|
Mkuu wa Chuo Cha IQRA Hamza Juma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa maafali ya tatu ya chuo hicho, wasomi 98 wamehitimu Astashahada na Shahada katika kozi mbalimbali za Utawala wa Biashara, Teknohama, Uhasibu, Manunuzi na Ugavi, Utenguzi mizigo Bandarini na usafirishaji, Mahusiano na Masoko. |
|
Meza kuu. |
|
Tunuku. |
|
Unastahili. |
|
Wahitimu. |
|
Na vyeti vyao. |
|
Naibu Meya wa jiji la Mwanza, John Minja akikabidhi cheti kwa mmoja kati ya wahitimu wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo cha Utawala wa Biashara na Teknohama cha IQRA, kilichopo Mabatini wilayani Nyamagana, jijini Mwanza.
|
MWANZA.
WASOMI hapa, wametakiwa kuacha kuiga tamaduni mbaya za
mataifa ya Magharibi, ikiwemo ndoa za jinsia moja, ambazo ni kinyume cha maadili
yetu na mila za kiafrika.
Wito huo ulitolewa juzi na Naibu Meya wa jiji la Mwanza,
John Minja wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo cha Utawala wa Biashara na
Teknohama cha IQRA, kilichopo Mabatini wilayani Nyamagana, jijini Mwanza.
Hivi karibuni kumekuwepo tetesi kwamba, baadhi ya wanafunzi
wanaume wa vyuo mbalimbali jijini Mwanza, tofauti na IQRA, wamekuwa
wakijihusisha na Ushoga.
Naibu Meya huyo alisema, wasomi wakiwemo wahitimu wa chuo
hicho, wanapaswa kuwa na tabia njema popote wawapo ikiwa pamoja na kufata
maadili na tamaduni za kiafrika, wakiiga mambo yasiyofaa ya mataifa ya
magharibi, watapotoka na kuongeza mmommonyoko wa maadili.
“Epukaneni sana na tabia za ushoga na ndoa za jinsia moja,
mambo hayo hata Marekani hayapo sana na Afrika hatuyahitaji kabisa, Uganda
wameyakataa sisi hapa ni kinyume cha sheria kabisa. Nyie mnaohitumu leo msiende
kubweteka, kajiendelezeni kielimu.” Alieleza Minja na kuwataka waliohitimu
taaluma ya Ugavi na Manunuzi wabishe hodi katika Halmashauri ya jiji la Mwanza,
waajiliwe.
Awali akimkaribisha Minja, Mkuu wa Chuo hicho Hamza Juma
alieleza kwamba, katika mahafali hayo ya
tatu, wasomi 98 wamehitimu Astashahada na Shahada katika kozi mbalimbali za Utawala
wa Biashara, Teknohama, Uhasibu, Manunuzi na Ugavi, Utenguzi mizigo Bandarini
na usafirishaji, Mahusiano na Masoko.
Juma alieleza kwamba, chuo chake kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
zikiwemo kukosa eneo la kujenga Chuo (wamepanga katika jengo la mtu binafsi), vifaa
vya kujifunzia kama Compiyuta na kumshukuru Minja ambaye aliahidi kushghulikia
kwa haraka wapate eneo la kujenga Chuo hicho.