii ni shule ambayo JPM alipata kufundisha kabla ya kuingia kwenye uongozi nyanja mbalimbali za Serikali hatimaye kuwa rais wa nchi, ambayo imepata huduma ya kukarabatiwa kati ya shule nyingi kongwe hapa nchini zilizokarabatiwa kwa fedha za Serikali.

Kwaniaba ya wanafunzi wenzao 543 wa kidato cha 6 wanaotarajia kuanza mitihani yao May 6  mwaka huu kupitia ofa ya kitoweo na ubweche wanasema kati ya ma milioni ya wanafunzi nchi nzima wao ni akina nani mpaka zari hilo la hamasa kuwaangukia? Nao kahawakusita kufunguka yale yaliyomo sakafuni mwa mioyo yao…......

Sehemu ya wanafunzi wa Sjule ya Sekondari Sengerema iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.