ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 10, 2018

DIALLO ATOBOA SIRI YAKE YA KUDUMU KWENYE SIASA LICHA YA FITNA ZA MJINI



GSENGOtV

"Wana siasa ni wanasiasa tu unakuta mtu anakwenda Magu lakini anaamua kupitia Misungwi sishangai" (PITIA jigrafia ya jiji la Mwanza utaelewa) Asema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo wakati akifungua Kikao cha Kamati ya Siasa mkoa wa Mwanza kujadili Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu, tangu Uchaguzi Mkuu Octoba 2015 hadi mwezi November 2018.

Katika muhtasari wake wa kufungua kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha VETA Mwanza, Dkt. Diallo amefunguka pia juu ya maneno yanayo sambaa kuhusu hali tete ya mahusiano baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, kwamba hawaivi chungu kimoja.










Akizungumza mbele ya Kamati ya Siasa na huku akitizamana uso kwa uso na Mongella, Mhe. Diallo amesema "Huu mkoa wetu unaangaliwa na karibu kila mtu, kwa hiyo maneno hayawezi kukosekana, utaambiwa mkuu wa Mwenyekiti wa Chama mkoa haelewani na Mkuu wa Mkoa, Katibu haelewani na Mwenyekiti wako"....... "Hayo ni maneno tu na sisi kwakuwa tumeshayazoea kwenye siasa, tunayaelewa na wala hayatupi shida" 

Aidha Katika mrejesho wanakamati kwa pamoja wameridhishwa na mwenendo wa ufuatiliaji, utendaji na usimamizi wa utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi unaosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Fuatilia yaliyojiri ikiwa ni pamoja na utambulisho wa aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe kwa tiketi ya CHADEMA na kutimkia CCM Joseph Michael Mkundi na pia utapata mrejesho mzima wa yale yaliyojadiliwa kwenye kikao toka kwa Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Mangelepa, vipi kuna mtu kawajibishwa?......

Friday, November 9, 2018

VIFAA TIBA VYACHELEWESHA UFANISI WA UTOAJI HUDUMA BORA KITUO CHA AFYA KARUME, RC MONGELLA ATOA SIKU 7.



GSENGOtV

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. John Mongella amefanya ziara katika Kituo cha Afya Karume, Manispaa ya Ilemela na kushtushwa na uhaba wa vifaa tiba kwenye majengo mapya yaliyojengwa na serikali kupitia utaratibu wa “Force Account”. 

Mhe. Mongella ametoa muda wa siku saba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo kuhakikisha majengo hayo yanaanza kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

TCU YAISHUSHIA RUNGU CHUO HIKI, YAAMURU WANAFUNZI WAHAMISHWE.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefuta usajili wa kituo cha chuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba 9, 2018 Katibu Mtendaji wa TCU) Profesa Charles Kihampa amesema mbali ya kufuta usajili wa chuo hicho imeamuriwa pia wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishiwe katika kampasi kuu ya chuo hicho iliyopo Masoka, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema TCU imezuia udahili wa wanafunzi wapya na kuamuru kuhamishwa mara moja wanafunzi wa shahada ya kwanza wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2018/19 katika programu tisa za shahada ya kwanza  katika vyuo vikuu vinne.

Profesa Kihampa amesema wanafunzi wote wanaosoma katika chuo kikuu cha kimataifa cha tiba na teknolojia (IMTU) Dar es Salaam programu ya shahada ya tiba na upasuaji, shahada ya sayansi na uuguzi.

Amesema wanafunzi wote wanaosoma programu ya udaktari wa binadamu kutoka chuo kikuu kishiriki cha Askofu Mkuu James (Ajuco), Songea- Ruvuma.

Ametaja programu nyingine zilizozuiliwa udahili ni kutoka chuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) Moshi, Kilimanjaro, za shahada ya Sanaa na mawasiliano ya umma na sanaa na utawala.

Amefafanua pia imezuia udahili kwa wanafunzi wanaosoma programu za shahada ya elimu na mahitaji maalumu (arts), shahada ya elimu na mahitaji maalumu (sayansi), shahada ya sayansi na elimu na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastiano Kolowa (SEKOMU),Lushoto-Tanga.

WANANCHI KATA YA UHAMBULE, WANGING’OMBE HAWAJARIDHIKA NA MRADI WA TASAF


GSENGOtV
Wananchi wa kijiji cha Msimbazi kata ya Uhambule wilayani Wanging’ombe mkoa wa Njombe hawajaridhika na ujenzi unaofanywa na mkandarasi anayejenga madarasa mawili na vyoo kwa ajili ya shule ya msingi ya mfano ya Msimbazi ambao unafadhiliwa na Mpango wa Kunusuru kaya masikini (TASAF) baada ya kutumia nguvu kazi zao za kusomba mawe na kuchanga zaidi ya shilingi milioni tisa kuunga mkono mradi wa shule, huku kiasi cha shilingi milioni 65  zikiwa zimetolewa na Tasaf, lakini hali hairidhishi baada ya kutumia kiasi cha shilingi milioni 45 hadi sasa….
TAARIFA YA AMIRI KILAGALILA KUTOKA WANGING’OMBE MKOA WA NJOMBE INAELEZA..

