Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Lena Hongole akiongea kwenye kongamano hilo lilofanyika katika kijiji cha Kisinga' kata ya Kising'a lakini pia viongozi mbalimbali walishiriki kongamano hilo.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Iringa Daktari Abery Nyamahanga akitoa neno kwa UWT wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama
cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Baadhi ya madiwani wa chama cha mapinduzi wakiwa wameshiriki katika kongamano hilo la UWT la kupongeza
Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama
cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Hii ndio ya pongezi iliyotolewa na UWT Iringa Dc kwa
Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama
cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Umoja wa wanawake wa CCM
(UWT) Wilaya ya Iringa wamefanya kongamano la kuunga mkono juhudi na kazi
zinazofanywa na Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama
cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Akizungumzia malengo ya
kongamano hilo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Lena Hongole amesema kuwa
Rais amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwa wananchi waliomchagua
2015.
“Sisi wanawake wa wilaya ya
Iringa tunampongeza sana Rais Daktari John Joseph Magufuli kwa kazi kubwa ya
kuleta maendeleo wananchi waliomchagua kwa kipindi hiki kifupi tangu aingie
madarakani”alisema Hongole
Hongole alisema kuwa Tanzania
inakuwa kimaendeleo kwa kasi kubwa kutokana na uongozi wa Rais ambapo
amefanikiwa kuwajenga watanzania kuwa wazalendo kwa kufanya kazi na kujituma
kuhakikisha wanapata maendeleo.
“Mafanikio yenye tija
tunayaona hivi sasa hivyo sisi kama wanawake hatuna haja ya kushindwa
kumpongeza Rais wetu ambaye amekuwa kiungo muhimu cha maendeleo ya nchi hii
hivi sasa” alisema Hongole
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Iringa Daktari Abery Nyamahanga amewapongeza wanawake hao kwa
kuunga mkono juhudi za Rais.
“Nyinyi akina mama mmekuwa
mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizi ambazo zinazaa matunda ya kuleta
maendeleo ndio maana tunaiona hata iringa inazidi kupata maendeleo kila kukicha
tunaona sura mpya ya maendeleo ya nchi” alisema Nyamahanga
Nyamahanga alisema kuwa Rais
Daktari John Joseph Magufuli amefanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi kwa
kuboresha sekta ya afya ,sekta ya elimu,uchumi,miundombinu na utalii na kufanikisha maendeleo haya
tunayoyaona hivi sasa.
“Hakuna mtanzania ambaye
haoni nini kinafanyika katika nchi hii kwa kila mtu mwenye macho na masikio
anajionea na kusikia maana hakuna ubishi kuwa Rais huyu amekuwa mzalendo kweli
kweli katika nchi yetu hii” alisema Nyamahanga
Nyamahanga aliwataka
wanawake hao UWT kukumbuka juu ya chaguzi zinazokuja hivi karibuni kuhakikisha
wanakuwa na Wagombea ambao wanakubarika katika jamii ili kuhakikisha CCM
wanashinda kwa kishindo.
“Wakina mama hakikisheni
kama mnasifa ahakikisheni mnajitokeza kwa wingi kushika nyadhifa mbalimbali
kwenye chaguzi hizi zinazokuja na kuhakikisha tunamuunga mkono mgombea wa CCM
na sio kutoka nje ya chama chetu” alisema Nyamahanga
Naye Diwani wa kata ya
Kising’a Bi Ritta Mlagala amesema toka mwaka 2015 hadi sasa wamefakiwa
kuboresha sekta ya afya na elimu kwa kutekeleza ilani ya CCM ya 2015 hadi 2020.
“Tumefanikiwa kujenga kituo
cha afya,kuendelea kujenga majengo mapya ya shule ya sekondari ya Ilambilole
iliyopo kata ya Kising’a na tumejenga madarasa manne na ofisi mbili katika
shule msingi kising’a hivyo hayo ndio maendeleo yanayofanywa na serikali ya
awamu ya tano” alisema Mlagala
Aidha Mlagala alisema kuwa
wameanza kujenga zahanati ya kijiji cha Mkungugu na nyumba ya waaguzi ambazo zote zinatarajia
kukamilika hizi karibuni licha ya kuwa na changamoto kadhaa ambazo zinatusukuma
kuhakikisha tunatafuta wadau watuunge mkono kumalizia.