Siku zote maamuzi magumu na kujitolea ndio hutupa matokeo makubwa yenye tija, sisi Binadamu tunakitu kinachoitwa woga, ni kitu kibaya sana kwani ndiyo chanzo cha wengi kushindwa kuyafikia mafanikio.
Wahenga walisema uoga wako ndiyo umaskini wako.
Kwa kulijua hilo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella jumamosi Aprili 27, 2019 amemwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana wilayani Sengerema ambapo alilazimika kutembea kiti baada ya kiti, meza baada ya meza akimnadi kuku aliyetolewa na mmoja wa waalikwa na hata kufanikiwa kumuuza kuku huyo kwa kiasi cha shilingi laki 3 na elfu 8 na mia tatu hamsini (Tshs 308,350/=) suala lililokuwa gumzo kwenye kusanyiko hilo.
Harambee hiyo imelenga kukusanya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya kwaya ya “New Life” ya kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji Leonard Giligwa pamoja na gari kwa ajili ya Parishi ya Bomani wilayani humo ambapo zaidi ya shilingi milioni 20 zimepatikana ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.