*DC MURO AUFYEKELEA MBALI MGOGORO WA ARDHI WA MASHAMBA YA MALULA ARUMERU*

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru *Mhe Jerry Muro* ametatua Mgogoro uliodumu kwa zaidi ya *Miaka Saba*  kati ya wakulima na wafugaji wa kata ya *Malula wilayani Arumeru* na  kuwataka wakulima waendelee kulima katika mashamba ya Malula ambayo ni ardhi ya serikali iliotengwa kwaajili ya uwekezaji wa *viwanda na bandari kavu*

Aidha *Dc Murro* amewataka wanasheria wanaowapotosha wakulima na *wafugaji wa vijiji vya kata ya Malula* kwa kutumia uwepo wa migoogoro ya ardhi kwa njia ya kujinufaisha  kuacha mara moja tabia hiyo na kufuta kesi hizo mahakamani kwani ardhi ni ya serikali na mwenye dhamana na ardhi hiyo ni  *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli*

*Dc Muro* Amezungumza wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya *MALULA*  ambapo mgogoro huo umetokana na wakulima na wafugaji kufanya maeneo ya mashamba hayo kuwa ya kwao na wengine kupeleka mashtaka mahakamani dhidi ya wananchi walioazimwa maeneo hayo na serikali kwaajili ya kilimo.

TPDC YAWEZESHA WANANFUNZI ZAIDI YA 1000 KUNUFAIKA NA VYOO BORA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzzania (TPDC)limewezesha ujenzi wa vyoo bora kwa shule ya Msingi ya Kivinje yenye jumla ya wananfunzi 1320 iliyopo katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

 Akiongea wakati wa kuikabidhi mfano wa hundi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyoo hivyo Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu ameweka wazi kuwa TPDC inatambua kuwa inawajibika kwa jamii ambayo inaendesha shuhguli zake mbalimbali na hivyo maendeleo ya jamii hizo ni suala la msingi kwa Shirika hilo.

 “Sisi kama Shirika la Umma tunaowajibu kurudisha sehemu ya kile tunachopata kwa jamii zetu hizi ili kuweza kuboresha maeneo mbalimbali ya huduma haswa Afya, Elimu, Maji na utawala bora na hivyo ujenzi wa vyoo bora kwa wanafunzi wa Shule hii ya Kivinje inaangukia katika maeneo yote mawili ya elimu na afya.”

 Alisisitiza kuwa suala la vyoo bora kwa wanafunzi ni muhimu sana haswa katika kuwapa faraja na kujiamini zaidi wawepo shuleni na hivyo kupelekea umakini zaidi katika masomo yao ambapo huwafanya wafanye vizuri zaidi kwenye masomo yao. Bi Marie Msellemu Meneja wa Mawasiliano akikabidhi hundi ya milioni 16 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Ramadhani Hatibu mara baada ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Kivinje Aidha akielezea maendeleo ya ujenzi wa vyoo hivyo, Bi Msellemu aliwahimiza Watendaji wa shule hiyo pamoja na Kamati ya ujenzi kuongeza kasi ya ujenzi wa vyoo hivyo ambavyo kwa sasa vilitakiwa kuwa vimekamilika kwa asilimia kubwa ili kuepuka kipindi cha mvua kubwa ambayo inatarajiwa kunyesha katika mwezi ujao.

 Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Ramadhani Hatibu alisema, ameridhishwa namna ambavvyo TPDC inavyoshirikiana na Halmashauri hiyo katika kusaidia katika uboreshwaji wa huduma mbalimbali za jamii.

 Hapa Kaimu Mkurugenzi anaeleza zaidi “kwakweli TPDC mmekuwa mstari wa mbele katika kutushika mkono sisi kama Halmashauri ya Kilwa katika maeneo mbalimbali ambapo katika kumbukumbu zetu zinaonyesha mmefanya mengi tu yakiwemo mchango mlioutoa kawa ajili ya uboreshwaji na ujenzi wa maabara katika Shule zetu za Sekondari, ujenzi wa nyumba za walimu katika Shule ya Sekondari ya Songo Songo, usambazaji wa huduma ya maji kwa Kijiji cha Songo Songo pamoja na Shule ya Sekondari Songo Songo pamoja na uendeshaji wa zoezi la upimaji wa afya na kukabidhi vifaa vya upimaji wa afya katika Kijiji cha Songo Songo” Akiweka msisitizo

Mkurugenzi huyo aliongezea kuwa “leo hii tunapokabidhiana rasmi kiasi cha milioni 16 lakini pia tunapokagua kwa pamoja utekelezaji wa ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Kivinje inazidi kuleta faraja na matumaini katika uhusiano tulioujenga miaka mingi iliyopita na hivyo kwanza ni himize Kamati ya Ujenzi wa Shule hii kuhakikisha ujenzi huu wa vyoo unatekelezwa kwa kasi na weledi ili kutendea haki thamani ya pesa ambayo TPDC wametoa kwa ajili ya uboreshwaji wa shule yetu ili watoto wetu wawe na mazingira rafiki ya kujisomea ambayo yatapelekea ufaulu mzuri kwenye mitihani yao.“

Meneja Mawasiliano akisikiliza muhtasari wa maendeleo yahusuyo maendeleo ya ujenzi wa vyoo toka kwa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Kivinje.

