ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 16, 2019

MKOA WA KWANZA KUTOKOMEZA MIFUKO YA PLASTIKI KUPATIWA Tsh. MILIONI 40


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano, Januari Makamba amesema watatoa motisha kwa mikoa itakayotokomeza kabisa mifuko ya plastiki itakapofika Julai Mosi mwaka huu kwa kuwapatia Tsh. Milioni 40 kwa mshindi wa kwanza huku mshindi wa pili akijinyakulia Tsh. Milioni 30 na watatu atakabidhiwa Tsh. Milioni 10.

Waziri Makamba amesema kuwa nchi ya Tanzania inaweza kufanikiwa azma hiyo kwa kuwa inazalisha mifuko mbadala ya karatasi ambayo hutumiwa kwa kiasi kikubwa na nchi jirani za Rwanda na Kenya kutoka Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.