Aidha akisoma taarifa ya ujenzi wa vyoo hivyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kivinje Ndg. Ngabuba alieleza kuwa, “Shule yetu ina jumla ya wanafunzi 1320 kati yao wakiwa Wasichana 696 na Wavulana 624 na jumla ya Walimu 17 ambao kwa ujumla wetu tulihitaji kuwa na vyoo bora situ kwa kujisitiri lakini pia kuhakikisha suala la afya bora linazingatiwa na hivyo basi kwa kubahatika kupata msaada ktuoka TPDC kwakweli sasa tunaenda kuwa na vyoo bora ambavyo vitasaidia wanafunzi wetu kuwa na amani na kujiamini zaidi wawepo shuleni hapa”

“Kwakweli ujenzi umechelewa tofauti na ilivyopangwa nahii ni kutokana na mambo mbalimbali ya kiutawala na kiutaratibu lakini pia uhaba wa seruji ulitokea katika kipindi cha mwezi Juni lakini hivi sasa tuna ahidi kundelea na ujenzi kwa kasi na ufanisi zaidi ili tufikie thamani halisi ya pesa ambayo Shirika letu la TPDC limetoa” aliongezea Mkuu huyo wa shule.

Thursday, November 8, 2018

MWILI WA MAMA MERCY ANNA MENGI UMEWASILI NCHINI KUAGWA LEO LUGALO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameungana na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt.  Reginald Mengi, familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kupokea Mwili wa mmoja wa waanzilishi wa makampuni ya IPP Mama Mercy Anna Mengi.

Mwili wa marehemu, Mama Mercy Anna Mengi ukiwa umewasili katika viwanja vya ndege vya Mw. J.K Nyerere, jijini Dar es salaam na kuzungukwa na waombolezaji.

Mwili huo umewasili nchini majira ya saa 9 Alasiri leo Novemba 7, ukitokea nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika hosptali ya Mediclinic Morningside ya Johannesburg na alifariki duniani tarehe 

WAHITIMU WA MAFUNZO YA RDP YA TBL WATUNUKIWA VYETI

 Mkurugenzi wa ukuzaji wa Masoko wa ABIn Bev,Kanda ya Afrika Mashariki, Carlos Bernitt,akiongea wakati wa hafla ya kutunuka vyeti wahitimu wa mafunzo hayo. Meneja Masoko na Ukuzaji Biashara wa TBL,Edith Bebwa, akiongea wakati wa hafla ya kutunuka vyeti wahitimu wa mafunzo hayo.
Baadhi wa wahitimu wa mafunzo wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo

Baadhi ya wahitimu wakionyesha vyeti vyao wakiwa na Maofisa wa TBL na ABIn Bev
---
Washiriki wapatao 167 wanaofanya biashara kwa kushirikiana na kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) walioshiriki mafunzo ya ujasiriamali na mbinu za biashara yanayojulikana kama Retail Development Programme (RDP) wametunukiwa vyeti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Wanufaika wa mafunzo haya ambao wengi wao ni wamiliki wa mabaa,mameneja wa baa na wafanyakazi wametokea katika wilaya za Temeke, Kinondoni, Kigamboni, Ilala Ubungo na yaliendeshwa na TBL chini ya kampuni mama ya ABIn Bev.

Mkurugenzi wa ukuzaji wa Masoko wa ABIn Bev,Kanda ya Afrika Mashariki, Carlos Bernitt,aliwapongeza wahitimu wa mafunzo hayo “Nawapongeza kwa kuhitimu mafunzo haya na nina imani mkitumia vizuri maarifa mliyoyapata yatawasaidia kukuza biashara zenu na kuleta maendeleo ya kwenu binafsi na jamii nzima kwa ujumla”,alisema Bernitt.

Akiongea kuhusu mafunzo hayo,Meneja Masoko na Ukuzaji Biashara wa TBL,Edith Bebwa,alisema mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa chini ya mpango unaojulikana kama Retail Development Programme (RDP), yanalenga kuwapatia mbinu za kufanya biashara kwa ufasaha wafanyabiashara wadogo wanaoshirikiana nao kibiashara ili kuwasaidia kukua kibiashara.

“Mafunzo haya yameendeshwa na wataalamu wa masuala ya ujasiriamali na washiriki wamewezeshwa kujifunza mambo mbalimbali ya biashara ikiwemo urasimishaji biashara zao,tunaamini yatawasaidia kufanya vizuri sambamba na malengo yetu yaliyokusudiwa”.Alisema Bebwa.

Akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo haya,Damas Asenga,alisema kuwa mafunzo haya yamewasaidia kujua masuala mbalimbali ya kuendesha biashara hasa za kuuza vinywaji kama vile utunzaji wa hesabu,mbinu za kuongeza mauzo,huduma kwa wateja,nidhamu ya matumizi ya pesa,jinsi ya kukabiliana na ushindani wa kibiashara na umuhimu wa kufuata kanuni za biashara zilizowekwa na serikali. “Mafunzo haya ni mazuri na tunaiomba TBL iangalie uwezekano wa kuyafikisha kwa wajasiriamali wengi zaidi nchini kote “,alisema Asenga.

Wednesday, November 7, 2018

WAJANE WA AJALI YA MV NYERERE KUNUFAIKA NA BPW.


Na James Timber, Mwanza

Taasisi ya Business and Professional Women Tanzania (BPW), inatarajia kujenga kiwanda cha kutengeneza taulo za kike pamoja na kuwasaidia kwa kuwainua kiuchumi wajane wa waliopoteza wenza wao katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kwenye Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe katika Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza na Waadishi wa Habari jijini hapa mapema hii leo Ofisini kwake Rais wa BPW Tanzania Bertiller Massawe amesema kwa sasa wana mikakati ya kuanzisha kiwanda kwa ajili ya kutoa taulo za usafi kwa watoto wa kike hizo zitakazopatikana kwa  bei nafuu pamoja na kugawa bure kwa watoto wa shule ambao ndio waathirika wakubwa kutokana na kutokuwa na ujasiri wa kutokujiamini pamoja na kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo hasa wafikiapo siku hizo za hedhi. 

"Huu mpango tulianzisha toka Mwezi Aprili Mwaka huu na baadhi ya shule tulizofikia ni Buhongwa, Mkuyuni, Ngaza, na nyingine katika Wilaya ya Misungwi, ambapo tunaamini utumiaji mzuri wa taulo hizo zitamwezesha mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo yake kwani atakuwa anafuatilia kimaumakini kile anachofundishwa ikiwemo uwezo wa kusimama darasani bila wasi wala hofu na kuhoji chochote na moja kati ya mikakati yetu kwa sasa iliyopo ni kufikia mwezi Januari 2019, chini ya ufadhili wa BPW kutoka nchini Italia na Malaysia tumeguswa na wanawake wajane  ambao wamekutwa na majanga tofauti ikiwemo lile na ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere," amesema.

Massawe amesema kuwa BPW inajihusisha na upimaji wa shingo ya kizazi na saratani ya matiti kwa akina mama kushirikiana na madaktari waliobobea katika taaluma hiyo, ambapo wanamwezesha mwanamke kujua hali yake kiafya kabla ugonjwa haujasambaa kwani ukiwa ugonjwa huo ukiwa sugu ni gharama kupata matibabu yake na utapekekea kudidimiza utendaji kazi wa mwanamke katika jamii.

Pia ameeleza kuwa zoezi hilo la upimaji wa shingo la kizazi na kansa ya matiti litakuwa endelevu ambapo kwa awali walitoa huduma ya upimaji kwa baadhi ya hospitali zilizopo Wilaya ya Nyamagana na Misungwi na wanatarajia kutoa huduma hiyo ya upimaji Desemba 2018, katika Chuo Kikuu cha St. Augustine SAUT  kwa wanafunzi.

Hata hivyo, mbali na upimaji wanatoa huduma ya mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi ya wananwake na vijana na kuunganishwa na taasisi ya mikopo ambayo haina riba inayotolewa na halmashauri pamoja na kuwezeshwa  kuunda vikundi vya uzalishaji mali, akiba na mikopo, ambavyo vitawapa kipaumbele kupata mikopo hiyo kwa haraka zaidi.

Aidha Rais huyo amefafanua juu ya takwimu zilizofanywa na BPW kuwa zinaonesha kuwa mabinti walioko mashuleni ni asilimia mbili ndio wanauwezo wa kutumia taulo hizo ipasavyo na wengine  kutohudhuria masomo kwa muda wa siku tatu hadi saba.

UZEMBE ULIOSABABISHA KIFO CHA MTOTO WA MAMA ALIYEKUWA AKIJIFUNGUA DC NYAMAGANA ANG'OA WATUMISHI WA 5



ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Jumla ya watumishi watano wa hospitali ya wilaya, Butimba wamesimamishwa kazi kufuatia kifo cha kichanga Novemba 3,mwaka 2018 kutokana na uzembe.

Akizungumza huku akilengwa na machozi Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Philis Nyimbi amesema kumekuwepo na malalamiko ya wananchi katika hosipitali hiyo ya Butimba kutokana na uzembe unaoneshwa na  baadhi ya watumishi wa hosipitali hiyo, rushwa na kauli mbaya kwa wagonjwa wanaofika katika hosipitali hiyo kupata huduma.

Hili limejiri baada ya kutokea taarifa za kupuuzwa kwa mzazi aliyefika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita kwa ajili ya kujifungua lakini akakosa msaada.

Watumishi waliosimamishwa kazi ni pamoja na daktari anayedaiwa kupokea pesa mkononi bila ya kutumia mfumo wa Kieletroniki wa ukusanyaji wa mapato unaotambuliwa na serikali sambamba na wauguzi wanne.

Mmoja kati ya wazazi waliokuwa wodini, Shanifa Lukas amesema licha ya hospitali hiyo kupokea wagonjwa wengi kwa siku, kuna shida kubwa kwa watumishi hususan wauguzi ambao mara nyingi wamekuwa wakitoa lugha chafu.

Tangu mwezi januari mwaka huu 2018 zaidi ya wototo wachanga wengi (TAKWIMU ZAJA) wamefariki dunia kutokana na uzembe wa baadhi ya madaktari wakati mama wajawazito wakiwa kwenye harakati za kujifungua.

Haya yanajtokeza wakati Serikali ya Tanzania ikiwa imewekeza nguvu zake katika kuimarisha mifumo ya utoaji huduma za afya ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga kwa malengo ya miaka mitano na ikiwa imekusudia kutokomeza kabisa vifo vitokanavyo na magonjwa yanayoweza kuzuilika ifikapo mwaka 2030 kama ilivyoelezwa kwenye dira ya kimataifa ya mkakati wa afya ya kila mama kila mtoto na vijana barubaru.

ALIKIBA KUDHAMINI WASAFI FESTIVAL

Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani.

Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine.

Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa .

Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa.

MFANYAKAZI WA UDSM AJISHINDIA GARI KUPITIA PROMOSHENI YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA'

Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, (kushoto)Meneja Udhamini na Mawasiliano wa TBL,David Tarimo (katikati) na Afisa Kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humid Semvua wakifuatilia namba ya mshindi wakati wa droo ya kwanza ya mshindi wa gari iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Kulia) ni Meneja Udhamini na Mawasiliano wa TBL, David Tarimo.

Na Mwandishi Wetu.
Mkazi wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julitha Kilawe, ameibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID kupitia promosheni ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’iliyozinduliwa mwezi uliopita itakayowezesha washiriki 3 wa promosheni hiyo kujishindia gari 1 kila mwezi katika kipindi cha miezi 3 ya promosheni hiyo. 

 Droo ya kuwapata washindi hao imefanyika jijini Dar e Salaam, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Taifa na kushuhudiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Mshindi huyo alipokea habari hizo kwa furaha baada ya kupigiwa na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, ambapo alieleza kuwa amefurahishwa na kujishindia gari ambalo litamrahishia usafiri katika shughuli zake za kila siku. “Natoa wito kwa wateja wetu wazidi kujitokeza kushiriki, tumejipanga vyema ili kuwafikia wote nchi nzima. 

Tumewaletea wateja wetu promosheni hii kwa lengo la kuwashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono”. alisema Tarimo. Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa muda wa miezi mitatu kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

 Kwa muda wote huu washiriki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa kabisa ya gari mpya. Kwa upande wake, Meneja wa Bia chapa ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema mbali na zawadi kubwa ya magari mapya zipo zawadi nyingi za kujishindia papo hapo kwenye promosheni ikiwemo bia za bure, fulana nakadhilika. 

Alisema promosheni itakuwa inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5000 nchini katika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. ‘Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.’ Alisema ili kuingia kwenye droo ya magari mapya ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ wateja watatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba, kisha watatuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wale wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL.

 Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz.

DC Jerry Muro : Arumeru ya wakulima na Wafugaji Inakuja

Na, Imma Msumba Arumeru

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jery Muro amejitolea  kuwasadia kuandika maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze ‘KUKOPESHEKA’ na taasisi za kifedha ambazo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo au andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.

Muro amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa ‘VIKWAZO’ vya maandiko ya mradi katika hatua za awali pindi wananchi wenye nia ya kuanzisha kilimo na ufugaji wa kibiashara wanapoanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa ‘vikwazo’ hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia wananchi kuondoa vikwazo hivyo.

Jerry Muro amesema tayari kampuni binafsi ya wawezeshaji wa wakulima ( PASS) Private Agricultural Sector Support imekubal kuwaandalia na kugharamikia mpango kazi wa kibiashara (Bussiness Planning) zitakazowasaidia wakulima na wafugaji katika kupata mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara.

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Mhe Muro kufunga maoyesho ya jukwaa la wakulima Meru ambayo yamefanyika kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo pamoja na kukubali kutoa msaada wa bure katika kuandaa na kuandika maandiko ya mchanganuo wa kibiashara pia amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa haraka zaidi, na kuahidi kuwatafutia kompyuta kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za taarifa za wakulima na wafugaji.

Kwa upande wake Meneja wa Tawi la kampuni ya (PASS) amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumerry, Jerry Muro Kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na Taasisi hiyo.

Tuesday, November 6, 2018

MAMA AMUUA MWANAE KWA KIPIGO AKIMTUHUMU KUIBA MAEMBE KWA JIRANI, AMTUNDIKA DARINI ILI KUPOTEZA USHAHIDI AKISEMA AMEJINYONGA.


GSENGOtV

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia mwanamke mmoja aitwaye RAHEL MATALAKA, miaka 41, mkazi wa kijiji cha lugenge, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake wa kiume aitwaye MALIATABU CONSTANTINE, miaka 10, mwanafunza wa darasa la pili shule ya msingi Ikeleg,Wilayani Misungwi.

Tukio hilo la mauaji limetokea tarehe 03.11.2018 majira ya 19:00hrs usiku, hii ni baada ya mama wa marehemu kuletewa malalamiko kuwa mtoto wake alikua akiangusha na kuiba maembe kwa jirani. Ndipo mtuhumiwa alipatwa na hasira na kumpiga mtoto kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyopelekea mtoto kupoteza fahamu na baadae kufariki dunia.

Mtuhumiwa alipoona mtoto amepoteza maisha alimchukua na kumtundika juu ya mwembe kwa kutumia kipande cha khanga ili apoteze ushahidi ili baadae ionekane kuwa amejinyonga. Ndipo majirani walipoona tukio hilo walitoa taarifa kituo cha Polisi.  Aidha baada ya polisi kupata taarifa hizo tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Polisi tunaendelea na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa  ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Katika tukio la pili, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tumefanikiwa kukamata gari moja lililoibiwa lenye namba T.233 CDG aina ya Toyota Carina mali ya RENATUS ELIUS, mkazi wa mtaa wa Ghana, likiwa limetelekezwa kando ya barabara huko maeneo ya Kitangiri Wilayani Ilemela.

Gari hilo liliibiwa tarehe 01.11.2018, ndipo mmiliki wa gari alitoa taarifa polisi juu ya kuibiwa kwa gari lake. Polisi baada ya kupata taarifa hizo tulifanya msako mkali kwa kushirikisha vikosi vyetu vya askari wa kufuatilia wezi wa magari na Intelejensia. Ndipo tarehe 04.11.2018 majira ya mchana tulifanikiwa kulikamata gari hilo likiwa limetelekezwa kando ya barabara huko mtaa wa kitangiri huku wezi wakiwa wametoroka.

Aidha baada ya kulikamata gari hilo, tulilifanyia ukaguzi na kugundua baadhi ya vifaa vya gari hilo vimetolewa ambavyo ni betrii ya gari moja, tairi  ya gari moja, jeki moja, radio ya gari, power window na show ya mbele ya gari. Polisi tunaendelea na msako mkali wa kuhakikisha wezi hao wanapatikana.

Katika tukio la tatu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia mwanamke mmoja aitwaye MALAGALITA MATHIAS, miaka 55, mkazi wa kijiji cha Nyatukala, kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi (gongo) kiasi cha lita 20 na dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilo moja, huko maene ya kijiji cha Nyatukala Wilayani Sengerema.

Tukio hilo limetokea tarehe 05/11/2018 majira ya 17:00hrs jioni, hii ni baada ya kupatikana kwa taarifa kwamba katika Vijiji vya Nyamizeze na Nyatukala vilivyopo Wilayani Sengerema wapo watu wanaojihusisha na uuzaji pamoja na utengenezaji wa pombe ya gongo na dawa za kulevya aina ya mirungi.

Aidha baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Polisi tulifanya msako mkali katika vijiji hivyo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa na kiasi hicho cha pombe ya moshi na mirungi huku wenzake wakifanikiwa kutoroka.

Polisi tunaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini wenzake anaoshirikiana nao katika biashara hiyo haramu ya gongo na mirungu, pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Katika tukio la nne, mtoto mmoja wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 2 hadi 3 ameokotwa akiwa hai baada ya kutupwa kichakani kandokando mwa ziwa Victoria na mtu asiyefahamika, huko maeneo ya Bwiru ziwani Wilayani Ilemela.

Tukio hilo limetokea tarehe 01.11.2018 majira ya 14:00hrs, hii ni baada ya watu waliokua wakipita njiani kusikia sauti ya mtoto akilia toka kichakani ndipo walifuatilia na walipoona ni mtoto walitoa taatifa polisi.

Polisi tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kukuta mtoto wa kike akiwa ametupwa kichakani hapo akiwa hai huku mwiliwake ukiwa umeviringishwa kwenye mfuko wa sandarusi.

Mtoto amepata matibabu na hali yake inaendelea vizuri amekabidhiwa katika shirika la Forever Angel lililopo Bwiru Wilayani  Ilemela  kwa ajili ya hifadhi. Polisi tunaendelea na upelelezi pamoja  na msako mkali wa kumtafuta mama wa mtoto huyo.

Katika tukio la tano; Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia tapeli/mwizi mmoja aliyefahamika kwa jina la BENEDICTO BAHATI, miaka 29, mkazi wa kiloleli, kwa tuhuma za kujifanya afisa wa TCRA, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Tukio hilo limetokea tarehe 02.11.2018, majira ya 16:30hrs, hii ni baada ya mtuhumiwa kwenda kwa mtumishi wa benki ya CRDB tawi la Nyegezi -Malimbe na kumtapeli kuwa yeye ni afisa wa TCRA Mkoa wa Mwanza, hivyo amefika hapo akidai anazo taarifa zake ambazo zinaonesha amekuwa akifanya mawasiliano yasiyo rasmi.

 Hivyo ametumwa na ofisi ya TCRA Mwanza kufuatilia taarifa hizo, na kumtaka atoe fedha kiasi cha laki tano ili aweze kumfichia siri ili asitoe taarifa hizo kwa mamlaka inayohusika yaani TCRA.

Baada ya hapo mlalamikaji alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambapo Polisi tulituma askari makachero na wamakosa ya mtandao na badae tulifanikiwa kumtia tapeli huyo nguvuni. Polisi tunaendelea na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.Aidha msako mkali wa kuwatafuta wenzeka anaoshirikiana nao katika uhalifu huo bado unaendelea.

Tukio la sita, Mafanikio ya misako Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tumefanikiwa kukamata gari moja aina ya IST rangi ya Silver lenye namba T.892 DFY/DKY na pikipiki mbili moja inanamba MC.836 ASK aina ya BOXER na nyingine aina ya FEKON lakini haina namba. Gari na pikipiki hizo zimekamatwa baada ya kutumika katika matukio ya kiuhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji na Mkoa wa Mwanza.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tunatoa onyo kwa wakazi wa Jiji na Mkoa wa Mwanza tukiwataka waache vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, pindi mtoto anapokosea apewe  kalipio na akanywe na kuonyeshwa madhara ya wizi ili atambue kosa na wala sio vipigo. Sambamba na hilo tunawataka vijana waache tabia ya kujihusisha na uhalifu kwani utawagharimu.

Imetolewa na:
Jonathan Shanna – ACP
Kamanda wa Polisi (M) Mwanza
06 November, 2018.

KUMEKUCHA NAMTUMBO MARATHON, MAMIA WAJITOKEZA KUJIANDIKISHA


Wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki Namtumbo Marathon inayotarajiwa kutimua vumbi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo maelfu ya wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake wamekuwa wakizitazamia mbio hizo kuanza wakati wowote ili nao wapate fursa mbalimbali za kushiriki katika mbio hizo.

Akizungumzia usajili unaoendelea katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo, Dokta Chihoma amesema watu wengi wameitikia wito na wamejitokeza kwa wingi wao kujiandikisha tayari kwaajili ya kushriki mbio hizo ambazo zilianzishwa rasmi mwaka 2017 kwa malengo mengi lakini kubwa likiwa ni kuchangisha fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo imefanikia kuanza kwa kiasi kikubwa. 

Aidha Chihoma ameongeza kuwa nafasi bado zipo wazi kwaajili washiriki watakaojitokeza kujiandika kwaajili ya bio hizo. 

Kwa upande wao wadhamini wa na waandaaji wa mbio hizo Mantra Tanzania au Uranium one wamesema kila kitu kipo sawasawa na kuwataka watanzania na wageni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo zinalenga kuleta maendeleo ya kiafya katika eneo la Namtumbo na vitongoji vyake. 

Mwakilishi wa Mantra Tanzania Bi. Khadija Pallangyo Kawawa amaesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba watanzania watafurahia mbio za mwaka huu kutokana na jinsi zilivyopata hamasa kubwa katika maeneo mbalimbali “Nawaomba sana watanzania wajitokeze kwa wingi waje washiriki nasi katika kufanikisha awamu ya pili ya Namtumbo Marathon” 

Alisema Khadija huku akiwaomba wana Namtumbo, Songea Ruvuma na vitongoji vyake hasa wafanya biashara na wenye makampuni katika maeneo mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi kuuchangia ujenzi wa hospitali ya wila ya Namtumbo akiitaja hospitali hiyo kuwa itakuwa msaada mkubwa wenye kuleta mafanikio na maendeleo katika eneo lote linalopakana na wilaya hiyo. 

Nao waratibu na wasimamizi wa tukio zima Corporate Info Limited ya jiji Dar Es Salaam wamesema mbio hizo zinaandandaliwa kuja kuwa moja kati yam bio kubwa kabisa nchini huku wakijivunia kuwa wasimamizi wa mbio hizo kwa mara nyingine. 

Wilaya ya Namtumbo imezungukwa na vivutio mbalimbali vya kiasili mojawapo ikiwa mbuga kubwa ya wanya ya Sloue ambayo imekuwa kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka mataifa mbalimbali na ndani nchi hivyo kufanyika kwa mbio hizo itakuwa sehemu mojawapo ya kuitangaza mbuga hiyo pamoja na vursa zingine kama madini aina ya Uranium ambayo yanapatikana kwa wingi wilaya Namtumbo. 

Monday, November 5, 2018

SSS

WANAFUNZI MWANZA SEKONDARI WANENA JUU YA PEPA LA LEO NATIONAL KIDATO CHA 4



GSENGOtV

Wanafunzi wa Kidato cha Nne kwa shule za Sekondari zaidi ya 250 mkoani Mwanza, mapema leo asubuhi wameanza kufanya mtihani wao wa kuhitimu ngazi hiyo.

Nimebahatisha kutembelea shule kadhaa kutizama ulinzi na hali inavyoendelea na taratibu zake hatimaye nikapata fursa ya kufanya mazungumzo kiduchu na wanafunzi wa Mwanza Sec.

VIDEO:- AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA HUDUMA UDHIBITI VVU NA UKIMWI MWANZA


Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella, akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza.



GSENGOtV
Asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia nchini Tanzania imetoa msaada wa magari mawili aina ya Nissan Patrol kwa halmashauri za wilaya za Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri hizo.

Magari hayo yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yana thamani ya shilingi milioni 186 yamenunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).

Hafla fupi ya Makabidhiano ya magari, imefanyika leo Jumatatu Novemba 5,2018 wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.

Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo kwa Mkuu huyo wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa alisema msaada huo wa magari ni kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za afya hususani za VVU na UKIMWI kwenye vituo vya kutolea huduma.

Dkt. Mwakyusa alisema, AGPAHI imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na halmashauri katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI kwa ajili ya ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

“Magari tuliyokabidhi leo yana thamani ya shilingi milioni 186, na hii ni sehemu ya vyombo vya usafiri (magari,pikipiki na baiskeli) vyenye thamani ya shilingi milioni 900.2 tulivyonunua katika kipindi cha kuanzia Oktoba 2017 hadi Septemba 2018 kwa ajili ya kuleta tija kwenye utendaji kazi ili kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri ambazo AGPAHI inafanya kazi,” alieleza Dkt. Mwakyusa.

Aliongeza kuwa katika jitihada za kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI, katika kipindi hicho, AGPAHI imefanyia ukarabati vituo 146 vya kutolea huduma vikiwemo 36 vya mkoa wa Mwanza. Pia imeweka mifumo ya umeme jua kwenye vituo 40 vya kutolea huduma kwenye halmashauri mbalimbali.

Akipokea magari hayo, Mkuu wa mkoa, Mheshimiwa Mongella aliishukuru AGPAHI kwa kuwa mdau muhimu katika sekta ya afya na kuomba waendelee kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Mheshimiwa Mongella aliwataka watendaji wa halmashauri zilizopewa magari kutunza na kuyatumia magari hayo kwa kazi za afya na maendeleo ya halmashauri na siyo vinginevyo.


Muonekano wa nyuma magari yaliyotolewa na AGPAHI.
 Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Florence Temu akiwasilisha jinsi shirika lake lilivyo shiriki katika utoaji huduma za Afya na Kupambana na VVU, kuelekea Disemba mosi 2018.
Shukuran.

Sunday, November 4, 2018

NAIBU WAZIRI ARDHI AHITIMISHA BONANZA LA MICHEZO CHUO CHA MIPANGO MWANZA YUMO MSHINDI WA NDIKO LA SERIKALI YA VIWANDA.


GSENGOtV

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, leo Jumapili ya Tarehe 4 Novemba 2018 amekabidhi zawadi kwa washindi wa nafasi za juu katika Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza, lililofanyika kwa takribani wiki nzima na sasa kuhitimishwa kwenye viwanja vya chuo hicho.

Sanjari na kukabidhi zawadi za fedha taslimu kwa washindi mbalimbali pia Mama Angeline ametia chachu kwa wanamichezo wa timu za soka wanawake na wanaume kwa kuwakabidhi seti mpya za jezi kwa kila timu washindi ikiwa ni pamoja na mipira.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akihutubia  Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza, lililofanyika kwa takribani wiki nzima na sasa kuhitimishwa kwenye viwanja vya chuo hicho kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Sehemu ya kusanyiko la wanafunzi Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akimkabidhi zawadi ya shilingi 150,000/= mshindi wa kwanza wa mbio za mita 100 wasichana Tabu Magesa katika Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza
Mpira wa Miguu wavulana washindi walikuwa Tiger Fc, 
Mpira wa Miguu wasichana washindi ni Golden Star Fc,
Mpira wa Pete (Netball) washindi ni Shooter Girls,
Mpira wa Kikapu washindi ni GIM
Riadha mita 100 wavulana mshindi ni Elisha John.
Pia katika Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza upande wa Elimu washindi mbalimbali wamepatikana.

Proposal Writing:- Mshindi ni Joseph M. Japan

Presentation Writing:- Mshindi ni Petro Mchumi

Computer:- Mshindi ni Shahban Abdalah

Map Drawing:- Mshindi ni Hashimu Munis


Sehemu ya kusanyiko la wanafunzi Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza.
Sehemu ya kusanyiko la wanafunzi Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza.
Sehemu ya kusanyiko la wanafunzi Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza.
Sehemu ya kusanyiko la wanafunzi Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza.
Sehemu ya kusanyiko la wanafunzi Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza.
Sehemu ya kusanyiko la wanafunzi Bonanza la Michezo la Chuo Cha Mipango Mwanza.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.